Wanaotaka kuagiza magari, vyombo vya muziki, vifaa vya elektronik kutoka Japan

KyelaBoy

JF-Expert Member
Nov 9, 2008
206
22
Kwa watanzania wenzangu ambao watapenda kuagiza magari,vyombo vya muziki,vifaa vya elektronik kutoka Japan,napenda kuwajulisha kuwa kuna kampuni ya Mtanzania anayeishi huko Japan inaitwa Brilliant Traders ,ni mtanzania mwenzetu,mwaminifu na amekaa Japan kwa zaidi ya muongo mmoja na watu wengi wameagiza magari na vifaa mbalimbali kutoka kwake na wakavipata,kama utakuwa unahitaji magari na vifaa mbalimbali kutoka Japan tuwasiliane kwa simu no 0786 585 490,pia unaweza kuona website ya kampuni Brilliant Auto & General Trading
 
Mpaka tushuhudie huo uaminifu wake. Wabongo na uaminifu ni kama maji na moto vichanganywe
 
Mionzi imekaguliwa? Au ndiyo ile ambavyo vinatakiwa viharibiwe halafu vinauzwa kwa mlango wa nyuma.
 
Jamani sio kila mtu ,au mfanyabiashara Mtanzania ni tapeli/mwizi/mdanganyifu? hapana wengine ni waaminifu,kama mtu haamini anaweza enda hata pale ubalozi wa Japani akahakiki kama kwele kampuni ni halali(wenzetu sio kama Brela)ambao husajiri kampuni hewa,pia kama mnataka references za watu waliopata magari na vyombo vya muziki kutoka hiyo kampuni mnaweza kupata ni watu na bendi maarufu hapa bongo
 
Hata hao wamilik wa bend nao c waaminifu,unamkumbuka JB wa xtra bongo?na kapuya wa Akudo Impakt?
Jamani sio kila mtu ,au mfanyabiashara Mtanzania ni tapeli/mwizi/mdanganyifu? hapana wengine ni waaminifu,kama mtu haamini anaweza enda hata pale ubalozi wa Japani akahakiki kama kwele kampuni ni halali(wenzetu sio kama Brela)ambao husajiri kampuni hewa,pia kama mnataka references za watu waliopata magari na vyombo vya muziki kutoka hiyo kampuni mnaweza kupata ni watu na bendi maarufu hapa bongo
 
Mionzi imekaguliwa? Au ndiyo ile ambavyo vinatakiwa viharibiwe halafu vinauzwa kwa mlango wa nyuma.

Umenikumbusha ya samaki wa Japan, kwanini siku hizi hao samaki hawaji tena? Watanzania tunauawa na Serikali yetu kwa kuruhusu ujinga ule! Ocean Road hospital wajiandae kupokea wagonjwa wa kansa za mionzi baada ya miaka 5.
 
Wabongo hatuaminiani kabisa hata mke mwenyewe kumuamini ni inshu sembuse mtu baki,labda awe analeta mzigo kwanza ndio anapewa cash.
 
Kwa watanzania wenzangu ambao watapenda kuagiza magari,vyombo vya muziki,vifaa vya elektronik kutoka Japan,napenda kuwajulisha kuwa kuna kampuni ya Mtanzania anayeishi huko Japan inaitwa Brilliant Traders ,ni mtanzania mwenzetu,mwaminifu na amekaa Japan kwa zaidi ya muongo mmoja na watu wengi wameagiza magari na vifaa mbalimbali kutoka kwake na wakavipata,kama utakuwa unahitaji magari na vifaa mbalimbali kutoka Japan tuwasiliane kwa simu no 0786 585 490,pia unaweza kuona website ya kampuni Brilliant Auto & General Trading

Sisi wabongo bado suala la uaminifu, dakika chache sana mtu anakuwa na mawazo mengine kabisa na anabadilika
 
Mdau miye nahitaji kuagiza gari ila hii kampuni yako (yake) inaonyesha imekaa kisanii zaidi. Ni vizuri kuunga mkono juhudi za mTz mwenzetu ila hakuna anayependa kuibiwa kirahisi rahisi namna hiyo. Nikiangalia stock mliyonayo inanitia mashaska zaidi zaidi maana kuna gari unazionyesha mnazo, ili nikizitafuta hazionekani. Kingine, hiyo web mbona inanaonyesha huwa hamuiupdate?
 
Tatizo wabongo wanapenda hili neno kupiga!!!!hapo ndo panaleta shida utasikia nimepiga jamaa!!sijui wamefundishwa na serikali zao???
 
Business Description
  1. Buying and selling motor vehicles such as cars, trucks, motorcycles. We also buy and sell spare-parts, earth moving equipment, music instruments, power generators, electronic items and gems.
  2. We do all other businesses related to the above mentioned.
 
Kwa watanzania wenzangu ambao watapenda kuagiza magari,vyombo vya muziki,vifaa vya elektronik kutoka Japan,napenda kuwajulisha kuwa kuna kampuni ya Mtanzania anayeishi huko Japan inaitwa Brilliant Traders ,ni mtanzania mwenzetu,mwaminifu na amekaa Japan kwa zaidi ya muongo mmoja na watu wengi wameagiza magari na vifaa mbalimbali kutoka kwake na wakavipata,kama utakuwa unahitaji magari na vifaa mbalimbali kutoka Japan tuwasiliane kwa simu no 0786 585 490,pia unaweza kuona website ya kampuni Brilliant Auto & General Trading

Nipe contact za huyo jamaa yako, nitakuwa japan next month, nitahitaji container la baiskeli na gari na pikipiki.
 
kyelaboy

mimi ninataka nikuhakikishieni kwamba kama hii kampuni na wamiliki wake watakua waaminifu basi watapata biashara mpaka wazichoke, inasikitisha kufanya biashara na kampuni za wa pakistan, sri lanka waliopo japan ambao hakuna jipya bali ni communication trust, lakini wanaweza kukupiga dana dana mzigo wako hata miezi mitatu huku wakiwa na hela yako ndipo wakutumie gari

kweli tunahitaji mtanzania shupavu tumuunge mkono, na kama huyu mtanzania ni mwaminifu mimi naomba tumsupport wana jf na watanzania wote

Watanzania tunaweza

I wish you all the best on your business endevours
 
Back
Top Bottom