Wananchi wataka mwekezaji aondolewe

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wananchi wataka mwekezaji aondolewe

Gordon Kalulunga, Mbeya

SAKATA la vurugu zilizojitokeza katika eneo la Ubaruku, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya limechukua sura mpya baada ya wananchi kumpa siku tatu Mwekezaji mwenye asili ya Kiasia (Mburushi) kuondoka katika Wilaya ya Mbarali.

Tamko hilo limetolewa juzi katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini waliofika katika eneo hilo wakiongozwa na Mchungaji William Mwamalanga ambaye pia ni mkurugenzi wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya kuhifadhi mazingira Mkoa wa Mbeya.

Wananchi hao ambao walikuwa wameshika silaha mbalimbali wakikusudia kuelekea kwenye makazi ya mwekezaji huyo aliyetajwa kwa jina la Abrahakh Phil Mohamed, kwa ajili ya kufanya uharibifu lakini walisalimisha silaha zao huku wakitoa tamko.

‘’Tumenyonywa vya kutosha na hawa waburushi tunataka waondoke katika maeneo haya kwa muda wa siku tatu, la sivyo tutafanya kile tunachokijua maana tumechoshwa nao wakiwemo viongozi wa serikali ambao hawamuungi mkono mbunge wetu tuliyemchagua kututetea,’’ walisema wananchi hao huku wakitulizwa na wazee waliokuwepo eneo hilo .

Kwa upande wake Mchungaji William Mwamalanga, aliwasihi wananchi hao kupunguza jazba na kudai atawasiliana na viongozi wa Serikali Kuu ili kutatua kero hizo pamoja na kupata ukweli wa sakata la polisi kuua raia na kusababisha kuchomwa moto gari la mafuta na kisima cha mafuta.

Aidha, Tanzania Daima Jumapili lilimtafuta Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Cosmas Kayombo, ambaye aliwashukuru wachungaji hao kwa kusuluhisha na kuwatuliza wananchi hao.

Kayombo alipoulizwa juu ya tamko la serikali kutekeleza tamko la wananchi la kumtaka mwekezaji kuondoka ndani ya siku tatu katika wilaya hiyo, alisema kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria hivyo tamko hilo si sahihi.

Chanzo: T. Daima Jumapili



My Take:

Serikali ya JK haina ubavu wa kumuondoa Mwekezaji huyo kwani ni binamu wa RA. Nyie mtaona tu. Labda watu wafe tena -- kwani huo sasa ndiyo umekuwa mtindo wa utawala huu wananchi wanapodai haki.
 
Back
Top Bottom