Wanandoa, hii imekaaje?

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
habari zenu wanandoa na wanajf kwa ujumla. imagine kabla ndoa ulikuwa na best friend wa kiume/kike ambaye alikuwa close na wewe (SIO MPENZI) mlikuwa mkisaidiana katika shida na raha ikafika wakati wa kuachana na ukapera yan kuingia ktk ndoa... je uliendelea na urafiki na huyo rafiki yako? kama uliendelea mkeo/mmeo aliuchukuliaje urafiki wenu? je uko huru na urafiki wenu kama awali? ama unau-handle vipi huo urafiki?
 
Mbona mimi na Eiyer tunaendelea kuwaenzi mabest friends zetu; tunaaminiana!

That is Kaeiyer world; back to ur world nyie vizazi vya....sisemi...

Mara nyingi kunakuwa na limit hasa pale mwenzi wako anapokuwa na wivu. Inabidi kupunguza mawasiliano, kupena siri na utani kama ulikuwepo. Ni vizuri usimpe mwenzio sababu za kukudoubt.
 
Mimi nimepunguza mawasiliano naye kwasababu wife wangu alikuwa hapendi. Hata kwa upande wake mume wake walikuwa wanagomba sana hivyo tukaamua kutumia busara kupunguza mawasiliano hasa wakati wa usiku na weekend. Ilikuwa ngumu lakini sasa tumezoea tunawasiliana mara chache sana na wakati mwingine tunapotaka kuombana ushauri au kuliwazana maana tulishibana sana. Ndio hivyo maisha yanaenda.
 
Zingatia hapo kwenye red, nyie ndo mnaofanya urafiki huo usiaminike sasa mnaliwazana kitu gani.kha!
 
Kaeiyer 4 ever,wenye vijino pembe jinyongeni!. . . . . . . .Back to the topic,ki kawaida katika mahusiano yoyote mkiaminiana itakuwa ndo salama yenu.Pia lazima pia mjiamini(kama mimi na Kaunga)suala la urafiki wenu uwe na mipaka.Sio kwa sababu ulikua unampigia simu usiku wakati hujaolewa/oa unataka utaratibu huo uendelee,no!
 
habari zenu wanandoa na wanajf kwa ujumla. imagine kabla ndoa ulikuwa na best friend wa kiume/kike ambaye alikuwa close na wewe (SIO MPENZI) mlikuwa mkisaidiana katika shida na raha ikafika wakati wa kuachana na ukapera yan kuingia ktk ndoa... je uliendelea na urafiki na huyo rafiki yako? kama uliendelea mkeo/mmeo aliuchukuliaje urafiki wenu? je uko huru na urafiki wenu kama awali? ama unau-handle vipi huo urafiki?

kutengana kwenu kunategemea na mtu uliyempata, pia inategemea na uhusiano mliokuwa nao kwani wengine baada ya kuona upande mmoja umeshakuwa bize na familia unaanza chuki na majungu
 
Hili swala linategemea mkoje. but kwa maisha ya kawaida its better mkapunguza ili kuwapa nafasi wenza wenu. inapendeza zaid mkabaki na marafiki wa jinsia moja kuliko kuwa jinsia tofauti.
 
Mahusiano yatapungua automatically sababu interests na priorities zitatofautiana.
 
Mimi nimepunguza mawasiliano naye kwasababu wife wangu alikuwa hapendi. Hata kwa upande wake mume wake walikuwa wanagomba sana hivyo tukaamua kutumia busara kupunguza mawasiliano hasa wakati wa usiku na weekend. Ilikuwa ngumu lakini sasa tumezoea tunawasiliana mara chache sana na wakati mwingine tunapotaka kuombana ushauri au kuliwazana maana tulishibana sana. Ndio hivyo maisha yanaenda.
huyo wife wako usipomwangalia ataua ukaribu hata wa baadhi ya ndugu zako wa mbali, maana wengine hawaamini mabinamu n.k. huyo rafiki ungekuwa unampenda sana si ungemuoa?
 
Kwa upande wa familia hana tatizo hata kidogo-amepata 100/100 toka kwa ndugu awe wa mbali au wa karibu.
Kwanza lazima ukubali ndoa ni baraka ya mwenyezi Mungu. Halafu ukumbuke kuna sababu na mazingira tofauti tofauti yanayokutanisha marafiki na mengine hufuata.
 
kila la heri. itabidi sasa uwe na marafiki manjemba tu...............lol! watu wengine wanapenda kudanganya! maana najua kabisa haiwezekani kabisa usiwe na rafiki wa jinsia nyingine........... jaribu lakini, maana ndoa ni BARAKA
 
Ahsante sana. Ila sijasema sina marafiki wa jinsia ya kike, hapa tunajadili yule special friend ambaye tulishibana sana. Wengine wapo ni kawaida katika maisha. Hata wewe tunaweza kuwa marafiki usiogope.
 
kama alikuwa ni best friend, siyo mpenzi, ni wazi kabisa huyo mtarajiwa atakuwa au ameshakutana naye au ameshamsikia sana kutoka kwako. kwa maana hiyo sidhani kama kuoa/kuolewa kwako kutabadilisha fact kwamba huyo ni rafiki yako.

mkùu we wasema, ktk u-bf/gf unakuta mtu anatoa masharti huyu rafiki yako ctaki kumsikia na urafiki wenu ufe. hapo hamjafunga ndoa je mkifunga ndoa je.... utachaguliwa marafiki
 
Back
Top Bottom