Wanaoutaka urais 2015: Yupi anafaa?

Wazee wa hekima wako kimya kabisa. Nyie hangaikeni, mtajapigwa na bumbuazi.

Bora umewaambia ndugu yangu, watu wanafikiri kubwabwaja na waandishi wa habari ni Urais. Quote again ''Wazee wa hekina na busara wako kimya kabisa ndio watakaotoa Rais wetu 2015''.:flypig:
 
hata sisi wachaga hatujawai kutowa RAIS 2015 lazima rais awe mchaga kutuka rombo kama mambo yenyewe ndio hivyo
 
kunakijana aliyesoma UDOM mwasisi wa kikundi cha class struggle na aliyewahi kuwa waziri wa chakula na uwekezaji anaitwa Richard Mtui naona huyo anafaa kuwa rais wa Tanzania tumtafute tumuombe anatufaa.
 
Kwa hali inayoendelea hivi Tanzania inatia shaka bado miaka mitatu kufika uchaguzi mkuu wa uraisi na wabunge 2015, lakini kila kukicha mapya yanajitokeza kwa watu kutaganza nia ya watu kujitangazia kuwa na sifa za kuutaka uraisi, mmoja alisema anasubiri Mungu amuoteshe na kudhihirisha akasema ana maadui 11 ambao 2016 mara baada ya kuoteshwa watakibiria kenya, hiyo inaonyesha dhamira iliyojificha na ulipaji visasi, bado kuna magwinji mengine ambayo yalishaanza harakati zamani kama EL, SS, FS, ambao wanamitandao ndani ya chama chao cha chukua chako mapema.....

Kwa Dr. John Pombe Magufuli ninakupa asilimia bilioni mara bilioni Mungu yuko juu yako katika kusema ukweli na wala wewe siyo mnafiki Magufuli akipewa Nchi hii ataimudu kutokana na msimamo wake usioyumbishwa. Nilidhani namuona peke yangu kumbe tuko wengi Long live Dr. John Pombe Magufuli God bless you abudantly, Anayemchukia MAGUFULI AMELAANIWA NA NI MVUNJA SHERIA, KWANI MAGUFULI HANA USHIRIKA NA WAHALIFU, MPAKA UPINZANI WANAMKUBALI UTHIBITISHO HOTUBA YAKE BUNGENI
 
Hapo kwenye rangi ya Mabwepande, amekahidi amri ya mahakama kitendo kilichomsababishia Gamba mwenza kuwa na wakati mgumu kwenye kesi ya uchaguzi mdogo jimbo la Igunga kesi inayoendelea huko wilayani Nzega....

Hana muda wa kuhangaika na mtu aliyekwisha shindwa kabla hajaanza Dalai lama wa Igunga asubiri kupumzika kwa amani magufuli keshaona dalali haponi kwenye hiyo kesi kwani makosa ni zaid ya ahadi za Magufuli chezee Pombe wewe ehhhh, kapaona mapemaaa CHADEMA hatubahatishi
 
Kuna mtu mmoja maarufu aliwahi kusema na nakuu "watanzania wasitarajie mabadiliko yoyote kutoka kwa rais yeyote atakayetoka ccm", mwisho wa kunukuu na kuchangia.
 
Kuwa mkuu wa nchi kunataka ujaliwe mambo mengi ya Msingi, kuwa Dikteta peke yake hakutoshi kuwa sifa ya kuwa rais. Magufuli hana sifa ya kuwa rais kwa mazingira ya sasa ambayo watu wengi wanauelewa mkubwa wa mambo mbalimbali ya kiutendaji, Nenda hata jimboni kwake hakuna la maana alilofanya na sasa hata akigombea ubunge hawezi tena kushinda
 
kwa Dr Magufuli kuna vijineno viwili VITATU tu dhidi yake!
1.NYUMBA ZA SERIKALI akiwa Waziri wa Ujenzi awamu ya Pili
2.VISASI kuna mtu kaelezea viiiiiiiizuri hapo juu
3.Peter's PRINCIPLE:KUNA HATARI YA KUMPANDISHA MAGUFULI HADI TAIFA ZIMA LIKATAMBUA UBINAFSI,UBABE, UDHAIFU WAKE>ANAHITAJI KUONGOZWA PIA MAANA NI MPENDA SIFA-OPPORTUNIST!
 
Kwa hali inayoendelea hivi Tanzania inatia shaka bado miaka mitatu kufika uchaguzi mkuu wa uraisi na wabunge 2015, lakini kila kukicha mapya yanajitokeza kwa watu kutaganza nia ya watu kujitangazia kuwa na sifa za kuutaka uraisi, mmoja alisema anasubiri Mungu amuoteshe na kudhihirisha akasema ana maadui 11 ambao 2016 mara baada ya kuoteshwa watakibiria kenya, hiyo inaonyesha dhamira iliyojificha na ulipaji visasi, bado kuna magwinji mengine ambayo yalishaanza harakati zamani kama EL, SS, FS, ambao wanamitandao ndani ya chama chao cha chukua chako mapema.

Ukija kwa upande wa CDM nako mambo yameanza kupamba moto mara nina sifa za kuwa amri jeshi mkuu wa nchi ili hali hata familia hana , mara kiongozi mkuu wa chama anataka, mara mheshimiwa Dr. Slaa, vile vile inetokea wengine wanasema tangu uhuru hatujatoa raisi wakati tuna uwezo, mara tunataka mwislam.

Hizi sio ishara nzuri vile vile kiongozi ambaye nimzuri sio lazima ajipe sifa mwenyewe kuwa anaweza kusema hivyo vyote alivyokuwa anafanya ni unafiki , vile kiongozi kuweza kumpita na kusema ni mwadilifu na mzalendo lazima awe amefanya kazi na kudhibitisha hilo bila shaka na sio kuongea na kukosoa tu, mfano bunge lililopita kilango, mwakembe, ole sendeka, sita tulifikiri ni wazalendo wanatetea watanzania lakini leo hii sio, vile vile zito kasi yake sio ile.

kwa hali hiyo tusidanganyike na porojo za kuwa naweza ili hali ni njaa tu. Kwa hali tuliyonayo na kuangalia ukomavu wa siasa Dr. Magufuli anafaa kuwa raisi ila sio kupitia CCM. Anasifa na amedhihilisha kwa kuwa na misimamo akiwa serikalini , sio mdini, mkanda wala mjenga mitandao.
me naona magufuli anafaa kua prime minister..
 
asante sana kaka Ezra kwa kuweka mambo bayana, mi mwenyewe natokea B.mulo najua fika chuki za magufuli zilipotufikisha wana Biharamulo.

Wilaya inadorora kila siku, miradi ya barabara inajengwa bila kuisha mara utaskia wakandalasi wamesimamishwa. Huyu mtu hafai kuwa raisi hata kidogo maana ni mbinafsi sijapata kuona. NASKIA KAMA ALIVYOPINDISHA CHATO KUWA WILAYA ALITAKA KUFANYA MAKAO MAKUU YA MKOA WA GEITA KUWA CHATO LOH?.

Wanabiharamulo tunapata shida na adha za usafiri kwa sababu ya chuki na visasi vyake. Aendee kuwa waziri lakini urais haumfai mbabe huyo.
 
washabiki na wapenzi wa Simba Sports Club
wamesusia kufturu Chapati zinazotengenezwa na
kiwanda cha Azam.
Hii inatokana na kipigo cha Gombania Daku
walichokipata hivi karibuni
 
Labda urekebishe toka mwanzo kauli yako. Dr. wa ukweli Slaa hajatangaza nia wala kamanda anga Mbowe iweje uwachanganye kati ya waliotangaza nia? kuwa wazi kwamba unampendekeza mchapakazi muoga Magufuli! kwa taarifa yenu mimi simpendekezi yeyote lakini kiongozi mjuu wa nchi lazima awe na ellement kidogo za udicteta. angalia Kagame na maendeleo ya Rwanda kwa muda mfupi hata baada ya vita ya ukabila!
 
I will vote for mabwepande kama dr magufuli atapitishwa kuwa mgombea urais
 
Anybody can be a President, lakini ki ukweli impact ya utawala sio nani ni Rais bali huyo Rais anakuja kusimamia Mfumo gani? Nchi ikishakuwa na mfumo m baya wa utawala hata Rais awe nani, hakuna lolote atakaloweza kufanya. lazima Mfumo Ujengwe kwanza ndipo watu wagombee kuuongoza huo Mfumo. Mfumo ambao hakuna Rais atakaeubadilisha vile anavyojisikia tu bali kuutumia huo mfumo Kusukuma mbele maendelo na Nguvu ya Nchi duniani.
 
ninichojua kiongozi mzuri hapimwi kwa uwezo wake wa kujenga hoja majukwaani...ule utaratibu wa zamani wa usalama wa taifa kufuatilia nyendo za vijana tangu wakiwa mashuleni sijui uliishia wapi?? zamani ilikua ukionekana una mashiko kwa jamii kulikua na watu wana trace background yako toka kijijini kwenu , familia yako, umesoma wapi na mambo kama hayo NDIO KILIKUA KIPIMO KIZURI CHA UONGOZI




Ndiyo niliyokuwa namwambia kijana wangu Zitto haya.
 
Back
Top Bottom