Wanaoutaka urais 2015: Yupi anafaa?

ni kweli mkuu...Kila aliyeutafuta urais hata kama alikua anang'ara vipi ikikaa tu miaka mitatu utaona anavyozeeka ghafla na kujichokea...Mwangalie JK yaani huwezi amini ndio yule kijana wa enzi hizo aliyekuwa anawaka kachoka mpaka unamwonea huruma...Hiki kiti sio cha lelemama
 
Kuna jambo huwa nadhani watu wengi huwa hawajiulizi kabla ya kufanya maamuzi ya kujitangazia kuwa wanautaka urais. Watu hawa huwa fikra zao huishia kuwa kuwa rais ni kula bata na starehe za kufa mtu. Kumbe lah. Nadhani mkimuuliza JK kwa sasa hamasa aliyokuwa na mawazo aliyokuwa nayo wakati anautafuta urais kwa udi na uvumba atakupa jibu tofauti ingawa kwa sasa hali ilivyo ni siri yake. Naelewa kuwa mtu yeyote anao uhuru wa kukitafuta kiti hicho lakini.....sidhani kama wengi huwa wanajiuliza unyeti wa nafasi hiyo.

Nina shaka pamoja na kuwa Ikulu miaka nane sasa hata JK hajajua sawasawa kazi halisi za Rais wa Nchi. Madaraka anayatumia sana lakini haoni kasoro za jinsi anavyoyatumia. Amelaumiwa kufumbia macho uharibifu wa wale wanaoitwa rafiki zake. Haoni, hekima yake inatokea pale anapolazimishwa na Bunge,mfano ni kuvunjwa kwa mabaraza ya Mawaziri kwa ufisadi, masikini JK hajui hata ufisadi uliupo anangoja kelele zikizidi kwa kuogopa kuhukumu wasio na makosa(?). Yaani hajui maswala magumu yalipo na yanatokea vipi. Mifano iko mingi sana, wizi wa fedha na kuficha fedha katika mabenki ya Uswiss amemwachia Zitto Kabwe kujibishana na Mgimwa badala ya yeye kuzinduka, kufuatilia na kukamata watu kama wapo, jambo ambalo linafanya sakata lote kuwa kama mchezo wa kuigiza tu.

Mwinyi amelipua kambi MBILI za Jeshi bado yumo tu, na huko alikohamia kumetokea utekaji nyara wa raia bado JK anaona kawaida tu. Membe ameboronga kutangaza vita na Malawi ndani ya ardhi ya Malawi JK anaona kawaida tu. Ukimwambia sasa hivi kuwa Jaji Kiongozi Jundu hatekelezi majukumu yake ipasavyo kwa sababu cheo hiko amekipata kama zawadi kutoka kwa JK bado haoni logic yake. Jaji huyu hata majukumu yake ya Ofisi anayakwepa na kujifanya hana lazima ya kuyatekeleza, muda wote Jundu fundi wa kukutana na waislamu wenzie tu kupokea hongera za kuteuliwa kuwa JK (Jaji Kiongozi).

Ukimwambia yeye mwenyewe JK nyendo zake huko Uswiss na Marekani zinatia mashaka ndiyo umetafuta hatari, atang'aka kabisa, utamskia Membe na Salva Rweyemamu wakisisitiza manufaa ya safari za JK ughaibuni.

La muhimu JK anataka kufanana na Julius Kambarage (Nyerere) kusimamia ukombozi wa Afrika lakini JK anapeleka majeshi katika nchi huru kuwafukuza waafrika kutoka kwa waafrika wenzao kama alivyofanya Madagaska kwa Kanali.

Je wewe unayehoji hao wagombea wengine unaona mbali na majukumu halisi ya Rais wetu au na wewe ndiyo kelele tu?
 
Kuna jambo huwa nadhani watu wengi huwa hawajiulizi kabla ya kufanya maamuzi ya kujitangazia kuwa wanautaka urais. Watu hawa huwa fikra zao huishia kuwa kuwa rais ni kula bata na starehe za kufa mtu. Kumbe lah. Nadhani mkimuuliza JK kwa sasa hamasa aliyokuwa na mawazo aliyokuwa nayo wakati anautafuta urais kwa udi na uvumba atakupa jibu tofauti ingawa kwa sasa hali ilivyo ni siri yake. Naelewa kuwa mtu yeyote anao uhuru wa kukitafuta kiti hicho lakini.....sidhani kama wengi huwa wanajiuliza unyeti wa nafasi hiyo.
kwa mtu ambae anania ya kweli yakufaya urais kama kazi hawezi kuung'ang'ania wala kuwa na kitambi akiwa ikulu. JK Ni mfano mzuri. unamuona alivyozeeka mzee!
 
JK anajuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuta kuutakam urais, yeye alichokuwa anawaza ni kupigiwa mizinga 21 na kusafishiwa njia anapopita barabarani, baada ya kugundua kuwa urais ni mzigo ndiyo akabuni kuwa mtalii dunia nzima , kila linapohuja jambo zito ambalo hana ufumbuzi wake ana zua safari za nje.
 
Urais siyo mgumu. Hata DJ anaweza kuwa raisi (mfano: Madagascar)!

Kasoro ya Demokrasia holela ndiyo hiyo, vijana ambao hawajui Ikulu ina madhara gani kwa nchi ndiyo nguvu kubwa ya Demokrasia yetu. Siku ya siku kila kukicha tunalalamikia ufisadi bila kujua umetoka wapi, wizi bila polisi wa kuushughulikia na maadili bila wa kujua kuyarekebisha. Dawa ni kungoja uchaguzi na kuingia mikenge mipya ya Rais mpya.
 
Uraisi si ulimbukeni wa madaraka kama wengi wadhaniavyo.

JK hakupaswa kuwa raisi,level zake ni ubalozi wa nyumba 10 na uenyekiti wa mtaa...uwaziri alikuwa kazidishiwa madaraka zaidi ya uwezo wake.

Zitto na wenye fikra kama zake hawatafit uraisi kwasababu wanataka madaraka hayo ili wapate 'ujiko' tu.
 
Ukiingia ndani ya moyo wa mtu kama kabwe zitto atakuambia kabisa kwamba yeye hatafuti urais bali kuvuruga chadema.Ameshajipima sana jukwaani akaona hafai kutokana na michango ya mawazo inayotolewa jukwaani.WATANZANIA tumejifundishwa tuition ya bure kabisa na urais wa daktar wa kuheshimiwa kwamba urais si kwa m2
 
Ukiwa muadilifu uraisi ni mgumu.

Ukitizama watu wako mabarabarani,hospitali,sokoni,mashuleni,majumbani,maofisini,mitaani n.k hasa kwa nchi hizi maskini uraisi ni mzigo na ni ugonjwa wa moyo.

Mtu pekee ambae angeweza kututhibitishia haya ni marehemu baba wa taifa ila siyo Mwinyi,Mkapa wala Kikwete.

Huo ndio ukweli.
 
Urais siyo mgumu. Hata DJ anaweza kuwa raisi (mfano: Madagascar)!
Unasema hata DJ anaweza?! Weka hata kibaka asiyewahi kuingia hata darasani, si ndiyo Demokrasia yenyewe inavyosema bwana? Akishafika huko lazima atashughulika tu na mtamwona Rais yuko Ikulu. Sasa hivi ukitaka kwenda Ikulu usiwaambie watu ukweli, ukweli sasa hivi wengi unawauma, ukiwaambia wanakuona mbaya, hawakupi kura. Ndiyo sababu wote wanaotarajia uRais wanakwenda wakitafuta maendeleo. Mtikila alipokwenda Mara akasema nchi ina ukabila wakampiga mawe, lakini kweli ukabila upo lakini ni waTz hao hao hawataki kukusikia ukiwaambiwa kuwa upo. Sema hakuna ukabila, waambie utajenga reli za kupita angani ....(makofi wawawawawa), sema utawapelekea maji mpaka mlangoni. Lowassa kishafika mpaka Korea kununua mvua ya kutungua kwa risasi (Yarabi mvua gani hiyo? Mbona jangwani Saudi wasingekuwa na matatizo ya kuomba mvua kwa Mola wao!). Ukishapata urais panga mambo yako jinsi unavyotaka kwa sababu hao waliokuchagua hawana uwezo wa hata kukuuliza unafanya nini, wachilia mbali kukunyang'anya kura zao......upo hapo? Kagombee tu, kila mtu uRais anauweza!
 
Kuna jambo huwa nadhani watu wengi huwa hawajiulizi kabla ya kufanya maamuzi ya kujitangazia kuwa wanautaka urais. Watu hawa huwa fikra zao huishia kuwa kuwa rais ni kula bata na starehe za kufa mtu. Kumbe lah. Nadhani mkimuuliza JK kwa sasa hamasa aliyokuwa na mawazo aliyokuwa nayo wakati anautafuta urais kwa udi na uvumba atakupa jibu tofauti ingawa kwa sasa hali ilivyo ni siri yake. Naelewa kuwa mtu yeyote anao uhuru wa kukitafuta kiti hicho lakini.....sidhani kama wengi huwa wanajiuliza unyeti wa nafasi hiyo.

nyerere alipata kusema urais ni mzigo
 
Tanzanians need to understand very well inside out of those who think they can be presidents of this country. Ni muhimu kuwachambua kinagaubaga watu wote wanaoutamani urais ili tuwalinganishe na Tanzania tunatoitaka- yaani nchi ya usawa wa hali na mali.

Hatutaki kupata marais ambao wanapitia mgongo wa nyumba- wanajificha ficha na kutotaka kujadiliwa. Wanataka wengine wajadiliwe lakini wao hawataki kujadiliwa. Kati ya watu ambao wameshajitangaza wenyewe kuutaka urais ni Zitto. Hivyo ni haki na ni wajibu wa wanachi wa Tanzania kumuelewa vizuri Zitto.

Ili tumuelewe tutajadili hoja zake, matangazo yake na matendo yake. Tunataka kila anayegombea urais apitie kwenye tanuru la kusafisha uchafu. Hatutaki tena kuwa na mgombea urais tusiyemjua. Tulishaumwa na nyoka mwaka 2005. Hatutaki tena kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
Jambo hili, tunataka lieleweke vizuri kwa wote wanaoutaka urais kuwa lazima wajadiliwe kwa uwazi.

Kila mmoja wao, awe Membe, Sitta, Lowasa, Zitto, n.k. Lazima wote wajadiliwe. Mtu kama Slaa ambaye wala hajajitapa kutaka kugombea urais mwaka 2015, amejadiliwa sana, na wananchi wanamfahamu vilivyo. Na huu ni ukurasa wa Zitto Kabwe, kurasa za wengine zitafunguliwa pia kwenye folder hii ya Tuwachambue wanaoutaka urais. Tunawataka hawa wanaoutamani urais wasiingilie kazi hii ya wananchi ya kuwachambua na kutaka kuwafahamu vilivyo.

Waache maongezi ya wazi ya wananchi juu yao yaendelee. Kama wanaufafauzi wanaweza kuutoa, lakini mwisho wa siku wananchi watachambua pumba na mchele.
Katika ukurasa huu wa Zitto, ninaanza kuchambua machapisho yake kwenye gazeti moja la kila siku la Kiswahili. Anatoa hoja kwamba wananchi wafuate misingi wasifuate watu. Na sidhani kuwa Zitto anatarajia watu waseme, Amin au Amen au Amina. Hapana, Tutachambua hoja zinazotolewa. Hoja hii ya Zitto imekosa grounding.

Usahihi ni kuwa huwezi kutenganisha misingi ya Taifa au taasisi na watu. Watu ndio huandaa misingi. Kwa mfano waasisi wa Taifa letu la Tanzania walianzisha misingi ya usawa wa binadamu, ujamaa na kujitegemea, n.k. Wananchi walipoikubali misingi hii wakawa wafuasi wa watu hawa. Kwa hiyo wananchi wataendelea kuwafuata watu kwa kuwa ndio wanaotengeneza misingi.

Huwezi kutenganisha watu na misingi
. Jambo lingine la kujadili kuhusu Zitto ni hoja yake ya kulinda umoja wa kitaifa. Amenukuliwa pia na gazeti la Kiswahili la Tanzania kuwa Kikwete na Serikali yake wanahatarisha umoja wa kitaifa kwa kushindwa kutoa nguvu ya hoja katika suala la gesi. Bali wanatoa vitisho na kutoa hoja za nguvu.

Tumjadili Zitto kama mtu anayeutamani urais juu ya uwezo wake wa kulinda umoja wa kitaifa. Je ni kweli Zitto ni aina ya watu wanaoweza kulinda umoja wa Tanzania? Mimi nadhani Zitto hana uwezo wala hana nia ya kuulinda umoja wa Tanzania.


Migogoro ndani ya chama chake cha siasa imemhusisha Zitto kwa njia moja ama nyingine. Mgogoro wa mwanzo ulimhusu yeye na Mbowe. Na hapa hoja za kibaguzi za kikabila zilitumika ili Zitto aonewe huruma na kukubaliwa kugombea uenyekiti wa chama chake. Pia gazeti la Mwanahalisi lililofungiwa na serikali ya Kiwete liliwahi kuripoti kuwa Zitto alikuwa na mahusiano ya karibu na watu wa usalama wa Taifa.

Bahati mbaya sana ukaribu huu wa Zitto na TISS haukusaidia hoja za udini kutumika dhidi ya Slaa katika mchakato wa kumpata rais wa awamu ya nne. Zitto anashirikiana kwa karibu na usalama wa taifa ambao wamechochea au wanaacha hoja ya udini dhidi ya Slaa na chama chake cha siasa itumike kuwapatia CCM urais huku umoja wa kitaifa ukiwekwa hatarini.

Hapa, Zitto hana uhalali wa kufikiriwa kuwa rais kwa kigezo cha umoja wa kitaifa. Hivi karibuni, Zitto amenukuliwa na mmoja wa walioasi kundi la masalia kuwa alikuwa akiwapatia msaada katika harakati za kumtukana Slaa kwa njia ya vyombo mbalimbali vya habari. Ingawa Zitto aliruka na kusema hamjui mtu huyo. Mhusika alisisitiza kuwa anamfahamu na anawapatia msaada katika mradi wao wa kumtukana Slaa.

Kitabu kimoja cha imani kinaeleza kuwa mfuasi mmoja alimkana Bwana wake mara tatu japo alikuwa anamfahamu. Kwenye mradi huu wa masalia ya Zitto hoja za ukabila, udini na ukanda zimetumika kumtukana Slaa kama njia ya kumwonyesha kuwa hafai kufikiriwa kugombea urais mwaka 2015.


Tunataka kuanza ukarasa mpya, na tunaomba wapambe wa hawa wanaoutaka urais waache watu wao wajadiliwe. Na tunawataka hao wanaoutaka urais wasifanye juhudi za kufunika habari za upande wa pili zinazowahusu. Hatutaki kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Urais siyo mzaha, tumeshapata funzo mwaka 2005. Tuwajadili wanaoutaka urais na huu ni ukurasa wa Zitto.
 
nimesoma kwa shida lakini nimekuelewa
hao waliojitangaza mapema ni mbinu tu....
propaganda kwenye siasa ni kawaida ndo maana sisi wana wa nchi hii tunamtaka Dr. ambae hacheki na kima.
 
nimesoma kwa shida lakini nimekuelewa
hao waliojitangaza mapema ni mbinu tu....
propaganda kwenye siasa ni kawaida ndo maana sisi wana wa nchi hii tunamtaka Dr. ambae hacheki na kima.

Shida gani umeipata ili marekisho yafanyike?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom