Wanaoishi Jana Wanatusumbua Leo; Tutaiokoaje Kesho?

majaliwa-3-jpg.322619
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Rais J.P. Magufuli inapozidi kujipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kimfumo na kifikra katika kuimarisha utendaji wa utumishi wa umma kuelekea 2020 ni watendaji na viongozi ambao bado wanaishi jana wakati nchi iko leo na hivyo wanatishia hatima ya taifa letu kesho.

Jana yetu ni miaka ya nyuma ambapo watendaji waliweza kufanya lolote bila kujali sana matokeo (with impunity) na wafanyakazi walijua watendaji wao walikuwa "hivi na vile" kiasi wkamba watumishi wa chini nao baadhi yao walianza kufanya mambo bila kujali matokeo. Mtu alipopata nafasi ya ajira au kupandishwa cheo fikra za kwanza ambazo inaonekana watu walikuwa nazo ni vipi katika nafasi hizo watachuma kwa haraka haraka kabla mambo hayajabadilika.

Taratibu za ajira na utendaji kazi zilifuatwa kama vipe ni jambo la hiari (optional) kiasi kwamba ulazima wa kusimamia sheria na taratibu ulionekana ni usumbufu mkubwa. Mwananchi alipoamua kwenda kupata huduma fulani kwenye taasisi ya serikali ni lazima afikirie mara mbili na kujiandaa kiakili (pyschologically) na usumbufu wowote ambao ataupata. Mwingine inabidi aulize kwanza kama kuna mtu yeyote anayemfahamu huku au kama anafahamu mtu anayeweza kuwa anafahamiana na mtu mwingine huko anakotaka kwenda. Sehemu nyingine katika kutafuta mtu wa kufahamiana naye mtu aliweza kwenda hata kipeo cha tatu na cha nne cha marafiki. Akipatikana anayejuana na fulani huko basi mtu anaweza kua na imani kuwa anaweza angalau kusikilizwa; akikosekana bajeti ya kulainisha mifumo inabidi ifikiriwe tena.

Maisha haya ya jana yamejionesha kwa kiasi kikubwa katika utendaji wa uzembe na usiojali fedha za wnaanchi kama ambavyo ripoti mbalimbali za CAG zimekuwa zikituonesha tangu 2006. Hii jana watu walikuwa wameizoea kiasi kwamba leo haikuruhusiwa ifike kamwe; watu waliipenda jana sana kiasi kwamba hata wakati wa kampeni za uchaguzi bado lilikuwepo kundi la watu ambao waliitamani leo lakini hawakuwa tayari kuiachilia jana.

Matukio karibu matatu yaliyotokea Alhamisi iliyopita yametudokeza kuwa bado tuna tatizo la watu wanaoishi jana. Muhimbli ilitarajiwa uongozi mpya kuanza kuondoa kero ambazo si za lazima; hii siyo tu uongozi wa Muhimbili bali pia Wizara ya Afya; lakini inaonekana mazoea magumu. Bado watu wamekutwa tena wamejazana wodini kama vile wako kwenye behewa la Daraja la tatu wakielekea Bara. Hivi kweli bado hakuna mtu mwenye akili za 'kawaida' tu kuwa watu wanaohitaji huduma safi, salama na mazingira mazuri kabisa ya tiba ni kina mama na watoto - kwa sababu ya udhaifu (vulnerability) yao? Kama watu hawa wanashindwa kuliweka hili kama ajenda yao nambari 1 hivi huko kwingine watapanga nini? Kama inabidi kufuta posho na mishahara ya viongozi wote ili kina mama na watoto wetu wapatiwe huduma sahihi na bora basi na liwe hivyo; lakini hili halieleweki?

Kabla hatujatulia Mwigulu Nchemba naye kazukia huko Pugu (kwa mara nyingine) kufuatilia machinjio. Akakuta kati ya ng'ombe 200 waliokuwa wanaenda kuchinjwa (au sijui wameshachinjwa) ni 20 ambao walikuwa na vibali; huku wale wengine wote kama wamelipiwa basi wamelipiwa kwenye mifuko ya mtu na labda kwa kiasi cha chini kidogo na hivyo kuikosesha serikali mapato; na hilo ni siku moja tu! Hawa watu wa machinjioni walikuwa wanaamini basi ile ya kwanza ni nguvu ya soda basi wacha waendelee kama ilivyokuwa (status quo was maintained). Hawakuwa tayari kuamini kuwa mtu atarudi tena na inawezekana hata watakaoingia bado watafikiria Mwigulu hatawazukia tena na hivyo wataanza na wao kutafuta 'mitkasi' ya hapa na pale. Warudi jana.

Na kabla hata hatujatulia Waziri Mkuu Kassima "Tabasamu" Majaliwa (nimempa jina la 'tasabamu' kwa sababu tabasamu lake linadanganya watu) karudi tena Bandari ambako nako akakuta madudu mengine yale yale na tena safari hii ikitisha zaidi. Kwamba, mpango wake wa kwenda huko kwa kushtukizwa baada ya kutoshwa na watumishi safi ukatibuliwa na 'mbeya' mmoja kiongozi wajuu tu ambaye aliamua kuwadokeza na hivyo kutaka kusaidia kuficha madudu huko.

Nakubaliana na wengine wote kuwa Waziri huyo akithibitika kweli ametuma ujumbe wa kumtonya mama Chuwa ili ajaribu kuvuruga ushahidi basi Magufuli hana jinsi; ni lazima amuondoe Waziri huyo bila kujali uwezo wake, ujiko wake, au sifa zake. Serikali hii haipaswi na haitakiwi hata kuuliza "mwenzetu ilikuwaje ukavuruga mipango ya waziri Mkuu". Hii ni hujuma ya ndani (internal sabotage). Tena hili inapaswa lifanyiwe kazi mapema sana ili kuleta heshima na woga kwa viongozi wengine. Magufuli akipepesa macho tu na kujikwaa tu atajitengeneza udhaifu usio wa lazima.

Nina uhakika wapo viongozi wengine na watumishi wengine ambao bado na wenyewe wanaombea kuwa safisha safisha hii haitowafikia na kwamba, hizi zote zilikuwa nguvu za soda. Siku 100 baadaye nguvu za soda bado zinachemka na kama tulisikia dokezo kidogo Bandari ni mojatu ambako kunahitaji kusafishwa ili safisha hii iendelee maeneo mengine. Hawa wa sehemu nyingine kama wana akili timamu wanapaswa ama kuanza kujiondoa wenyewe au wasubiri shoka la Magufuli liwekwe kwenye mashina yao!

Jana imepita; waliotumikia fikra za wa jana wajue kuwa siku mpya imefka. Hili nililisema mwanzoni lakini bado watu hawaamini kuwa kuna siku mpya. Hawaamini kuwa kiongozi huyu siyo yule na fikra zinazomuongoza siyo zile. Waliozoea kubebana, kufichiana na kusaidiana kufika hujuma, rushwa, magendo na hujuma za kila namna wakati wao uliishia jana.

Ni lazima washughulikiwe leo kama tunataka kesho iliyo bora; kama tunataka watoto wetu na vijana wetu wanafikiria kutumikia umma kuwa na misingi mizuri, ni lazima uchafu wa jana usafishwe. Usafishwe na kila mtu ajue kuwa tunahitaji utumishi wa umma ulio msafi na ambao uchafu kidogo tu ukitokea hauchelewi kushughulikiwa. Na katika kushughulikia ni lazima tuwatoe mfano wale wenzetu wote ambao tulidhani wanaijua leo lakini bado kifikra wametiwa pingu za jana na bado hawajaziachilia; kwani hawa ni hatari kwa kesho yetu na ya keshokutwa ya watoto wetu na mtondogoo wa watoto wa watoto wetu.

Siku mia zimepita lakini siku mamia bado zinakuja. Mwendo wa kurudisha heshima katika utumishi wa umma na weledi wa watumishi unapaswa kuongeza kasi. Mpaka Watanzania tuheshimiane na tuheshimu utumishi wa umma.

Hadi hivi sasa hakuna majuto.

MMM
Hofu yangu kwako ni kuwa utabadilika tu kumuunga mkono Magufuli pindi watanzania wengi saidi watakapojitokeza mitandaoni na kumuunga mkono rais, kwani unapenda saaana kuwa wa tofauti
 
Mkazo ni ule ule kama baba mwenye nyumba huruhusu jiwe kurushwa kwake anapokosea atatoa wapi dhamira safi ya kukemea wengine?.
Raisi aanze na Katiba hata kile kijikifungu kimoja tu ajifungulie mlango wa kuweza kushitakiwa mbele ya Mahakama Kuu awe madarakani au awe amestaafu kama atatenda makosa yanayohusu ufisadi wa mali ya Umma ,mauaji ya halaiki au makosa mengine makubwa kadri itakavyo kubaliki na Bunge ! Hatua hii itaitikisa nchi na wale wote waliozoea kukwapua wataelewa kama kweli Mkuu wa Nchi anamanisha nini!

Kinyume na hivyo tuendelee kubadilishana aina na majina ya wakwapuaji kila miaka mitano au kumi!
Yes nakubaliana nawe kabisa. Tazama, wakati walitumia mabilioni kwenda kuomba misaada nje, nyumbani watu wanapima mafuta kwa vijiti na nyakati nyingine kukadiria
Ndio maana tulisema, kama anasimama na sera za CCM , hakuna miujiza ya aina yoyote, the same oold story

Serikali ikiwa na uongozi 100% ilikuwa api madudu haya yakitendeka. Leo wanakula pensheni wanapewa hata taasisi kubwa kuzisimamia tukijua walilitia taifa hasara kubwa
 
majaliwa-3-jpg.322619
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Rais J.P. Magufuli inapozidi kujipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kimfumo na kifikra katika kuimarisha utendaji wa utumishi wa umma kuelekea 2020 ni watendaji na viongozi ambao bado wanaishi jana wakati nchi iko leo na hivyo wanatishia hatima ya taifa letu kesho.

Jana yetu ni miaka ya nyuma ambapo watendaji waliweza kufanya lolote bila kujali sana matokeo (with impunity) na wafanyakazi walijua watendaji wao walikuwa "hivi na vile" kiasi wkamba watumishi wa chini nao baadhi yao walianza kufanya mambo bila kujali matokeo. Mtu alipopata nafasi ya ajira au kupandishwa cheo fikra za kwanza ambazo inaonekana watu walikuwa nazo ni vipi katika nafasi hizo watachuma kwa haraka haraka kabla mambo hayajabadilika.

Taratibu za ajira na utendaji kazi zilifuatwa kama vipe ni jambo la hiari (optional) kiasi kwamba ulazima wa kusimamia sheria na taratibu ulionekana ni usumbufu mkubwa. Mwananchi alipoamua kwenda kupata huduma fulani kwenye taasisi ya serikali ni lazima afikirie mara mbili na kujiandaa kiakili (pyschologically) na usumbufu wowote ambao ataupata. Mwingine inabidi aulize kwanza kama kuna mtu yeyote anayemfahamu huku au kama anafahamu mtu anayeweza kuwa anafahamiana na mtu mwingine huko anakotaka kwenda. Sehemu nyingine katika kutafuta mtu wa kufahamiana naye mtu aliweza kwenda hata kipeo cha tatu na cha nne cha marafiki. Akipatikana anayejuana na fulani huko basi mtu anaweza kua na imani kuwa anaweza angalau kusikilizwa; akikosekana bajeti ya kulainisha mifumo inabidi ifikiriwe tena.

Maisha haya ya jana yamejionesha kwa kiasi kikubwa katika utendaji wa uzembe na usiojali fedha za wnaanchi kama ambavyo ripoti mbalimbali za CAG zimekuwa zikituonesha tangu 2006. Hii jana watu walikuwa wameizoea kiasi kwamba leo haikuruhusiwa ifike kamwe; watu waliipenda jana sana kiasi kwamba hata wakati wa kampeni za uchaguzi bado lilikuwepo kundi la watu ambao waliitamani leo lakini hawakuwa tayari kuiachilia jana.

Matukio karibu matatu yaliyotokea Alhamisi iliyopita yametudokeza kuwa bado tuna tatizo la watu wanaoishi jana. Muhimbli ilitarajiwa uongozi mpya kuanza kuondoa kero ambazo si za lazima; hii siyo tu uongozi wa Muhimbili bali pia Wizara ya Afya; lakini inaonekana mazoea magumu. Bado watu wamekutwa tena wamejazana wodini kama vile wako kwenye behewa la Daraja la tatu wakielekea Bara. Hivi kweli bado hakuna mtu mwenye akili za 'kawaida' tu kuwa watu wanaohitaji huduma safi, salama na mazingira mazuri kabisa ya tiba ni kina mama na watoto - kwa sababu ya udhaifu (vulnerability) yao? Kama watu hawa wanashindwa kuliweka hili kama ajenda yao nambari 1 hivi huko kwingine watapanga nini? Kama inabidi kufuta posho na mishahara ya viongozi wote ili kina mama na watoto wetu wapatiwe huduma sahihi na bora basi na liwe hivyo; lakini hili halieleweki?

Kabla hatujatulia Mwigulu Nchemba naye kazukia huko Pugu (kwa mara nyingine) kufuatilia machinjio. Akakuta kati ya ng'ombe 200 waliokuwa wanaenda kuchinjwa (au sijui wameshachinjwa) ni 20 ambao walikuwa na vibali; huku wale wengine wote kama wamelipiwa basi wamelipiwa kwenye mifuko ya mtu na labda kwa kiasi cha chini kidogo na hivyo kuikosesha serikali mapato; na hilo ni siku moja tu! Hawa watu wa machinjioni walikuwa wanaamini basi ile ya kwanza ni nguvu ya soda basi wacha waendelee kama ilivyokuwa (status quo was maintained). Hawakuwa tayari kuamini kuwa mtu atarudi tena na inawezekana hata watakaoingia bado watafikiria Mwigulu hatawazukia tena na hivyo wataanza na wao kutafuta 'mitkasi' ya hapa na pale. Warudi jana.

Na kabla hata hatujatulia Waziri Mkuu Kassima "Tabasamu" Majaliwa (nimempa jina la 'tasabamu' kwa sababu tabasamu lake linadanganya watu) karudi tena Bandari ambako nako akakuta madudu mengine yale yale na tena safari hii ikitisha zaidi. Kwamba, mpango wake wa kwenda huko kwa kushtukizwa baada ya kutoshwa na watumishi safi ukatibuliwa na 'mbeya' mmoja kiongozi wajuu tu ambaye aliamua kuwadokeza na hivyo kutaka kusaidia kuficha madudu huko.

Nakubaliana na wengine wote kuwa Waziri huyo akithibitika kweli ametuma ujumbe wa kumtonya mama Chuwa ili ajaribu kuvuruga ushahidi basi Magufuli hana jinsi; ni lazima amuondoe Waziri huyo bila kujali uwezo wake, ujiko wake, au sifa zake. Serikali hii haipaswi na haitakiwi hata kuuliza "mwenzetu ilikuwaje ukavuruga mipango ya waziri Mkuu". Hii ni hujuma ya ndani (internal sabotage). Tena hili inapaswa lifanyiwe kazi mapema sana ili kuleta heshima na woga kwa viongozi wengine. Magufuli akipepesa macho tu na kujikwaa tu atajitengeneza udhaifu usio wa lazima.

Nina uhakika wapo viongozi wengine na watumishi wengine ambao bado na wenyewe wanaombea kuwa safisha safisha hii haitowafikia na kwamba, hizi zote zilikuwa nguvu za soda. Siku 100 baadaye nguvu za soda bado zinachemka na kama tulisikia dokezo kidogo Bandari ni mojatu ambako kunahitaji kusafishwa ili safisha hii iendelee maeneo mengine. Hawa wa sehemu nyingine kama wana akili timamu wanapaswa ama kuanza kujiondoa wenyewe au wasubiri shoka la Magufuli liwekwe kwenye mashina yao!

Jana imepita; waliotumikia fikra za wa jana wajue kuwa siku mpya imefka. Hili nililisema mwanzoni lakini bado watu hawaamini kuwa kuna siku mpya. Hawaamini kuwa kiongozi huyu siyo yule na fikra zinazomuongoza siyo zile. Waliozoea kubebana, kufichiana na kusaidiana kufika hujuma, rushwa, magendo na hujuma za kila namna wakati wao uliishia jana.

Ni lazima washughulikiwe leo kama tunataka kesho iliyo bora; kama tunataka watoto wetu na vijana wetu wanafikiria kutumikia umma kuwa na misingi mizuri, ni lazima uchafu wa jana usafishwe. Usafishwe na kila mtu ajue kuwa tunahitaji utumishi wa umma ulio msafi na ambao uchafu kidogo tu ukitokea hauchelewi kushughulikiwa. Na katika kushughulikia ni lazima tuwatoe mfano wale wenzetu wote ambao tulidhani wanaijua leo lakini bado kifikra wametiwa pingu za jana na bado hawajaziachilia; kwani hawa ni hatari kwa kesho yetu na ya keshokutwa ya watoto wetu na mtondogoo wa watoto wa watoto wetu.

Siku mia zimepita lakini siku mamia bado zinakuja. Mwendo wa kurudisha heshima katika utumishi wa umma na weledi wa watumishi unapaswa kuongeza kasi. Mpaka Watanzania tuheshimiane na tuheshimu utumishi wa umma.

Hadi hivi sasa hakuna majuto.

MMM
Tuliposema ccm na serikali yake vimeoza hukuamini?
 
Hii nchi ilikuwa imeoza kabisa.

Na huu uozo ambao sasa unaanza kujitokeza ni indictment kubwa sana dhidi ya CCM na serikali zake.

Wasiwasi wangu ni kuna watu ambao ndo wamechangia kuuleta huo uozo lakini hawataguswa kabisa.
Hivi huwezi kuongea au kujenga hoja zako bila kuihusisha na CCM au CHADEMA? Mbona unaonesha fikra ndogo mbele ya hadhara?
 
Hahahahahaaa aibu yako we kizee kinafiki ona ulivyojibú kwa aibu!!!

Ktk wizara iliyoongoza kwa uzembe ni ujenzi na unajua hii inareflect nn

This time needs smart people na hao smart people hakuna zaidi ya kutafuta sifa tu!!!

Huko muhimbili mbona ni yale yale?

Walugaluga mnaamini mabadiliko ni kufukuza na kubadilisha sura!!

Na mabadiliko inategemea yanaletwa na nani si hawa waliokuwa sehemu ya uchafu!!!

Mwambie msukuma mwenzio atumbue na jibu la uuzaji wa nyumba za serikali!!!

Huu ndo mwisho wa unafiki wako
Nadhani hata Magufuli kaisoma vizuri post yako hii. Japo pia kwa kiasi fulani Rais pamoja na Waziri mkuu wameonyesha angalau ile hali ya kujaribu. Hisia zangu kwa sasa huenda Rais anajaribu kushughulikia zile sehemu ngumu ambazo zinaongozwa na wajanja wachache wenye kujita miungu watu. Ukifuatilia kwa ukaribu sehemu Magufuli amegusa ni sehemu nyeti zenye watu wenye mtandao mrefu sana, Tuli comment posts za nyuma kwamba Dawa ya Mtu mjanja mwenye kutumia migongo ya watu wengine kufanya biashara zake na ufisadi wake ni Kwenda kufunga na kubana zile sehemu anazofanyiwa biashara zake ili mwisho wa siku ajitokeze yeye mwenyewe akiwa mchovu. Ukianza kumfuata Ridhiwani na kumwambia ana husika kwenye biashara za mafuta na ukataka kumtia hatiani unaweza ukajikuta unapoteza fedha za serikali kama kwa kina Mramba. Bana pale kwenye vile vitega uchumi vyao maana pale una uhakika wa kuvi control. Baada ya hapo ina kuwa rahisi kutumbua vijipu vidogo vidogo huko kuliko baki kama alivyo jaribu kueleza Mwanakijiji. Wizara ya ujenzi anaifahamu na huenda anaivutia kasi. Tumpe muda kama alivyo sema MMM. Japo na najua anacho fanya hapa ni kumsifia Rais ili na akumbukwe pasipo kufikiria kwamba na yeye ni mtu wa jana . Si dhambi lakini.
 
Hii nchi ilikuwa imeoza kabisa.

Na huu uozo ambao sasa unaanza kujitokeza ni indictment kubwa sana dhidi ya CCM na serikali zake.

Wasiwasi wangu ni kuna watu ambao ndo wamechangia kuuleta huo uozo lakini hawataguswa kabisa.

Uozo huu mkiweka katika matokeo ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar ndio network zenu zinakata kabisa, lakini ikiwa ni Bandari Dar zinarudi bar zote zinasoma. Jecha akiwaambia kulikuwa kuna hitilafu na kufuta uchaguzi Zanzibar mnasimamia vidole gumba yaani acheni watumbua majipu watumbue kokote yalipo hata kama yamekaa vibaya achene yatumbuliwe tu.
 
Kutumbua jipu pekee hakutoshi, bali atoe kabisa kiini. Maana kutumbua jipu bila kutoa kiini nikupoteza muda.
 
Mimi huko kwenye vyama nishatoka.

Haijalishi ni nani anasafisha huo uozo.

Kikubwa kinachoogopesha zaidi ni kuona ni jinsi gani ambavyo tulikaribia kuwa 'a failed state'.

Inavyoonekana ni kana kwamba kila mtu mwenye mamlaka fulani alikuwa anajifanyia tu mambo atakavyo utadhani hakuna serikali na dola.

Tunapenda kujisifia kuwa sijui tuna amani na blah blah zingine kama hizo....hiyo amani ina faida gani kama nchi ilikuwa imeoza hivi?

Shaking my head!!!!
Nsumba ntale! Unaweza ku trade uozo kwa amani?
 
Hii in hofu ya kweli; na ni kweli haya yote ni mashtaka yasiyopingika dhidi ya utawala wa CCM. Ubaya ni kuwa badala ya wapinzani ambao tulitarajia wangekuja na kusafisha leo wanaosafisha ni wana CCM wenyewe...
Mkuu, ulitaka Mbowe ndio akahoji mita za mafuta wakati hao uliowaita 'wambeya' wanawajibika kutoa taarifa za kimbea serikalini? Wapinzani watawalipa nini mashushushu wakati hawakusanyi kodi?
 
Inawezekana uko sahihi sana mzee mwenzangu; lakini ukiniuliza mimi kati ya 'mabadiliko yale' ya kuzungusha mikono yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja na haya tunayoyashuhudia ya wanamuziki wale wale; nitayachukua haya any day of the week. La maana kwangu ni kuzidi kuyasukumiza mabadiliko haya na kuhakikisha tunaendelea kuwakalia mgongoni viongozi hawa ili wasituangushe. Hata kubadili mifumo; huwezi kubadili hivi hivi; you deal with people.. sioni ni kwa namna gani kwa mfano Lowassa angebadili mifumo zaidi ya anavyofanya Magufuli; kwangu, Magufu ameanza sahihi kabisa. you deal with corrupt elements within the system as you continue revamping the system. Kama gari ni bovu na dereva mbovu; vitu vya kanza ni deal na dereva mbovu kwanza... you can always fix the car.
Mzee mwenzangu, hapa utakuwa umetoka katika mstari kidogo
Siku zote ninapambana na vijana wanaokushambulia au ku'invoke' hoja nje ya mada zako. Husema hivi'shambulieni mada'

Katika bandiko lako moja umeeleza umuhimu wa kuwa na chombo kama FBI.

Hukusema hayo kwasababu ya Magufuli, CCM au Wapinzani. Umesema kwa maana ya Taifa kwanza.
Na kama hoja yako itafaniwa kazi nadhani ni tija kubwa kwa Taifa. Hivyo, tuweke Taifa mbele kabla ya watu au vyama

Nadhani unakumbu kumbu za kupinga mabadiliko ya upinzani kuchukua watu wale wale.
Ulinitia moyo sana niliposimama kidete hata pale umma ulipokuwa unasombwa kwenda eneo jingine.

Nilisimama katika jangwa nikipigwa na upepo mkali wenye dhoruba ya mchanga kisa nilisema la 'UKAWA' kuchukua wale wale sikubaliani nalo. Kumbu kumbu zipo, lakini pia nilisema CCM kukaa pembeni ndiyo mwanzo wa hatua mpya

Kuhusu mfumo, hili nimeliongea hata kabla ya UKAWA. Nilileleza katika uzi mrefu sana wa Katiba.

Kwa bahati nzuri wapo walioona hoja ya mfumo, wakaichukua ! hakuna tatizo kwa hilo iwe UKAWA au Magufuli na wala sihitaji hata kuwa 'mentioned' kwasababu niliandika kwa faida ya Taifa na kama anavyosema Mohamed Said ''elimu ni dhamana'' mwenyewe akitaka unampa

Nipo katika rekodi nikisema mabadiliko yatotokea pale tu CCM itakapokaa pembeni, bila kujali ni Dovutwa au Mama Anna Mghwirwa au mwingine aliyepo madarakani.

Leo tunasafisha uchafu wenzetu wakichanja mbuga. Uchafu uliosababishwa na hao hao wanao uona leo

Magufuli alikuwepo miaka 20, katibu mwenezi/waziri walitueleza mambo mazuri chama/serikali kidedea kuwaletea maendeleo wananchi. Hao hao wanarudi kutuambia tulikuwa 'porini' Hii ni 'castle in the sky'

Serikali iliyoundwa imejaza wale wale walioachia mafuta yapimwe kwa vijiti au macho ya wanadamu

Na katika kuhakikisha tunarudi jana, wanavujisha hata siri za kukamata wezi.
Hoja ni rahisi, unawezaje kupata quality product kutoka recycled material?

Na hao 'recycled material' ndio walivuruga katiba, bado tuna amini watabadilisha hali tofauti na kile dhamira yao inachowatuma, kubaki na jana.

Hatuwezi kuwasha tochi usiku tukasema ni leo kwasababu kuna mwanga' false hope'

Na hapa niseme, as long as CCM na genge zima la 'wahujumu' wanaongoza hili taifa, mengine ni hadithi

Hivi kwanini ni ''taboo'' kuzungumzia 'felia' ikiwa tunaziona na tunaishi nazo?

Kiongozi aliyesema nchi ina maendeleo sana mwezi wa 10 2015 halafu mwezi wa kwanza 2016 anasema tumefika pabaya, inakupa picha gani? Hivi huyu si felia kweli, na kwanini anapewa fursa ya kuendeleza felia nasi tukishangilia ?

Hatuwezi kulisaidia taifa kama hatutasimama kuhesabiwa tukisema 'this is right , that is wrong'
 
Nadhani hata Magufuli kaisoma vizuri post yako hii. Japo pia kwa kiasi fulani Rais pamoja na Waziri mkuu wameonyesha angalau ile hali ya kujaribu. Hisia zangu kwa sasa huenda Rais anajaribu kushughulikia zile sehemu ngumu ambazo zinaongozwa na wajanja wachache wenye kujita miungu watu. Ukifuatilia kwa ukaribu sehemu Magufuli amegusa ni sehemu nyeti zenye watu wenye mtandao mrefu sana, Tuli comment posts za nyuma kwamba Dawa ya Mtu mjanja mwenye kutumia migongo ya watu wengine kufanya biashara zake na ufisadi wake ni Kwenda kufunga na kubana zile sehemu anazofanyiwa biashara zake ili mwisho wa siku ajitokeze yeye mwenyewe akiwa mchovu. Ukianza kumfuata Ridhiwani na kumwambia ana husika kwenye biashara za mafuta na ukataka kumtia hatiani unaweza ukajikuta unapoteza fedha za serikali kama kwa kina Mramba. Bana pale kwenye vile vitega uchumi vyao maana pale una uhakika wa kuvi control. Baada ya hapo ina kuwa rahisi kutumbua vijipu vidogo vidogo huko kuliko baki kama alivyo jaribu kueleza Mwanakijiji. Wizara ya ujenzi anaifahamu na huenda anaivutia kasi. Tumpe muda kama alivyo sema MMM. Japo na najua anacho fanya hapa ni kumsifia Rais ili na akumbukwe pasipo kufikiria kwamba na yeye ni mtu wa jana . Si dhambi lakini.
Swali ni je? Kama ya ujenzi yalitokea angali waziri ilikuaje asishughulikie?

Bottom line: sina nia ya kukatisha tamaa ila niseme kweli i cant see the clear picture ktk hili!!!
 
Hii nchi ilikuwa imeoza kabisa.

Na huu uozo ambao sasa unaanza kujitokeza ni indictment kubwa sana dhidi ya CCM na serikali zake.

Wasiwasi wangu ni kuna watu ambao ndo wamechangia kuuleta huo uozo lakini hawataguswa kabisa.
Rais Magufuli ajue kuwa watanzania watampima kwa hili! Hapaswi kuwa na double standard! Shoka la Magufuli litumbue hili jipu la aina yake la WAZIRI wake kumhujumu WAZIRI MKUU kwa kumtonya mhusika kuhusu ujio wa kushtukiza wa Majaliwa!
Napendekeza amtumbue WAZIRI wake nasikia ni profeso mkweli ndani ya masaa 24 mbele ya waandishi wa habari!
 
Hivi huwezi kuongea au kujenga hoja zako bila kuihusisha na CCM au CHADEMA? Mbona unaonesha fikra ndogo mbele ya hadhara?
Vipi mmeshakumbukwa? JK anaacha kusisitiza madaktari na watu muhimu wakumbukwe anawashadadia hopeless creatures kama nyie!!!
 
Hahaaaa one man army!

Ila nchi imeharibika hii....daaah.

Your point bado ni strong!!

Trust me hakuna one man army!! Hakuna nchi inajengwa na mtu mmoja!!

Unaweza tofautisha vipi vionjo hivi na vya mwanzoni mwa utawala wa mwinyi... mkapa na JK mwisho ulikuwaje?

Mwinyi alionekana hopeless mbele ya Mkapa na Mkapa alionekana so hopeless mbele ya JK kiasi cha kufikia kuzomewa na kususia kabisa sherehe au dhifa za hadhara.....

Yanayoendelea leo ni yale yale japo wanajitahidi sana kupika matukio!!!

Na the way huyu bwana anavyopenda sifa sana anajitahidi kuwa one man army lkn ndio msingi mkuu wa failure yake.
 
inaonekana unaniona kila sehemu; sifuti mada yoyote hapa JF, sina uwezo huo na sijawahi kuomba mtu yeyote afute mada. I don't really care much mtu akishindwa hoja akianza kuleta vihoja.

Post zangu nyingi tu unafuta mkuu... huko nyuma ulinipa sana ban but try kuwa fair mkuu....

Btw kuna hoja imeshindwa hapa?
 
Ina maana huu uozo umeanzia wakati wa Kikwete?

Nasita kuamini aisee....
Hata kama haukuanzia kwake, hakuonyesha nia ya dhati ya kuupiga vita, hivyo kutia wasiwasi! Kilichofanywa na Magufuli kwa Siku 100, hakikuwahi kujaribiwa na mtangulizi wake katika miaka 10!
 
Kuna wana ccm waliochukulia hilo swala la Waziri kutuma SMS kama jambo la kitoto na kuishia kulitetea kwa Nguvu zote na pia Muhongo katoa taarifa kama Manyerere alivyolifikisha hapa jukwaani kwamba hilo swala halina uhusiano na wizara yake

Magufuli alikua sahihi alipomwambia Jk pale Lumumba siku alipokabidhiwa cheti cha ushindi kwamba ccm wamejaa wanafki
Nahisi Profesa Mkweli halikuwa chaguo la Magufuli! Ni kati ya mawaziri waliobebwa na chama twawala na Magufuli kushinikizwa awaweke kwenye baraza lake ikiwa ni pamoja na Mr. February!
Ni hisia zangu anyway!
 
Hii nchi ilikuwa imeoza kabisa.

Na huu uozo ambao sasa unaanza kujitokeza ni indictment kubwa sana dhidi ya CCM na serikali zake.

Wasiwasi wangu ni kuna watu ambao ndo wamechangia kuuleta huo uozo lakini hawataguswa kabisa.
Nami nasikitika dagaa watakuwa kondoo wa kafara wakati kambale hawata guswa.
Kama kweli jpm ana nia ya dhati kuinyoosha nchi hii aache mchezo wa kuwawajibisha dagaa
 
Kama ulivyoainisha, old/bad habits die hard... tulifikia pabaya sana..people commited crime with impunity!
Overhauling culture/utamaduni mzima wa corruption si kitu ya siku moja na Magufuli pekeyake hawezi...anahitaji msaada wetu sote... when it comes to fighting corruption, everyone is a stakeholder.
Exactly!
Watu wanataka misingi ya usafi isimamiwe, Ila sio na wao na Magufuli na Majaliwa! Wanataka watu waguswe Ila sio wao ni wale waliokuwa kwa wapinzani wao! Akitajwa mgombea wao wanasema kama mnaushahidi mkamateni, wakishughulikiwa mnasema ccm wanataka kuua upinzani!
So if we think sheria ni msumeno and we want nothing but usafi then tusiingilie mamlaka zinapotaka kutenda wajibu wake!
 
Back
Top Bottom