Wananchi wamtetea Waziri Magufuli; Wahoji iweje JK, Pinda wamzuie kutekeleza sheria?

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797




*Wahoji iweje JK, Pinda wamzuie kutekeleza sheria

KATIKA hali inayoashiria ni ya kumtetea waziri wa ujenzi nchini, Dkt. John Magufuli baadhi ya wananchi wameeleza kusikitishwa na mashambulizi yanayoelekezwa kwake na
wakuu wake wa kazi kutokana na agizo lake la bomoabomoa katika maeneo ya hifadhi ya barabara.

Wananchi hao wamesema kauli za hivi karibuni zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kupinga agizo lililotolewa na Dkt. Magufuli kuhusiana na suala la ubomoaji wa majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara zimetolewa bila ya kutumika kwa busara.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana mjini Shinyanga, wananchi hao wamedai kauli hizo za Rais Kikwete na Bw. Pinda zinaweza kumuathiri kisaikolojia Dkt. Magufuli kwa njia moja ama nyingine na kusababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake mengine kikamilifu.

Walisema agizo lilitolewa na Dkt. Magufuli ni suala la kisheria, na kwamba alichotekeleza yeye ni kuweka mkazo ili sheria hiyo iweze kuheshimiwa, na hali hiyo inatokana na sehemu kubwa ya Watanzania kujenga utamaduni wa kutoheshimu sheria za nchi zilizopo hasa katika sekta ya ardhi.

Wananchi hao walisema hata kama ungekuwepo umuhimu wa kumtaka Waziri Magufuli kupunguza kasi ya utekelezaji wa agizo lake hilo, basi busara ingetumika zaidi kwa kulijadili suala hilo ndani ya kikao cha Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais Kikwete mwenyewe badala ya kumkemea hadharani.

Kwa kweli Dkt. Magufuli hajatendewa haki, alianza kushambuliwa na kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni, Bw. Pinda, tena kibaya zaidi yeye aliamua kwenda kumshambulia mbele ya wapiga kura wake jimboni Chato, sasa kwanini Bw. Pinda hakupeleka suala hili ndani ya Baraza la Mawaziri, ambapo angemuomba huyu bwana apunguze kasi yake?

Mimi binafsi sipingani sana na Bw. Pinda au Rais Kikwete, lakini kinachonisikitisha ni jinsi ya hawa viongozi wetu walivyoamua kumzuia mbele ya kadamnasi, wengine tumehisi serikali haiko pamoja katika utekelezaji wa majukumu yake, maana haya ni mambo ya ndani wangekaa na kuelezana huko badala ya utaratibu uliotumika.

Kwa kawaida Magufuli anafahamika, kila anapokabidhiwa wizara hupenda kuona sheria inafanya kazi yake, hata kule kwenye uvuvi alibadili hali ya mambo, watu waliheshimu sheria, kwa vile hakuna wakubwa huko wanaofanya kazi ya uvuvi mdogo mdogo hakuna aliyepiga kelele.

Sasa leo kwenye bomoabomoa imekuwa tatizo, na nafikiri wakubwa na vigogo wengi hapa nchini wamejenga katika maeneo ya hifadhi, ndiyo maana anapigwa stop kubwa, kwa kweli hajatendewa haki, maana rais naye juzi kakomelea msumari kwenye kauli za Pinda alizotoa kule wilayani Chato,” alieleza Bw. Shija Stephen mkazi wa Maganzo.

Kwa upande wake mmoja wa makada wa CCM mjini Shinyanga ambaye hata hivyo hakupenda kutajwa gazetini alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete iliyodai kuwa Bw. Magufuli anatumia ubabe zaidi katika utekelezaji wa shughuli zake.

Kada huyo alisema kauli hiyo haikuwa nzuri kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu nchini, na kwamba huenda ikasababisha watu wenye tabia ya kuvunja sheria waendelee kufanya hivyo kwa vile wataamini yupo atakayewatetea na kwamba ameagiza walipwe fidia pale wanapovunjiwa.

“Binafsi sijafurahishwa na kauli ya Rais Kikwete kudai kuwa Bw. Magufuli anatumia ubabe katika utekelezaji wa shughuli zake, hii wizara ya ujenzi pamoja na ile ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi zinahitaji watu kama Bw. Magufuli, ukitumia siasa zaidi katika wizara hizi ni wazi utakwama.

Wapo watu wamekuwa wakitumia uwezo wao wa kifedha kufanya lolote wanalotaka hata kama linapingana na sheria, sasa leo tishio la Bw. Magufuli limewashtua alipoelezea dhamira yake ya kubomoa majengo yote yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara wakaona na wao wataguswa.
Bw. Magufuli alianza kwa kuonesha mfano wa uvunjaji wa ofisi za Tanroads jijini Dar es Salaam, jengo lilijengwa ndani ya eneo la hifadhi, alitumia busara, maana huwezi kuvunjia watu wengine wakati wewe mwenyewe jengo lako limejengwa kimakosa, na alisema hata kama ni jengo la CCM atabomoa, hii imetisha watu,” alieleza kada huyo wa CCM.

Aidha baadhi ya wananchi hao wameonesha wasiwasi iwapo Bw. Magufuli ataendelea na utekelezaji wa majukumu yake mengine ya kikazi kwa vile anaweza kuogopa kukemewa tena na viongozi wake wa ngazi ya juu, kitu ambacho kitasababisha akae ofisini na kusubiri kupokea ujira wake wa mwezi kama walivyo baadhi ya mawaziri.

Hata hivyo, Bw. Magufuli mwenyewe amemthibitishia Rais Kikwete kuwa ataendelea kutekeleza majukumu yake na kusimamia sheria bila kulegea na kwamba daima ataongozwa na kiapo chake alichokula alipokuwa akiapishwa kushika wadhifa huo.

Wakati huohuo Wizara Ujenzi imekanusha madai ya gazeti moja kuwa gharama za ujenzi wa barabara zimepanda baada ya Magufuli kuingia katika wizara hiyo hadi kufikia sh bilioni 1.4 kwa kilometa moja ya lami.

Katika taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, wizara hiyo ilitoa ufafunuzi kuwa utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 260 ambao umegwanyika sehemu tatu ili kuhakikisha utendaji kazi.

Ilieleza kuwa sehemu ya kwanza ni ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Migori yenye urefu wa kilomita 95.1 sehemu hiyo imejengwa na mkadarasi SIETCO kwa gharama ya sh. bilioni 84 ambayo ni wastani wa sh. milioni 886 kwa kilomita moja ya lami na inategemewa kukamilika Januari 13, 2014.

Ilieleza kuwa sehemu ya pili ni kutoka Migoli hadi Fufu escarpment yenye urefu wa kilomita 93.8 na itajengwa na mkandarasi SIETCO kwa gharama sh. bilioni 73.61 ambayo ni wastani wa sh. milioni 785 kwa kilomita moja ya lami na inategemewa kukamilika Januari 13, 2014.

Ilieleza sehemu ya tatu ya ujenzi huo ni Fufu hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 70.9 inajengwa na Mkandarasi China Communication Construction kwa gharama ya sh. bilioni 64.33 ambayo ni wastani wa sh. milioni 907 kwa kilomita moja na inatarajiwa kukamilika Aprili 26, 2013.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Msemaji wa Wizara hiyo, Martini Ntemo ilieleza kuwa gharama za ujenzi huo ziko chini sh bilioni 1 kwa kilomita moja kwa lami tofauti ha gharama za miradi mingine ambayo iko zaidi ya sh. bilioni 1 kwa kilomita.
 
... kama nilivyoandika kwenye thread ya Mwanakijiji narudia tena kwamba tatizo sio bomoa bomoa ila ni pamoja na KUMTOA yule MREMA pale TANROADS na kwa hivyo KUKATISHA ulaji wa zile bilioni zitokanazo na gharama ya kutengeneza kilomita moja ya barabara ya lami kupandishwa hadi 1.5 billion. MAFISADI wenzake walifaidika sana na hilo. Ikumbukwe pia kwamba mkataba wake uli-expire siku nyingi ila AKAWA na ubavu na WATETEZI akabaki pale. Follow the money trial na WATETEZI wake ni kina nani na hapo utapata jibu ni kina nani wamekasirishwa na hilo.
Kwanza mtoto wa mkulima akatumwa kumdhalilisha kule Chato, halafu BOSI wao akarudia hayo hayo pale WIZARANI. Cha ajabu na kituko kingine ni kwamaba ile sheria ya eneo la barabara kuwa mita 30 ilisainiwa na BOSI huyo huyo!!! Chew that.
 
ccm wote wakola! ccm wote wazabizabina! mambo ya 2015 njia nyeupe kwa El
 
Kwahiyo kama ni hivyo kwanini wasimbadilishe wampe Wizara nyingine? Au kumuondoa? Watu wamehonga wamepewa viwacha uchwara

Nchi Zingine Sheria ni Mkononi unabomoa kesho kila mtu ana akili ya kujua what to do to be alocated a correct plot na sio kuhonga.
 
Nchi hii hatuna viongozi, PINDA na JK lao moja kwa vile hata kusimamia sheria za nchi wameshindwa wanabaki kuangalia nani anakichafua chama chao kwa akili yao ilivyofinyu. Hivyo wao wanaona wanaotekeleza sheria si watu wazuri wanachafua chama chao. Sijawahi kuona serikali inayoongoza bila kufuata sheria za nchi kama ya JK.

Wanasahau hata serikali ikiwa ya Chadema sheria za nchi zinafuatwa.
 
Back
Top Bottom