Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,602
- 5,569
Hayo ndiyo yalikwa makosa makubwa ya BABA WA TAIFA! walioharibu baadhi yao waliadhibiwa lakini wengi wao WALIHAMISHWA! Ndio maana nimekuwa nikimaanisha nyumba yenye msingi mbovu ibomolewe tujenge nyumba mpya. Shimo la siafu tulimwagie mafuta tulitie moto siafu wasitusumbue tena.Kwanini tumkosoe Kikwete ilhali naye sio Malaika just like Nyerere?Si kwamba namuunga mkono JK,bali hapa najenga hoja.Pili,unaposema huenda akuna mahali alikosea,hiyo HUENDA inaashiria huna hata hakika kama aliwahi kukosea au la,lakini mwishoni unahitimisha kuwa HAIKUWA MAKUSUDI.How did you know?
Hivi,Nyerere hakutambua kuwa amezungukwa na mbwa mwitu walio kwenye ngozi ya kondoo (eg akina Kingunge)?Hivi Nyerere alipokuwa anatoa adhabu za kuwapa watu ubalozi wanapoboronga hakuwa analea matatizo ambayo leo hii yametuzalishia viongozi wa ajabu kabisa in the form of Kikwete au watangulizi wake Mkapa na Mwinyi?Hudhani kuwa kwa kukumbatia uongozi kama privilege kwa wateule wachache,Nyerere ametuachia CCM inayoamini kuwa uongozi ni u-mUngu mtu kwa wateule wachache hao na si utumishi kwa umma.
Of course,ametufanyia mengi mazuri.Lakini hiyo sio sababu asikosolewe pale alipokosea.Na kumkosoa si dhambi,anyway.