Wanaotaka Muungano Uvunjike watoke kwanza Bungeni na BLW

Koti likibana unalivua!.. kweli maneno haya lakini utavaa koti jingine. Je, koti jingine ni lipi!
Huwezi kurekebisha koti au kununua jingine ikiwa wewe mwenyewe una tamaa na ulafi wa kula..Ni ushauri mzuri wa madaktari (wataalam) ujitazame wewe mwenyewe afya yako na sio size ya koti....
 
Mkandara, haya ndiyo nilikuwa nasema; sasa huyo Mbunge kweli kabisa ameapa kuwa atakuwa "mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" halafu anapewa jukwaa la kuzungumzia kuivunja Jamhuri hiyo na watu hawaoni tatizo?. It boggles my mind.
 
Njia iliotumika ni tofauti sana na kile ulichopendekeza huko juu Mkuu.
Muungano umekosa uhalali wa kisiasa na kikatiba.
Wakati wa kuunganishwa nchi mbili huru hizi hakuna kura ya maoni iliopigwa kuulizwa iwapo tunaridhia au la.
Sasa tupige kura ya nini tukitaka kurudi katika hali yu kama zamani?
Mkuu "muungano" huu ni bomu, uvunjie tu.
Fafanua uhalalai upi wa kikatiba ba kisiasa, kauli yako ina hang!

Si nchi zote zilizoungana zilikuwa na kura ya maoni (kwahiyo hiyo si formula) mfano mzuri ni Canada. Quebec walipolilia kujitenga iliitishwa kura ya maoni(miaka 1980 na P.Trudeau) majority wakakataa. Hata baada ya hapo kukawa na separatist wanaojiita Block Quebecoir ambao walikuwa na hoja kama za Wzbar. Uchaguzi uliokwisha wananchi wa Quebec wamewaona wapuuzi kwa madai ya kijinga ili hali wanaofaidika ni wao. Katika viti 50 wamepata 3 tu na suala la kujitenga limefia mbali. Halikuwa na maslahi ya watu bali kikundi cha walafi fulani.

Kuna wakati watu wanadhani Wzbar hawataki muungano, ukweli ni kuwa ni kikundi cha watu wachache wenye kelele sana na waroho. Kama Wzbar hawataki muungano tusingewaona malaki wakifanya biashara na ajira za bara. Tusingeona wanajenga majumba bara ili hali nyoyo zao hazipataki. Huwezi ku invest mahali usipopataka! kwanini hawakwenda Malindi, Ngazija, Comoro au Somalia! tena huko wapo wa nywele zao.

Unaposema muungano ni bomu uvunjike, ni afadhali usingesema. Tulitarajia utuambie uvunjike kwa taratibu zipi!
Southern Sudan wamejitega lakini kuna utaratibu bado unafuatwa kuhakikisha maslahi ya wananchi yanalindwa.
Tukisema vunja tu asubuhi moja kama unavyoshauri, watakaoumia ni Wbar maana Mtanganyika ana nini cha kupoteza!!!!

Toa na Jenga hoja na ufafanue ukizingatia mada iliyopo mbele bila kuvuruga mtiririko wa mjadala.
 
Mwanakijiji kwa mtazamo wako

  • issues ya Mzee malechela PM akiwa kipindi kile kurushu Hoja ya muungano ya wale G52 kama sikosei ujadiliwa bungeni ( kina njelu kasaka)
Nadahni wale jama nao agenda yao ilikuwa serikali tatu . Vipi unalichukuliaje hilo ?
 
Swala la serikali tatu halivunji Muungano ni sawa na kufanya marekebisho ktk katiba.
Labda ktk mapana ya sheria na uzalendo swala la kutaka kuuvunja muungano linafanana sana na swala la kuunda katiba mpya ambayo kama mbunge uliapa siku ya kwanza kwamba utailinda. Sasa unapokuja na kutaka katiba mpya au Muungano unakuwa umekiuka kiapo chako mwenyewe kwani kama kweli hawa wabunge wameingia bungeni kutoilinda katiba au Muungano wasichukua kiapo..

Nadhani hii ndio maana ya Mwanakijiji.... lakini pamoja na yote haya nadhani utaratibu wa mbunge kuleta hoja ya katiba au Muungano ni lazima iwe ktk maudhui yasiyokiuka ethics - Principle
 
hapa kwa kweli mwanakijiji mtoa mada kwa asilimia zote siyo mweledi wa mambo haya ya siasa wa katiba. hivyo mimi sioni unachokiongea kabisa au mantiki ya unachokiongea. kila kitu ni kiapo hivi unajua maana yake. hivi kula kiapo ndo maana yake hutakiwi kuhoji kitu chochote kwa yaliyoandikwa ndani ya katibu huo ni wehu sasa wabunge watajadili nini. ikiwa katiba yenyewe inatoa fursa hata ya kuijadili na kuibadilisha mahitaji yakitoikea na imeshatokea hivyo zaidi ya mara tatu kwa nini iwe ajabu kujadili kijisehemu tu cha katiba hiyo. tatizo nadani ni muungano kwa sababu mbona tumesikia mambo mengi tu yakijadiliwa wakati katiba illishaeleza na yanabadilishwa iweje kuhoji muungano. huo ni unyerere tu ila angalau ya mwl akichanganya na elimu kidogo ila yako ww mwanakijiji ni siasa tupu.
sitta siye mungu naye ni mkosefu tu kama ulivyo wewe. haya mambo yanahitaji busara kuliko jazba kama uliyonayo pamoja na kuwa ni mtazamo wako kama huo wa wabunge unawakemea kwa kisingizio cha katiba.
 
Nadhani hii ndio maana ya Mwanakijiji.... lakini pamoja na yote haya nadhani utaratibu wa mbunge kuleta hoja ya katiba au Muungano ni lazima iwe ktk maudhui yasiyokiuka ethics - Principle
Excellent!
Tumekaa pamoja kwa miaka 50. Bila kujali uhalali au uharamu wa muungano kuna vitu vinaitwa Intermmariage,Cultural mingling, investment and dependence in government level. Ni kwa msingi huo lazima uwepo utaratibu wenye nidhamu katika kufikia suluhisho.

Kinachojitokeza ni watu kutaka kukiuka taratibu kwa nia ya kuchochea. Tanganyika kama Wzbar wamechoshwa na malalamiko dhidi yao.
Taratibu zinaruhusu hoja zijadiliwe, lakini utaratibu wa kuamka na kusema tuvunje muungano tena kwa yule yule aliyekubali sera za chama chake na katiba chini ya kiapo ni aina ya 'uasi'. Kwani kuna ugumu gani kufuata taratibu kufikia hitimisho?

Suala la serikali 3 kwa sasa ni ndoto. Kwa umimi wa Wzbar, Wabara nao wamejifunza. Swali ni je hizo serikali tatu zinagharamiwa vipi na zinafanyaje kazi? Nini role ya serikali ya shirikisho na rais wake hasa ukizingatia ubinafsi uliotawala.

Waswahili wanasema, mwiba hutoka mahali ulipoingilia, kwanini tutake kutoa mwiba jichoni tukijua uliingia mguuni!
 
Mwanakijiji kwa mtazamo wako

  • issues ya Mzee malechela PM akiwa kipindi kile kurushu Hoja ya muungano ya wale G52 kama sikosei ujadiliwa bungeni ( kina njelu kasaka)
Nadahni wale jama nao agenda yao ilikuwa serikali tatu . Vipi unalichukuliaje hilo ?

Naomba upitie kijitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania - kipo hapa. Nashukuru kuwaona siku hizi kina Sitta na wenzie wameanza kureason kwa namna ile ile ya Nyerere. Ninachokisema hapa ndicho Nyerere pia alikisema. Sera ya CCM ni serikali mbili, wabunge wake 55 hawakuwa na mandate ya kuja na serikali tatu. Aliwaambia wakitaka kwenda serikali tatu, lazima kwanza wabadilishe sera ya serikali mbili.
 
Kinachojitokeza ni watu kutaka kukiuka taratibu kwa nia ya kuchochea. Tanganyika kama Wzbar wamechoshwa na malalamiko dhidi yao.
Taratibu zinaruhusu hoja zijadiliwe, lakini utaratibu wa kuamka na kusema tuvunje muungano tena kwa yule yule aliyekubali sera za chama chake na katiba chini ya kiapo ni aina ya 'uasi'. Kwani kuna ugumu gani kufuata taratibu kufikia hitimisho?

Well, hawa walioapa kuilinda Katiba wanajua hiyo Katiba inasema nini ili kuwez akuuvunja Muungano. Katiba inasema hivi:

(Imetajwa katika ibara 98 (1) (b))
Mambo ambayo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na
theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi
mbili
ya Wabunge wote kutoka Tanzania Visiwani.
1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.
2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
4. Kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.
6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.
7. Orodha ya Mambo ya Muungano.
8. Idadi ya Wabunge kutoka Zanzibar

Utaona kuwa kuvunja Muungano siyo kazi hivyo. Kama kweli kuna watu wanataka Muungano uvunjwe, hawahitaji kumuuliza Waziri Mkuu au hata Rais, threshold imewekwa chini kweli, haiitajiki hata referendum! BlW na BJMT wanaweza kukubaliana hata kesho na kuazimia Muungano usiwepo na Muuingano unafutika. Ni namba hiyo hiyo ilitumika kuuleta. BlW la Zanzibar lilipiga kura theluthi mbili kuridhia Muungano, na Bunge la Tanganyika likafanya hivyo hivyo (April 22, 1964) na siku nne to baadaye Muungano ukawepo. Hata leo, wakitaka kuvunja tunauvunja tu bila haja ya referendum kwama wenginwanavyotaka. Kama wawakilishi wa watu wanasema tuvunje na theluthi mbili za kila upande wa Muungano zikakubaliana - na ninaamini Zanzibar watatakiwa waanze - basi Muungano kwishnei. Of course watahitaji kushughulikia mambo yoteeee mengine ndipo watajua gharama ya kuvunja Muungano itakuwaje.
 
Well, hawa walioapa kuilinda Katiba wanajua hiyo Katiba inasema nini ili kuwez akuuvunja Muungano. Katiba inasema hivi:

Utaona kuwa kuvunja Muungano siyo kazi hivyo. Kama kweli kuna watu wanataka Muungano uvunjwe, hawahitaji kumuuliza Waziri Mkuu au hata Rais, threshold imewekwa chini kweli, haiitajiki hata referendum! BlW na BJMT wanaweza kukubaliana hata kesho na kuazimia Muungano usiwepo na Muuingano unafutika. Ni namba hiyo hiyo ilitumika kuuleta. BlW la Zanzibar lilipiga kura theluthi mbili kuridhia Muungano, na Bunge la Tanganyika likafanya hivyo hivyo (April 22, 1964) na siku nne to baadaye Muungano ukawepo. Hata leo, wakitaka kuvunja tunauvunja tu bila haja ya referendum kwama wenginwanavyotaka. Kama wawakilishi wa watu wanasema tuvunje na theluthi mbili za kila upande wa Muungano zikakubaliana - na ninaamini Zanzibar watatakiwa waanze - basi Muungano kwishnei. Of course watahitaji kushughulikia mambo yoteeee mengine ndipo watajua gharama ya kuvunja Muungano itakuwaje.

Ala! Kumbe Kuvunja Muungano kunawezekana Kikatiba!, sasa kumbe tunajadiliana nini hapa!
Kumbe wale wabunge wanaosimama Bungeni na Kutaka Muungano Uvunjike bado wako ndani ya msitari wa kisheria kwa sababu Katiba imetoa nafasi ya kufanya hivyo, ilimradi tu theluthi mbili ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri na Theluthi mbili ya Wawakilishi wawe wameridhia!.

Kumbe wabunge hao "walioapa kuilinda Jamhuri ya Muungano" bado wanaweza kushiriki katika mchakato/kura za kuuvunja huo muungano.
mimi hapo awali nilidhani kwamba mjadala wa kuwepo au kutokuwepo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni off-limit.

Maadamu katiba imeruhusu uwezekano wa kuuvunja huo Muungano tuwaache Wabunge wetu walete maoni ya wananchi bungeni kuhusiana na suala hilo, na ikibidi walete hoja binafsi ya kuwezekana kuupigia kura Muungano.
 
Naomba upitie kijitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania - kipo hapa. Nashukuru kuwaona siku hizi kina Sitta na wenzie wameanza kureason kwa namna ile ile ya Nyerere. Ninachokisema hapa ndicho Nyerere pia alikisema. Sera ya CCM ni serikali mbili, wabunge wake 55 hawakuwa na mandate ya kuja na serikali tatu. Aliwaambia wakitaka kwenda serikali tatu, lazima kwanza wabadilishe sera ya serikali mbili.

lakini nadhani hapa ndio tunataiwa natakiwa tufumbue macho zaidi na zaidi macho kuwe na uwiano nguvu ya vyaama visiue demokrasia na mawazo mbadala.

Mfano Chama XYZ kinaweka kuwa prority kwenye sekta ya Kilimo au ya ufugaji au madini. Lakini vipi mbunge GGG kama yeye jimbo lake rasilimari nauchumi m kubwa iliyopo jimboni kwake ni misituti na asali.

  • Je mbunge huyu GGG hatakiwi kupinga au kuomba mtazam wake ufikiriwe kwa manufaa ya wananchi wa jimbo lake kwa sbabau tu sera ya chama chake haijataja vipaumbele kwa rasiliali za jimboni mwake.
Sasa hapa nakuja na hoja/swali lingine. Kwa faida na afya ya demokrasia nini inatakiwa uwa mipaka ya hoja za mbunge Vs Chama.??? Sababu wabunge wakisema serikali tatu hawamaaishi uvnja muungano.

Maana wenzetu huko naona sometme waunge wa democta wanaubali hoja za Republican na Vice versa kulngana na hoja ina maslahi gani kwa jimbo lake.
 
My apolgy for intejection. Based on the remarks made by minister in BLW, I find them aligning well with the topic in discussion.
Zanzibar minister says 2-government structure `outdated`
By The guardian reporter
15th July 2011
Comments :Zanzibar Minister for Agriculture and Tourism Mansoor Yussuf Himid said yesterday that the two-government arrangement in the Union between Zanzibar and Tanganyika "is outdated."
He told the House of Representatives here that an ideal arrangement was that of three governments – the union, Zanzibar and Tanganyika government.
Himid cautioned against using forums for discussing the union to threaten people, especially Zanzibaris, airing their views freely on the best form of the Union between the two countries.
He said it was surprising to see some leaders in the National Assembly repeatedly maintained that oil resource didn't belong to Zanzibar on grounds that the deposits were located in the ocean border between Tanga and Zanzibar.
"I don't want to disclose their names…they are trying to threaten the people," he said.
He elaborated that the three government arrangement was the best approach for the two countries, which formed the United Republic of Tanzania way back in 1964, "to free Zanzibaris from uncalled for threats."
"We are supposed to educate Zanzibaris on how to discuss about the Union," said Mansoor, who is also member of the powerful ruling CCM national executive committee.
Mansoor added that Zanzibaris should not fear stating openly that they need a system that would free them from ongoing debates.
He said the decision by the House to demand removal of oil and natural gas from the list of union matters few years ago was still valid and should be accepted."Honourable Speaker, I won't accept the issue of natural gas and oil remaining on the list of union matters," stressed MansoorZanzibar Minister for Lands, Housing, Water and Energy Juma Shamuhuna encouraged the people in the Isles to push ahead with one voice the decision to strike off the list of union matters both oil and gas.
My Take: On perspective of the on going discussion in JF, it is apparent that Hon.Mansoor wants to confuse the public by echoing the words from different forums which he condemns ab initio.
Mansoor as a minister is ruling out the 1 or 2 government systems.His best choice is 3 government system which many Zanzibaris are demanding being in Mzalendo.net, JF etc.Very unfortunate hon. Mansoor did not go further to elaborate how the system is going to work.

Deliberately he doesn't answer the following questions the likes of many Zbaris.
1. What will be the role and responsibilities of the union government
2. Who is going to meet the running cost of union government
3 what could be the matters in the union government which have mutual interest and benefits
4. How much Zbar is contributing to run the current government

Secondly, it seems as if oil is driving Zanzibar nut! If at all there is oil it belongs to them.
I wonder if this union was formed on the pillar of oil as hon. Mansoor would like the world to understand. Sad!

Hon. is urguing the people to stress on the need of stripping off some matters not included in the article of union. Well ,it sound good! however he should remind Zbaris that higher education was incorporated into 22 matters by the same government.
Other matters were the results of collapse of the then EA community. Mansoor could be aware of this, unfortunate when emotion overrides the intelligence, the outcome is unpleasant.

Obliviously that energy(electricity) is not among the 11 matters, Mansoor should tell his people on free ride they enjoy plus 50 billion debts at the cost of union government which the only player is Tanganyika tax payers. Undisputed facts

We are closely observing the nationality Zbar is exercising, the time is on horizon we will question the legality of Zbaris to own the land, getting free education and health, depriving Tanganyika their employement opportunities and sometime collecting salary from government coffer.We will do this on the same motto of nationality.

Minister Mansoor has a venue(BLW) to galvanize Zbar for secession in legal procedure instead of incendiary words.
I urge the Tanganyikan to have due diligence on the matter not to be drawn in the politics of arson because human life is precious than anything on the planet. We can separate amicably as human not necessarily arsonist.
 
Fafanua uhalalai upi wa kikatiba ba kisiasa, kauli yako ina hang!

Si nchi zote zilizoungana zilikuwa na kura ya maoni (kwahiyo hiyo si formula) mfano mzuri ni Canada. Quebec walipolilia kujitenga iliitishwa kura ya maoni(miaka 1980 na P.Trudeau) majority wakakataa. Hata baada ya hapo kukawa na separatist wanaojiita Block Quebecoir ambao walikuwa na hoja kama za Wzbar. Uchaguzi uliokwisha wananchi wa Quebec wamewaona wapuuzi kwa madai ya kijinga ili hali wanaofaidika ni wao. Katika viti 50 wamepata 3 tu na suala la kujitenga limefia mbali. Halikuwa na maslahi ya watu bali kikundi cha walafi fulani.

Kuna wakati watu wanadhani Wzbar hawataki muungano, ukweli ni kuwa ni kikundi cha watu wachache wenye kelele sana na waroho. Kama Wzbar hawataki muungano tusingewaona malaki wakifanya biashara na ajira za bara. Tusingeona wanajenga majumba bara ili hali nyoyo zao hazipataki. Huwezi ku invest mahali usipopataka! kwanini hawakwenda Malindi, Ngazija, Comoro au Somalia! tena huko wapo wa nywele zao.

Unaposema muungano ni bomu uvunjike, ni afadhali usingesema. Tulitarajia utuambie uvunjike kwa taratibu zipi!
Southern Sudan wamejitega lakini kuna utaratibu bado unafuatwa kuhakikisha maslahi ya wananchi yanalindwa.
Tukisema vunja tu asubuhi moja kama unavyoshauri, watakaoumia ni Wbar maana Mtanganyika ana nini cha kupoteza!!!!

Toa na Jenga hoja na ufafanue ukizingatia mada iliyopo mbele bila kuvuruga mtiririko wa mjadala.

Uhalali wa "muungano" huu haupo tangu pale ulipoundwa maana Articles of Union hazikufuatwa. Makubaliano yalivunjwa kwani hakukuundwa Bunge la Katiba kupitisha Katiba hii ya "muungano" na badala yake Bunge lililokuwepo kutumika kufanya hivyo.

Kisiasa, wananchi hatukuulizwa ridhaa yetu iwapo tunataka au laa.

Baraza la Mapinduzi halikuridhia "muungano" huu.

Mkataba wa "muungano" huu umedaiwa Mahkamani na haukutolewa.

Huo ndio uhalali ambao nauzungumzia.

Hii habari ya kuwa Wazanzibari wanajenga, ku invest na kufanya biashara ni kutumia fursa tu iliopo ambayo ni matokeo ya fitna alioleta Nyerere Zanzibar. Wazanzbari kwa makundi walihamia bara baada ya Mapinduzi ambayo mkono wa Nyerere umo. Walikimbia mateso waliokutishwa na wakakimbilia hapo karibu na ambapo walihakikishiwa usalama wao. Ujue kuwa Wazanzibari wapo sehemu nyingi duniani ingawa si uomgo kuwa hapo bara wako wengi. Wazanzibari wametumia fursa ambayo nyinyi hamkuiona kabla. Ni hivi karibuni tu ndio mmeanza kuzinduka katika usingizi wenu mzito.

"Muungano" huu wa Serikali mbili utake usitake ni kiini macho tu cha kuitawala Zanzibar kinyemela.

Without any question, the manner and the implications of the union between Tanganyika and Zanzibar is the most misunderstood aspect of Tanzania’s political development. It may not matter very much when foreigners get confused, but unfortunately there are many times when Tanzanians themselves appear to misunderstand it.”

Wazanzibari sasa wameona huu "muungano" hauwafai na sasa wanachotaka ni kujipapatua na uvamizi wa Tanganyika. Ndio maana hivi sasa hata viongozi wa SMZ na CCM wanakuja juu.

Hata baba yenu alijua hivyo kuwa yatatokea:

"Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu NCHI shiriki itakapoamua kujitenga" by Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

The end justifies the means Mkuu, Wazanzibari walio wengi hawautaki "muungano" huu na hilo linajulikana na hata nyinyi.

Kinachosaidia mpaka sasa ni hawa viongozi wachache wahafidhina na wanaofaidi katika mfumo huu lakini kila kukicha, Wazanzibari wanazidi kuelewa na kuunganisha nguvu zao katika kuudai Utaifa wao ulioporwa na mtake msitake mtaondoka tu

Zanzibar for Zanzibaris

@Mwanakijiji naona tunatatizo kubwa sana watanzania la upeo wa kuelewa mambo especially thread zako mimi nizisoma kwa umakini na kuelewa concept na hata kwenye fb nilichat na ww nikakuambia hilo na kukupongeza, huu ugonjwa sijui utaisha lini maana ndio unatupelekea kwenye mikataba mibovu, sheria kutofuatwa, maisha kuwa ya ujanja ujanja n.k. Tatizo hawajakuelewa unachomaanisha! ni sawa na ile thread ya " Dikteta nyerere"

Neno kuvunja muungano halitakiwi kutamkwa na mtu alieapa kuulinda muungano badala yake atumie lugha nyingine ya kama kuuboresha, kuujadili muungano etc na kama anataka kuuvunja kuna taratibu zake pia jamani ambapo inabidi ajivue hiyo kofia au pingu ya kuulinda then ndio auvunje!! nadhani nimeeleweka!!

mwanakijiji tuna tatizo kubwa sana la kulinda viapo vyetu watanzania inakuwa kama unaimba tu wimbo basi, inanikumbusha vyuoni copy and paste. tunakazi kweli kwenye society to take seriously when it comes to oaths! hata mahakamani mashahidi wanaapa huku hawajui maaana ya kiapo. lakini tutafika tu mwanakijiji na endelea kuweka thread za kuelimisha watu humu jamvini maana kunawatu wanataka kulibadili hili jamvi liwe kama la watu mbumbumbu maana GREAT THINKERS they think!!
 
