Wanaotuhubiria juu ya demokrasia ni wanafik na wanatucheleweshea maendeleo

Endeleeni na ngonjera za demokras ila Ikulu mtaendelea kuisikia to.
Kwa style hiyo ya kidikteta uchwara staki hata kuhusishwa na yeyote mwenye kuelekea ikulu kidikteta uchwara namna hiyo,

fanya yote mazuri yenye maendeleo huku ukiwapa wananchi matumaini ya maisha yao salama na huru kabisa.
Lakini kinyume chake hapana maana hata mabepari na madikteta ya wakati wa utumwa Africa yalileta maendeleo pia tena sehemu nyingine mpaka leo maendeleo yao yanaonekana , sasa vipi tuwarudishe mabepari waendelee kutatawala kisa tunataka kuendelea?

Nasema hapana No. Fanya mazuri yenye neema kwa wananchi na watu wote, pia watu hao wape uhuru wao bila kunyanganya hata punje ya uhuru wa kujieleza kifkra kukutana na kufanya siasa sawa kwa wote vinginevyo wewe dikteta uchwara tuu.

Tusisahau enzi ya kuminya maoni na uhuru wa watu kisa tunafanya maendeleo imepita karne nyingi tu.
 
Hivi kuna faida gani kupiga soga wakat hatuna hospitali, unabwata na matusi juu alaf watu wanakufa njaa, watu hawana barabara na ulinzi wao na mali walizochuma huku mkiruhusiwa kumtusi hata Rais wenu kwa mgongo wa semokrasia, to me demokrasia ni pale watu wanakua na ulinzi wao na mali, hospital zipo ma madawa, shule, hali ya maisha iwe nzuri, barabara na miundombinu mingine iwe sawia, lkn kama tunabwabwaja tuu na mwisho hata mhugo unapiga chenga hapo danganya toto ya mzungu atukwibieeee mpaka tukate roho
 
kwa mtazamo wako enery unasupport udikteta(whichever way you wanna phrase).Ukiamini hata hapa tunaye.Sasa suala la kujiuliza.mbona mtu huyo akiitwa dikteta,watu hukamatwa na kufunguliwa mashtaka,yakiwemo ya uchochezi na kumtukana mkulu?
 
Mungu ni mwema leo nimekuta uzi nnlioshi nao ktk fikra, unajua wengi wetu hatujui maana halisi ya neno democracy tena democracy haswa lazma iendanene na local settings, hata waandishi wakubwa kama akina Samwel Hutington ambao ndio mababa wa dekrasia walishaasema ili Afrika iendelee lazma tuwe na model yetu ya demokrasia(African democracy) na sio demokrasi iliyoingizwa kama kitumbua kutoka Ulaya tena iliyotengenezwa kwa kwa setting za hukooo..na hata hao wazungu demokrasia yao imekuja baada ya mapinduzi ya kijani(Green Revolution) na baadae Mapinduzi ya Viwanda(Industrial Revolution) ikajumuishwa na Ukomavu wa Taasisi, sasa sie Afrika tumekabwa koo na wazungu na kulazimishwa twende nayo bila kuzingatia hayo mambo makuu matatu..Kama dikteta ni kwa maendeleo na afanye popote Afrika maana hili dudu limetukwamisha na ndio chanzo cha mabalaa mengi na machafuko huku kwetu
Mkuu asante sina la kuongezea hapo kabisa, natumain utaendelea kuwaelewesha hawa watu wasioelewa.
 
Machadema ndio wanahubiri democrasia wakati ndani ya chama chao hamna hata tone la democrasia!!

Miaka yote mwenyekiti ni Mbowe huyohuyo.

Shame on them
 
Nimependa hii ya korea kusini " Despite many criticism about his style of rule, there is no doubt that South Korea would bfe a very different nation without him"

Watanzania hawataki haya wanataka Democrasia ya Marekani na mijadala ya CNN,
Hiyo ikifanyika wao ndiyo wanaridhika. Wanadhani Marekani na mataifa ya Ulaya yaliendelea tu kwa kupiga soga bungeni na kisiasa.
Watanzania sijui nani katuroga sisi.

