Wanaohama CCM ni vinyago - NAPE

Akisema Lema huyo nabii.
Akisema Nape huyo Maiti.

Du! msifikiri wtz hawasikii.
 
Si busara kwa mwanasiasa yeyote yule kutukana wapiga kura. Kwa namna hiyo, hata wale ambao ni wanachama wanaweza kukerwa na matusi ya mwanasiasa huyo na kuamua kukiacha chama.

Si ndio hapo sasa.

Huyu bwana anajionyesha ambavyo hajakomaa kisiasa.
 
Sasa kama wanaotoka ccm na kwenda vyama vingine hawana madhara kwa nini ana watusi kwa kuwaita majina ya ajabu?
Nnauye Jr hebu acha mipasho.
Laiti ningekuwa wewe ningewaasa wanaoma wawe makini na kuwaambia kuwa milango iko wazi kama hawataridhishwa na sera na mienendo ya huko walipohamia.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Akisema Lema huyo nabii.
Akisema Nape huyo Maiti.

Du! msifikiri wtz hawasikii.

A reasonable man judged by his act.
Kama umefanya tukio la kipuuzi utaitwa mpuuzi, na ukifanya tukio la kishujaa utaitwa shujaa.
Kuna tatizo hapo??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu huyo jamaa yupo kazini kuibomoa CCM,uchaguzi mkuu ukikaribia anasepa na wenzake wa CCJ. Huoni walivyo busy kuonyesha ambavyo ni wao tu ndiyo watetezi wa Watanzania?
Si busara kwa mwanasiasa yeyote yule kutukana wapiga kura. Kwa namna hiyo, hata wale ambao ni wanachama wanaweza kukerwa na matusi ya mwanasiasa huyo na kuamua kukiacha chama.
 
Nape akiwa Makambako leo kwenye mkutano wa hadhara amesema kwamba waanzilishi wote na viongozi wote wa vyama vya upinzani akiilenga CDMA kwa wote wametokea CCM, hivyo CCM haitishwi na kinyago ilichokichonga chenyewe!!!!
 
Nikweli ccm ni chama kikongwe kwa umri,kwani toka uhuru hadi leo lakini MH.NAPE mbona kimeshindwa kazi,mfano;Mwalimu alikuwa anapambana na ujinga,maradhi na umasikini lakini hadi leo hamna kupungua chazaidi ni kuongezeka,sasa HM.NAPE unalalamika kuhusu ufisadi mbona mafisadi kwenye kikao mnao,mikutano yenu mnao,kabla ya kupendekeza kuhusu sheria za mahakama anzeni kwenye chama kwanza maana mlisema ktk ccm huruhusiwi kupokea wala kutoa rushwa mbona wanatoa na kupokea hamchukuwi hatua,unakimbilia sheria za mahakama za nini? kama wanachama wanavunja kanuni za chama hatua hazichukuliwi,acha maneno utakujakujuta baadae MH anza kuwa makini hiki ni kizazi cha digital mambo yako wazi wazi utaumbuka.
 
Mimi kama mwanachama wa CCM ambae nilikuwa na imani sana na Nape hapo awali nimeanza kukatishwa tamaa na kiongozi huyu. Hapo awali nilikuwa sikubaliani na kauli za baadhi ya wanachama wenzangu wa CCM kwamba Nape anakiharibu chama. Lakini taratibu naanza kuona mashiko ya hoja hii yapo wapi, ingawa bado nina amini pia kwamba baadhi ya viongozi wa CCM wanao toa kauli hizo dhidi ya Nape nao ni mzigo na tishio kubwa kwa uhai wa CCM katika zama hizi za ushindani wa kisiasa. Nimeanza kuhisi kwamba Nape ameanza kupwaya katika medani za siasa, hasa katika nafasi yake ambayo viongozi wenzake kama John Mnyika wanaimudu kwa ustadi mkubwa sana. Nape anahitaji ajenge uwezo wa kushindana kwa hoja na vijana wenzake wenye nafasi kama yake, mfano John Mnyika wa Chadema. Vinginevyo, CCM itapoteza vijana wengi ambao awali walimiminika CCM kwa imani kwamba Nape atasaidia kukirudisha chama katika mstari katika nyakati hizi za siasa za ushindani.

Kwa kweli kauli kama hizi kutoka kwa Nape ni za kutuvunja sana moyo sisi vijana wenzake ndani ya chama ambao kwa muda mrefu tuliamini kabisa kwamba Nape ni hazina ya chama chetu na ni moja ya sababu za msingi kwanini tunaendelea kubaki ndani ya CCM pamoja na chama kuwa ‘out of touch' na wananchi katika maeneo ya itikadi, dira, maadili ya uongozi na mikakati ya kutatua kero za mbalimbali za wananchi. Matumaini yetu ya awali kwamba mtu kama Nape ndiye atakayeweza kusaidia chama chetu cha CCM kirudi katika mstari yanaanza kuingia shaka kubwa.

Jambo lingine muhimu kulisema hapa pia ni kwamba kwa mtindo huu, wengi wetu taratibu tunaanza kuona kwamba hoja kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM kwamba Nape anakiua chama ni hoja zenye mashiko kwa namna fulani, pamoja na kwamba baadhi ya viongozi wanaotoa kauli hizo nao ni mzigo kwa CCM. Vile vile kauli kama hizi zinatufanya tuanze kuamini kwamba kumbe hoja kwamba Mwenyekiti wa CCM – Kikwete anaangushwa na wasaidizi na washauri wake, ni hoja zenye mashiko. Kwa mfano, Kikwete alitoa kauli ya kiungwana sana kama njia ya kujibu mapigo kutokana na wana ccm wengi kuhamia Chadema: Kikwete alitamka kwamba "wanaotaka kuhama CCM wahame".

Kauli ya Kikwete ni sahihi kabisa kutoka kwa kiongozi wa chama chochote cha siasa kwani katika mazingira ya demokrasia ya vyama vingi, njia pekee ya kujibu mapigo kama haya ni aidha kuja na mikakati ya kupunguza kasi ya wanachama kuhama au kuweka wazi kwamba wanachama kuhama ni haki yao ya msingi, hakuna wa kuwazuia. Na misimamo kama hii inaweza kutolewa na kiongozi katika mazingira yoyote ya demokrasia, hata katika nchi zilizokomaa kisiasa na kidemokrasia. Lakini kitendo cha Nape kuita wanaohama CCM kwamba ni vinyago ni ushahidi tosha kwamba Kikwete anaangushwa na wasaidizi wake/watendaji kwani, wakati Kikwete anatoa kauli y akuheshimu maamuzi ya wanachama wanaotumia haki yao kuhama CCM, wasaidizi wake kama Nape wao wanaenda mbali zaidi na kuwaita wanaohama CCM kwamba ni vinyago. Hii ni ishara kwamba Nape anaanza kupoteza sifa za kiongozi bora na badala yake anaanza kujijengea sifa za bora kiongozi.

Katika mazingira ya siasa, matumizi ya neno ‘vinyago' hayana tofauti kubwa na matumizi ya neno ‘wapambe'. Matumizi ya neno Wapambe (hence vinyago) yapo more relevant katika kuelezea aina ya wanasiasa kuliko aina ya wanachama. Nadhani wengi wenu mtakubaliana nami kwamba katika sababu kubwa juu ya kwanini wanachama wengi wa CCM wanahamia Chadema, "upambe" sio moja ya sababu hizo. Kuwaita wapambe/vinyago wanachama wa CCM wanaotumia haki yao ya msingi kuhamia chama wanachoona ni cha matumaini – Chadema ni dalili za kuishiwa hoja. Vile vile nadhani wengi wenu mtakubaliana nami kwamba ni jambo lililo wazi kwamba wanasiasa wanaotoa kauli za ovyo ovyo kama hizi katika mazingira na matukio ambayo wangeweza kuyafanyia kazi kimya kimya, wao ndio wanaoonyesha kila dalili ya upambe au kuwa vinyago kwa maana moja tu kubwa kwamba – kazi ya msingi ya vinyago au wapambe ni ku ‘amuse'. Kwa hiyo wanasiasa vinyago au wapambe ndani ya CCM, kazi yao kubwa ni kuwa ‘amuse' wanasiasa waliowaweka madarakani ili waendelee kukidhi mahitaji yao binafsi. Uzuri ni kwamba tumeshaona jinsi gani baadhi ya mawaziri waliofukuzwa hivi majuzi – wakati bado wapo madarakani, walikuwa wanatoa kauli kama hizi za upambe na ukinyago, lakini baada ya kumwaga unga, kauli na misimamo yao imebadilika kabisa.

Hii aina maana kwamba Nape hana nafasi na muda wa kujirekebisha, vinginevyo kwa maslahi ya Chama changu cha CCM, nitaendelea kusema ukweli daima kwani fitina kwangu mwiko. Yeyote anaemshauri Nape kwamba yupo katika mstari kwa kweli hamtakii mema. Hii ni constructive criticism kutoka kwangu kwenda kwa Nape, na kwa wale wanaoona vinginevyo, hawamsaidii Nape bali kuzidi kumdidimiza. Bila ya Nape kujirekebisha, pole pole imani yetu kwamba Nape ni kiongozi bora na tegemeo letu sisi vijana wa CCM litaanza kufifia, kwani kwa mwenendo wake wa sasa, kuna dalili kubwa kwamba kumbe Nape might just be another "political jester."
 
Operesheni mabadiliko ya CHADEMA inayoshika kasi nchi nzima kwa sasa na kuendelea hadi kieleweke, yampa homa Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM. Sasa abadili msimamo wake kwa mara nyingine, baada ya kuona “Magamba” imedhoofisha CCM akaleta “Mizigo” nayo ikawasukuma wanachama zaidi kutimkia CDM, ndipo amekuja na kali Jana akiwa huko kusini mwa Tanzania katika juhudi zake za kujaribu kuzuia “hama hama” ya CCM na alipoona hali ni ngumu akaleta usemi mpya, yaani “Vinyago” na kusisitiza, “Wanaohamia vyama vya upinzani ni vinyago. Hakuna chama cha upinzani ambacho hakikuanzishwa na wanachama kutoka CCM.” Aliongeza, “Sasa! kinyago ukichonge mwenyewe kikuogopeshe?”

SWALI:

Je, CCM ina wanachama wa namna gani?
(Labda Wanachama hawa wanazo sifa zifuatazo! Lakini; Chagua jibu au majibu sahihi kati ya haya yafuatayo au ongeza/punguza mengine)
1) Kero
2) Magamba
3) Mizigo
4) Vinyago
5) Wasahaulifu
6) Mafisadi
7) Waongo
8) Wapenda amani
9) Wasema ilani na sera
10) Waigaji
11) Wachapa kazi
12) Wawekezaji,
13) ….........................
14) ….........................
15) ….........................
16) ….........................
17) ….........................
18) ….........................
19) ….........................
20) …........................
 
Mimi kama mwanachama wa CCM ambae nilikuwa na imani sana na Nape hapo awali nimeanza kukatishwa tamaa na kiongozi huyu. Hapo awali nilikuwa sikubaliani na kauli za baadhi ya wanachama wenzangu wa CCM kwamba Nape anakiharibu chama. Lakini taratibu naanza kuona mashiko ya hoja hii yapo wapi, ingawa bado nina amini pia kwamba baadhi ya viongozi wa CCM wanao toa kauli hizo dhidi ya Nape nao ni mzigo na tishio kubwa kwa uhai wa CCM katika zama hizi za ushindani wa kisiasa. Nimeanza kuhisi kwamba Nape ameanza kupwaya katika medani za siasa, hasa katika nafasi yake ambayo viongozi wenzake kama John Mnyika wanaimudu kwa ustadi mkubwa sana. Nape anahitaji ajenge uwezo wa kushindana kwa hoja na vijana wenzake wenye nafasi kama yake, mfano John Mnyika wa Chadema. Vinginevyo, CCM itapoteza vijana wengi ambao awali walimiminika CCM kwa imani kwamba Nape atasaidia kukirudisha chama katika mstari katika nyakati hizi za siasa za ushindani.

Kwa kweli kauli kama hizi kutoka kwa Nape ni za kutuvunja sana moyo sisi vijana wenzake ndani ya chama ambao kwa muda mrefu tuliamini kabisa kwamba Nape ni hazina ya chama chetu na ni moja ya sababu za msingi kwanini tunaendelea kubaki ndani ya CCM pamoja na chama kuwa ‘out of touch' na wananchi katika maeneo ya itikadi, dira, maadili ya uongozi na mikakati ya kutatua kero za mbalimbali za wananchi. Matumaini yetu ya awali kwamba mtu kama Nape ndiye atakayeweza kusaidia chama chetu cha CCM kirudi katika mstari yanaanza kuingia shaka kubwa.

Jambo lingine muhimu kulisema hapa pia ni kwamba kwa mtindo huu, wengi wetu taratibu tunaanza kuona kwamba hoja kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM kwamba Nape anakiua chama ni hoja zenye mashiko kwa namna fulani, pamoja na kwamba baadhi ya viongozi wanaotoa kauli hizo nao ni mzigo kwa CCM. Vile vile kauli kama hizi zinatufanya tuanze kuamini kwamba kumbe hoja kwamba Mwenyekiti wa CCM – Kikwete anaangushwa na wasaidizi na washauri wake, ni hoja zenye mashiko. Kwa mfano, Kikwete alitoa kauli ya kiungwana sana kama njia ya kujibu mapigo kutokana na wana ccm wengi kuhamia Chadema: Kikwete alitamka kwamba "wanaotaka kuhama CCM wahame".

Kauli ya Kikwete ni sahihi kabisa kutoka kwa kiongozi wa chama chochote cha siasa kwani katika mazingira ya demokrasia ya vyama vingi, njia pekee ya kujibu mapigo kama haya ni aidha kuja na mikakati ya kupunguza kasi ya wanachama kuhama au kuweka wazi kwamba wanachama kuhama ni haki yao ya msingi, hakuna wa kuwazuia. Na misimamo kama hii inaweza kutolewa na kiongozi katika mazingira yoyote ya demokrasia, hata katika nchi zilizokomaa kisiasa na kidemokrasia. Lakini kitendo cha Nape kuita wanaohama CCM kwamba ni vinyago ni ushahidi tosha kwamba Kikwete anaangushwa na wasaidizi wake/watendaji kwani, wakati Kikwete anatoa kauli y akuheshimu maamuzi ya wanachama wanaotumia haki yao kuhama CCM, wasaidizi wake kama Nape wao wanaenda mbali zaidi na kuwaita wanaohama CCM kwamba ni vinyago. Hii ni ishara kwamba Nape anaanza kupoteza sifa za kiongozi bora na badala yake anaanza kujijengea sifa za bora kiongozi.

Katika mazingira ya siasa, matumizi ya neno ‘vinyago' hayana tofauti kubwa na matumizi ya neno ‘wapambe'. Matumizi ya neno Wapambe (hence vinyago) yapo more relevant katika kuelezea aina ya wanasiasa kuliko aina ya wanachama. Nadhani wengi wenu mtakubaliana nami kwamba katika sababu kubwa juu ya kwanini wanachama wengi wa CCM wanahamia Chadema, "upambe" sio moja ya sababu hizo. Kuwaita wapambe/vinyago wanachama wa CCM wanaotumia haki yao ya msingi kuhamia chama wanachoona ni cha matumaini – Chadema ni dalili za kuishiwa hoja. Vile vile nadhani wengi wenu mtakubaliana nami kwamba ni jambo lililo wazi kwamba wanasiasa wanaotoa kauli za ovyo ovyo kama hizi katika mazingira na matukio ambayo wangeweza kuyafanyia kazi kimya kimya, wao ndio wanaoonyesha kila dalili ya upambe au kuwa vinyago kwa maana moja tu kubwa kwamba – kazi ya msingi ya vinyago au wapambe ni ku ‘amuse'. Kwa hiyo wanasiasa vinyago au wapambe ndani ya CCM, kazi yao kubwa ni kuwa ‘amuse' wanasiasa waliowaweka madarakani ili waendelee kukidhi mahitaji yao binafsi. Uzuri ni kwamba tumeshaona jinsi gani baadhi ya mawaziri waliofukuzwa hivi majuzi – wakati bado wapo madarakani, walikuwa wanatoa kauli kama hizi za upambe na ukinyago, lakini baada ya kumwaga unga, kauli na misimamo yao imebadilika kabisa.

Hii aina maana kwamba Nape hana nafasi na muda wa kujirekebisha, vinginevyo kwa maslahi ya Chama changu cha CCM, nitaendelea kusema ukweli daima kwani fitina kwangu mwiko. Yeyote anaemshauri Nape kwamba yupo katika mstari kwa kweli hamtakii mema. Hii ni constructive criticism kutoka kwangu kwenda kwa Nape, na kwa wale wanaoona vinginevyo, hawamsaidii Nape bali kuzidi kumdidimiza. Bila ya Nape kujirekebisha, pole pole imani yetu kwamba Nape ni kiongozi bora na tegemeo letu sisi vijana wa CCM litaanza kufifia, kwani kwa mwenendo wake wa sasa, kuna dalili kubwa kwamba kumbe Nape might just be another "political jester."

Mchambuzi, hatua ya Nape kuwatukana wananchi wa Tanzania ambao kwa hiari yao na uhuru walio nao wenye kulindwa na katiba ya nchi demokrasia yao kubakwa kwa kutukanwa kwamba ni vinyago.

Hii haijakaa vizuri wala kutulia kichwani mwangu kwamba kiongozi wa kitaifa mwenye kujali demokrasia na haki za raia kuwageuka na kuwatukana hadharani jukwaani kwamba ni vinyago.

Matusi kama hayo ndiyo yanayowakasirisha zaidi watu hata wale ambao bado wana mapenzi na chama chao CCM kuamua kuvua magamba, kwani heshima inazidi kushuka kila kukicha.
 
Mimi kama mwanachama wa CCM ambae nilikuwa na imani sana na Nape hapo awali nimeanza kukatishwa tamaa na kiongozi huyu. Hapo awali nilikuwa sikubaliani na kauli za baadhi ya wanachama wenzangu wa CCM kwamba Nape anakiharibu chama. Lakini taratibu naanza kuona mashiko ya hoja hii yapo wapi, ingawa bado nina amini pia kwamba baadhi ya viongozi wa CCM wanao toa kauli hizo dhidi ya Nape nao ni mzigo na tishio kubwa kwa uhai wa CCM katika zama hizi za ushindani wa kisiasa. Nimeanza kuhisi kwamba Nape ameanza kupwaya katika medani za siasa, hasa katika nafasi yake ambayo viongozi wenzake kama John Mnyika wanaimudu kwa ustadi mkubwa sana. Nape anahitaji ajenge uwezo wa kushindana kwa hoja na vijana wenzake wenye nafasi kama yake, mfano John Mnyika wa Chadema. Vinginevyo, CCM itapoteza vijana wengi ambao awali walimiminika CCM kwa imani kwamba Nape atasaidia kukirudisha chama katika mstari katika nyakati hizi za siasa za ushindani.

Kwa kweli kauli kama hizi kutoka kwa Nape ni za kutuvunja sana moyo sisi vijana wenzake ndani ya chama ambao kwa muda mrefu tuliamini kabisa kwamba Nape ni hazina ya chama chetu na ni moja ya sababu za msingi kwanini tunaendelea kubaki ndani ya CCM pamoja na chama kuwa ‘out of touch’ na wananchi katika maeneo ya itikadi, dira, maadili ya uongozi na mikakati ya kutatua kero za mbalimbali za wananchi. Matumaini yetu ya awali kwamba mtu kama Nape ndiye atakayeweza kusaidia chama chetu cha CCM kirudi katika mstari yanaanza kuingia shaka kubwa.

Jambo lingine muhimu kulisema hapa pia ni kwamba kwa mtindo huu, wengi wetu taratibu tunaanza kuona kwamba hoja kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM kwamba Nape anakiua chama ni hoja zenye mashiko kwa namna fulani, pamoja na kwamba baadhi ya viongozi wanaotoa kauli hizo nao ni mzigo kwa CCM. Vile vile kauli kama hizi zinatufanya tuanze kuamini kwamba kumbe hoja kwamba Mwenyekiti wa CCM – Kikwete anaangushwa na wasaidizi na washauri wake, ni hoja zenye mashiko. Kwa mfano, Kikwete alitoa kauli ya kiungwana sana kama njia ya kujibu mapigo kutokana na wana ccm wengi kuhamia Chadema: Kikwete alitamka kwamba “wanaotaka kuhama CCM wahame”.

Kauli ya Kikwete ni sahihi kabisa kutoka kwa kiongozi wa chama chochote cha siasa kwani katika mazingira ya demokrasia ya vyama vingi, njia pekee ya kujibu mapigo kama haya ni aidha kuja na mikakati ya kupunguza kasi ya wanachama kuhama au kuweka wazi kwamba wanachama kuhama ni haki yao ya msingi, hakuna wa kuwazuia. Na misimamo kama hii inaweza kutolewa na kiongozi katika mazingira yoyote ya demokrasia, hata katika nchi zilizokomaa kisiasa na kidemokrasia. Lakini kitendo cha Nape kuita wanaohama CCM kwamba ni vinyago ni ushahidi tosha kwamba Kikwete anaangushwa na wasaidizi wake/watendaji kwani, wakati Kikwete anatoa kauli y akuheshimu maamuzi ya wanachama wanaotumia haki yao kuhama CCM, wasaidizi wake kama Nape wao wanaenda mbali zaidi na kuwaita wanaohama CCM kwamba ni vinyago. Hii ni ishara kwamba Nape anaanza kupoteza sifa za kiongozi bora na badala yake anaanza kujijengea sifa za bora kiongozi.

Katika mazingira ya siasa, matumizi ya neno ‘vinyago’ hayana tofauti kubwa na matumizi ya neno ‘wapambe’. Matumizi ya neno Wapambe (hence vinyago) yapo more relevant katika kuelezea aina ya wanasiasa kuliko aina ya wanachama. Nadhani wengi wenu mtakubaliana nami kwamba katika sababu kubwa juu ya kwanini wanachama wengi wa CCM wanahamia Chadema, “upambe” sio moja ya sababu hizo. Kuwaita wapambe/vinyago wanachama wa CCM wanaotumia haki yao ya msingi kuhamia chama wanachoona ni cha matumaini – Chadema ni dalili za kuishiwa hoja. Vile vile nadhani wengi wenu mtakubaliana nami kwamba ni jambo lililo wazi kwamba wanasiasa wanaotoa kauli za ovyo ovyo kama hizi katika mazingira na matukio ambayo wangeweza kuyafanyia kazi kimya kimya, wao ndio wanaoonyesha kila dalili ya upambe au kuwa vinyago kwa maana moja tu kubwa kwamba – kazi ya msingi ya vinyago au wapambe ni ku ‘amuse’. Kwa hiyo wanasiasa vinyago au wapambe ndani ya CCM, kazi yao kubwa ni kuwa ‘amuse’ wanasiasa waliowaweka madarakani ili waendelee kukidhi mahitaji yao binafsi. Uzuri ni kwamba tumeshaona jinsi gani baadhi ya mawaziri waliofukuzwa hivi majuzi – wakati bado wapo madarakani, walikuwa wanatoa kauli kama hizi za upambe na ukinyago, lakini baada ya kumwaga unga, kauli na misimamo yao imebadilika kabisa.

Hii aina maana kwamba Nape hana nafasi na muda wa kujirekebisha, vinginevyo kwa maslahi ya Chama changu cha CCM, nitaendelea kusema ukweli daima kwani fitina kwangu mwiko. Yeyote anaemshauri Nape kwamba yupo katika mstari kwa kweli hamtakii mema. Hii ni constructive criticism kutoka kwangu kwenda kwa Nape, na kwa wale wanaoona vinginevyo, hawamsaidii Nape bali kuzidi kumdidimiza. Bila ya Nape kujirekebisha, pole pole imani yetu kwamba Nape ni kiongozi bora na tegemeo letu sisi vijana wa CCM litaanza kufifia, kwani kwa mwenendo wake wa sasa, kuna dalili kubwa kwamba kumbe Nape might just be another “political jester.”

Mkuu, huyu Nape anawatia aibu vijana wote mlioko ccm.
Mambo yakizidi kuwa ndivyo-sivyo nakushauri uchague upande mzuri wa historia ya hapo baadaye.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Saa ikishavunjika mshale, haisomi majira milele.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Name of job holder: Nape Nnauye.
Company: CCM Company (2005) Ltd.
Position: Public image destructor.
Duration of contract: to 2015 fixed.
 
Nape ! Umeishiwa huna jipya nenda kajipange vizuri ' mwisho utakuja mtukana mpaka rais wako jk
 
attachment.php
 
Back
Top Bottom