Wanaohama kwenye vyama wapokelewe kwa tahadhari

CCM ilipofika, hata aje raisi ,safi vipi ni vigumu kusafishaka, inawezekana rais wa sasa akawa na mawazo mazuri lakini mfumo wa utawala ndani ni mbovu, ndio wananchi watachagua chama mbadala
 
Ndugu wana JF,

Kila anayefuatilia siasa za hapa nyumbani anajua nchi yetu inapitia kwenye mageuzi makubwa ya kisiasa huku CCM ikiangamia, CHADEMA wao wanashamili kwa afya. Kwa sasa Chadema wamekuwa wakivuna wanachama toka CCM, binafsi jambo hili sio zuri kwa chama kinachotaka kuleta mageuzi ya kweli, hizi ndo sababu zangu kwa nini naanza kuona mwisho mbaya kwa CHADEMA:

1. Itashindwa kudhibiti hawa watu wanaokimbilia maana ni watu ambao haijawalea, ni sawa na kuchukua mtoto aliyekulia malezi ya wazazi wengine ukataka kumlea wewe, atakusumbua sana sana. Chadema wameweza kuwazibiti kina Zito, Mnyika na wengine kwa sababu wamewalea tokea utoto wao wa kisiasa.

2. Italeta chuki kwa wanachama ndani ya Chadema ambao wapo muda mrefu maana wengi wa wanaohamia wanataka nafasi za uongozi mfano kugombea ubunge, wale walikitumia chama kwa muda mrefu wanaachwa, hii ni hatari kubwa.

3. Harufu ya U-CCM haijaondoka kwa hawa wanaohamia, mimi naamini mabadiliko ya kweli yatapatikana kwa kuanza upya na watu wapya wasiokuwa na harufu ya enzi tunazozichukia, hawa wahamiaji wana damu za CCM, wana mitandao yao bado inayowaunganisha. Huwezi kushona nguo mpya ukawa unaiwekea viraka vya nguo ya zamani iliyozeeka.

4. Chadema kwa kupokea wakimbizi toka CCM itaonekana haina tofauti kabisa na CCM maana watu ni wale wale ila wamekuja upande wa pili na kubadili mavazi yao tu.

Mwisho nawashauri CHADEMA wawapokee hawa wakimbizi toka CCM ila isiwapatie uongozi bali wawe wanachama wa kawaida na waanzie ngazi za chini kama ilivyo kwa watu wengine wa chini ndani ya chama na si leo tu kahamia kesho anagombea ubunge, kama Chadema wataendelea na tabia hii, basi mie nasema wajiandae kwa kifo cha kisiasa, wao eti wanasema wanapokea watu safi tu kutoka CCM, wanajidanganya sana, haitachukua muda kabla hatujaanza kuona mwisho wa CHADEMA.

Nawasilisha.

Kiongozi Mbona CUF na NCCR wamekufa? inamaana na walifanya hivyo...

Tunahitaji watu kutoka kwenye system kuja kuwa wanachama wa kawaida ili kuwatoa hawa magamba
 
Ndugu wana JF,

Kila anayefuatilia siasa za hapa nyumbani anajua nchi yetu inapitia kwenye mageuzi makubwa ya kisiasa huku CCM ikiangamia, CHADEMA wao wanashamili kwa afya. Kwa sasa Chadema wamekuwa wakivuna wanachama toka CCM, binafsi jambo hili sio zuri kwa chama kinachotaka kuleta mageuzi ya kweli, hizi ndo sababu zangu kwa nini naanza kuona mwisho mbaya kwa CHADEMA:

1. Itashindwa kudhibiti hawa watu wanaokimbilia maana ni watu ambao haijawalea, ni sawa na kuchukua mtoto aliyekulia malezi ya wazazi wengine ukataka kumlea wewe, atakusumbua sana sana. Chadema wameweza kuwazibiti kina Zito, Mnyika na wengine kwa sababu wamewalea tokea utoto wao wa kisiasa.

2. Italeta chuki kwa wanachama ndani ya Chadema ambao wapo muda mrefu maana wengi wa wanaohamia wanataka nafasi za uongozi mfano kugombea ubunge, wale walikitumia chama kwa muda mrefu wanaachwa, hii ni hatari kubwa.

3. Harufu ya U-CCM haijaondoka kwa hawa wanaohamia, mimi naamini mabadiliko ya kweli yatapatikana kwa kuanza upya na watu wapya wasiokuwa na harufu ya enzi tunazozichukia, hawa wahamiaji wana damu za CCM, wana mitandao yao bado inayowaunganisha. Huwezi kushona nguo mpya ukawa unaiwekea viraka vya nguo ya zamani iliyozeeka.

4. Chadema kwa kupokea wakimbizi toka CCM itaonekana haina tofauti kabisa na CCM maana watu ni wale wale ila wamekuja upande wa pili na kubadili mavazi yao tu.

Mwisho nawashauri CHADEMA wawapokee hawa wakimbizi toka CCM ila isiwapatie uongozi bali wawe wanachama wa kawaida na waanzie ngazi za chini kama ilivyo kwa watu wengine wa chini ndani ya chama na si leo tu kahamia kesho anagombea ubunge, kama Chadema wataendelea na tabia hii, basi mie nasema wajiandae kwa kifo cha kisiasa, wao eti wanasema wanapokea watu safi tu kutoka CCM, wanajidanganya sana, haitachukua muda kabla hatujaanza kuona mwisho wa CHADEMA.

Nawasilisha.
Acha ngonjera zisizo na mantiki wewe mwanzoni unaonyesha wazi hukutaka hao "wageni" wapokelewe mwishoni "wawapokee lakini wasipate vyeo. CDM ni Gwiji la kisiasa TZ na Africa huwezi kutoa utabiri wa ajabu kama huu.
Ninahisi wewe ni Gamba unayetapata hujui uende wapi wakati nyumba inaanguka. Unaifahamu Historia ya mageuzi Kenya? Wote waliopo sasa walitokana na mfumo wa KANU. Unakumbuka wakati makamu wa Rais wa Moi, Prof George Saitoti alipokimbia na kujiunga NARC? Wapo watu ndani ya CCM haupendi mfumo na CCM yenyewe wapo wapo tu!! Wanatafuta upenyo sasa wameona washindi ni CDM waache waende! Unakumbuka Mkapa alivyomkumbatia wakili maarufu na mpinzani wa kutisha Dr Masumbuko Lamwai alipoenda magamba?
Wapo akina Tambwe Hiza na wengineo USIPOTOSHE WEWE!!
 
hapana nia ya chama chochote ni kutoa sera na watu wakaziamini na kuhamia kwako so wanaohamia chadema ni waliojitambua na kuona ndio njia sahihi so haina madhara kwa chama zaidi ya kujijenga isipokua ndio maana hawaingiii straight na kupewa uongozi wa juu mpaka watapoonyesha uwezo wa nguvu!
 
Dr. Slaa alitoka CCM
Shibuda alitoka CCM
Professor Kahigi alitoka CCM
Wanachama wengi wenye umri wa miaka zaidi ya 40 walikuwa CCM.

Si vibaya kuwapokea wanaotoka CCM. Si uungwana kuwakataa ingawa kuna ukweli kuwa si wote watakao kuwa wema. Kuwapokea wanaotoka CCM nao ni mkakati sahihi kabisa wa kuinyong'onesha.

Watajitutumua kuwaponda (mara oh ni mafisadi) lakini mwisho wa siku ukweli utabaki palepale kuwa inawauma. La muhimu tujihadhari kutowaingiza wageni vyumbani kwetu haraka.
 
Tutajie ufisadi wa walio hamia Chadema...

Mkuu iko wazi kuwa Millya ni mtu wa Lowassa? Sina lengo baya na CDM ninachotoa hapa ni angalizo. Ukicheck wall za Nape FB zote anatamba kuwa mkakati wao wa kujivua gamba unafanikiwa. Kama hivyo ndivyo, CDM itakuwa inapokea magamba kutoka CCM kitu ambacho kitakifanya CDM kibebe tuhuma za ufisadi za CCM.

Hivi pata picha EL, RA na kambi zao wahamie CDM nini kitatokea? CDM si ndiyo itakuwa chama cha Magamba na kilichobeba watuhumiwa wa Ufisadi?

Always CCM wamekuwa wakiiba ajenda za CDM, walianza na vita dhidi ya ufisadi kwa kuunda kundi la Wapambanaji (Sitta, Sendeka, Mwakyembe nk), wakahamia kwenye ajenda ya katiba (wameiteka), sasa ni muda wa kuiwin ajenda ya mapambano dhidi ya ufisadi. CDM itajengewa taswira ya kuwa chama cha mafisadi na CCM watalitangaza hilo.

Provided kuwa, kuna tetesi za EL kuachia nafasi zake zote ndani ya CCM ni suala la kusubiri tu.

Kati ya mambo ambayo sisi wana mageuzi tunataka kuona CDM inatake serious ni zoezi la kupokea wafuasi kutoka kambi ya RA na EL. Lazima umakini utawale na intelligence ya chama isimame kweli ijue in and out. Tukicheza
 
Kweli,cha muhimu ni KUFUATA kanuni za CHADEMA,lakini under DR.WILLBROD SLAA wamechemka mapema mno watastukiwa,wamuulize Shibuda ambaye anabye time kidogo waachane naye. MUHIMU NI MBOWE,ARFI,DR.SLAA,ZITTO NA NAMAKAMANDA WA UKWELI WAPOKEENI MAANA NI HAKI YAO KUJIUNGA CHADEMA,LAKINI KUWENI MAKINI HASA WASIJE WAKAWAKUTA VIJANA HALISI WA CHADEMA AFU MKAANZA KUWAPUUZA,HAPO ITAKUWA NI MBAYA SANA.WAJE LAKINI WAHESHIMU CHAMA NA MUWAANGALIE MIENENDO YAO MAANA WANAMARAFIKI MAFISADI WATOKAKO NA HATA WAO WANA ELEMENT HIZO MSIPOWAZIBITI. WATAWEZA KUSEMA KWELI "SISI TUNA MUNGU WAO WANA PESA" AU NDO WANATAKA KUGEUZA KAULI WAKIJA CHADEMA. WACHUNGUZWE KWA MAKINI SANA.

Offcoure kadri wanachama wengi na majembe yatakavyo jiunga chamani ndivyo ubingwa wa waratibu mfumo wa chama wa kutoa ajira kwa watu wake utakavyojidhihirisha na hatimaye kuuridhisha umma kwamba 2015 CDM ITAWEZA KUUNDA DOLA IMARA.CHA MSINGI IFIKAPO 2014 CDM IFUNGIE MAGAMBA WATAKAO CHELEWA KUJIUNGA MAPEMA,WAACHE MADARAKA YAO NDANI YA MAGAMBA SASA AU 2013 ILI TUWAAMINI.TUNATAKA MTU KUTOKA MAGAMBANI ASAFISHWE ANGALAU MIAKA 2 NDANI YA CDM,NDIYO MAANA NAPENDEKEZA CDM ILIONE HILI.
 
Ni angalizo zuri, nakupongeza. Ila CDM na wapenda mabadiliko wote hawa tuwaangalie vizuri, fikiria tungekuwa na Shibudas kama 10 hivi CDM ingesalimika? Iwe iwavyo hao wageni wote wanaoingia wapewe majukumu kukijenga chama kwenye maeneo wanayokubalika, ikiwa ni kupeleka elimu ya uraia ambayo syllabus yake inaandaliwa na CDM wenyewe wakafundishe tu, ili hata kama wakiamua kusaliti tayari watakuwa wameshaelimisha vyakutosha na hawawezi kuondoka na raia atakayekuiwa amehitimu vema
 
nashauri WAPOKELEWE LAKINI WASIPEME NAFASI YA KUGOMBEA CHOCHOTE wala UONGOZI WOWOTE NDANI YA CHAMA kwa muda.
 
Binafsi sina shaka na wanaohamia chadema toka ccm kwa wameshaisoma katiba ya chadema na kuielewa pia dira ya chama kama wamekurupuka kuhamia chadema basi siku zao ndani ya chama zinahesabika kwani nawajua viongozi wa chadema ni watu makini sana chini ya uongozi wa mtu makini Dr wa ukweli sio wa zali kama wa jamaa fulani Dr slaa.
 
CHADEMA ni Alfa na Omega ktk mapinduzi ya siasa ya kweli ktk kupigania haki za walipa kodi, Na bado, 2015 ndo hasa gharika kuu la CCM, Yanayotokea Arusha na maeneo mengine ni mvua za rasharasha. Its total M4C

Matatizo ya kushabikia siasa kutoka Makanisani. Matokeo yake ndiyo hayo ya harufu kameguka.
 
Habari za usiku huu wana Jf. Inawezekana baadhi ya wana-CHADEMA watakuwa wanafurahia kitendo cha viongozi wa CCM kuanza kuhamia CDM. Katika hali ya kawaida hii ni dalili ya ushindi kwa CDM, lkn pamoja na mtazamo huo, hebu tujiulize; hivi kwanini iwe sasahivi? Zamani walikuwa wapi? CDM sio chama pekee cha kisiasa, kwanini waje CDM tu na sio vyama vingine? Kwa mtazamo wangu majibu juu ya maswali haya naweza kuyaweka makundi mawili. (I) "Mfa Maji Hakosi Kutapatapa". CCM ni kama jahazi linalozama. CDM inakuja juu, kwa hiyo hao akina Miliya wameshtuka mapema, na sasa wanaangalia ulaji unakoelekea kuangukia (in this case ulaji unaelekea CDM). (II) Labda kuna njama ya kuihujumu CDM, naomba tuwe makini sana na hili, nimesoma humu jamvini kuwa inawezekana kwamba eti EL yuko mbioni kutinga CDM. Tutafika kweli, au ndio tutakuwa tunarudi tunakotoka...??
 
Something is not right about all these CCM people who are defecting to our CHADEMA side. WE SHOULD BE CAREFUL THAT THEY DONT FINISH OUR PARTY FROM WITHIN. Tuwakaribishe ila tuwe macho. # Airing My Thoughts
 
Something is not right about all these CCM people who are defecting to our CHADEMA side. WE SHOULD BE CAREFUL SO THEY DONT FINISH OUR PARTY FROM WITHIN. Tuwakaribishe ila tuwe macho. # Airing My Thoughts
 
Ingawa wengi wanafurahishwa na CCM kupoteza mvuto na kukimbiwa na makada wake wakubwa kwa wadogo, nafikiri pia ni muhimu CHADEMA wakawa makini. Wasikubali kupokea GAMBA lolote ambalo lina tuhuma au limehusishwa na uporaji wa rasilimali za nchi yetu. Hata kama ni maarufu kupindukia, CHADEMA wasimpokee kwa kigezo cha umaarufu wake bali kwa misingi na maadili ya uongozi atakayokuwa anayasimamia. Ikiwezekana kuwepo na utaratibu maalumu wa kuwapiga msasa wanachama wanaohama kutoka huko kwa MAGAMBA. CHADEMA kama chama kimejijenga na kufikia hapo kilipo bila kutegemea majina makubwa ya wanasiasa uchwara wanaotoka chama tawala. Wengi wetu tulikuwa hatuwajui akina Mbowe, Slaa, Zitto au Mnyika lakini leo hii wameweza kujijingea heshima ndani na nje ya chama hivyo kusiwe na mhemko wa kuwapokea wanachama wasiokuwa na sifa zinazotakiwa kujiunga na CHADEMA! Naamini mzee Slaa na akina Kabwe mko humu hivyo fuatilieni hoja zinazotolewa humu na kuzifanyia kazi ipasavyo!
 
Chadema ndo chama ambacho kimeibukia kupata umaarufu sana, na kumekuwa na wimbi kubwa sana la wanachama wa vyama mbali mbali kuvihama vyama vyao ama kwa hiari au kutimuliwa na kukimbilia cdm hasa hasa ccm. Watu hawa ni wa aina tofauti tofauti, wasafi kwa wachafu, na wengi wao ndo tabia walizo nazo, na kama wahenga wasemavyo 'tabia ni kama ngozi' ni ngumu kuivua.

Wasi wasi wangu ni kuhusu chama cha chadema kuwadhibiti hawa watu ki mienendo na kitabia, kwa mfano, wapo ambao watatimuliwa ccm wakiwa ni mafisadi, na kuamua kuhamia chadema.

kwa kuwa watakuwa wengi wanaweza kuambukiza tabia zao walio wasafi, au kupata nyadhifa mbali mbali, na siku waamue kukitikisa chama kwa kuamua kupindisha ukweli kisa wingi wao.

au huenda kwa kuwa ni wageni wakaamua kuficha makucha, ila wakiwa wenyeji, na hiyo siku itakayowadia nayo chadema ikishika hatamu (dola) nao wakapewa nyadhifa mbali mbali, serikalini, nao wakaona huo ndiyo wakati muafaka kuonesha makucha yao na kuendeleza tabia walizo kuwa nazo.

Je chadema wamejiandaaje na changamoto hizi na zaidi ya hizi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom