Waalimu wanaosahihisha mitihani katika Chuo cha Ualimu, Mandaka katika Mkoa wa kilimanjaro wameingia mgogoro na serikali na wanataka kugoma kuendelea kufanya kazi hiyo baada ya pesa waliyokuwa wameandikiwa katika barua zao kuchakachuliwa na kupewa ziingine kinyume cha makubaliano. Pesa zimepungua toka 900 kwa kila karatasi ya mtihani hadi 700 kwa kila karatasi kwa waalimu wote waliopo huko. Kwa mujibu wa idadi yao na hesabu ya pesa wanayokatwa wanasema ikikatwa yote yaweza kufikia milioni 300. Wenye taarifa zaidi waliopo pale watujuze zaidi.