Hebu tuanze na nchi ambazo zimepiga maendeleo makubwa ambapo kuna nyakati udikteta ilibidi uingie:

1. China- tokea mwaka 1949 hadi leo ni nchi ya chama kimoja lakini tumona hali yao ya kiuchumi. Huku kulikuwa na ubabe kweli kweli lakini leo ni matajiri kuliko nchi ambazo wanasema wanafuata demokrasia.

2. South Korea- Utawala wa kijeshi toka 1961 hadi 79 lakini ona hali yao ya uchumi leo. Hawa walimfunga hadi raisi wao waliyempindua na hata kupeleka majeshi Vietnam ulitumika ubabe, wengi walipinga.

3. Malaysia- Mahathir Mohamad alitawala kwa zaidi ya miaka 22 tokea mwaka 1981 hadi 2003, tofauti kabisa na demokrasia ya wazungu. Leo Malaysia ni nchi kubwa ya viwanda na uchumi wao unazidi kukua.

4. Urusi- Utawala wa kikomunisti tokea mwaka 1925 hadi 1991 ndiyo umeifanya urusi kuwa na viwanda vikubwa hadi leo. Jehuri yote ya Putin imejengwa na vizazi vilivyopita ambavyo walikuwa madikteta.

5. Ujerumani- Tangu mwaka 1871 hadi 1945 utawala wa Kijerumani umekuwa wa kijeshi na kifalme. Lakini hata wakina Willy Brandit walikuta teknolojia kubwa sana imeachwa na dikteta Hitler pamoja na wanazi wenzake.

6. U.S.A- Baada ya kupata mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 1929-1933 Roosevelt alipewa madaraka makubwa ambayo hata George Washington hajawahi kupewa tangu nchi iundwe. Republicans wakaanza kumuita raisi mfalme (Imperial President) na makakama kuu ya Marekani ilipinga sheria nyingi sana za NEW DEAL hasa mwaka 1936.
Huyu huyu mwandemokrasia akapitisha sheria mwaka 1937 iliyompa nguvu kuchagua majaji kumi na tano wa Supreme Court of America. Hawa ndiyo waliomsaidia kupitisha sheria nyingi za kibabe hata kama mahakama za chini zitapinga, hii inaitwa COURT PACKING. Huyu jamaa alitawala awamu tatu kinyume kabisa na katiba ya Marekani na sidhani kama kuna raisi ataweza tena kufanya hivyo.
Huyu dikteta Roosevelt ndiye amelifanya taifa la Marekani kuwa kubwa hapa duniani, na liwakataze wengine wasijaribu kuiga wao walivyofanya.
enery kwa tuliotoa ukungu kidogo kwenye shule tunakubaliana na wewe kwa 100%. Kipindi nikiwa ulaya nikisomo na moja ya professor wangu wa mambo ya theory za ethics na maendeleo aliwahi kutuonesha model fulani ikidai kuwa huwezi kuendelea bila demokrasia, ila tulipojadiliana naye alikiri theory za maendeleo za kiulaya haziwezi kufanya kazi nchi kama afrika au asia. Ila wazungu ni wanafiki sana, hizo habari za demokrasia ni za wajukuu ndiyo walikuja kuzileta baada ya babu zao kuwa wameishi kwenye udikiteta na kuendelea wajukuu eti ndiyo wakaanza kujiuliza kwanini wameendelea, wakaanza kufanya angalia nyuma, wakati huo walikuwa wameshaimarisha demokrasia, wakadhani hata babu zao walikuwa na demokrasia, kumbe wapi! Mfano nchi kama ujerumani walichoma wachawi moto (kuna siku walichoma hadi wachawi 300). Hitler wajerumani wanampenda sana (nina jamaa zangu wajerumani), na wanamkubali kuwa alichangia sana wao kuendelea, lakini leo wanasema eti afrika bila demokrasia haiwezi kuendelea! Ethiopia wanasifiwa kila siku ila ukijua kabila la oromo (ambao ndiyo wengi kwa kabila) wanapinga hayo maendeleo kila kukicha
 
Back
Top Bottom