Wanaoishi katika migogoro ya mapenzi someni alama za nyakati

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WANANDOA wanaoendelea kuishi katika misuguano isiyopatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu ni vyema wakajifunza kutokana na matukio yanayoendelea kuibuka maeneo mbalimbali nchini.

Ni hatari kuendelea kuishi katika uhusiano mbaya na mtu uliyeshirikiana naye kwa kiasi cha kupata watoto ambao kimsingi wanahitaji ushirikiano wa wazazi ili wapate malezi na makuzi bora.
Ingawa msingi wa ndoa ni upendo, Watanzania wengi wanaishi katika uhusiano mbaya wa mapenzi kiasi kwamba ndoa nyingi zimejengwa katika misingi tofauti na upendo wa kweli.

Hakuna ubishi kwamba wanandoa wengi wamegeuka waigizaji ambao wakiwa machoni pa jamii wanatambulika kama wanandoa wakati maisha yao halisi siyo hayo.

Jambo hili linasababisha mateso ya kisaikolojia na limeanza kusababisha maafa katika jamii. Ingawa maandiko ya dini kama ya Kikristo yanazuia ndoa kuvunjika, haiingii akilini watu wanaoishi bila chembe ya upendo kati yao, kiasi cha kugeuka maadui kuendelea kuishi chini ya mwamvuli wa ndoa.

Ni jukumu la kila anayeishi katika uhusiano wa aina hiyo, kufanya uamuzi na kuutekeleza kwa dhati. Ikiwa anaamua kuendelea kuishi na mwenzi kama mke na mume ni vyema kufanya hivyo kwa dhati.
Siyo leo mmeachana, kesho unataka kufahamu alichovaa amenunuliwa na nani au anaishi vipi. Ikiwa wewe ndiye mwenye makosa na umebaini hilo, jishushe, omba msamaha ukimaanisha na badili tabia yako.

Sababu nyingi zinatajwa kuwa chanzo cha uhusiano mbaya ndani ya ndoa, lakini moja kubwa ni wanandoa kukosa uaminifu. Tabia hiyo imewavaa wanandoa wa jinsi zote, mke na mume.

Upungufu wa uaminifu katika ndoa za sasa unaoongoza ni wa mtu mmoja au wanandoa wote kuwa na uhusiano wa mapenzi nje ya mwenzake. Lakini pia kuna upungufu wa uaminifu katika umiliki wa mali.

Kukosekana uaminifu ndani ya ndoa kunaibua matatizo mengine ambayo yasipoangaliwa kwa kina yanaweza kudhaniwa kuwa ndiyo chanzo cha ndoa kusambaratika.

Kwa kuwa dhana ya uchambuzi huu siyo aina ya uaminifu katika ndoa, narejea kwenye mada ya kuwataka waliyo ndani ya uhusiano mbaya wa mapenzi kufanya uamuzi na kuutekeleza kwa dhati.
Unakuta mtu ameishi na mwenzake kwa miaka 10 hata 20 anaibuka na kumtwisha mwenzake tuhuma akidai ni mwizi mchawi, mchafu au mzinzi.

Hivi mtu anaweza vipi kuishi chini ya paa moja na mke au mume mwenye tabia hizo kwa miaka zaidi ya 10, zaidi ya hayo akubali kuzaa naye watoto ilhali ikifahamu kufanya hivyo ni kuongeza uzao wenye asili ya tabia mbaya.

Hali hii inaibua hisia sahihi kwamba kiini cha mgogoro wa ndoa nyingi ni mmoja wa wanandoa au wote kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi ya nje jambo linalosababisha imani na upendo kupotea.

Mfano wa kilele cha kulea matatizo ndani ya ndoa ni tukio la usiku wa kuamkia Januari 8, mwaka huu ambapo mkazi wa Kijiji cha Gekrum, Wilaya ya Karatu, Evans Damian (43) aliua watoto wake wanne kabla ya yeye mwenyewe kujinyonga mpaka kufa kwa madai kwamba alikuwa na ugomvi na mke wake.

Watoto waliouawa kwa kukatwa kwa shoka na baba yao vichogoni ni Theophil (10) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Karatu Mission, Ritha (8), Dibimo (4) na pacha wake Theodory (4) ambao walikuwa wanafunzi wa Shule ya Awali Karatu Mission.
Baada ya maziko ya watoto hao ambao hawakuwa na hatia yoyote, mama yao mzazi Paskaria Sixbelt (30) akazungumzia maisha ya ndoa yake kwamba yalikuwa na mgogoro uliowatenganisha tangu Agosti, mwaka jana.

Katika maelezo yake anasema walikutana na mumewe Karatu Mjini siku ya tukio na baada ya kuonana ugomvi mkubwa baina yao ulizuka. Mama huyo anadai kuwa kisa cha yote hayo ni baada ya mumewe kumuona akiwa amesuka nywele na kuvaa pete ambayo marehemu mumewe alihisi kuwa amevishwa na mwanamume mwingine.

Katika ugomvi huo, mwanamume huyo alimng'ata mkewe kidole cha kushoto mpaka akakikata kisha kukitema alipotoka hapo ndipo likafuata hilo la mauaji ya watoto wote na yeye mwenyewe kujinyonga mpaka kufa.

Inaelezwa kwamba kisa cha kuachana kwao ni madai kwamba mke alikuwa akiiba fedha dukani kwao hayo mengine ya wivu yanatokea wapi hasa ikizingatiwa kwamba walishatengana kwa takriban miezi mitano?

Kwa akili ya kawaida isiyohitaji mafunzo ya saikolojia ni dhahiri kwamba mwanamume huyo alishaathirika kisaikolojia. Asingejiua, angepimwa baada ya kuua watoto wake au hata baada ya kumng'ata mkewe kidole hadi kukikata, hilo lingethibitika.

Sasa kwa nini watu wafikishane huko? Unayeishi na mke, mume au mzazi mwenzako kwa migogoro isiyo na ukomo tena usiyofahamu hatima yake, unafiki nini unaposikia hayo yakitokea?

Wahenga walisema, “ukiona mwenzako ananyolewa na wewe za kwako tia maji.” Mambo mengi yanatokea katika familia nyingi za nchini ambayo bahati mbaya yanawatesa watoto wasio na hatia.

Ingawa dini zote zinachukia talaka lakini kuliko wanandoa kutesana mpaka kufikia hatua ya kusababisha maafa ni bora uamuzi mbadala ukachukuliwa na kutekelezwa kwa dhati ili wasio na hatia wasiendelee kuumia.
 
Sijakueelewa unataka tufanye lipi? Maana hii ndoa unayozungumzia ni kwamba madhara yametokea baada ya kuachana, mke aliona shida akaamua kujiweka pembeni kama unavyoshauri..huenda angevumilia maafa makubwa kama hayo yasingetokea. Halafu mtu kukaa na mtu miaka 20 si lazima huyo mwenzi awe ameanza hiyo tabia toka mwaka wa kwanza, wengi huanza baada ya miaka kadhaa so hata kuanza hiyo tabia mwaka wa 20 inawezekana sana, tunaona familia zinaharibika wengine watoto wao wakiwa tayari vyuo vikuu au wanafanya kazi kabia. Naona hujatoa suluhisho ila unataka kuongeza vifo kutokana na wivu!
 
Asante sana sana,ushauri mzuri na analysis nzuri......nimeipenda.

Natamani ningekuwa na la kukupa zaidi ya thanks,any way nikutakie wikiendi njema na akili iliyotulia utuletee tena article kama hii.:clap2::clap2:
 
Sijakueelewa unataka tufanye lipi? Maana hii ndoa unayozungumzia ni kwamba madhara yametokea baada ya kuachana, mke aliona shida akaamua kujiweka pembeni kama unavyoshauri..huenda angevumilia maafa makubwa kama hayo yasingetokea. Halafu mtu kukaa na mtu miaka 20 si lazima huyo mwenzi awe ameanza hiyo tabia toka mwaka wa kwanza, wengi huanza baada ya miaka kadhaa so hata kuanza hiyo tabia mwaka wa 20 inawezekana sana, tunaona familia zinaharibika wengine watoto wao wakiwa tayari vyuo vikuu au wanafanya kazi kabia. Naona hujatoa suluhisho ila unataka kuongeza vifo kutokana na wivu!

Umesema vema mpenzi!
Mwanaume ukitaka kumwacha hakikisha unaenda kuishi mbali kabisa asikutie machoni hata siku moja. Sijui wenzetu hawa wwako vipi!Ndiyo maana niliamua kuhamia Solom Island kabisa kuepuka maafa!

Huku anakufanyia visa ukimwacha anataka kukutoa roho.Ukiendelea kuishi naye unaishia kwenye mental asylum maana ile psychological torture inayokupata ya kumuona kila uamkapo inazidi maelezo.Maisha mazuri ni yale yenye kukupa amani moyoni.Huwezi ukawa unalala na huzuni na kuamka nayo kila siku.

The good thing is hata ukiumizwa na mmoja bado utapata mwenye kukupenda na kuziba pengo tena haraka kuliko unavyoweza kutarajia.
 
Asante sana sana,ushauri mzuri na analysis nzuri......nimeipenda.

Natamani ningekuwa na la kukupa zaidi ya thanks,any way nikutakie wikiendi njema na akili iliyotulia utuletee tena article kama hii.:clap2::clap2:

ila tukubali mara nyingi kwa waliopendana kuachana huwa ni vigumu sana hata kukawa na ugomvi ukiona wameachana ujue hapo upande mmoja haukuwa na mapenzi ya dhati
 
Sijui kwa nini ndoa zimekua jehanam, yani ziwa la moto kabisa. Maskini watoto alo wazaa kutoka kwa viuno vyake, ayamalize maisha yao kwa njia hiyo.mh inatisha kama ndo ndo hivyo sijui.
 
Yaliyotokea Karatu ni climax ya domestic violence, jambo ambalo linapaswa kuzungumziwa sana katika jamii zetu ili matukio kama hayo yasiyokee tena, na kukatisha maisha ya watoto innocent....jamani I fail even to think of it....
 
Yaliyotokea Karatu ni climax ya domestic violence, jambo ambalo linapaswa kuzungumziwa sana katika jamii zetu ili matukio kama hayo yasiyokee tena, na kukatisha maisha ya watoto innocent....jamani I fail even to think of it....

Yes muda mwingine tusiruhusu hasira zitutawale kiasi cha kufikia kujiua au kuua mmoja wetu na hata kuchinja au kunyonga watoto kweli yale matukio yalimgusa kila mtunadhani Taasisi zinazoshughulika na ustawi wa jamii na haki za binadamu inabidi zijipange ili kuhakikisha matukio ya namna hiyo hayajirudii tena sheria hairuhusu mtu kujiua au kumuua mtu mwingine!
 
Waliwahi kusema kuwa mwanzo wa ndoa ni tamu kama chungwa, katikati ya ndoa ni tamu kama limao na mwisho wa ndoa chungu kama shubiri!
pata picha!
 
Thanx Kilimasera ujumbe ni wa maana sana, familia nying zimeteketea kwa kivuli cha ndoa, na gender based violance imekuja juu sana, kuna baba mwingine makere wilaya ya kasulu nae kaua watoto watatu,kabla ya hapo wakike alimbaka, na yeye kajinyonga . Chanzo ni mahusiano mabaya na mama yao.Nowdays watoto wamekuwa victims.
 
Ya nini malumbano,
ya nini maneno,
najiweka pembeni,
naepusha msongamano,
mola...................
 
Back
Top Bottom