... MKJJ, you are quite a visionary. Unaona mbali sana. For a Mzee, that ought to be a wake up call to other Wazees in that they have quite a potential. Kudos.
 
Uhalali wa "muungano" huu haupo tangu pale ulipoundwa maana Articles of Union hazikufuatwa. Makubaliano yalivunjwa kwani hakukuundwa Bunge la Katiba kupitisha Katiba hii ya "muungano" na badala yake Bunge lililokuwepo kutumika kufanya hivyo.

Kisiasa, wananchi hatukuulizwa ridhaa yetu iwapo tunataka au laa.

Baraza la Mapinduzi halikuridhia "muungano" huu.

Mkataba wa "muungano" huu umedaiwa Mahkamani na haukutolewa.

Huo ndio uhalali ambao nauzungumzia.

Hii habari ya kuwa Wazanzibari wanajenga, ku invest na kufanya biashara ni kutumia fursa tu iliopo ambayo ni matokeo ya fitna alioleta Nyerere Zanzibar. Wazanzbari kwa makundi walihamia bara baada ya Mapinduzi ambayo mkono wa Nyerere umo. Walikimbia mateso waliokutishwa na wakakimbilia hapo karibu na ambapo walihakikishiwa usalama wao. Ujue kuwa Wazanzibari wapo sehemu nyingi duniani ingawa si uomgo kuwa hapo bara wako wengi. Wazanzibari wametumia fursa ambayo nyinyi hamkuiona kabla. Ni hivi karibuni tu ndio mmeanza kuzinduka katika usingizi wenu mzito.

"Muungano" huu wa Serikali mbili utake usitake ni kiini macho tu cha kuitawala Zanzibar kinyemela.

,"Without any question, the manner and the implications of the union between Tanganyika and Zanzibar is the most misunderstood aspect of Tanzania's political development. It may not matter very much when foreigners get confused, but unfortunately there are many times when Tanzanians themselves appear to misunderstand it."

Wazanzibari sasa wameona huu "muungano" hauwafai na sasa wanachotaka ni kujipapatua na uvamizi wa Tanganyika. Ndio maana hivi sasa hata viongozi wa SMZ na CCM wanakuja juu.

Hata baba yenu alijua hivyo kuwa yatatokea:

"Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu NCHI shiriki itakapoamua kujitenga" by Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

The end justifies the means Mkuu, Wazanzibari walio wengi hawautaki "muungano" huu na hilo linajulikana na hata nyinyi.

Kinachosaidia mpaka sasa ni hawa viongozi wachache wahafidhina na wanaofaidi katika mfumo huu lakini kila kukicha, Wazanzibari wanazidi kuelewa na kuunganisha nguvu zao katika kuudai Utaifa wao ulioporwa na mtake msitake mtaondoka tu

Zanzibar for Zanzibaris

Mkuu Tanzania sio nchi ya kwanza kuungana na muungano wao ukawa halali. Hizo taratibu ulizozisema, mimi naomba unipe nchi ambazo imezipitia zote hivyo kuweka mfumo kamili wa uhalali ktk Muungano wa nchi mbili laa sivyo ni mawazo yako wewe mwenyewe. Act of Union pia inategemea na kila nchi, Uingereza wao wameunganisha koloni zao ambazo zote zilikuwa na mtawala mmoja. Wao wana serikali lakini chini ya Utawala wa Queen, hivyo historia ya nchi hiyo ndiyo inatunga muundowa act..

Mkuu Mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika January tarehe 12 1964, na hiyo artical of Union imepitishwa tarehe 22 April 1964 ulitaka bunge lipi lipitishe kisheria maanake sijui kama kuna bunge hapo..Ulitaka muungano ufanyike baada ya Zanzibar kufanya uchaguzi mwingine wa wabunge au huelewi kama yale yalikuwa Mapinduzi kukiondoa chama cha Hizbu hivyo kuondoa demokrasia na kuvunjika kwa vyama.

Ridhaa ipi ya wananchi unayozungumzia haswa, mbona hamsemi hata Mapinduzi yalihitaji ridhaa ya wananchi isipokuwa muungano na artical of Union hali wengi wanaochombeza leo hii walikuwa wafuasi wa Hizbu?. jamani mbona mnachanganya vitu kiasi kwamba mnaonyesha hamfahamu nini Mapinduzi na kwamba baraza la Mapinduzi ndilo pekee lilokuwa na nguvu na mamlaka ya kuamua nchi inakwenda wapi.
 
Huuu Muungano ni ujinga ambao hauna maana kwa pande zote ila kwa mabebari
na wachumia tumbo unawasaidia. hivi jiulize wewe mdanganyika unaleta ushabiki wako
wa kijinga muungano umekusaidia niniiii ?pande zote zinaumia tuwaache wanzanzibar
wafanyie maendeleo yao wanataka kuwa kama Dubai na China ila wanaona wabara
wanawabani .

hawa watu tunawabembeleza mpaka inakuwa kero umeme awalipi ,maji awalipi,
kwao umeme awana mgao?SISI tunaowalipia tunakatiwa umeme hata kwa siku
mbili hivi kuna faida gani yakuwangangania wanyonyaji hawa kila kukicha wanalalama
tu washenzi sana hawa watu bila tanganyika wangekuwa hivyo walivyo nyanya ,maziwa
vitunguu ,unga maji yakunywa na vingine vingi vinatoka bara hawo watu niwavivu sana
sasa tuwaache waaende ,kikupacho raha na uchungu kitakupa ,salam zao zenj udebedooo
 
Zanzibar minister says 2-government structure `outdated`
By The guardian reporter
15th July 2011
Comments :Zanzibar Minister for Agriculture and Tourism Mansoor Yussuf Himid said yesterday that the two-government arrangement in the Union between Zanzibar and Tanganyika "is outdated."
He told the House of Representatives here that an ideal arrangement was that of three governments – the union, Zanzibar and Tanganyika government.
Himid cautioned against using forums for discussing the union to threaten people, especially Zanzibaris, airing their views freely on the best form of the Union between the two countries.
He said it was surprising to see some leaders in the National Assembly repeatedly maintained that oil resource didn't belong to Zanzibar on grounds that the deposits were located in the ocean border between Tanga and Zanzibar.
"I don't want to disclose their names…they are trying to threaten the people," he said.
He elaborated that the three government arrangement was the best approach for the two countries, which formed the United Republic of Tanzania way back in 1964, "to free Zanzibaris from uncalled for threats."
"We are supposed to educate Zanzibaris on how to discuss about the Union," said Mansoor, who is also member of the powerful ruling CCM national executive committee.
Mansoor added that Zanzibaris should not fear stating openly that they need a system that would free them from ongoing debates.
He said the decision by the House to demand removal of oil and natural gas from the list of union matters few years ago was still valid and should be accepted."Honourable Speaker, I won't accept the issue of natural gas and oil remaining on the list of union matters," stressed MansoorZanzibar Minister for Lands, Housing, Water and Energy Juma Shamuhuna encouraged the people in the Isles to push ahead with one voice the decision to strike off the list of union matters both oil and gas.
Sioni kosa lolote hapa isipokuwa Kiitikadi! Kama mbunge wa CCM anaamini kuundwa kwa serikali tatu, nadhani kisiasa anatakiwa ajiondoe chama hicho na kwenda chama chenye malengo hayo..UCCM ni pamoja na kulinda muungano wa serikali mbili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom