Wananchi wakamata Punda mia mbili wanaodaiwa kuibwa Mkoani Arusha

OGTV

JF-Expert Member
May 22, 2016
353
167
Wakazi wa kijiji cha Naberera kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji wamekamata zaidi ya Punda Kihongo miambili wanaodaiwa kuibwa kwenye maboma ya wananchi na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma huku sabini kati yao wakiwa kwenye gari aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 983 ABK na hadi sasa watu sita wamekamatwa kwa tuhuma hizo wakiwemo Afisa mtendaji na Bwana mifugo wa kijiji hicho.
 
Hivi aliyeruhusu biashara ya hawa Punda ni nani. Punda wenyewe hata kabla ya kuanza hii bis=ashara ni wachache mnooo. |Hivi walifanya research kwanza?!?!?!
 
Hivi Dodoma ndio kuna kiwanda cha Punda cha Wachina.....ambacho kilitaka kumfukuzisha kazi Heche Suguta?
 
Hivi Heche Suguta baada ya kurudishwa kazini kimya kimya alikatazwa kuonekana kwenye vyombo vya habari? sioni tena zile harakati zake.
 
Kwani alirudishwa Mkuu..nilimuona siku moja maeneo fulani ya faragha pale Dodoma akilia na kusaga meno mbele Januari Maropes akimuomba amrudishe maana "atakuwa mzigo kwa familia masikini"
 
Hiki kiwanda kingefungwa tu watatumalizia hawa punda nasikia kwa siku hao wachina wanachinja sio chini ya punda mia 3.
 
Wachina bwana, nawachukia kuliko. Na wa TZ, tumekuwa kama tumerogwa na biashara huria, tunaiga tu na kushiriki biashara hii! Ajabu sana!
 
Back
Top Bottom