Wananchi legelege ndio chanzo cha serikali legelege!

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
Kelele za JK ameshindwa nchi zimezidi. Serikali haitekelezi wajibu wake na viongozi wanajifikiria wao ni maneno ambayo yamesemwa toka enzi za mababu! Watendaji wabovu wamekuwa nembo ya Taifa. Lakini bado wananchi wale wale ndio wanaowaacha madarakani. Ni wananchi hao hao ambao wanaruhusu dhuluma, uonevu, wizi, dharau nk vitendeke dhidi yao.

Ifike mahali wananchi waseme basi inatosha. Uwezo huo wanao. Kusema BASI ni HAKI yao ya msingi.
 
Ulichosema ni kweli kabisa,mwenyewe binafsi nachukizwa na haya maneno ya chini kwa chini dhidi ya JK..ila nashindwa nianzie wapi ktk kukemea kwa vitendo maovu ninayo yaona.....namwachia Muumba tu
 
vijana tumechoka na 2015 tutachukua hatua kali dhidi ya hii serikali dharimu ya mizigo!!!!
 
Kelele za JK ameshindwa nchi zimezidi. Serikali haitekelezi wajibu wake na viongozi wanajifikiria wao ni maneno ambayo yamesemwa toka enzi za mababu! Watendaji wabovu wamekuwa nembo ya Taifa. Lakini bado wananchi wale wale ndio wanaowaacha madarakani. Ni wananchi hao hao ambao wanaruhusu dhuluma, uonevu, wizi, dharau nk vitendeke dhidi yao.

Ifike mahali wananchi waseme basi inatosha. Uwezo huo wanao. Kusema BASI ni HAKI yao ya msingi.

Hakika tena hiyo legelege yao ni ya kutojitambua...hivyo kutengeneza ombwe ambalo wachache wanalitumia kwa manufaa binafsi
Wananchi hao hao wanaoongoza kwa kulalamika ikiwa uduni wa maisha katika elimu,afya,huduma za jamii huku wakipambana na makali ya maisha kwenye kodi mbalimbali,umeme,gesi,ukosefu wa maji na ada lukuki zisizo na uwiano na Elimu ndio hao hao wasioitambua haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wa kuwaletea maendeleo.
Ni haki yao,mtaji wao wanaoutafuna kama mkulima anayekula MBEGU na mvua zikinyesha Hana cha kupanda
Huko kula MBEGU kunawanyima fursa za kushiriki maamuzi mbalimbali ambayo yana matokeo hasi kwa maisha yao ya kila siku

Wananchi hawa ambao akili yao imegoma kujiongeza wamebaki wakiadhani mafanikio ya maisha ni usanii na ujanja ujanja- mtu akiweza kuwa na simu,TV,kausafiri,anatundika t-shirt na jeans na anagonga castle lite anajua maisha ni hayo amemaliza
hiyo TV hata kuangalia taarifa ya habari ni kosa la jinai,wao ni miziki na maigizo tu

Wananchi hao hawataki kutumia haki yao kwa visingizio kuwa wao si waajiriwa wa serikali na pia si wafanyabiashara wakubwa hivyo hata kodi haiwahusu,wanasahau akinunua vocha..akipiga simu..akinywa soda/bia ama akipanda Daladala na bodaboda kote huko analipia kodi!

Mwananchi huyo huyo kama ni wa mjini akihitaji hati za utambulisho anazipata kwa ofisi ya Mtendaji iliyopo CCM..akipaki gari anapaki CCM..wa kijijini kukiwa na chanjo,sinema au mkutano wa hadhara vinafanyikia CCM..akikamatwa mwizi wa mifugo anashikiliwa kwenye ofisi za CCM wamefikia kudumaa akili wakijua CCM ni serikali na si chama.Wamesahahau kuwa hata shule yenye walimu bora na vifaa ndio hufaulisha na kukimbiliwa na wazazi wengi.wamebaki kuwaacha wanafunzi wao kwenye shule isiyoisha na ufanisi halafu wanabaki wakitegemea watoto wao wafaulu!Kisa? Eti wao wazazi walisoma shule hiyo hiyo zamani

Jamani watu hawajui hata kifungu kimoja cha katiba! Hawajui sheria ,kanuni wala haki zao za msingi,hawajui seriikali inatengenezwa na sio DUDE fulani hivi lililopo tu.Hawajui chama hakishiki hatamu bali hushikishwa! Na washikishaji ni wao

kwa mtindo huu wa kujitoa fahamu..wa kutojiandikisha kupiga kura,kutohudhuria mikutano ku Sikiliza sera na hatimae kutopiga kura ni U-LEGELEGE unaozalisha serikali LEGELEGE
Huwa najiuliza kitu KURA ni jambo la SIRI sasa ukihongwa kofia ama kanga ama pesa UNAZOZIHITAJI lakini unaona mbele kiza kinene kwani ukipiga kura yako pale unapoona pana mwanga mbele na ukaielekeza kura yako hapo UNAPOTEZA NINI?

kwani unakaguliwa ukipiga kura? Ama utadaiwa?

Ulegelege huu hauwaachii maumivu wao tu bali unawaongezea ugumu WAKAKAMAVU ambao inabidi wamege mkate wao kuwasaidia njaa LEGELEGE wachovu


Tubadilike..vinginevyo mbele GIZA
Tusipobadilika tusilalame,tusinung'unike kwani tumeyaumba kwa mikono na akili zetu
Ahh vinginevyo tutajuta kuzaliwa kwetu badala ya kufurahia rehema hii ya muumba

MsandoAlberto
walimu huwa hawaachi kufundisha hata kama wanafunzi ni wagumu kuelewa...ni kufundisha tu we fundisha tu ipo siku wataelewa
 
Msando,
Hiyo hali haiwezekani kuondoka tu kama mvua; maana ukweli ni kuwa ujinga (wewe umeuita ulegelege) ulipandwa na watawala kwa maslah maovu.

Hivyo elimu ya uraia, kujitoa, nidhamu na uongozi imara (mbadala wa CCM) ndio dawa. Kuwalaumu wananchi kijumla-jumla ni kutozingatia (aidha kwa makusudi au kwa kutojua) historia ya nchi hii.
 
Msando,
Hiyo hali haiwezekani kuondoka tu kama mvua; maana ukweli ni kuwa ujinga (wewe umeuita ulegelege) ulipandwa na watawala kwa maslah maovu.

Hivyo elimu ya uraia, kujitoa, nidhamu na uongozi imara (mbadala wa CCM) ndio dawa. Kuwalaumu wananchi kijumla-jumla ni kutozingatia (aidha kwa makusudi au kwa kutojua) historia ya nchi hii.
Yatakiwa tuibadili hiyo historia sisi wenyewe
ulegelege umo hata humu,mambo ya maana wanakimbia kuyajadili wanakimbilia udaku na kusutana
 
Back
Top Bottom