Wanaofaa kuwania urais 2015 kwa ticket ya CCM hawa hapa

Wewe unawakilisha kundi gani hilo mnalofikiria kuwapa urais,kundi langu litaamua baada ya kupitia sifa za wagombea wote,hatupo kichama,kidini,kikabila, kiukanda wala kimagazeti!!

Kweli ila niongezee jambo moja ambalo ni kuiweka Ccm pembeni 2015 ili kuirudisha Tz kwenye hadhi yake
 
Nadhani kwa hii post inavyoendelea kucommentiwa inanipa shaka kama JF ni great thinker kweli kwani mambo ambayo tunajadili hivi sasa si wakati wake badala yake tungejadili mambo yanayotugusa sasa ambayo yapo mengi tu ikiwemo ya mfumuko wa bei, viongozi wasiyo waadilifu kutowajibishwa na mambo mengine kama hayo
 
Umemsahau Nape,ana ushawishi kwa vijana wote,ni bright guy awe rais wetu ajae.Makamu wa rais Abdulah Salehe,Waziri mkuu,January Makamba.Bonge la serikali.
 
Mimi huwa natamani sana siku moja mtu aje na facts zinazoonyesha kwanini Lowassa hafai kuwa president lakini badala yake wana wanakuja hapa na maharisho yao waliyojiharishia huko. Lowassa is a tough decision maker, is charismatic, brave, experienced leader, innovative ,etc
Tafuta hotuba ya baba wa Taifa ya mwaka 1995 ndio iliyomchambua Lowasa Sio sisi. Sisi hatumchambui kwanza nani kakwambia uchaguzi utakuwa mwaka 2015? Uchaguzi ni mwakani 2013? Tafuta sababu humuhumu JF utazipata kwa nini mwakani.
 
Mi naona tuweke sifa za mtu kuwa rais then tuangalie nani anafit kwenye hizo criteria. Zaidi ya hapo tutakuwa tunapiga gumzo lisilokuwa na tija. Kwa hao uliowataja wanasifa moja kubwa wamesababisha tz kuwa hapa tulipo either kwa kufumbia maovu ya viongozi wenzao au kuchukua maamuzi mabovu ambayo yana/yameligharimu nchi. Mifano ipo mingi kuuza nyumba za serikali kwa bei sawa na bure. Kujenga shule za kata bila ya kuwa na plan maalum ya kujenga nyumba za walimu, maktaba, maabara, nk matokeo yake jengo likikamilika linaitwa shule na watoto wanasoma bila vitabu vya kutosha na miundombinu isiyokidhi haja na ndio maana 82% ya wahitimu wa kidato cha nne walifeli.
 
Tafuta hotuba ya baba wa Taifa ya mwaka 1995 ndio iliyomchambua Lowasa Sio sisi. Sisi hatumchambui kwanza nani kakwambia uchaguzi utakuwa mwaka 2015? Uchaguzi ni mwakani 2013? Tafuta sababu humuhumu JF utazipata kwa nini mwakani.
kumbe wewe binafsi hauna hoja, unaongozwa na mizimu! shame on you:peep:
 
Sie hatuna tatizo na majina yenu yote hayo hata kama angerudi Ben.M,nia yetu ni moja,kukiondoa CCM madarakani 2015...tunataka kutoa funzo kwamba kuna chama nje ya CCM ambacho kinatufaa na kinafaa pia kupewa ridhaa ya kukaa magogoni na maisha yakanyooka..

Kwahiyo mkuu achana na habari za majina hapa
 
Mimi huwa natamani sana siku moja mtu aje na facts zinazoonyesha kwanini Lowassa hafai kuwa president lakini badala yake wana wanakuja hapa na maharisho yao waliyojiharishia huko. Lowassa is a tough decision maker, is charismatic, brave, experienced leader, innovative ,etc
Kama sheria na taratibu zinafuatwa na kutekelezwa hamna issue ya tough decision maker ni kila mtu kufuata sheria na mambo yote anakwenda sawa
 
kweli zimetuharibia watoto! kwa upande mwingine ni bomu litakayoing'oa ccm madarakani. kwani wahitimu wa shule za kata wanahasira na matokeo mabaya wanayopata na chanzo ni ccm. mpaka 2012 kutakuwa na wapiga kura wengi mno kutoka shule za kata.
 
1. Edward Lowassa
2. Dr. John Pombe Maghufuli

Akiteuliwa mmoja kati ya hawa, watanganyika tutafikiria kuwapa CCM urais, tofauti na hawa tutawapa chadema nchi.

Naona mkuu unawasemea watanganyika; sa sijui ni kundi gani unaliwakilisha maana ni wengi tu hawayataki hayo majina
 
1. Edward Lowassa
2. Dr. John Pombe Maghufuli

Akiteuliwa mmoja kati ya hawa, watanganyika tutafikiria kuwapa CCM urais, tofauti na hawa tutawapa chadema nchi.
chadema bado wachanga hawawezi pewa nchi acha utani kabisa
 
Back
Top Bottom