Wanaongoza nchi hii ni wengine, Mkuu wa kaya ni mtendaji tu

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,794
18,513
Kabla ya kujua mengi zaidi kuhusu secret societies na conspiracy theories mbali mbali nilipata ugumu kujua kwanini baadhi ya viongozi wanafanya mambo kinyume kabisa na waliowachagua na wanashindwa kubadilika hata kama kufanya hivyo kunawaangamiza wao wenyewe binafsi.

Sababu kubwa ni watu wachache wenye nguvu kubwa mara nyingi wanatumia nguvu ya fedha au spying na hata assassination(kuua).

Ndivyo ilivyo Marekani, Uingereza na nchi nyingine. Marekani Inaongozwa na "corporations" mashirika makubwa na haya ndio yanaamua nani awe rais, na ni wafadhili wakubwa wa kampeni za uchaguzi.

Wengi wao ni wanachama wa vyama vya Kisiri (secret societies) kama vile Illuminata, Knitts of Malta, Mafia, Scull and bone society, nk.

Wapo dunia nzima na wana nguvu ambayo huwezi kuamini na ndio wanao tawala dunia nzima, raisi asipokubaliana nao anajiweka kwenye hatari na kupinduliwa ama kufa, Kabila wa Congo, Kennedy wa Marekani, na wengine wengi

Na hapa kwetu ni hivyo hivyo kwahiyo msishangae kwanini Mkuu wa Kaya hawezi kufanya lolote, kuna mabwana wamemdhibiti anahiataji kuchagua kati ya maji au moto.
 
Back
Top Bottom