wananchi, Madiwani, Wabunge, Mawaziri, wote "tunaishauri serikali", serikali ni nani?

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Waheshimiwa kuna hii kitu inanitatiza sana siku zote,
kila siku mitaani na kwenye vyombo vya habari ukisikia wananchi wakizungumza kuhusu tatizo flani likiwa limetokea utasikia wanatumia hii kauli ya tunaishauri serikali, Madiwani, wabunge na hata mawaziri wakati mwingine huwa wanasema tunaishauri serikali.., hivi serikali ni nani?? kwa mtazamo wa Watanzania. Kwa sababu inashangaza sana mpaka waziri wa wizara husika nae anapohojiwa kuhusu ishu inayomhusu yeye moja kwa moja kama waziri badala ya kujibu anasingizi serikali..?? nisaidieni mwanzenu manake nashindwa kuelewa serikali ni nani kwa mtazamo wa Watanzania.
 
Hawajakosea, serikali ni rais na mawaziri wake. Waziri wa maji anaweza kuishauri serikali juu ya suala linalohusu wizara ya mambo ya ndani. Sasa tatizo ni kwamba wananchi wenye upeo mdogo uchanganya majukumu ya bunge na ya serikali, hivyo basi suala lihusulo bunge, mfano utungaji sheria, wanahusisha moja kwa moja na jukumu la serikali (utekelezaji wa sheria) na ndio maana kila jambo utasikia wakisema "tunaishauri serikali."
 
Back
Top Bottom