Wanaotafuta Kwenda Majuu

Aje fasta tuje tulime naye mchicha bonde la Msimbazi ,''Maisha bora bila ya kuajiriwa yanawezekana hapa bongo''
 
Haaa Jamaaa kapigika mbaya halafu ni engineer du kweli box noma ngoja nibaki tanzania niendelea kukoga vumbi.
 
Jamani saidieni taarifa hizi ziwafikie walengwa ,Hata na Serikali inahusika pia kwani huyo ni Mtanzania nguvukazi hiyo jamani. Asaidiwe arudi zake home atatufaa mahali fulani, Pia tutamnusuru uhai wake kama mwanadamu. Yamkini taarifa hizi hazipo serrikalini .Basi ziwafikie woote jamaa arudishwe nchini.
 
Kwanini asiende ubalozini ili wamasaidie? Kazi za ubalozi zetu nje nini kama sio kusadia watz?

Kila wizara ni ufisadi aibu hii nchi
 
Story ina walakini kidogo,

Kwa kifupi Sakara alienda nchini Bulgaria kwenye miaka ya 1980 kusomea uhandisi, lakini hali ilimuendea vibaya mpaka kujikuta hana uwezo kabisa wa fedha na akiishi kwa shida mitaani. Angependa kurudi Tanzania lakini hana uwezo wa kujilipia nauli. Inasemekana baada ya kutangazwa amekufa, ndugu zake hawakuendelea kumtafuta, lakini ukweli ni kuwa yuko hai. Taarifa zake nyingine ni:

Amezaliwa mwaka 1961
Inakisiwa alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1982 - 1984 halafu akaenda Bulgaria ambako alikuwepo mpaka kipindi napata taarifa hizi.

Mara kaenda Bulgaria miaka ya 1980, halafu tena kasoma UD 1982 - 1984.
Na pia miaka ya 1980s jamaa alikuwa na miaka mdogo sana, ina maana tayari alikuwa kaanza chuo kikuu mlimani?? au mie ndio sijalelewa mtiririko wa hii story??
 
Tanzania ni nchi yangu na nitaendelea kutumika hapahapa.
Kama alivyosema Air Tanzania ubalozini angepata msaada lakini Tunao Ubalozi wetu Bulgaria?
Pole sana Bro! Karibu Tanzania na Pole na maswahibu ya dunia
 
Hili sio swala la ushabiki kwani hakuna mtu anayejua anamatatizo gani! siku hizi kila nchi ina Mtanzania sithani kama Watanzania wenzake wangeshidwa kumsaidia. Vilevile kuna watu wanaenda nchi za nje hasa hizo ambazo si tajiri na wanaanza kutumia vitu kama madawa ya kulevya n.k hivyo matatizo mengi yanatokana na watu wenyewe.

Kama unataka kwenda nje ni lazima uelewe nchi hazifanani! Bulgaria na Marekani au Canada ni sehemu mbili tofauti. Mbona sisi tumekuja hapa USA miaka kumi tu mambo shari! Mambo mengine ya ma Box ni hate ya watu tu lakini maisha yanaweza kuanzia kwenye box wakati kijana anaenda shule lakini yakaishia kwenye wall. Hapa marekani watu wengi wanaweza kupanda ndege na kwenda bongo kimoja lakini hawafanyi hivyo!
 
Story ina walakini kidogo,

Kwa kifupi Sakara alienda nchini Bulgaria kwenye miaka ya 1980 kusomea uhandisi, lakini hali ilimuendea vibaya mpaka kujikuta hana uwezo kabisa wa fedha na akiishi kwa shida mitaani. Angependa kurudi Tanzania lakini hana uwezo wa kujilipia nauli. Inasemekana baada ya kutangazwa amekufa, ndugu zake hawakuendelea kumtafuta, lakini ukweli ni kuwa yuko hai. Taarifa zake nyingine ni:

Amezaliwa mwaka 1961
Inakisiwa alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1982 - 1984 halafu akaenda Bulgaria ambako alikuwepo mpaka kipindi napata taarifa hizi.

Mara kaenda Bulgaria miaka ya 1980, halafu tena kasoma UD 1982 - 1984.
Na pia miaka ya 1980s jamaa alikuwa na miaka mdogo sana, ina maana tayari alikuwa kaanza chuo kikuu mlimani?? au mie ndio sijalelewa mtiririko wa hii story??
Kaka unatakiwa ujifunze lugha yako ya Taifa namaanisha ujifunze Kiswahili.

Hiyo sentensi inajumuisha kuanzia 1980-1989 ndio kwa kiingereza wanaandika hivi 1980's

Mtu wa miaka 21 anaweza kabisa kuwa chuo kikuu, hakuna tatizo hapo... Piga hisabati vizuri, utagundua kuwa labda ameanza shule ya msingi akiwa na umri wa miaka sita (6) au saba (7).
 
aisee!!lazima atakuwa teja,haya nyie mnaokimbilia nje pateni lesson hapo,mambo sio easy kama tunavyofikiri
 
Huyu mtu alikwenda kutafuta elimu, na alikuwa anajitegemea hakuwa analipiwa na serikali au mtu yoyote...! Kwa hiyo uwezekano wa kutofanikiwa ni mkubwa sana... Huyu mtu anapaswa kupongezwa kwa sababu ameonyesha ujasiri mkubwa katika maisha yake...! Amejaribu.
 
Nadhan ni lugha ya 2 kwake
Kaka unatakiwa ujifunze lugha yako ya Taifa namaanisha ujifunze Kiswahili.Hiyo sentensi inajumuisha kuanzia 1980-1989 ndio kwa kiingereza wanaandika hivi 1980'sMtu wa miaka 21 anaweza kabisa kuwa chuo kikuu, hakuna tatizo hapo... Piga hisabati vizuri, utagundua kuwa labda ameanza shule ya msingi akiwa na umri wa miaka sita (6) au saba (7).
 
Huyu mtu alikwenda kutafuta elimu, na alikuwa anajitegemea hakuwa analipiwa na serikali au mtu yoyote...! Kwa hiyo uwezekano wa kutofanikiwa ni mkubwa sana... Huyu mtu anapaswa kupongezwa kwa sababu ameonyesha ujasiri mkubwa katika maisha yake...! Amejaribu.

i like this
 
Back
Top Bottom