Wananchi wa Arumeru Mashariki kumsindikiza Nassari bungeni

Kwa kweli hili siyo lazima kabisa; nguvu hii inaweza kutumika kwa namna bora zaidi badala ya kufurahisha hisia.

hivi unajua maana ya hisia?
Watu kam nyie ambao huwa ni mpo vuguvugu kisiasa yani haupo chama chochote wal huegemei upande wowote ktk kutetea jambo fulani ndo huwa ni JANGA LA TAIFA, usilete upinzani ndani ya upinzani wewe kunguru kwani niwewe ulokuja na thread humu JF ukishinikiza viongozi wa juu wa CDM wajiuzulu tena bila kutoa facts zenye maana sasa na leo hii baada ya kushinda arumeru unaanza ukilaza wako wa mawazo mgando humu, kiumri na kielimu unaonekana umenizidi lakini KIAKILI NA UPEO hujanizdi kwani thread zako tu zinajidhihirisha wazi´. Unafiki wako rudisheni huko huko CUF na utuachie CHADEMA yetu.
MOVEMENT 4 CRITICAL CHANGES
CHADEMA 4 LIFE
SOLIDARITY FOREVER MORE
 
Hiyo pesa badala ya kunufaisha wenye magari ingetumika kuchimba visima kila kijiji na kujenga sekondari za bweni kila kata watoto wasome na kina mama wasisumbukie maji kama ilivyokuwa chini ya ccm. Karata ikichezwa vibaya bila focus itawagharimu cdm. Muda uliobakia kuelekea 2015 ni kidogo sana, mbunge mpya angeanza kusimika alama kila kijiji ili hata ccm wajue hawana chao huko tena. Akitapanya resource ya ukubaliko wake atakumbuka sana baadaye kwa uchungu. Akumbuke historia ya Mrema kusukumwa na umati wa watu kwenye gari lakini na amri ya siku saba mpaka kirarachi walimfuata huko na kuacha kitu kidogo, akasomwa tabia yake mbaya na akaandikiwa umarufuku kuwa rais milele hata haelewi mpaka sasa nini kilitokea. HUO NI USHAURI WA BURE KWA CDM Arumeru mashariki. Kuwa kimya lakini matendo yaseme sana, utaheshimiwa zaidi. mbwembwe zina madhara ya kudumu.

tatizo lako mkuu hujui maana ya siasa zinazotumia harakati kama ambazo CDM inatumia kufikisha ujumbe kwa serikali kiziwi kam hii ya CCM. Newei basi subiri tutoke kwanza dom kwenye maandamano ya kumsindikiza nassary ndio utaelewa 2 somo na maan maana ya chadema ktk harakati hii.
 
kila la heri mpelekeni kijana akawatoe jasho walalavi(walala usingizi) awaambie bado wengine wanakuja hatujaisha. ila choonde wanaintelijensia wanalijiua hilo? wasje wakasema tunaandamana kuelekea mjengoni wakatuzuia ubungo.
 
tatizo lako mkuu hujui maana ya siasa zinazotumia harakati kama ambazo CDM inatumia kufikisha ujumbe kwa serikali kiziwi kam hii ya CCM. Newei basi subiri tutoke kwanza dom kwenye maandamano ya kumsindikiza nassary ndio utaelewa 2 somo na maan maana ya chadema ktk harakati hii.


Nakubali mkuu, hilo ni tatizo langu. Lakini tatizo langu pia ni kutoona uzuri wa kukaa kimya pasi kumshauri rafiki yako anayedhani anajua njia hata kama anapotea njia. Umesema vema, nakubali kuubiri na kuona, hata kama majuto ni mjukuu.
 
we si upo kamati kuu ya chama? kwa nini usishawishi viongozi wenzako humo ndani ya vikao wasifanye hivyo?. au hakuna platform mpaka utolee mawazo yako humu?. Impact ya maneno yako haya ni kubwa
uko sahihi kabisa huyu anayo nafasi ya kuongea na wakuu wenzake afanye hivyo
 
Wadau naomba kuwapongeza sana kwa hoja nzuri! kweli nimeamini kuwa tuna wananchi makini sana ndani ya CDM. kumbe CCM walikuwa wanavifunika vipaji vyetu! Wazo la mdau hapo juu ni la msingi sana! Tuna TV za kutosha, nakutokana na ushindi wa arumeru sisi kama wanachadema wote tumejewa na furaha! basi badala ya hizo fedha kutumika kwa ajili ya usafiri basi zitumike kwa ajili ya hayo mambo na wote kwa nguvu kubwa tuliyonayo tuangalie Tv majumbani kwetu na CCM watapata ujumbe tu! isipokuwa wale wa Dodoma wasiache kwenda kutuwakilisha!

Ningependa kuziona aibu za Lusinde siku akiingia bungeni akakutana na kamanda wetu wa arumeru pamoja na makamanda wengine wa Chadema! ahaaa Mwkt wetu Mbowe! sijui ataweza kusema Kudadadeki???
Sijawahi kuona mpuuzi kama huyu!
 
Mimi ninawapongeza kwa mawazo mazuri ya kuonyesha mshikamano wa dhati, 2015 sio mbali, hakuna kulala mpaka kimeeleweka. Ni M4c mpaka ukombozi na uhuru wa kweli unawafikia Watz wote.
 
Hongereni san kwa wazo la kuchanga fedha,

Naungana na MM na wengine walio changia uzi kuhusu upetzaji wa rasilimali. Kumbukeni Kuna Muda na fedha itakayohitajika na criticaly Muda hautarudi tena maishani.

Napendekeza kuwa fedha waendelee kuchanga ila wafanye kutu cha kumbukumbu kwa wana Arumeru, wanaweza wakachimba KUSIMA kikubwa kitakacho weza kusaidia maelfu ya watu(nammanisha kisimakikubwa) watuambie hata sisi tuwaunge mkono ili liwe kumbukumbu njema kwa vizazi vyote!! sasa hii ya kwenda dd hii itapita na hisia zake!! Wajenge hata shule hata madarasa mawili ya Mfano, Nyumba ya walimu sehemu yenye shida ya ukweli alafu waweke bango kubwa (Kisima Hiki, Jengo hili limefadhiliwa na Wananchi wa AR kama kumbukumbu ya kufurahiya Ushindi wa nguvu ya Masikini dhidi ya nguvu ya Pesa!! Na hii iwe kumbukumbu kwa vizazi nyote kwamba inawezekana!!) hii nakwaambia itakuwa ni historia Nchini TZ!!
 
Ingefanyika mbinu mbadala!
Gharama zingetumika kutimiza machache waliyoahidi ikiwa kama mwanzo wa kutimiza malengo.
 
Hongera chungeni ajali msije punguza idadi ya wapiga kura 2015
 
kila 1 na sababu yake
kuhusu hiyo safari ya dodma
wapiga kura- kuufurahisha moyo na kuhanikiza matumaini mapya ya ukombozi baada kuibwaga ccm iliyoongoza tangu 1955 baada ya kirilo kurelegate jukumu kwa TANU kuleta ukombozi ambao haukuletwa kwani ardhi bado zimekaliwa na masetla hali wakazi wanalia ukosefu wa ardhi.
mbunge mteule- kujenga taswira ya kujiamini na kusimika kiapo chake cha utii katika mapambano ya kuleta ukombozi , utetezi na kuondoa ukandamizaji wa karne nyingi kabla na baada ya uhuru wa tanganyika.
CHADEMA- KUJENGA MSTAKABALI MPYA KUELEKEA KILELE CHA UCHUKUAJI WA DOLA.
PLAN B
KAMA SI HIVYO- NAWASHAURI MUWEKE MIKAKATI YA KUMOBILISE RESOURCES KWA AJILI YA KULETA HALI BORA YA MAISHA YA WATU WA ARUMERU. KUBORESHA MAZINGIRA YA SEKTA KUU YA AJIRA; KILIMO, UFUGAJI, UPATIKANAJI WA MAJI, UBORESHAJI WA ELIMU, USHIRIKI WA JINSIA KTK MAAMUZI YA KULETA MAENDELEO NK
 
Hii hoja ina mgawanyiko. Na kila hoja ina mantiki fulani.

  1. WAZO LA KWENDA NAUNGA MKONO KUWA ITAKUWA IMETOA IMPACT KWA JAMII KILA WATAKAPOKUWA WAKIPITA. TUKUMBUKE UCHAGUZI WA ARUMERU UMEKUWA NI GUMZO KUBWA HAPA NCHINI ESPECIALLY TANGU SIKU YA UPIGAJI KURA MPAKA HIVI SASA, KILA MAHALI WATU WANAZUNGUMZIA ARUMERU. KWA HIYO ITAAMSHA HISIA ZA WALIOLALA KISIASA MAENEO MENGINE KAMA MOROGORO NA DODOMA
  2. WAZO LA KUTOKWENDA PIA LINA MSHIKO UKILIONA KWA MTAZAMO MWINGINE NA KUWA HELA HIZO ZINGEELEKEZWA KWENYE VIPAUMBELE VYA MAENDELEO JIMBONI KAMA DR. MKUMBO ALIVYOSEMA. LAKINI SHIDA YAKE NI KWAMBA MIOYO YA WATU HAWA KWA SASA IKO KWENYE KUMSINDIKIZA NASSARI, IWE TUU KAMA WANAFANYA TOUR.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom