Wananchi warudi kwenye makazi yao bila ukaguzi?

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
966
537
katika jambo lililonisikitisha jana ni jinsi ambavyo serikali yetu isivyokuwa makini katika kushugulikia majanga. Rais wa nchi tena amiri jeshi mkuu anawatangazia wahanga kuwa warudi majumbani kwa sababu hakuna mabomu yatakayolipuka tena hali imedhibitiwa. Au kwa vile yameacha kulipuka kwenye kambi ndo hali imezibitiwa? Wao wenyewe wamewatahadharisha watu kuwa kuna wabomu ambayo yametawanyikia kwenye makazi ya watu hivyo watu wachukue tahadhari. kwa layman tahadhari ya kuokoa maisha si ni kukaa mbali na eneo la tukio. Wanafikiri wananchi wamesahau yaliyotokea mbagara baada ya wananchi kurudi kwenye makazi yao huku kukiwa na mabomu ambayo hayajaripuka?

Mi nilitegemea kwa kuongozi wa nchi kuwaagiza wanajeshi wake wote kuingia mitaani kwenye maeneo yaliyoathirika na kufanya ukaguzi kuhakkikisha kuwa hakuna mabomu kwenye makazi ya watu ndipo wananchi wahamasishwe kurudi majumbani kwa kuwa maeneo yao ni salama. Lakini wapi ni rais yule yule wa utendaji uleule wa kulegalega.
 
Back
Top Bottom