Wanaoishi kwenye dampo... Utawatambua kwa usanii

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,756
Mbunge Kilango aandaliwa mkutano na waandishi wa habari bila kujua
Na Jackson Odoyo
Date: 3/23/2009


MBUNGE wa Same, Anne Kilango amedai kuwa alipangiwa kuzungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) bila ya kuomba kufanya hivyo, lakini ameona kuwa kuna haja ya kufanya hivyo ili kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na Mwananchi jana, mke huyo wa waziri mkuu wa zamani, John Malecela alisema alishangazwa na idadi ya simu kutoka kwa waandishi wa habari waliokuwa wakiuliza angefanya mkutano muda gani.

"Baada ya kupata simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakisema kuwa wananisubiri, nililazimika kwenda Maelezo kujua undani wa taarifa hizo,” alisema mbunge huyo machachari.

“Nilienda kuangalia katika kitabu cha usajili na nikakuta kweli kuna jina langu kuwa nitazungumza na waandishi leo (jana), lakini nilipowauliza walikiri kuwa walikosea.”

Alisema kutokana na kubaini kuwa waandishi wana hamu ya kuzungumza naye, sasa ataitisha mkutano na waandishi licha ya kwamba hakuwa amepanga hivyo.

“Inanifurahisha kuona wananchi wana hamu ya kusikia maneno yangu, nami niko tayari kufanya hivyo angalau nitoe hata salamu,” alisema mbunge huyo.

Lakini, Kilango hakusema atazungumzia nini kwenye mkutano atakaoitisha wala siku atakayozungumza.


Out, out damned spot, out I say. Even all the perfumes of Arabia will not cleanse this little hand - Lady Macbeth
.
Believe this and you'll believe anything !! - James Hadley Chase
 
Bila shaka kuna waandishi waliandaliwa rasmi kumtumbukiza ktk mgongano na wapiganaji wenzake,afadhali alivyochomoa ili akajipange vema.
 
Yeye anaona furaha kuona wananchi wanataka kumsikiliza aseme nini, wala si kutuambia tangu tuhuma za ufisadi yeye amefanya nini, tangu alipoanza kusema, maana hata sisi tunasema sana, lakini yeye ni mmoja wa watu wa kufanya 'kitu'

je amezungumza nao??
 
Back
Top Bottom