Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
Maelezo ya Awali...

Njia za uzazi wa mpango hutumika na wanaume na wanawake kuzuia ujauzito kwa madhumuni ya kupanga uzazi ili kuwa na familia bora. Ni vigumu kusema kuwa kuna njia iliyo bora zaidi ya uzazi wa mpango kwa kuwa kila njia ina faida na hasara zake. Wote kati ya mwanamke na mwanaume wana maamuzi juu ya mipangilio wa kupata watoto.

Kufanya uchaguzi utumie njia ipi kwa ajili ya kupanga uzazi siyo kitu rahisi kwa kuwa kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla ya kufanya maamuzi yeyote. Lakini awali kabisa, inabidi ujifunze njia mbali mbali, ili kuweza kubaini ni njia ipi itakayokufaa pamoja na mwenzi wako kupanga uzazi. Mnaweza pia kuwasiliana na muuguzi au daktari anayeusiana na masuala ya uzazi wa mpango kwa ushauri, ili muweze kuchagua njia sahihi itakayowafaa.


Kabla ya kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango, inabidi ufikirie kuhusu mambo yafuatayo:
  • Afya yako kwa ujumla.
  • Ni kwa kiwango gani njia husika ya uzazi wa mpango inafanya kazi.
  • Unajamiiana mara ngapi?
  • Matarajio ya kupata mtoto siku za usoni.
  • Je ni nini faida na madhara ya kutumia njia husika ya uzazi wa mpango?
  • Je unafurahia kutumia njia husika uliyochagua?
Yakupasa kufahamu kuwa, hata kama njia unayotumia ni bora zaidi, wakati mwingine njia hiyo yaweza kushindwa kufanya kazi. Lakini uwezekano wa kupata ujauzito utakuwa mdogo sana endapo njia uliyochagua itatumika kwa usahihi wakati wa kujamiiana. Pia ikumbukwe pia, njia za uzazi wa mpango za kutumia homoni na dawa, hazitakukinga na maambukizi ya HIV na magonjwa ya zinaa.

======
Dawa au vifaa vya uzazi ni baadhi ya taratibu zinazotumiwa kuzuia mimba kutungwa. Ikiwa msichana au wanamke atafanya mapenzi pasi na kutumia mojawapo ya mbinu hizo basi, kuna uwezekano wa theluthi moja kwamba atapata mimba.

Hata hivyo aina yoyote ya kuzuia mimba utakayoichagua ni lazima itumiwe kama ilivyoagizwa, ili kuleta matokeo ya hakika.


Baadhi ya njia hizo kama vile kutumia kondom wakati wa ngono, pia kwa kiasi fulani humpa mtu kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya HIV, na magonjwa mengine yanayoathiri afya ya uzazi.

Kwa vile mbinu za kuzuia uzazi ni za aina tofauti tofauti, ni muhimu basi uchague kwa makini ile inayokufaa. Utapata usaidizi wa kitaalam kama utashauriana na daktari wako, au pata usaidizi katika kituo cha kwenu cha upangaji uzazi, au kituo cha vijana.

Mbinu za kuzuia mimba (Contraception)
Hivi ni vifaa au dawa zinazotumiwa kwa minajili ya kuzuia mimba kutungwa wakati wa kufanya ngono. Kuna zile zinazotumiwa kwa mda mfupi na nyengine kwa mda mrefu. Nyengine hufanya kazi papo hapo na nyengine huitaji maandalizi ya muda.

Kondom au tembe maalum ndizo njia bora zinazojulikana zaidi za kuzuia mimba.

Pia kondom zina manufaa bora zaidi zinapotumuwa kwani mbali na kuzuia mimba zinapotumika kama inavyopaswa zinaweza pia kumkinga mtu asiambukizwe vurusi vya HIV, na magonjwa mengine ya zinaa.


Tuangalie kwanza vifaa vya kuzuia mimba:
Moja ya mbinu bora na rahisi za kuzuia mimba, ni kuweka kizuizi, kwa lengo kuwa mbegu ya mwaname na ile mwanamke zisikutane. Kwa maana hiyo kifaa maalum kinaweza kuwekwa katika njia inayotumiwa na mbegu ya kiume ndio isilifikie yai la mwanamke.

Baadhi ya vifaa hivi (hasa kondom) pia vinaweza kukinga kuambukizwa virusi vya Ukimwi, na magonjwa mengine ya kuambukizana kupitia ngono.Kuna aina kadhaa za vifaa vya kuzuia mimba. Kondom za wanaume na zile za wanawake ndio vifaa vinavyofahamika zaidi, hata hivyo kuna pia vifaa vyenginevyo viitwavyo diaphragm na caps kwa kimombo ambavyo vinaweza kutumiwa na wanawake.


Kondom za wanaume: Hivi hutengenezwa kutokana na aina maalum ya mpira uitwao latex, au plastiki nyembamba. Kondom ya mwanaume huvaliwa kwenye uume iliyosimama, tena kabla ya uume kuingizwa ukeni. Ikitumiwa kama inavyotakikana inakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98. Kwa kawaida kondomu hupatikana kwenye vituo au kliniki za upangaji uzazi, kwenye maduka ya madawa au hata maduka ya kawaida.

Kondomu za wanawake: Halkadhalika hutengenezwa kwa mipira laini ya latex au plastiki nyembamba maalum. Huvaliwa ndani ya uke, huku sehemu iliyowazi ikichomoza nje kidogo. Kwa kawaida kondom za wanawake ni ghali, na pia utendaji kazi wake unakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 95.

Aina nyenginezo na vifaa vya kuzuia mimba huwa hazipendekezwi kwa vijana lakini ni vyema kuvijua.Kuna aina nyenginezo za vifaa vya kuzuia mimba viitwavyo diaphragms na caps. Hivi hutengenezwa kutokana na kitu kiitwacho silicone au mpira laini maalum. Vikiwekwa ukeni hutumika kama vizibo vya kuzuia mbegu za mwanamme kupenya hivyo basi haiwezi kukutana na yai la mwanamke.

Kwa kawaida caps ni ndogo kuliko diaphragms lakini kwa vile wanawake pia wana maumbo tofauti, ni sharti upate saizi utakayokutosha. Hapa ni sharti upate usaidizi wa daktari wako, au muuguzi, kuiweka.

Inapowekwa mahali pake ndani ya uke, iwe diaphragm au cap, huziba kilango cha mfuko wa uzazi hivyo basi mbegu ya mwanamme haitapatanafasi ya kupita. Ukishaonyeshwa na daktari jinsi ya kuipachika, baadae unaweza kuipachika mwenyewe kabla ya kufanya mapenzi.


Kwa matokeo bora zaidi, diaphragms na caps hutumiwa pamoja na dawa iitwayo (spermicide) ambayo huuwa mbegu za uzazi za mwaname. Hapo diaphragms au caps humpa mwanamke kinga dhidi ya mimba kwa asilimia kati ya 92 na 98.

Hata hivyo itachukua mazoezi ya muda ili kuvitumia itakikanavyo. Wakati mwengine pia hutumiwa na gel yake maalum lakini bado havina hakikisho la asilimia moja kuzuia mimba.

Faida yake nyengine ni kuwa, kwa kiasi fulani, vinaweza kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na saratani ya (cervix) lango la nyumba ya uzazi.

Ikiwa wewe hutumia vifaa kama diaphragms au caps, au hata kondom, ni vyema kujipangia mapema ndio usikose akiba, ndio haitakuwa karaha kuvitafuta pale unapovihitaji.


Mbinu nyingine za kuzuia mimba
Kuna chembe chembe za kimaumbile, zinazojulikana vyema kama homornes ambazo hutumiwa kutengeneza tembe au chanzo ya kuzuia mimba.

Chembe chembe hizi kwa jina maalum progestogen yaani mchanganiyko wa oestrogen na progestogen, huingizwa mwilini mwa mwanamke kwa mpangilio na kiwango maalum ili kuzuia mimba kutungwa. Hufanya kazi kwa namna hii:


* Kwa kuzuia ovari kuangua mayai
* Kwa kuzuia mbegu za mwanamme kulifikia yai (kwa kufanya majimaji ua ukeni kuwa mazito na kunata hivyo kuzuia mbegu ya mwanamme kupenya)
* Kwa kulizuia yai kujipachika kwenye kiota cha nyumba ya uzazi.


Tembe mchanganyiko - huwa ni kidonge cha dawa kilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa chembe chembe za oestrogen na progestogen. Hii huzuia mimba kwa njia zote tatu tulizozitaja hapo juu na ikitumiwa itakikanavyo, vinategemewa kuzuia mimba kwa asilimia 99.

Tembe ni rahisi kutumia - Mradi tu unakumbuka kumeza vidonge kulingana na maagizo. Wakati mwengine pia huifanya hedhi, kupungua na kupunguza pia maumivu wakati wa hedhi.

Lakini athari zinazoandamana na utumiaji wa vidonge hivyo ni pamoja na kuchafukwa na moyo, kuongezeka unzani, na athari mbaya zaidi ni iwapo itatokea hali ya kuganda kwa damu kwenye mishipa ya kupitisha damu.

Vidonge vya Progestogen pekee (POP) - Aina hii ya Tembe huitwa pia "mini pill" na huwa ina chembe chemba za progestogen pekee. Huzuia mimba kwa njia kama zile zile zinazozuia tembe za mchanganyiko, na ina utendaji kazi wa kati ya asilimia 96 na 99. Hata hivyo kama una uzani wa zaidi ya kilo 70 uwezo wake wa kuzuia mimba hupungua

Faida kuu ya kutumia vidonge hivi ni kwamba vina athari ndogo za kiafya. Lakini tatizo ni kuwa ni sharti tembe imezwe wakati ule ule kila siku , kama umechelewa basi isipitishe zaidi ya masaa matatu.
Sindano - Hii ni chanjo ya kuzuia mimba inayotengenezwa na chembe chembe hizo hizo za homoni ya progestogen. Tofauti na tembe, ambazo ni sharti kumeza moja kila siku, sindano pindi inapodungwa inakupa kinga dhidi ya mimba, kwa mda wa kati ya wiki nane hadi 12 kuambatana na aina inayotumiwa.


Hudungwa takoni, na dawa kuingizwa ndani ya mishipa ya damu na ina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 99.

Faida kuu ya njia hii ya sindano, ni kwamba hutakuwa na wasiwasi wa kupata mimba unapofanya ngono, kwa mda wa angalau wiki nane au 12.

Lakini pia ina athari zake - ni kwamba huenda dawa hii ikavuruga mpangilio wako wa kawaida wa kupata hedhi, au ukatoka hedhi kiwango kisicho cha kawaida cha damu, au kwa mda mrefu, au hedhi ikapotea kabisa. Pia inaweza kusababisha kuongezeka uzani.

Homoni au Vidonge vya kupachika chini ya ngozi Hapa dawa kama ile ile ya tembe au chanjo, hutengenezwa na kuwekwa kwenye kifaa cha plastic mfano wa kijiti cha kiberiti. Hupachikwa ndani ya ngozi chini ya kwapa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo.Hii ni njia ya mda mrefu ya kuzuia mimba. Inaaminika kuzuia mimba kwa aslimia 99 na inaweza kufanya kazi kwa mda wa hadi miaka mitatu.
Kuna aina nyenginezo za upangaji uzazi ambazo, ingawa kwa hali ya kawaida hazipendekezwi kwa vijana, si vibaya kuzijua.


Kitanzi au koili, ambacho kwa lugha ya kitaalam kinajulikana kama Intra-uterine device au IUD hutengenezwa kwa plastiki na shaba, na hupachikwa kwenye mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.Vitanzi huanza kufanya kazi pindi kinapopachikwa. Hufanya kazi kwa njia mbili kuu. Kwanza, kwa kuzuia mbegu za kiume kutangamana na yai, na pili kuzuia yai kukubaliwa kujipachika ndani ya mfuko wa uzazi.

Kitanzi au koili kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98 na 99. Na pindi kikitolewa asili ya uwezo wa wanamke wa kushika mimba anapofanya ngono, unarudi vilevile.

Hata hivyo moja ya matatizo ya kitanzi ni kwamba vinaweza kuifanya hedhi yako kuwa nzito (damu kutoka nyingi) na pia huenda ukapatwa na maumivu, mara nyengine inaweza kutoka mahali kilipowekwa na kusukumwa nje ya mfuko wa uzazi.Hivyo ni vyema kumuona daktari mara kwa mara ili kama imechomoka, ipachikwe tena vyema.

Njia asilia ya mpango wa uzazi:
Njia hii inahitaji makini sana kuitumia. Kwani inafanya kazi tu ikiwa wanamke anafanya mapenzi tu wakati ule ambao kiasilia hawezi kushika mimba.

Hii inawezekana kwa kutayarisha tarakimu za siku za hedhi, na kupima hali ya joto la mwili. Njia hii inahitaji uangalifu na uzoufu mkubwa &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Kwa vile ni ya kubahatisha haipendkezwi kwa vijana ambao hawako tayari kupata mtoto.


Kwa bahati mbaya watu wengi hudhani kwamba kutoa uume kutoka ukeni, pindi tu kabla ya kufikia kilele cha kumwaga manii, ni moja ya njia za kuzuia mimba.

La sivyo kwani mara nyingi mbegu za kiume hutangulia kutoka hata kabla kufikia kilele katika hali ya kufanya mapenzi. Hivyo basi hata ukitoa uume huenda umeshachelewa!Vasectomy au Tubuligation, Hii ndiyo njia pekee ya kudumu ya kuzuia mimba.

-Vasectomy ni njia ya kumfanya mwanamme asiwe na uwezo wa kutunga mimba ilhali Tubuligation ni njia ya kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kushika mimba. Hii inafanyika kwa njia ya upasuaji mdogo.Mwanamme anafanyiwa upasuaji kwa kukata vibomba vinavyopitisha mbegu za kiume kutoka kwenye makende hadi kwenye uume. Upasuaji huu kwa mwanamke unahusisha kukatwa au kuzibwa kwa vibomba vinavyopitisha mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi.

Baada ya upasuaji huu, ni vigumu mwanamke au mwanamme kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya kuweza kuzaa, kwa hivyo njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki tena kupata watoto (zaidi).

Kitanzi cha Intra uterine system au IUS - Hiki nacho kimetengezwa kwa plastiki, yenye muundo wa T kikiwa na chechembe za homoni ya progestogen ndani. Kinaweza kupachikwa ndani ya mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.

Kitakapopachikwa, progestogen pole pole huingia ndani ya mwili, na kuzuia mimba katika njia ile ile kama vinavyozuia tembe. Kinaweza kutumika kwa mda wa miaka 5, na kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 99.


-Kitanzi cha IUS ni kizuri kwa wale walio na matatizo ya maumivu wakati wa hedhi, kwa sababu kinapopachikwa (ingawa wakati wa kupachikwa huenda ukapata maumivu kidogo) baadaye husaidia kupunguza hedhi au hata kuisitisha kabisa, kutokana na homoni hizo za progestogen. Madhara ya njia hii nayo ni kama, kuongeza uzani, kuumwa na kichwa, kutokwa na damu kusiko na mpango, na mabadiliko ya majira ya hedhi. Pia inaweza kuchopoka, hivyo itabidi kumwona muuguzi au daktari kila mwezi kuhakikisha kiko sawa.

Ni vyema kujadili juu ya aina mbalimbali za mpango wa uzazi ili kuchagua vyema. Daktari wako au muuguzi atakushauri ipasavyo. Hata hivo kumbuka njia hizi za kuzuia mimba hutumiwa zaidi kwa minajili ya mpango wa uzazi, hivyo basi haziwezi kukukinga dhidi ya maambukiko ya virusi vya Ukimwi, au magonjwa mengine yayayosambazwa kupitia ngono.

Ni busara kutumia kondom kila unapofanya mapenzi na mtu ambaye afya yake ya uzazi huifahamu - Hakikisha pia unaufahamu vizuri jinsi ya kutumia kondom na unajua jinsi ya kufanya ngono salama kwa jumla.

SWALI
Msaada jamani.

Wife anadai condom zina msumbua sana.

Akienda uwani anakuta mafuta mengi ya condom ukeni.na kama ikipasuka huwa inabakiza vipande ukeni.

Msaada jamani.

Kalenda pia imetushinda.

JIBU
Vizuizi vya Ghafla (Emergency Contraception)
Hii hutumika wakati mwanamke amefanya mapenzi kiholela kupitia kwa uke (vaginal sex) ili kumzuia kupata mimba. Inaweza kutumika pia kama njia za kizuizi zilizokuwa zimetumika hazikufaulu. Hufaa sana kama itachukuliwa kabla ya masaa 72 kutoka wakati wa mapenzi. Huhusisha kunywa dawa mbili za &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Hormone' zikiachana kwa masaa 12. Hizi dawa vidonge hufaa kwa asilimia 75-89 kuzuia mimba.

Njia nyingine ya kizuizi cha ghafla ni kuwekwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];copper T IUD' kwenye tumbo la uzazi kabla siku 7 hazijaisha kutoka wakati wa mapenzi (ngono). Hii njia hufaa asilimia 99.9 kuzuia mimba na inaweza kutolewa wakati wa muezi huo mwingine. Kama tayari ushaishika mimba njia hizi hazitakusaidia. Hii njia za ghafia hazifai kutumika kama desturi.

Povu na utando,

Povu na utando au vidonge vilivyo na kemikali ya kuua mbegu (manii) &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; spermicide huwekwe ndani ya uke si zaidi ya saa moja kabla ya kufanya mapenzi. Huwa zinafanya kazi kwa kuua manii. Huachwa papo hapo kwa masaa 6-8 baada ya kufanya mapenzi. Kemikali hizi (spermicides) zingine huwa na Nonoxynol-9 ambayo kukulinda kutokana na kisonono na Chlamydia. Nonoxynol-9 hatakulinda kutokana na ukimwi. Kemikali hizi (spermicides) hufaa kwa asilimia 74 kukulinda kushia mimba.

IUD (Intrauterine Device)

Hiki ni kifaa cha plastiki au shaba kilicho na umbo la &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];T' na huwekwa kwenye mji wa mimba/tumbo la uzazi (uterus) ili kuzuia manii kulifikia yai. Hukaa kwa muda wa miezi kadha hadi miaka 10. Hiki kufaa husaidia asilimia 98-99 kuzuia mimba. Kinapowekwa, huanza kazi yake papo hapo. Unaweza kupata kiharusi siku chache baada ya kuwekwa IUD. Kati ya mwezi wa 3 na 6 unaweza kutoa damu kidogo juu zaidi ya damu ya hedhi. Pia mwezi wako/wakati wako wa hedhi utakosa kubainika. Wanawake wengine hutoa damu kwa wingi.

Njia ya kutumia kizuizi

Kondomu za Wanawake/kike
Huu ni mrija mtegevu wa plastiki huvaliwao kwenye uke. Pande iliyafungwa husaliwa ndani karibu na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Cervix' na upande uliowazi huvaliwa tu nje ya uke. Hii njia ya kutumia kizuizi hiki huzuia manii kufikia yai. Hii kondomu yaweza kuvaliwa aghalabu masaa 24 kabla ya kufanya mapenzi na hufaa kwa asilimia 79-95 katika uzuizi wa mimba. Kondomu hizi hupatikana kwenye maduka ya dawa. Pia hospitali za mikoa na kliniki hupatiana kondomu hizi bure.

Diaphragm/Cervical Cap (Kiwambo-diaphragm)

Hii njia huzuia manii kulifikia yai. Kiwambo hiki huwa na umbo kama kikombe nayo &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Cerival cap' huwa na umbo kama kastabini (thimble). Hizi hufunikia &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];cervix' (mwanzo wa tumbo la uzazi) ili manii yasiingie kwenye tumbo la uzazi (womb). Zinafaa kuvaliwa/kuwekwa ndani ya uke kabla ya kufanya mapenzi. Kiwambo hiki hufaa kwa asilimia 80-94 kwa kuzuia mimba. Nayo &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];cervical cap' hufaa asilimia 80-91 kuzuia mimba kwa wanawake ambao hawajawahi pata mtoto, na hufaa asilimia 60-80 kwa wanawake ambao keshajifungua. Unafaa kumwona daktari au mtaalamu wa mambo yahusuyo uke ili
akuweke kiwambo au &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];cap'.


Njia za Hormoni


Vidonge Vya Kumeza (Pill)

Kidonge hufaa kunywewa kila siku na huwa na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];hormones' mili ambazo ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ostrogen' na progestin ambazo huzuia kifuko cha mayai kwenye uke kutoa mayai. Inapotumika ipayasavyo hufaa kwa asilimia 95-99.9 kuzuia mimba. Kama una miaka zaidi ya 35 na huwa unavuta sigara* au umewahi kuwa na historia ya kuvilia damu au kansa ya maziwa (matiti) au &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];endometrial' daktari wake anaweza kukushauri usitumie kidonge hiki.

Vidonge hivi huongezea hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo, kukimbia kwa damu, kuvilia damu na kufungamana kwa mishipa ya damu. Kuna aina mbali mbali ya vidonge hivi na huwa na vipimo tofauti vya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];oestrogen' na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];progestin'. Unafaa kualiza shauri kutoka kwa daktari wako au kutoka kwa hospitali/kliniki kabla hujaanza kunywa vidonge hivi. Vidonge hivi hupatianwa bure katika hospitali za mikoa na kliniki nyinginezo.


The Mini Pill

Hiki kidonge (vidonge) hufaa kunywewa kila siku na huwa na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Hormone' moja (progestin) ipunguzayo na kuafanya ute wa ngozi ya ndani ya uke (cervix) kuwa mzito/mnene ili kuzuia manii kulifikia yai. Kidonge hiki pia huzuia yai uliloungana mbegu kukomaa (kujiimarisha) kwenye uke. Hiki kidonge hufaa sana kwa wanawake ambao hawawezi kunywa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];oestrogen' au kwa wale wana hatari ya kuvilia damu. Akina mama wanaonyonyesha wanaweza kukitumia kidonge hiki kwa sababu hakiadhiri utuaji wa maziwa. Kitumiwapo ipasavyo, hufaa kwa asilimia 95-99.9% kwa uzuizi wa mimba.

Sindano &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Depo-Provera

Depo-Provera ® huzuia utoaji wa mayai na hufanya ute wa ngozi ya ndani ya uke (cervix) kuwa mzito hivyo kuzia manii kupenyeza kwenye tumbo.* Pia hufanya tabaka (lining) la tumbo kunenepa hivyo kuwa vigumu kwa yai lililoungana na mbegu kujishikilia. Wanawake hsindano hii kwenye makalio (******) au mkono baada ya kila miezi mitatu. Hufaa kwa asilimia 99.7 kwa kuzuia mimba. Sindano hii haistahili kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 21 ila tu kama wameshawahi kujifungua au hawawezi kutumia njia nyingine ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Harmone' kwa sababu ya matatizo ya kiafya. Daktari wake/mtaalamu atakudunga sindano hii.



Njia za kitabia

Hii huwa mwanamume kuondoa uume wake kutoka ndani ya uke kabla ya kutoa manii ili kuzuia mbegu kufikia yai. Hii njia huhitaji uzuifu mwingi sana (kutokana na msongo) upande wa mwanamume. Hata kwa kutumia njia hii unaweza pata

mimba KABLA mwanamume hajatoa uume wake. Kabla hajatoa manii mwanamume anaweza kutoa manii mengine kabla ya kufika kileleni (pre-ejaculation) nah ii inaweza kusababisha mimba. Hivyo basi hii njia haifai sana kwa kuzuia mimba. Pia,


haitakulinda kutokana na maradhi ya zinaa. Kujinyima/kujifunga kutoka kufanya mapenzi wakati wa mwezi/hedhi au &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Fertility Awareness' ni njia nyingine, na inayofaa zaidi ya kuzuia uzazi kitabia.

Njia za kupanga uzazi milele


Kufanywa Tasa au Gumba kwa kutumia Upasuaji

Hizi njia za upasuaji huazimiwa kwa watu walio maliza uundaji wa familia au hawataki watoto.

Kufungwa mirija (tubal ligation/tying tubes') hufunga/hukata mirija unaobeba mayai ndiposa kuyazuia mayai kuingia tumboni la uzazi ambako yanaweza ungana na mbegu (manii).

&[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Vasetomy' (kufungwa kwa mrija ubebao manii kutoka wakati ufanyapo mapenzi.

Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Kufungwa mirija hufaa kwa asilimia 95-99.5 % kwa kuzuia mimba. Hata hivyo hazifai katika kuzuia maradhi ya zinaa, kwa hivyo kama wewe si wa mke mmoja utafaa kutumia kondomu.

Family Planning Association of Kenya wana habari kuhusu mambo hayo kwa wanawake na wanaume. Unaweza kuwapigia simu kwa maelezo zaidi au uulize kwenye hospitali au kliniki iliyokaribu nawe. Wanaume wanaweza kufanyiwa upasuaji na warudi makwao lakini kwa wanawake itawabidi walazwe.

MKUU CHAGUA NJIA UNAYOIONA NI NZURI KWAKO KATI YA HIZI NJIA ZA KUZUIA MIMBA.
SWALI
Wasalaam
Hivi wakuu hili suala la uzazi wa mpango ni nani hasa anaetakiwa kufunga au kujizuia, maana hapa home tunawatoto wawili na kwetu tunaona imetosha ila mke wangu hataki kufunga analazimisha mimi ndio nifanye hivyo, nimejitahidi sana kumuelezea na kubembeleza kwao ilivyorahisi kufanya hivyo lakini amekuwa mgumu kuelewa.

Mara anasema basi tutumie condoms na mi siwezi kufanya hivyo wakati nipo kwenye ndoa sasa imebaki kubahatisha siku ambazo ni salama kwake mi inanikera sana mliwezaje wanandoa wenzangu.

Mnalichukuliaje hili swala, nyie mliwezaje kuwashawishi na wanawake wa siku hizi mbona mnakuwa viburi kiasi hiki.

JIBU
Kwanza ni muhimu ujitambue wewe binafsi vp uwezo ulionao unakutosha na unaweza kuwatunza vyema na hapo ndio unachukua uamuzi.

Pili, unamshirikisha mwenzio kuhusu wote kufunga uzazi sababu ni ngumu kumwambia mmoja funga wakati wewe bado risasi ziko ok,kama mnafunga fungeni wote,mimi niliamua na tukafanya maamuzi na wote tumefunga na hakuna tatizo.
SWALI
Mwanamke aliyetumia sindano za uzazi wa mpango humchukua mda gani kupata ujauzito pindi aachapo kutumia?

JIBU
Inatarajiwa aweze kurudi katika hali ya kawaida miezi mitatu baada ya kuacha kutumia (tangu sindano ya mwisho), kwa maana ya kwamba kuwa na uwezo wa kubeba ujauzito.Hata hivyo baadhi(wachache) huchelewa kidogo kubeba ujauzito, uchelewaji huu hauwezi kuzidi miezi 24(miaka miwili).

Threads zinazofanana


CONFESION: Madhara ya Vidonge vya Uzazi Wa Mpango...

Njia ya uzazi wa mpango wa asili (natural birth control)
Vikwazo vya Viongozi wa Dini kuhusu kampeni ya uzazi wa Mpango
Athari za kutumia njia za uzazi wa mpango za kisasa
 
Last edited:
Habari zenu wana MMU.

Mimi ni buheri wa AFYA njema kabisa.Hapo nyuma tuliangalia athari kubwa zitokanazo na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango.

Member wengi humu hasa wamama kwa wadada walijumuika nasi katika kushuhudia madhara ambayo kimsingi ni matatizo makubwa sana kwa afya za hawa mama zetu.Ingawa serikali na vyombo vyake vya afya vimekuwa vikitumia fedha nyingi katika kuhimiza matumizi ya hivi vidonge.Kwa mchango wa wadau humu MMU tutajifunza mengi sana na Mwishoni kila mdau atachagua njia sahihi ya uzazi wa mpango.

Leo tena tutapata muda wa kutafakari hayo maudhi madogo madogo ambayo ndio msingi mkubwa wa matatizo ya kiafya ya uzazu ya hawa mama zetu.

Ntaziangalia njia mbali mbali na matatizo yake kwa ufupi sana, na wadau wengine wataongezea katika kufanikisha somo letu.

NJIA mbali mbali......kama zifuatavyo...

1.KITANZI
Kifaa cha plastiki inakaa kwenye mji wa mimba.Inafaa kwa wale wenye mume mmoja mwaminifu

INAVYO FANYA KAZI

Inazuia yai la mwanamke lisikutane na mbegu za mwanaume

MAUDHI YAKE

Watu wengine kutokwa na damu nyingi,Kusababisha magonjwa ya zinaa yaingie kwenye mji
wa uzazi kwa urahisi ikiwa umeambukizwa.

2.KUFUNGA KIZAZI
Ni operesheni kuziba njia ya mayai ya mama au mbegu za baba ili zisikutane
Inafaa kwa wale ambao wamekamilisha familia


MAUDHI YAKE

Huwezi kuzaa daima
Ni rahisi zaidi kwa baba kwa sababu njia yake ni juu juu kuliko ya mama, lakini zote ni operesheni ndogo tena bure.

3.Vidonge (Combined Oral Contraceptive)
4.NJIA YA SINDANO(DEPO PROVERA)
5.VIPANDIKIZI

Vidonge vya Uzazi wa Mpango vyadaiwa kusababisha upofu,Pamoja na kuwa ni njia nzuri ya kuzuia ujauzito, vidonge vya Uzazi wa Mpango vinatajwa kusababisha ugonjwa wa macho ujulikanao kama Glaucoma, unaoelezwa kuwa ni chanzo kikuu cha upofu.

Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa Afya na Lishe uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).

Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.

Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen vina umuhimu katika seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.

"Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho," anasema Dk Pasquale.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.

"Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge," anasema(Mwananchi 20/jan/2014)

.....Kwa wale walotumia njia hizi watuambie hayo maudhi madogo madogo kama wanavyo yaita wenyewe wahusika ni yapi.

------------------------

Kuna njia tofauti za uzazi wa mpango ambazo unaweza kuzifata kutokana na matakwa yako. Njia ambayo hutumika na wengi ni ya KALENDA,na kwa njia hii unahesabu siku zako ni muhimu ujue una mzunguko wa siku ngapi ili kuweza kuheshabu siku ipi upo hatarini(unaweza kubeba ujauzito) na siku ipi upo salama.

Njia nyingenezo ni:


  • HORMONSPIRAL:Kwenye picha ya kizazi unaona spiral ipo kwenye mfuko wa uzazi hii inadumu kwa miaka 5.
  • View attachment 113067
  • VAGINAL RING ina umbo la mduara na muonekano wa mviringo,hii huwekwa nje ya kizazi.View attachment 113069
  • BIRTHCONTROL PILLS:Vidonge vya uzazi wa mpango,vipo vya aina tofauti vyenye homoni moja tu nayo ni gestagen au mchanganyiko wa gestagen na estrogen
  • Kuna PLASTER ambazo unaweza kutumia,Hizi plaster zina mchanganyiko wa homoni mbili gestagen na estrogen.Unaiweka kwenye eneo la ngozi safi siku ya kwanza unapopata siku zako,unabadili baada ya siku 7,unabadili tena siku ya 15,kisha unachukua mapumziko ya siku 7(kwa wale wenye mzunguko wa siku 22-28)
  • SINDANO ambayo inachomwa kila baada ya miezi mitatu
  • IMPLANTANT:Ni kijiti ambacho unaweka chini ya ngozi ya mkono kwa ndani,hiki hudumu kwa miaka 3 au 5,kutokana na chaguo lako.
  • View attachment 113068

--------------------------------

Kwa Ushahidi wa madhara ya matumizi ya njia hizi - https://www.jamiiforums.com/mahusia...idonge-vya-uzazi-wa-mpango-8.html#post8429829

Mjadala juu ya nini Madhara ya njia hizi - https://www.jamiiforums.com/jf-doct...i-madhara-ya-vidonge-vya-uzazi-wa-mpango.html
 


uzazi wa mpango ni jambo muhimu sana katika jamii yetu, lakini kuna njia nyingi sana ukitaka kupanga uzazi na familia nyingi waliotumia uzazi wa mpango wanasema hawajutii kutumia njia hizo....

lakini najiuliza ni njia gani nzuri ya kutumia? kwasababu watu wengine hupendelea kuweka vijiti japo wengine husema vijiti hivyo hutembea mwilini na kuleta madhara ya cancer.

wengine hutumia kitanzi, hiki hukaa muda mrefu wa miaka kumi lakini pia wengine huniambia tatizo la kitanzi style yako kamwe ni kifo cha mende maana ukijifanya unatoa machejo kinafyatuka, na wengine wanasema mwenza wako akiingia kinamtia kero kwa kumgasi...

na wengine wanatumia vidonge, lakini wengine husema ukikosea kumeza kimoja tu na ukacheza basi goli lazima liwe lako, na wengine wamepata ujauzito pindi wanatumia hizi dawa...

ama kutumia condom? sawa kwa mwanzoni mnaweza kutumia condom lakini mpaka lini, maana wanaume wengi wanasema yani mke wangu mwenyewe nimvalie condom???????????? ama kwa wale walevi najua pindi pombe zimekolea nivigumu sana kukumbuka condom....

je wewe umeshawahi kutumia njia za uzazi na ni ipi na je kunamadhara gani uliyokutana nayo???? maana kunawanawake wanaotaka kutumia njia hizi lakini hawajui ipi ni salama maana maneno yanasemwa mengi...

Kama wewe na mpenzi wako hawataki kuwa na mtoto kwa wakati huu, unaweza kuuliza "jinsi ya kuzuia mimba?". Bahati nzuri, kuna bidhaa nyingi tofauti ambayo inaweza kusaidia kuzuia mimba. Aina ya uzazi ambayo ni ya uhakika kwa ajili ya kuzuia mimba ni kuzaliwa kudhibiti dawa, sindano, implantat, IUDs, na sterilization. Ya wanawake 100 ambao kila kutumia moja ya aina hizi za uzazi wa majira kwa mwaka, juu ya 1 hadi 5 wanawake mimba.

kondom ya wanaume na diaphragms na spermicide ni chini ya ufanisi. Ya kila wanawake 100 ambao wanategemea yao kwa mwaka, kuhusu 14-20 mapenzi kuwa mimba. Njia nyingine ya uzazi, kama vile spermicide peke yake, kondomu za kike, na mipango ya asili ya familia, kufanya kazi pamoja.

Jinsi ya kuzuia mimba

Jinsi ya kuzuia mimba? Kuna njia kuu 2 kuzuia mimba: unaweza kupata bidhaa bila dawa moja au unahitaji kuona daktari wako.

Kuzuia mimba bila dawa

Baadhi ya aina ya bidhaa uzazi ambayo yanaweza kuzuia mimba zinapatikana bila daktari dawa. Wao hawana madhara kwa watu wengi. Lakini baadhi ya watu inaweza kuwa na mzio yao na kupata vipele kama matumizi yao.

Kondomu kwa ajili ya Wananchi

Watu wakati mwingine wito kondomu kwa rubbers watu, safes, au kinga. Unaweza kununua kondomu bila ya dawa katika drugstores, maduka makubwa, na maeneo mengine mengi. Ni njia inayojulikana zaidi kuzuia mimba.

Kutumia, kuweka kondom kwenye uume uliosimama kabla ya kujamiiana. Kutumia kondomu kila mara moja tu. kondomu wengi ni alifanya kutoka mpira mpira. Wengine ni alifanya kutoka matumbo kondoo na mara nyingi huitwa lambskins. Baadhi ya kondomu ni alifanya kutoka polyurethane. Kama wewe si mzio wa mpira, unapaswa kutumia kondom kwa sababu ni njia bora ya kuzuia mimba na pia kulinda bora dhidi ya ukimwi, herpes, na magonjwa mengine ya zinaa (STDs). Kondomu haipaswi kutumiwa na Vaseline au bidhaa nyingine za mafuta ya petroli jelly, lotions au mafuta. Lakini inaweza kutumika kwa kulainisha uke na kukuza creams kike kwamba hawana mafuta, kama vile "KY jelly.

Wanawake kondomu

Haki kondomu Mwanamke ni wa maandishi polyurethane. Unaweza kununua kondomu za kike katika drugstores bila dawa. Kutumia, Insert ya kondomu ndani ya uke haki kabla ya ngono na matumizi ya kila mara moja tu kuzuia mimba. Wala kutumia wakati huo huo kama kondomu kiume. Kama wewe kuwa na uchaguzi, ni bora kwa ajili ya mtu kutumia kondomu mpira kwa sababu ni njia bora ya kuzuia mimba kuliko kondomu ya kike.

Spermicide Alone

Spermicides za kutosha bila ya dawa katika drugstores na maduka mengine. Wao vyenye kemikali ya kwamba unaua manii kuzuia mimba. Spermicides ni kuuzwa katika aina kadhaa ikiwa ni pamoja na cream povu na jelly.

Kutumia, kuweka spermicide ndani ya uke angalau dakika 10 kabla ya kujamiiana. Kipimo kimoja cha spermicide kawaida kazi kwa saa moja, lakini lazima matumizi ya dawa nyingine kila wakati wa kujamiiana hata kama chini ya saa moja amepita. Unapaswa douche au safisha uke wako kwa angalau saa 6 mpaka 8 baada ya kufanya mapenzi.

Udhibiti wa kuzaliwa unahitaji kuona daktari wako

Hatari na faida za aina mbalimbali za kuzuia mimba ni tofauti kwa kila mtu. Hivyo ni bora kuamua na daktari wako ambayo namna ya kudhibiti kuzaliwa ni bora kwenu.

Diaphragm

diaphragm The na spermicide ni kuweka ndani ya uke kabla ya ngono ili kwamba inashughulikia mlango wa kizazi, au shingo ya uzazi. Kuweka spermicide katika dome wa kiwambo kabla ya inserting. Lazima uwe utrustade kwa diaphragm katika ofisi ya daktari au kliniki kwa sababu diaphragms kuja katika ukubwa mbalimbali. diaphragm lazima kukaa katika nafasi ya masaa 6 baada ya ngono ili kuzuia mimba, lakini si kwa zaidi ya saa 24. Kama una ngono zaidi ya mara moja wakati amevaa diaphragm, lazima kuongeza zaidi spermicide bila kuchukua nje diaphragm. Spermicide inapatikana bila ya dawa katika drugstores.

Sura ya kizazi

Cap kizazi ni mpira laini kikombe kwa mdomo pande zote kwamba ni kuweka ndani ya uke kwa kufaa juu ya mfuko wa uzazi, au shingo ya uzazi. cap ni ndogo kuliko diaphragm, lakini wakati mwingine vigumu zaidi Insert. Lazima uende kwa daktari wako au kliniki kuwa zimefungwa kwa ajili ya tak kizazi. Inakuja katika ukubwa mbalimbali. cap wa kizazi lazima kutumiwa na spermicide, ambayo inapatikana katika drugstores bila dawa. Unaweza kuondoka katika nafasi kwa masaa 48 basi ni kazi na kuzuia mimba.

Udhibiti wa kuzaliwa Vidonge

Unahitaji dawa daktari wa kupata dawa za uzazi wa mpango, pia hujulikana uzazi wa mpango ya mdomo. Kuna aina mbili za dawa za uzazi wa mpango: "pamoja simulizi za uzazi wa mpango" na "dawa mini."

Pamoja uzazi wa mpango simulizi kuwa na mchanganyiko wa homoni mbili - estrogen na progestin. Kazi kwa kushika ovari kutoka ikitoa yai. kidonge lazima kila siku kuchukuliwa kuzuia mimba.

Mini vyenye dawa moja tu homoni, progestin. Kazi na thickening kamasi kizazi kuweka mbegu kutoka kufikia yai. Wakati mwingine pia kushika ovari kutoka ikitoa yai. Lazima kuchukua vidonge moja kila siku. Mini dawa ni kidogo chini ya ufanisi zaidi kuliko uzazi pamoja mdomo.

Depo-Provera

Depo-Provera ni aina ya progestin, sawa na homoni katika kidonge mini. Depo Provera-lazima kuwa sindano na sindano katika ****** ya mwanamke au misuli mkono na daktari. Lazima kupata sindano kila miezi mitatu kabla ya kuzuia mimba.

Norplant

Norplant ni aina ya progestin kwamba ni kuwekwa chini ya ngozi. Norplant ni wa maandishi viboko mpira ili kuangalia kama matchsticks. Daktari maeneo viboko chini ya ngozi ya mkono wa mwanamke juu, ambapo taratibu kutolewa progestin. Daktari lazima pia kuondoa fito. Kuna aina mbili za Norplant. Ya Norplant fimbo sita wanaweza kuzuia mimba kwa miaka mitano. Ya Norplant mbili fimbo wanaweza kuzuia mimba kwa muda wa miaka miwili.

IUDs

IUD An (Intrauterine hila) ni kuingizwa ndani ya tumbo na daktari. aina mbili za IUDs sasa kutumika katika Umoja wa Mataifa: Copper T 380A Paragard, ambayo releases shaba, na ya Progestasert T progesterone, ambazo releases progesterone, aina ya progestin. Ya IUD Paragard inaweza kukaa katika nafasi kwa miaka 10. Ya Progestasert lazima kuwa kubadilishwa kila mwaka. Daktari lazima kuondoa hiyo.

Mwanaume sterilization (vasectomy)

Outpatient upasuaji ni muhimu kufanya mtu kuzaa, au hawezi kuzalisha kutosha manii na kufanya mwanamke mimba. Hii ni kufanyika kwa muhuri, tying au kukatwa tube kwa njia ambayo manii kusafiri kwa uume kutoka korodani ya. operesheni ya kawaida inachukua chini ya dakika 30 na ni kosa chini ya anesthesia mitaa. Hii ni njia ya ufanisi zaidi ili kuzuia mimba lakini watu ambao wana vasectomies lazima kuwa na uhakika wao kamwe wanataka watoto baba katika siku zijazo.

Wanawake sterilization

Wanawake sterilization ni kawaida operesheni ya muda mrefu zaidi ya vasectomy a, ingawa wakati mwingine unaweza kufanyika kama upasuaji outpatient. Ni kawaida kufanyika chini ya anesthesia ujumla. upasuaji inahusisha tying, kukata au kuzuia zilizopo kwenye fallopian hivyo mayai hawezi kufikia tumbo. Mara nyingine tena, hii ni njia nzuri sana ya kuzuia mimba lakini wanawake walio na hii ni lazima kuwa na uhakika wa upasuaji wao kamwe nataka kuwa na mtoto katika siku zijazo.

Asili ya Uzazi wa Mpango

Hii pia hujulikana kama uzazi ufahamu au kutokufanya mapenzi mara kwa mara. Kwa njia hii ya kufanya kazi, ya mtu na mwanamke hawezi kufanya ngono siku ya mwanamke anaweza kupata mimba bila kutumia aina nyingine ya majira. Siku hizi ni pamoja na kawaida ya siku saba kabla ya mwanamke ovulates (releases yai) kwa siku tatu baada ya yeye ovulates. Mwanamke anaweza kuuliza daktari wake jinsi ya kumwambia wakati yeye ovulates. Hii ni kufanyika kwa kuzingatia wakati wa mwisho alianza hedhi, mabadiliko ya hali ya joto ya mwili, na mabadiliko katika kamasi uke. Njia hii inaweza kuwa na uhakika wa wewe kuzuia mimba kwa sababu mbalimbali mabadiliko ndani yenu mizunguko yanaweza kutokea.

