Wananchi wahofia maji kuwa na sumu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,267
33,039
Waiomba serikali iwachunguze afya
Wakazi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wameiomba serikali kupeleka wataalamu kuchunguza afya zao kutokana na hofu ya miili yao huenda imeathirika kwa kutumia kwa muda mrefu maji ya miferejini yaliyochanganywa na sumu ya madawa ya kuulia magugu na wadudu.
Walisema sumu hiyo ni ile inayotokana na madawa ya kuulia magugu na wadudu pamoja na mbolea mbalimbali ambayo ilikuwa ikitumika kwenye mashamba ya mpunga ya Kapunga.
Wananchi hao walitoa ombi hilo jana baada ya jopo la waandishi kutoka mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma na Rukwa ambao wapo kwenye mafunzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa (Climate Change) yanayoendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) walipotembelea kijiji hicho kuona ni changamoto zipi wanazokabiliana nazo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa dunia.
Walisema tangu mwaka 1990 wakati mashamba hayo ya Kapunga yakiwa chini ya Nafco walikuwa wakitumia maji ya mifereji kwa matumizi ya kunywa na kupikia kutokana na tatizo la maji lililokuwa likilikabili eneo hilo kwa muda mrefu.
Waliongeza kuwa kutokana na kutumia maji hayo ya mfereji ambayo yalikuwa yakitiririka kutoka kwenye mashamba ya mpunga yaliyokuwa yanawekwa mbolea mbalimbali zenye sumu kipindi hicho kulizuka magonjwa ya matumbo ambapo sasa hawana imani kama miili yao ipo salama kutokana na kuyatumia maji hayo kwa muda mrefu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maji ya kijiji cha Kapunga, Gerevas Siyame alisema wananchi wa kijiji hicho wanalishukuru Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) ambalo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali limeweza kufadhili ujenzi wa mradi wa kisima cha maji na hivyo wananchi kuachana na kutumia maji ya miferejini.
Fundi maji wa kijiji hicho, Brighton Ngeja alifafanua zaidi kuwa kutokana na kukamilika kwa mradi wa kisima cha maji umewezesha wananchi 2250 kupata huduma ya maji safi ambapo vituo 13 vya kuchotea maji vimefunguliwa katika maeneo mbalimbali ya kijiji hicho.
Ngeja alisema utaratibu uliowekwa ni kwamba maji yanafunguliwa kila siku kuanzia saa tisa alasiri hadi saa mbili usiku ambapo wananchi muda huo hupata fursa ya kuchota maji kwenye vituo hivyo ambapo kila mwezi kaya inachangia Sh.2600 kama gharama za kutumia maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, George Kagomba alisema tatizo la maji kwa wilaya hiyo siyo kubwa sana kama ilivyo kwa wilaya nyingine kwani upatikanaji wa huduma ya maji ni wa kiwango cha zaidi ya asilimia 70.
Kagomba alisema kutokana na msaada wa Benki ya Dunia ambayo inakusudia kutoa zaidi ya sh.milioni 170 kwa ajili ya kusaidia miradi ya maji kwenye wilaya hiyo, tatizo la maji litakuwa historia miaka miwili ijayo.

http://www.ippmedia.com/?item=15032007news
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom