Wanaotaka serikali 3 zamuungano,wanatupeleka kuzimu; Mkuchika

Muungano unaupungufu kisheria hilo liko waz,na uwepo wa serikali ngapi sio suluhisho bali mgawanyo wa utawala unauzingatia usawa wa kisheria ndo kilio kikubwa...wote tunalengo moja sema njia ndo tofauti.
 
Hoja alizotoa Lissu ni nyingi za msingi ambazo zinahitaji umakini ya siyo kukurupuka wala ushabiki wa kisiasa. Inawezekana kuwa serikali mbili ndiyo mfumo mwafaka lakini iwekwe wazi kwa nini mfumo huo unakuwa bora kuliko mingine? hiyo ndiyo inatakiwa kutolewa ufafanuzi ili kuepuka migogoro isiyoisha. Kuongea tu kuwa serikali mbili ni nzuri haitoshi bila kufafanua vyema. Serikali hivi sasa inatumia gharama kubwa sana kujadili masuala ya muungano kwa kamati zisiszoisha, jambo ambalo linafanya uwe kama mradi wa baadhi ya watu bila kuwa na majibu na muafaka.
 
Hao wanaodai na kutaka serikali mbili hivi hamuwaelewi ni watu wepi ???

Hao kwa taarifa rasmi ni wale ambao hivyo vyeo wanavyoringia vitatoweka ,wabunge watapoteza ubunge na mawazi na na na wote watakwenda na maji pindipo Muungano ukibomoka kama inavyotarajiwa na wengi.

Sitegemei yeyote yule kutoka CCM haswa hao walio bungeni kusema kuwa wanataka serikali tatu ,hao wanaosema mbili ambao ni wabunge kutokea zanzibar ukiwambia moja basi pia wataruka .

Serikali tatu ni kifo cha CCM na uwongozi wake serikalini ,lakini ndio jahazi linazama ,WaZanzibari haoooo !!!
 
Bungeni LIVE,

Mkuchika amesema serikali 2 ndio muundo bora kabisa, pia akasisitiza wanaotaka serikali 3 wanatupeleka kuzimu. Naona serikali sikivu wameweka msimamo wa serikali 2 rasmi na inatisha.

Che Guevara. Point of correction: aliyetoa kauli hiyo si Mkuchika ni Chiligati. Mimi niliipenda kauli ya Mch. Msigwa kuhusu hifadhi ya Mazingira "HATUWEZI KUENDELEA KUVUMILIA KUONGOZWA NA SERIKALI INAYOTUPELEKA JANGWANI"
 
Che Guevara. Point of correction: aliyetoa kauli hiyo si Mkuchika ni Chiligati. Mimi niliipenda kauli ya Mch. Msigwa kuhusu hifadhi ya Mazingira "HATUWEZI KUENDELEA KUVUMILIA KUONGOZWA NA SERIKALI INAYOTUPELEKA JANGWANI"

Mkuu ni kweli, naona nimeboreka sana leo na hili bunge.
 
Wange comment tusubiri mapendekezo ya katiba mpya! Cyo hivy
Hiyo hoja mimi nina tatizo nayo kidogo. Kama kila mjadala wa Muungano inabidi tusubiri mapendekezo ya Katiba mpya, Waziri wa Muungano amesimama bungeni kufanya nini?

Wizara ya Muungano kwa nini isiwe dissolved na waziri afutwe mpaka baada ya Katiba mpya ili wote tusubiri kupeleka mapendekezo kwenye Tume na kuokoa matumizi ya hii wizara kwa sasa?
 
Mwanasheria mkuu; Lissu ni mpotoshaji, anashauri lissu asome maandiko ya prof.Kabudi, Mwakyembe na wengineo sio prof.Shivji pekee. Anasisitiza ni sahihi znz kutamka neno nchi katika katiba ya zanzibar, kwa kuwa ili muungano upatikane, lazima nchi ziwepo.

kwenye red: Sasa kwanini Tanganyika nao wasiwe na katiba yao?

Wakati fujo za UAMSHO zilipoteka Zanzibar, Waziri wa mambo ya ndani Dr Chimbi alienda Zanzibar akifuatana na balozi wa Marekani na yule wa Norway. Sasa pengine tujue, wakubwa wanautetea huu muungano ubaki kama ulivyo kwa maelekezo ya wafadhili wao (Marekani na Norwary na wengine) au ni kwa matakwa ya nani?

Zanzibar wamekinai muungano, Tanganyika wamekinai muungano, kwanini wao CCM wanaziba masikio?
 
Back
Top Bottom