Magonjwa ya ngono kuzuia

Aina pekee ya kudhibiti kuzaliwa kwamba pia ni yenye ufanisi katika kuzuia UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa ni mpira kondomu zivaliwe kwa mtu huyo. Kondomu ya kike inaweza pia kutoa ulinzi, lakini siyo mazuri kama ya kondomu mpira kwa ajili ya watu. Kama matumizi nyingine za kuzuia mimba lakini pia wanataka ulinzi dhidi ya UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa, mtu lazima pia kutumia kondomu mpira.

Muhtasari

Na Dawa Tawala Chakula ina kibali idadi ya mbinu za uzazi wa mpango ili kuzuia mimba. Uchaguzi wa uzazi inategemea sababu kama vile afya ya mtu, mzunguko wa shughuli za ngono, idadi ya wapenzi, na tamaa ya kuwa na watoto katika siku zijazo. Kushindwa viwango, kwa misingi ya makadirio ya takwimu, ni sababu nyingine muhimu. Njia ya ufanisi zaidi ili kuepuka wote mimba na magonjwa ya zinaa ni kutofanya mazoezi jumla (kuacha ngono).

Dhati,
Mtandao wako Doc

 
Ahsante Mzizi-Makvu kwa hii thread. Watu wengi sana wana 'negative attitude' kwa njia mbali mbali za uzazi wa mpango, lakini wengi kati ya hawa sio watumiaji wa njia za uzazi wa mpango, lakini wako mstari wa mbele kuhakikisha watu hawatumii njia za uzazi wa mpango.

Natumai kupata real testimonies za watu/wanawake ambao wanatumia/wametumia njia za uzazi wa mpango kupitia thread hii!
 
Mzizimkavu,

"Usalama/salama" ni nini katika muktadha wa swali lako? Je unakusudia kusema ufanisi (effectiveness) - yaani kufanya kile inachotakiwa kufanya kwa wakati unaotakiwa? Au usalama kwa maana ya kutokuleta madhara kwa mtumiaji?
 
Njia salama kabisa ni kalenda

Nakubaliana nawe Malaika....kalenda ndio njia salama kupita zote, lakini ndio njia ngumu kueleweka na kuifuata kwa uhakika kwa watu wengi tu. Kuna nyingine inaitwa 'coitus inturruptus'...hii ni ile mwanaume akikaribia 'kukojoa' (kumradhi lugha) basi anachomoa uume na kumwaga nje. Nayo ni salama lakini ina ugumu kwenye timing especially kwa wanaume wanaopenda kusikilizia bao. Na si reliable kama mwanaume ni mtu wa mabao zaidi ya moja.
 
vidonge.jpg


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal, katika Mkutano wa mwaka wa Uzazi wa Mpango, Oktoba mwaka huu. Katika Mkutano huo Tanzania ilionekana bado ina matumizi ya chini ya dawa za uzazi wa mpango. Picha na Maktaba




KWA UFUPI

  • Kupanga uzazi ni jambo muhimu katika kujenga familia bora lakini njia za uzazi wa mpango zinatajwa kuzua changamoto kadha wa kadha kwa watumiaji.


Pamoja na kuwa ni njia nzuri ya kuzuia ujauzito, vidonge vya Uzazi wa Mpango vinatajwa kusababisha ugonjwa wa macho ujulikanao kama Glaucoma, unaoelezwa kuwa ni chanzo kikuu cha upofu.

Ugonjwa huu unaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha upofu kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi kwa muda mrefu.

Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa Afya na Lishe uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).

Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.

Wanawake zaidi ya 3,400 wenye umri wa zaidi ya miaka 40 walifuatiliwa kwa zaidi ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya utafiti huo.

Profesa Shan Lin wa Chuo Kikuu cha Carlifonia, San Francisco anasema wanawake wanaotumia vidonge hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu, wanatakiwa kupima maradhi ya macho aina ya Glaucoma na afya zao zifuatiliwe kwa uangalifu na wataalamu wa macho.

Utafiti huo umebaini kuwa wanawake waliotumia vidonge hivyo kwa miaka zaidi ya mitatu walikuwa na hatari kwa asilimia tano ya kupata upofu usababishwao na glaucoma ukilinganisha na wasiotumia vidonge hivyo.

Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen vina umuhimu katika seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.

“Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho,” anasema Dk Pasquale.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.

“Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge,” anasema Dk Masawe anasema si vyema watu kuzitumia dawa za Uzazi wa Mpango kwa mazoea na endapo wataona ni vyema kufanya hivyo, washauriane na wataalamu wa afya.
Anasema kuwa elimu inahitajika kwa kina kuhusu matumizi ya dawa hizo kwani wapo baadhi ya watu wanaozitumia bila mpangilio wala utaratibu maalum.

“Hizi dawa zinasaidia lakini zisipotumiwa kwa uangalifu, huenda zikasababisha madhara,” anasema Dk Masawe.

Kwa upande wa utafiti huo uliojikita kuangalia madhara ya vidonge hivyo kwa wanawake, watu wanaovitumia wanatakiwa kuwa makini na uhusiano uliopo kati ya afya ya uzazi na maradhi ya macho hasa kama mtumiaji amefunga hedhi mapema.

Matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa katika mkutano wa kila mwaka wa Chuo Kikuu cha Mfumo wa Macho Marekani (USP), yanasema wanawake zaidi ya 3,046 walifanyiwa uchunguzi kuhusu afya ya uzazi na maradhi ya macho.

Pamoja na sababu nyingine za maradhi ya macho, wanasayansi waliofanya utafiti huo wanasema kutumia vidonge vya uzazi kwa muda mrefu, ndicho chanzo kikuu cha upofu na kutaja sababu nyingine kuwa ni historia ya familia, shinikizo la ya macho na kisukari.

Watalaamu wa afya nchini wanasema bado madhara ya dawa hizo yanatofautiana kulingana na aina ya dawa anayotumia mhusika.

Madhara mengine ya dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu, kichwa kuuma, matiti kuuma, kuongezeka uzito na kupata hedhi bila mpangilio.

Dk Joseph Matiku wa Kituo cha Afya, Mugumu, Serengeti anasema, hatari zaidi ni kwa binti wanaotumia dawa hizo kwa muda mrefu kabla hawajaanza maisha ya ndoa.

“Wapo wanawake ambao wanapata uvimbe kwenye kizazi kutokana na matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi. Ingawa hakuna utafiti uliofanyika kuthibitisha hili, lakini wanawake wengi wanaotumia dawa hizi hapa nchini wanapata uvimbe maarufu wa Fibroids” anasema.

Hata hivyo, Oktoba mwaka huu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi anasema Wizara ya Afya ipo kwenye harakati za kutafuta fedha ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanawake wanaostahili kupanga uzazi wanapata dawa husika.

Mwaka jana wakati wa Mkutano wa Uzazi wa Mpango uliofanyika London Uingereza, Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania itafikisha asilimia 60 katika huduma za uzazi wa mpango. Vilevile katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Uzazi wa Mpango uliofanyika Oktoba mwaka huu, Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal alisema juhudi za ziada zinahitajika kuhakikisha kiwango cha watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango, kinaongezeka ili kutimiza lengo la kimataifa ya kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hiyo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kuwa, kiwango cha matumizi ya huduma za uzazi wa mpango kwa nchi zilizoendelea ni asilimia 72, huku Tanzania iliyo kwenye kundi ya nchi zinazoendelea ikiwa ni asilimia 27 tu.

Dawa za uzazi wa mpango hufanyaje kazi?

Vidonge vya uzazi wa mpango hufanya kazi ya kuweka uwiano katika kiwango cha vichocheo.

Katika hili, kazi kubwa ni kuzuia homoni za estrogen kuongezeka na kufikia kiwango cha kati au cha juu.

Bila homoni ya estrogen, tezi ya pituitari haiwezi kuifanya mirija ya uzazi kuruhusu mayai yaliyochavushwa kwenda kukutana na mbegu za kiume kwa ajili ya utungishwaji wa mimba.



Ugonjwa huu unaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha upofu kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi kwa muda mrefu.

Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa Afya na Lishe uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).

Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.

Wanawake zaidi ya 3,400 wenye umri wa zaidi ya miaka 40 walifuatiliwa kwa zaidi ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya utafiti huo.

Profesa Shan Lin wa Chuo Kikuu cha Carlifonia, San Francisco anasema wanawake wanaotumia vidonge hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu, wanatakiwa kupima maradhi ya macho aina ya Glaucoma na afya zao zifuatiliwe kwa uangalifu na wataalamu wa macho.

Utafiti huo umebaini kuwa wanawake waliotumia vidonge hivyo kwa miaka zaidi ya mitatu walikuwa na hatari kwa asilimia tano ya kupata upofu usababishwao na glaucoma ukilinganisha na wasiotumia vidonge hivyo.

Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen vina umuhimu katika seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.

“Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho,” anasema Dk Pasquale.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.

“Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge,” anasema

chanzo.
http://www.mwananchi.co.tz/Vidonge-...596774/2092992/-/item/2/-/wp9iiv/-/index.html
 
Hii njia ya kalenda ilikuwa nzuri enzi za wazee wetu sababu tarehe zilikuwa costant sasa hivi na mamisosi haya watu wanayokula, pilikapilika za maisha mara frustuation, mara unawaza kuibiwa, mara sijui nini tarehe zinabadilika badilika utashangaa unaanza kumhisi mkeo vibaya kuwa mimba siyo yako kumbe mambo hayako kama unavyofikiri. Hormone za watu sasa very disturbed ndiyo maana sasa mwanamke makini anatakiwa kuwa tayari kwenda ile safari ya kila mwezi muda wote bila kujali kalenda yake. Nadahani mshasikia mtu anasema jamani mbona siku ilikuwa haijafika. Thats how things is nowdays
 
Kalenda ndiyo the best kwa usalama; lakini ni vizuri ikatumiwa pamoja na mbinu ya kuangalia mabadiliko ya joto la mwili na hali ya ute unaotoka katika sehemu ya siri ya mwanamke.
Tatizo kubwa la njia hii ni kwamba katika kipindi cha kupata mimba mwanamke anakuwa na joto na hamu sana kuliko wakati mwingine. Lile ongezeko la joto huwavutia sana pia wanaume; hivyo inabidi wote wawili wawe na tahadhari.
Inapotokea kuwa wanaona dalili zote hizo - yaani kalenda hairuhusu na ute na joto vinaonyesha hali ya hatari, lakini wote wanaona hawawezi kujizuia then watumie condom hasa za kiume!
 
Njia nzuri na salama ni IUD sababu imeleta suluhisho kwa mapungufu ya njia zingine
1. Condom: ukishindwa kuitumia vizuri haisaidii, na kuna wakati huna condom ndani.
2. Diaphragm and cervical ring: it is not hygienic, tuseme tu ukweli.
3. Pills: They affect the mood na unaweza kusahau au kushindwa kuzinywa wakati fulani (umelala msibani, hujanywa, ukirudi home unakaribishwa na baba...
4. Sindano: Ikiwa unataka kuzaa kati kati ya process, utashindwa kui-reverse, hadi dawa idisolve yote mwilini

Kweli na IUD ina matatizo yake kama heavy bleeding (coper T) au less bleeding (hizi za plastic) ila unakua more in control. Pia ikikutana na mwanamke mwenye hygiene pungufu au wanawake wenye kusafiri sana kama mimi, inaweza kusababisha au ku-worsen infections.
Ila uzuri wake unaweza kuitoa saa yoyote au kubaki nayo for 3, 5 to 10 year, huna pressure ya kukumbuka iko wapi, next check ni lini etc. Na last but not least, you are in control, your partner plays a little role (if at all) in the whole process.
 
Kijiti cha mkononi nimesikia wanawake 3 tofauti kimefanya mapigo yao ya moyo kwenda mbio sana. Mmoja kati yao amepata tatizo la presha kupanda.
 
Russian nimependa maelezo yako. Hapo kwenye IUD za plastic,hiyo less bleeding inaambatana na kuskip kabisa au inapungua tu uwingi? Please elimisha.
Kuna ambao inapoteza kabisa japo sio kawaida. Normally inapunguza sana kiwango cha damu ingawa inaweza kuongeza siku za kubleed (ex: few dark spots the first and last 2 days with 2 light bleedings kati kati). Na hata kwa wale wanao skip, wanaweza kuskip mwezi huu, mwezi ujao ikatoka kidogo etc.

Uzuri ni kwamba hata kama huoni damu huna stress sababu rate of failure ni 1/10 000 which is namna ya kusema "virtually impossible".
 
.....Kalenda njia salama, lakini inabidi mumeo awe muelewa na mshirikiane kwa pamoja. Kama una mume anayependa sex mara nyingi na bila schedule maalum hii haifai. Vile vile kuna hii njia, unaweza kuzaa hata mfululizo idadi ya watoto unaohitaji and then funga mirija.

Madawa hayo siyo mazuri hata kidogo, hao wenyewe madaktari wa kike hata hawatumii.
 
Ok hasa tunafikia bilioni 7......
Kwa TZ wanasayansi jamii wanasema asilimia 96 ya wakinamama wenye umri wa miaka 15 mpaka 49 ambapo wengi wao wanaweza kupata ujauzito bila kipingamizi wameshawahi kusikia kwamba kuna njia za kupanga uzazi. ambao hawajaolewa ni asilimia arobaini na ushehe hizi ndio wanaotumia njia za uzazi wa mpango na wale walio kwenye ndoa watumiaji ni asilimia 27.
Hebu niendelee kuona wapi wanajamvi wataangukia na kutujuza wadhaniavyo wao.
Good staff MM
 
Mimi nadhani njia salama ni kalenda tu. Mimi nina mfano wa rafiki yangu ambaye alikuwa mtumiaji mzuri sana wa sindano
mwanzoni hazikumpa shida lakini baada ya mwaka 1 ndipo alipoanza kuona joto ya jiwe yaani amebleed kwa muda kama wa miezi 8 mfululizo.

Mpaka akahisi ataishiwa damu, ametumia dawa kwa muda mrefu mpaka akahisi amelogwa lakini Mungu ni mwema sasa hivi amepata nafuu, amesema amekoma hatarudia tena kutumia hizo njia za uzazi wa mpango.
 
Back
Top Bottom