Wananchi wa Bumbuli waanza kumchoka January Makamba

Hata mimi nimefurahishwa sana na matendo ya January kama kweli ndio haya, maana hakuna watu wanafiki kama wananchi wa Bumbuli, yaani mzee wa watu kaongoza vita kubwa sana dhihi ya unyonyaji wetu sisi wote, walichofanya ni kumdhalilisha kwa namna ya ajabu leo wanasema nini? kwanza nasikia hao wenyewe huko sio kwao dingi alikuja kutoke iringa kama manamba, sasa leo wanamtakia nini. Heko January mwendo mdundo kama watu wenyewe hawana internet ama skype na hawajanunua ipads sasa wewe ufanye nini? kwanza kitabu chenyewe cha kuwaombea misaada umekiandika kiingereza sasa kama wao wanajua kisambaa tu wewe ufe? halafu watamchaguaje muwakilishi asiyeongea lugha yao? imekula kwao teh teh tehe kweli wajinga ndio waliwaao.. kula kwa kwenda mbele hayo mambo ya 2015 watajiju wakati huo dili lako la Dowans litakua lisha tiki huku wao umaskini ukwaparami mpaka kwenye kope

Daah Mzee hii ni kali,wanaweza kuwa wamekosea lakini daah umewapa makavu sana as if everbody alikuwa anajua yote hayo,wengine hufata mkumbo kaka na wengine sincerely hakuna wanalojua,so jamaa ndo ana-take advantage ya wao kutojua kitu..inasikitisha
 
Kwanza natoa lawama zangu kwa wananchi wa Bumbuli kwa kuikumbatia CCM kwa mika mingi huku wakiendelea kupigika kimaisha na kwa ujumala mkoa mzima wa Tanga umekuwa ngome kubwa ya Chama Cha Mafisadi namatokeo yake wamekuwa mafukara wa kutupwa. Nafikri sasa wameanza kufumbuka macho na kugundua kuwa kuichagua CCM ni kuchagua umasikini. Pili natoa lawama kwa Uongozi wa juu wa Chadema, kwani mwezi Juni 2010 nilikuwa Bumbuli na nilikuta vugu vugu kubwa la uchaguzi na kulikuwa na kambi kubwa mbili, ya Shelukindo na ya Januari Makamba, mpambano ulikuwa mkali nami kwa vile siipendi CCM nilifurahia mpamabano huo na kuona ni neema kwa upande wa upinzani, na nikaenda hatua moja mbele kumwandikia barua Mwenyekiti wa Chadema Taifa kupitia email adres niliyopata kwenye tovuti ya CDM, kuelezea hali hiyo na kushauri kuwa waitumie nafasi hiyo lakini sikupata jibu wala sikuona kama ushauri wangu kufanyiwa kazi matokeo yake ndiyo hayo ya huyu fisadi mtoto kupita bila kupingwa.
 
Ushabiki ukizidi tunakuwa kama wehu. Najua hili ni jamvi la Chadema, but irrationality will not save us.

Umesema Bumbuli kuna shida ya maji na barabara mbovu, halafu u blame Mbunge Makamba (Who was just elected last year) and then you go and praise Mzee Shelukindo kuwa ni mpiganaji but he was mbunge for 15 years? How do u explain that kind of intellectual dishonesty?

Huku Tegeta kwetu kuna shida ya maji, as the matter of fact, tunanunua maji kila siku. But It would be stupid to blame that on Halima Mdee, she just started ubunge.

Maybe its not really worthy arguing with this kind of thinking/posting. The motive of mtoa mada ni kupaka matope.

Mtoa hoja anasema mbunge hana mikakati yoyote ya kuleta maendeleo, this is FALSE. Mtoa hoja kaamua kutudanganya, mipango ya kuleta maendeleo ipo hadi kwenye kitabu. Ukiamua kupiga fitina ungesema kwamba mipango ya kuleta maendeleo haitekelezeki, hapo labda tungekuelewa. Ndio maana nikasema hii post imekaa kimajungu.

Sijui unaishi Tegeta ipi isiyo na maji. Mimi niko Tegeta maji bwerere
 
Ndugu, give him a brake! Mwenzetu ndo kwanza tu amechaguliwa - leo hii miezi minne tu. Na ana mipango mingi ya maendeleo na Mungu atampa uwezo wa kuitekeleza. Mimi nimepitia website yake na kusoma mambo mengi sana pale; kiukweli ana ndoto nyingi kwa Bumbuli na ndo kwanza ameanza kazi - tusubiri tuone utekelezaji wake. Sina shaka katika kipindi chake ataibana serikali ifanye mengi iliyoahidi kwa Bumbuli, na yeye atawezesha mengi kwa ushawishi wake. Tumpe nafasi afanye kazi.

Ubunge si kazi ya mchezo hata kidogo! Kuna mambo mengi, majukumu mengi, na kwa Mbunge serious kama January, kusinzia ukiwa unatoka jimboni si jambo la ajabu - unakuwa umechoka kweli. Kila nikiwa Jimboni nachelewa kulala na kuwahi kuamka kuliko kawaida!

Majungu na fitna za namna hii si nzuri. muacheni mtu afanye kazi, akishindwa mtaweka mgombea wakati ukifika, na hii ndo maana halisi ya demokrasia ya upinzani na ushindani! Siyo kumchafua mtu. Na ameanza vizuri kazi kama Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati Nyeti. Wana Bumbuli mnaosoma hii habari watulizeni wenzenu, waambieni wana kila sababu ya kujivunia Mbunge wao; ni kijana msomi, ana upeo mkubwa na zaidi ya yote anakubalika (ndiyo maana kachaguliwa kwenye kamati nyeti na muhimu kama hiyo katika kipindi tete kama hiki!)
 
mimi naona wewa ni adui yake wa kisiasa, inawwzekana wewe ni upande wa mzee mzima alyeshindwa wakati wa kura za maoni. kwani kama mito imekauka kwa sababu ya kukata miti ovyo, unataka mbunge afanye nini? apande miti na kuimwagilia?
 
Hizi ni hadithi za kawaida,, ukienda karibu kila jimbo utaseikia tu maneno kama haya. Kwanini? Kwa sababu wapo ambao ni wapinzani na wasiompenda mbunge aliyechaguliwa. Nenda popote utaniletea maneno hayo. Sasa wewe unaona hii nayo ni point kuileta hapa? Unamchoka mtu in 4 months? Kisa eti alijifanya kasinzia? Na je kama alikuwa kasinzia kweli? Huyu kijana mimi namfahamu vyema, Bumbuli wamelamba DUME, na hawatajuta.
 
sijaipenda sana threat, but kwa vyovyote ilitegewa hivyo, like father like son, walitegemea nini wana Bumbuli zaidi ya hayo?
 
Hamkuweka mgombea 2010 (Slaa ain't no dummy), and I double dare you kuweka mgombea Chadema Bumbuli 2015, u will be obliterated. Thats all I can say.
Hii statement kama imetolewa na mbunge ni totally unnecessary.It will cause more hatred.Hakuna tofauti na George Bush aliposema "bring them on" baadaye alijuta
 
Swali ni moja tu? hivi baada ya kuandika haya umejisikiaje?

Kwanini mpembe wenu amewatupa wananchi?

Hivi kile kitabu alichoa andika alienda kugawa mashuleni angalau wawe wanasoma Bumbuli story?
 
Ndugu, give him a brake! Mwenzetu ndo kwanza tu amechaguliwa - leo hii miezi minne tu. Na ana mipango mingi ya maendeleo na Mungu atampa uwezo wa kuitekeleza. Mimi nimepitia website yake na kusoma mambo mengi sana pale; kiukweli ana ndoto nyingi kwa Bumbuli na ndo kwanza ameanza kazi - tusubiri tuone utekelezaji wake. Sina shaka katika kipindi chake ataibana serikali ifanye mengi iliyoahidi kwa Bumbuli, na yeye atawezesha mengi kwa ushawishi wake. Tumpe nafasi afanye kazi.

Ubunge si kazi ya mchezo hata kidogo! Kuna mambo mengi, majukumu mengi, na kwa Mbunge serious kama January, kusinzia ukiwa unatoka jimboni si jambo la ajabu - unakuwa umechoka kweli. Kila nikiwa Jimboni nachelewa kulala na kuwahi kuamka kuliko kawaida!

Majungu na fitna za namna hii si nzuri. muacheni mtu afanye kazi, akishindwa mtaweka mgombea wakati ukifika, na hii ndo maana halisi ya demokrasia ya upinzani na ushindani! Siyo kumchafua mtu. Na ameanza vizuri kazi kama Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati Nyeti. Wana Bumbuli mnaosoma hii habari watulizeni wenzenu, waambieni wana kila sababu ya kujivunia Mbunge wao; ni kijana msomi, ana upeo mkubwa na zaidi ya yote anakubalika (ndiyo maana kachaguliwa kwenye kamati nyeti na muhimu kama hiyo katika kipindi tete kama hiki!)

Ndo zenu hizo miaka 5 sio mbali.

2015 atakuja na gia kuwa alikuwa busy na majukumu ya kitaifa maswala ya umeme n.k

Kisha atawamaliza wananchi kwa kusema hakuwa mzoefu na bunge sasa wampe miaka 5 aanze kuwatatulia kero zao.
 
Hamkuweka mgombea 2010 (Slaa ain't no dummy), and I double dare you kuweka mgombea Chadema Bumbuli 2015, u will be obliterated. Thats all I can say.

The rest is nonsense! Hii post imekaa kimajungu.

Waswahili bhaana, u blame Mbunge for actually visiting schools and look at madaftari ya wanafunzi. What is wrong with that? lol. Some majungu are so stupid. Kama unataka kumpiga mtu fitina, find something tangible.

By the way, ungekuwa kada wa CCM, wadau wa Chadema humu ndani wangekwambia UMETUMWA wewe--your 7th post jamvini ni jungu.
afadhari mkuu umekuja mwenyewe kuongea!
 
Mzeee Makamba wewe piga kazi huku watu waione achana na maneno mkuuu! Usiongee kama cdm ndiyo adui zako wakubwa mimi ninakuamini saana utaleta changes PIGA KAZI MAKAMBA! Usikae kulalamika kama ndugu yako JK!
 
Ndugu, give him a brake! Mwenzetu ndo kwanza tu amechaguliwa - leo hii miezi minne tu. Na ana mipango mingi ya maendeleo na Mungu atampa uwezo wa kuitekeleza. Mimi nimepitia website yake na kusoma mambo mengi sana pale; kiukweli ana ndoto nyingi kwa Bumbuli na ndo kwanza ameanza kazi - tusubiri tuone utekelezaji wake. Sina shaka katika kipindi chake ataibana serikali ifanye mengi iliyoahidi kwa Bumbuli, na yeye atawezesha mengi kwa ushawishi wake. Tumpe nafasi afanye kazi.

Ubunge si kazi ya mchezo hata kidogo! Kuna mambo mengi, majukumu mengi, na kwa Mbunge serious kama January, kusinzia ukiwa unatoka jimboni si jambo la ajabu - unakuwa umechoka kweli. Kila nikiwa Jimboni nachelewa kulala na kuwahi kuamka kuliko kawaida!

Majungu na fitna za namna hii si nzuri. muacheni mtu afanye kazi, akishindwa mtaweka mgombea wakati ukifika, na hii ndo maana halisi ya demokrasia ya upinzani na ushindani! Siyo kumchafua mtu. Na ameanza vizuri kazi kama Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati Nyeti. Wana Bumbuli mnaosoma hii habari watulizeni wenzenu, waambieni wana kila sababu ya kujivunia Mbunge wao; ni kijana msomi, ana upeo mkubwa na zaidi ya yote anakubalika (ndiyo maana kachaguliwa kwenye kamati nyeti na muhimu kama hiyo katika kipindi tete kama hiki!)

Kwa kujitetea Ong'wise hamjambo! Lakini kama shutuma za kuhamisha ofisi ni za kweli huoni kama ameenda kinyume na matarajio ya wapiga kura wake? Maana kama Bumbuli ni katikati ya Tarafa mbili halafu unapeleka ofisi pembezoni hili siyo jambo jema kwa Mbunge makini. Anyway, ngoja tumpe muda labda atafanya yale yanayotarajiwa na wapiga kura wake!!

By the way Mh. yale maandamano yako yameishia wapi? na una mkakati gani wa kuhakikisha kuwa ujumbe wako unawasilishwa kwa njia nyingine?
 
Kaka nashukuru kwa ujasiri wako na kuweza kutufahamisha habari kama hizi,kumbe ni kweli kabisa kazi ya mbunge ni kupigania maendeleo ya wananchi yake.! Jana nilitoa thread yenye "niliyoyaona karatu" lakini nilipokea matusi makali sana kwavile tuu ilikuwa ikiigusa chadema,leo naona asilimia kubwa wakikuunga mkono kama vile wamefika bumbuli kwavile tuu umeongelea ccm,hawasemi january ni mgeni na matatizo kama ya maji ni ya nchi nzima,mimi kimsingi kama kweli january ameyafanya hayo hawajibike kwa wananchi wake,nduguzangu wanacdm tuwe tayari kupokea changamoto za majimbo yetu na si kutoa matusi kwavile tuu hayakupendeza! Very soon nitawaletea hali halisi ya jimbo la hai la ndugu mbowe afu tutoe mawazo yetu!
 
JF ilipo anza awali lengo ilikuwa kuweka pamoja Tanzani great thinker, people who think independently. Lakini naona sasa hali imebadilika watu wengi wamekuwa busy kwenye who is up and who is down in politics.

Bumbuli ni kwetu mimi, i know mbuli you don't know Bumbuli my friend. Barabara ya kwenda kule milimani haikutengenezwa wakati barabara ya Mombo to Lushoto inatengenezwa. Umasikini wa Bumbuli ni very challenge kama umasikini wa sehemu nyingine across Tanzania. Namba ya wanajua kusoma na kuandika ni less than 30% ya wakazi wote. Majority ya wakazi ni primary school drop out, with less than 7% wenye form four education. These are very complex number, kufanya mabadiliko in four month katika namba kama hizi ni ndoto.

Did January set a goal too high kwake na Bumbuli? May be yes, January like many Tanzania politician hana background ya kutransform poverty into prosperity, most of the theory wanazotaka kuapply ni base on Books or Plan form International Financial Organization. Hizi policy kufanya kazi sehemu kama hizi ni ngumu, how can you introduce credit system in the place ambapo majority don't have even a plan to prosperity? Those are challenges ahead of wabunge wote vijana ambao wamekuja na big ideas from West. Again am not saying this challenges can't be overcome, but am saying there is a need subira and smart move by leaders and wananchi.

2015 Lushoto will be next kwenda kwa mbuge kijana, maana yule babu doesn't know anything about maendeleo period....

To all who are out there run their mouth up and down, trust me maendeleo hayaletwi kwa mijadala isiyo na kichwa wala miguu, instead maendeleo yanaletwa kwa agenda ambazo ni realistic.
 
jamaa sijui kawakosea nini JF lakini naona kuwa hiii chuki ina run so deeo labda wenye forum ndio wanaweza kutupa undani zaidi

haiwezekani kati ya wabunge wote mbunge huyu kijana ndio aandamwe namna hii tena na vijana wenzie kwa sababu tuu ni wa chama tawala au kwa sababu baba yake ni SG huko CCM aua hata sijui tatizo ni nini

something is not right
 
Hata mimi nimefurahishwa sana na matendo ya January kama kweli ndio haya, maana hakuna watu wanafiki kama wananchi wa Bumbuli, yaani mzee wa watu kaongoza vita kubwa sana dhihi ya unyonyaji wetu sisi wote, walichofanya ni kumdhalilisha kwa namna ya ajabu leo wanasema nini? kwanza nasikia hao wenyewe huko sio kwao dingi alikuja kutoke iringa kama manamba, sasa leo wanamtakia nini. Heko January mwendo mdundo kama watu wenyewe hawana internet ama skype na hawajanunua ipads sasa wewe ufanye nini? kwanza kitabu chenyewe cha kuwaombea misaada umekiandika kiingereza sasa kama wao wanajua kisambaa tu wewe ufe? halafu watamchaguaje muwakilishi asiyeongea lugha yao? imekula kwao teh teh tehe kweli wajinga ndio waliwaao.. kula kwa kwenda mbele hayo mambo ya 2015 watajiju wakati huo dili lako la Dowans litakua lisha tiki huku wao umaskini ukwaparami mpaka kwenye kope

Nimeipenda komentsi zako mkuu............nimeshikilia mbavu zangu for 2 minutes kwa sababu iti izi veri interesting. Na ukiangalia kwa undani zaidi utagundua ulichosema ni kweli kabisa. Ikishaulamba ubunge basi unawasahau hao waliokuweka hapo. Kazi kweli, naamini watakuwa wamepata fundisho.
 
Ushabiki ukizidi tunakuwa kama wehu. Najua hili ni jamvi la Chadema, but irrationality will not save us.

Umesema Bumbuli kuna shida ya maji na barabara mbovu, halafu u blame Mbunge Makamba (Who was just elected last year) and then you go and praise Mzee Shelukindo kuwa ni mpiganaji but he was mbunge for 15 years? How do u explain that kind of intellectual dishonesty?

Huku Tegeta kwetu kuna shida ya maji, as the matter of fact, tunanunua maji kila siku. But It would be stupid to blame that on Halima Mdee, she just started ubunge.

Maybe its not really worthy arguing with this kind of thinking/posting. The motive of mtoa mada ni kupaka matope.

Mtoa hoja anasema mbunge hana mikakati yoyote ya kuleta maendeleo, this is FALSE. Mtoa hoja kaamua kutudanganya, mipango ya kuleta maendeleo ipo hadi kwenye kitabu. Ukiamua kupiga fitina ungesema kwamba mipango ya kuleta maendeleo haitekelezeki, hapo labda tungekuelewa. Ndio maana nikasema hii post imekaa kimajungu.
Afande Sele punguza mungkari kidogo hapa:

Makamba ni wa kulaumiwa tena sana na wa si Mzee Shelukindo kwa sababu zifuatazo:

1. Alikopa sawa ya thamani ya hela za Ki-Tanzania Bilioni 15 kutoka Wall Street Marekani ka jina la na kwa ajili ya maendeleo ya Wa-Tanzania waishio jimbo la Bumbuli hivyo kudai maji, barabara zuri, zahanati na shule za kisasa kwake tena kwa haraka ni HAKI YA WANA-Bumbuli waliotumika kama chambo kujipatia mkopo.

Mzee Shelukindo hakuwahi kukopa nje ya nchi kwa jina la wananchi hao wanaotamani kweli maendeleo.

Ushauri: Wana-Bumbuli fuatilieni kwa karibu huo mkopo kwa jina lenu ambalo limechukuliwa kwa jina lenu na kukusudiwa kurejeshwa katika kipindi cha miaka 10 ambayo sawa na kusema ndicho kipindi Makamba anakusudia kuwa mbunge wenu kabla ya kula kona naye kulenga Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo hivi sasa unaonekana kama jambo la mchezo tu kwa baadhi yetu.

2. Makamba kahamisha ufisi ya wananchi na kuipeleka penye mwanga wa umeme tata wa Dowansi na kuwaacha wanakijiji solemba watafutane wenyewe kwenye giza huko milimani.

Mzee Shelukindo yeye ameishi na wananchi hao huko huko kwa shida na raha bila kutoka unyoya kihivi. Naamini kwamba kwake yeye hata kwa kibatari tu bado alikua anaendelea kuwatolea huduma huko huko maana kawaida ya nchi yetu sisi ni wa vijijini tu na ninapenda kweli maisha ya kijijini kusiko na adha ya umeme wa Dowansi hata siku moja.

Shauri yenu mnaoogopa minyoka, fisi na nungunungu na wanga wote ndani ya giza vijijini. Sie wengine hivyo viumbe ni kawaida sana tena ndio kama tatizo la msongamano wa magari mijini na majambazi kila kona. Utamu wa kuchunga ngombe katikati ya milima ukiwa na vijana wa rika lako ndio usipime.

Kwa eneo hili la kutokuogopa umande wa vijijini, matope, salamu barabara zima na na kila mtu kujihisi ndugu toka nitoke ni kati ya mambo machache yanayonifanya nimepende 'Mtoto wa Mkulima' Mhe Pinda, na Mwalimu Nyerere; husemekana kuchanja mbuga tu kwa miguu kam mwanakijiji yeyote yule pale anapoenda kijiji cha pili kusalimia wazee wake.

Hakika hata teknolojia ya kutuma tu SMS ng'ambo ya pili haikamilishi vilivyo raha ya kutembea kijijini kwenu mguu kwa mguu.

3. Makamba lazima alaumiwe kwa sababu ni damu changa ambayo ilitarajiwa kuonyesha utofauti mkubwa na kuleta mema mengi zaidi kuliko uongozi wa mzee Shelukindo ulivyokua huko nyuma.

Sina uhakika wananchi wa Bumbuli watakavyokua wanamuona hadi hivi sasa wakiwekwa na mtangulia wake kwenye mzania!!!

Badala yake sauti ya makamba husikika tu kwenye siasa za kuwafitini na kuwakejeli wachaguliwa wengine wa wananchi katika itikadi na ngazi mbalimbali za uongozi.

Hata mchezaji Drogba kabla hajawika kote kimatifa kwenye kusakata kabumbu kwanza kule viwanja vya kijijini kwao watu humtambua na kumheshimu bila makeke.

4. Makamba, sawa na Mzee Shelukindo, wote wamebahatika kupewa dhamana ya KUWA JICHO LA CHOMBO KINACHOITWA BUNGE kulisimamia serikali (The Executive) katika utendaji wake wa kila siku kwa kupata uenyekiti wa kamati muhimu sana za Bunge.

Wala mtu haitaji kukumbushwa kwamba jukumu kama hilo mpaka hivi sasa imeshawapokonya wananchi wa Bumbuli uwakilishi halali bungeni. Nasema hivyo nipo tayari kunukuliwa kwamba Makamba ni kati ya wenyeviti wa kamati za bunge ambao BADALA YA KUISIMAMIA SERIKALI katika wizara zake mbalimbali na mashirika yake, kwa masikitiko na kero kubwa kwa wengi, hawa jamaa wamekiuka misingi ya Utawala Bora kwa KUJITWISHA USIMAMIZI KWA SERIKALI PAMOJA NA UTENDAJI WA KILA SIKU ZAIDI HATA YA MAWAZIRI WENYE dhamana husika; hivyo sharti wawe bize sana na jimbo kama la Bumbuli, Monduli na kule kwa Zitto Chigoma lazima uwakilishi hafifu ujitokeze unless wako OMNIPRESENT kama ambavyo Mwenyezi Mungu alivyo.

Mzee Shelukindo hakusikika kurandaranda barabarani kujitangazia umashuhuri na nguvu za uwenyekiti wake wa kamati kule bungeni. Alikua ni mtu mwenye hekima sana, jicho la mwewe, subira ya kobe lakini hutoa adhabu ya chui na ujasiri wa kifaru pale mambo yakienda kombo bila maslahi ya taifa kubainika wazi kwenye matendo fulani.

Wala hakuwahi hata KUHISIWA KUCHEZA UDALALI WA AINA YOYOTE kama ambavyo hivi sasa hata watoto wadogo wanajua kwamba hata bungeni kuna ma-mishentauni!!

Sababu za kulaumiwa kwa huyu bwana mzee ni mengi mno ndani ya kipindi kifupi sasa lakini kwa leo bora niachie hapa huku nikimmegea neno kauli ya busara kwamba, wakati tunatamani ajirekebishe haraka sawa naye Zitto ajirekebishe haraka naye na wawe vijana wa kawaida na tumaini la kesho nchini, KIONGOZI MZURI HAKUMBUKWI KWA KELELE ZAKE KWENYE VYOMBO VYA HABARI, FEDHALI ALIZOJIKUSANYIA WALA UMASHUHURI WA KUWADONDOSHA WENZIE KAMA MCHWA bali kumbukumbu hizo hutokana na MWANGWI WA MATENDO YA MEMA na haki kwa wote wakati wote.

Katika kauli hiyo ya busara; picha kubwa zing'aazo gizani ni kama vile picha za watu mashuhuri na wengine wa kawaida sana nchini kama vile wanavyoendelea kukumbukwa kgusa maisha ya jamii kwa mema mengi kuliko hila:

(1) Mwalimu Nyerere,

(2) Ed Moringe Sokoine,

(3) Kijana fulani Ogutu aliyewahi kwepo Marie Stopes [Uwezo hadimu wa kijana mdogo wa Ki-Tanzania],

(4) Mzee Arnold Kileo aka chapa TBL ya kizalendo [awezo hadimu wa Ki-Tanzania],

(5) Augustino Mrema [hata ukimuona ngedere leo baba huyu ni Simba na lule kwa walalahoi - msaada kwa wajane na wadhulumiwa]

(6) Banana Zoro na Mr II [wala hawana habari kama tunajua wanavyowasaidia wasiojulikana kimuziki kupata jina na maisha hata bila yeye kutangaza walichowafanyia]

(7) John Ulanga [Kijana huyu wengi wala hatumjui lakini muziki wake ni mkubwa kwa maisha yetu wavuja jasho nchini]

(8) Joyce Mhavile na Mama Nkya - usipime na wala hawarandirandi mitaani kujitangaza ila wananchi tunawajua.

(9) Marehemu Rashid Kawawa - Mradi wake wa Uyoga kijijini kwake na kupendelea kufanya ile kazi kwa mikono yake mwenyewe.

(10) Madaraka Nyerere - [Umakini wa makala yake na kuonyesha kwa vitendo kwamba hata mtu wa kijijini analo la kuwamegea enyi wa kwenye Mwanga wa Dowansi]

(11) Samwel Sitta The Speaker aka Shimita wa siasa [nadhani ukiingia katika darasa lolote shule za msingi tu hasa huko vijijini na ukawauliza swali moja tu; Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ni nani na wala usishangae ukijibiwa Samuel Sitta - baba huyu hakujisumbua kuweka matangazo ya matendo mema lakini tunamtabua]

(12) Mabalozi we mahiri - Mama Mulamula (heshima mbeeeele mama), Balozi Salim Ahmed Salim na Balozi Benjamin William Mkapa [sitosubiri mpaka mfe ndio niseme heshima mliotuletea]

(13) Jaji Mwalusanya - Japo aliishia kupooza, huyu baba alikua akikuhukumu, kwa mujibu wa watu waliowahi kujitokeza mbele yake mahakamani, kwa jinsi alivyokua na mapenzi makubwa na kitu HAKI na kuwa so serious na kazi yake, inafika mahala hata mhukumiwa naye rohoni anatamani apate japo kanafasi ya kumpa mkono kabla ya kupelekwa Ukonga kwa kuwa japo ni chungu lakini hakuna jiwe hata moja ambalo utakuta Jaji Mwalusanya kaacha bila kulifunua na kukagua pande zote za kila kimojawapo.

(14) Saed Kubenea, Mwanakijiji, Rioba, Jenerali Ulimwengu, Wakuhenga, Karl Lyimo, Mhe Tegambwage, Prince Bagenda (japo siku hizi uvivu unamuingia) na Majjid Mjengwa, Halima Mchuka, Boniface Charles ... ni miongoni mwa watu wa kawaida sana tu lakini wakiingia msituni kushupalia jambo, mama yangu, lazima walalahoi tupate sababu ya kutabasamu.

(15) Mzee Ndesamburo (Moshi) / Joseph Mungai (Mufindi) na darasa kubwa alilotujengea juu ya namna gani jimbo liendeshwe kuwaletea wananchi maendeleo nakuambia usipime lakini katu hutowasikia wakipayuka hovyo huku na kule.

(16) Kuna Baba Moja kilema wa Viungo kule Zanzibar ambaye kakataa kata kata kilema chake kumzuiya kubadilisha maisha ya watu wa kawaida nchi, huandaa tamasha kila mwaka (BUSARA) na vijana kuburudika na kujitengenezea fedha pia.

(17) Yusuf Makamba [kama binadamu mwingine yeyote yule huyu baba ana mapungufu yake kama vile hasira zisizodhibitika kiurahisi, ila ni mtu mmoja ambaye kwa maoni yangu udini haumpi shida hata chembe nchini, hajui kuhifadhi chuki bali hubwatuka na kwisha pale pale, ila kilema chake alichokipata toka kwenye kazi yake muda mrefu sana jeshini ni AMRI BILA KUPOKEA MAWAZO YA WALIOKO CHINI YAKE, na kwa upande mwingine ni UTII WA MAJI KWENYE MTUNGI BILA HATA SIKU MOJA KUMHOJI MKUBWA WAKE juu ya jambo kabla hajalitenda]

Wapo Wa-Tanzania wengi sana sana waliogusa maisha ya watu wa kawaida sana na kuchangia kuleta mema na wala hawajikwezi na kujigamba hovyo kama mbegu hii ya akina Makamba Junior, Zitto na Lowassa nchini.

Bado kuna nafasi Zitto, Makamba na wengine kama nyinyi mbadiliken na muache kabisa michecheto, mtambue kwamba NGUZO IMARA ISIOTETEREKA WALA KUHITAJI KUHONGWA MTU NI UKWELI NA UADILIFU WAKATI wote!! Dr Slaa kaonyesha kwa mapana na marefu hili ninalolisema kivitendo katika siasa zetu hivi leo na jinsi ambavyo watu mashuhuri kisiasa, matajiri wa kupindukia lakini kwa sababu tu SI WAKWELI WALA WAADILIFU KUTETEA MASLAHI YA UMMA wote hivi sasa nyuso zimewashuka, mitumbo joto maandamano yanapoelekezwa makwao na akili kuwaagiza kwenye kutenda dhambi zaidi kuzuia mwanga wa jua usifike ardhini.

Vijana wenzetu chukueni hatua bila kujali itikadi zetu kwa kuwaSIKILIZA na sikio la tatu, bila bughudha na kero za kujipitishapitisha na wakati wote KUJIHISI MTI WA MATUNDA NA LULU wa kutafutwa na watu, ili siasa zenu zikue katika njia nyoofu. Na mjue tangu leo kwamba tunawapenda sana ndio maana tunachukia mno mnapojihiari kuwa pagasi wa Rostam Aziz na Edward Lowassa walioifilisi nchi yetu kupitia kampuni za kitapeli.

Huu ujumbe si kwa January makamba tu bali ni kwa vingozi vijana wote nchini wakiwemo John Mnyika, Hussein Mwinyi, Vuai Nahodha, Mr II, Regia, Ndungai, Malisa, Nchimbi, Ridhiwani Kikwete, Hussein Bashe, Halima Mdee, Mnauye, David Kafulila, Kitila Mkumbo, Salasini, na wengine wengi tu kwamba tunawapenda sana ndio maana hata siku moja HATUTOACHA KUFUATILIA MIENENDO YENU na hasa ile yenye lengo la kutuliza zaidi sisi walalahoi!!!

Badilikeni leo.
 
Back
Top Bottom