Wanaotumia dawa za kukuza matiti,****** hatarini kupata saratani

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Wana JF, My wife wangu ni kama amewahi kutumia hizi cream, sasa sijui kama kuna solution kabla mambo hayajaanza kwenda Kombo! Naomba msaada wenu wadau.

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imewatahadharisha wanawake wanaotumia vipodozi vya kuongeza makalio na matiti kwamba wanaweza kupata madhara ya figo, ubongo na kansa ya ngozi.

Mkaguzi wa dawa vipodozi na vifaa vya tiba wa TFDA Kissa Mwamwita alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wanawake wanaotumia vipodozi hivyo ambavyo havijasajiliwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mwamwita alisema vipodozi hivyo vimekuwa vikiingizwa nchini na kuuzwa kwa kificho huku ikidaiwa kuwa wateja wake wakubwa ni wanafunzi wa sekondari na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Mwamwita aliwataka wanawake wanaotumia vipodozi kuwa makini wakati wanaponunua vipodozi kwa kuangalia kama vimesajiliwa kwani vipo vipodozi vinavyouzwa kwa kificho.

“Matumizi ya vipodozi hivyo vinavyoongeza ukubwa wa makalio na matiti ni hatari kwa afya na pia yanawaweka katika hatari ya kupata magonjwa ya saratani,” alisema Mwamwita.

Alisema watumiaji wa vipodozi wanatakiwa kuwa makini wanapotaka kununua bidhaa hizo ili kuepuka kununua vipodozi vyenye viambata vya sumu.

Hata hivyo TFDA imetoa tahadhari kwa wananchi wanaoendelea kutumia vipodozi vyenye viambata vya sumu zikiwemo ‘losheni’ kuacha kutumia kwa kuwa kiafya vina madhara makubwa.
Mwamwita alitaja baadhi ya vipodozi vyenye viambata kuwa ni Chloqinone,Chloroform na Mercury Compound.

Source: Mwananchi 02 Julai 2009
 
mhhhhhhh imeanza ya saluni za kunyoa sehemu nyeti,matattoo,dawa za kuboost makalio na tits...mhh na kuna ya kurudisha bikira.....watz kazi 2nayo.......2nabeba kila kitu......
 
Si matiti na makalio tu hata miguu wanaishepu kutegemea na size unayotaka. Nasikia hiyo sehemu ni balaa! Wauzaji virutubisho hivyo wanauza kwa usiri mkubwa sana wasikamatwe! Biashara inaanza saa kumi na moja alfajiri hadi 12.30, baada ya hapo huwapati ng'o!! Ila foreni ni kubwa balaa, akina dada wanapishana kama ilivyokuwa wamama wa MEWATA!
 
Kazi ipo, ni Mambo ya Urembo tu hayo, Mtu aridhiki na jinsi alivyo umbwa na Mwenyezi Mungu!!!
 
Lisemwlo lipo tuombe mwenyazi MUNGU atunusuru na majanga yote hasa sisi watz tunaopenda kuiga.
Our lives begin to end the day we become silent about things that matter! Martin! Luther King, Jr.
 
mhhhhhhh imeanza ya saluni za kunyoa sehemu nyeti,matattoo,dawa za kuboost makalio na tits...mhh na kuna ya kurudisha bikira.....watz kazi 2nayo.......2nabeba kila kitu......
Mpwa hiyo dawa ipo na inapatikana wa bei poa sana .teh teh teh
 
Last edited:
Si matiti na makalio tu hata miguu wanaishepu kutegemea na size unayotaka. Nasikia hiyo sehemu ni balaa! Wauzaji virutubisho hivyo wanauza kwa usiri mkubwa sana wasikamatwe! Biashara inaanza saa kumi na moja alfajiri hadi 12.30, baada ya hapo huwapati ng'o!! Ila foreni ni kubwa balaa, akina dada wanapishana kama ilivyokuwa wamama wa MEWATA!

We unafurahisha kweli, wala hauziuzwi kwa kificho, vibanda vyote vinavyo uza urembo zimejaa, nenda Mwenge pale kila kibanda wanauza hizo lotion, na wanazitangaza wazi wazi bila kificho!

Sema kama kawida serikali yetu/mamlka husika mpaka mambo yaharibike ndo utasikia kamata kamata.
 
Lakini hii ni reflection ya demand curve, inaonekana demand ya makalio makubwa na maziwa makubwa sijui wanaita boobs watoto wa siku hizi ni kubwa, na ni sisi wanaume ndo tunaisababisha,, sasa hili swala la monalisa slimming belt litakuwaje?

on a serious note, kwa nini mtu asiridhike alivoumbwa hadi afanye modification? kila mtu mwanamke anataka kuonyesha cleavage....tutafika?
 
Si matiti na makalio tu hata miguu wanaishepu kutegemea na size unayotaka. Nasikia hiyo sehemu ni balaa! Wauzaji virutubisho hivyo wanauza kwa usiri mkubwa sana wasikamatwe! Biashara inaanza saa kumi na moja alfajiri hadi 12.30, baada ya hapo huwapati ng'o!! Ila foreni ni kubwa balaa, akina dada wanapishana kama ilivyokuwa wamama wa MEWATA!

Mbona haya mambo yapo wazi kabisa ukienda kwenye maduka ya vipodozi unazikuta bust firming cream, sabuni na cream za kupunguza uke na hata kwenye magazeti yale matangazo mafupi mafupi yamejaa tele. soma hizo ingredients sasa kama mtu ni muelewa sidhani kama angeweka hata dukani kwake. Mtu anajimaliza mwenyewe polepole.
 
Back
Top Bottom