Wananchi wachoshwa na Mwananyamala

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
BAADA ya siku chache toka sakata la kuchomwa sindano kwa mtoto na kusababisha mkono huo kuoza na kukatwa wananchi wafika katika hospitali hizo kuonana na uongozi wa hospitali hiyo. Watu kadhaa walifika hospitalini hapo kuomba uongozi wa hospitali hiyo kuonea huruma wananchi kwa vitendo vinavyofanyika hospitalini hapo na kuomba wajirekebishe watawadhuru wananchi wengi.

“Tunaomba mtuonee huruma jamani vitendo vya mauaji vimezidi hapa, tutakwenda wapi jamani na hii ni hospitali ya wilaya” au wauguzi hawalipwi mishahara jamani tuhurumieni” walilalama baadhi ya wakina mama kwa huzuni baada ya kutokea kwa tukio hilo

Mtoto Sabry Ibrahim alikatwa kiganja chake cha mkono baada ya kuchomwa sindano na muuguzi wa hospitali hiyo wakati alipolazwa hospitalini hapo.

Awali mtoto huyo alizaliwa katika Hospitali ya Mwananyamala wiki hii, na baada ya kuruhusiwa alirudi nyumbani lakini siku chache baadae mama wa mtoto huyo alihisi mwanaye anaumwa hivyo akaamua kumrudisha hospitali hapo.

Ilidaiwa kuwa mara baada ya kumfikisha hospitalini hapo muuguzi mmoja wapo aliyempokea alimchoma sindano, lakini siku chache tu mkono wa mtoto huyo ulivilia damu na ulianza kuoza.

Baada ya kuona hali hiyo, alimpeleka hospitalini ya Taifa Muhimbili MNH na alipofika hapo madaktari walimshauri mwanaye akatwe mkono kwa kuwa ulikuwa ukwishaoza kabisa.

Hivyo kutokana na ushauri huo, mtoto huyo alikatwa kiganja chake cha mkono.
 
Back
Top Bottom