Elections 2010 Wananchi kujitokeza kwenye kampeni za rais kikwete

Hiyo ni lugha ya kujiridhisha tu.CCM kwa asilimia kubwa imejipanga vizuri kuanzia maeneo ya vijijini hadi mijini ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.Hivyo,ushindi wa ccm katika kiti cha urais hauna mjadala na kwamba idadi ya watu wanaokwenda kuhudhuria mikutano ya jk wanabebwa na malori kutoka eneo moja hadi jingine siyo kweli. Hakuna chama cha upinzani kitakachoweza kushinda kiti cha urais katika uchaguzi huu wa 2010,na hii ni kutokana na vyama hivyo kushindwa kujipanga vizuri hasa katika maeneo ya vijijini. Nguvu na mbinu zinazotumika sasa na vyama vya upinzani zilipaswa kutumika katika kuvijenga vyama vyao hapo awali, sasa hivi wamechelewa na watakuwa wasindikizaji tu wa ccm. USHAURI WANGU KWA VYAMA VYA UPINZANI NI KWAMBA BAADA YA KUMALIZA KAZI YA KUMSINDIKIZA CCM IKURU KATIKA UCHAGUZI WA 2010, WARUDI NA WAJIPANGE UPYA HASA KATIKA MAENEO YA VIJIJINI,WASIKAE MIJINI KUSUBIRI RUZUKU

Wewee sisi tunayaona mafuso kwa mafuso au hujasikia yaliyojiri Dodoma....halafu watu wanafuata fuata burudani za muziki kwenye mikutano ya JK na si hoja zake...jaribuni kuondoa hizo burudani muone nani atakuja.....kama huamini muulize Dr Bilal
 
Utafiti wangu umeonyesha kuwa katika kipindi hiki tangu Dk Slaa azindue kampeni watu wengi, wakiwemo polisi, wanamuunga mkono. Juzi nilikuwa naongea na jamaa mmoja wa Usalama wa Taifa, naye anasema anamkubali sana Dk Slaa na anaamini atakuwa rais bora kabisa kutokea katika taifa hili. Dk Slaa ana msukumo wa dhati wa kuleta maendeleo kwa nchi hii.
 
Nimejaribu kufuatilia kwa ukaribu zaidi Kampeni za Rais aliyemaliza muda wake na sasa anaomba ridhaa tena kwa Wananchi wamchague Rais Kikwete nimegundua Asilimi kubwa inayojitokeza kwanza kundi lingine ni wale waliopewa pesa na Kundi linalofuata ni kuwa hawamjui Rais Kikwete kwani ukiangalia utaona watu wanashangaa yaani huyu naye anaomba kura baada ya kustaafu kwa heshima.Hata ukiwauliza wanasema yeye ndo mara ya kwanza kumwona. Mfano. Watu wanoenda kumwona Mtarajiwa Dr. Slaa wanakwenda kusikiliza kazi alizofanya na atakazofanya. Chagua CHADEMA kwa maendeleo ya nchi yako kwani nchi sasa inaliwa na wachache ili tugawane kila mtanzania chagua dr.Slaa


Hii haitoshi kuwashawishi wapiga kura wake. kwani watz wanaotembelea JF ni wachache sana kulinganisha na idadi ya watz waliojiandikisha kupiga kura hali kdhalika na watz watakaopiga kura.
 
Hii haitoshi kuwashawishi wapiga kura wake. kwani watz wanaotembelea JF ni wachache sana kulinganisha na idadi ya watz waliojiandikisha kupiga kura hali kdhalika na watz watakaopiga kura.

Pole sana; muda wako wa kuendelea kula bila kufanya kazi umekwisha.....kaungane na yule mkuu wa wilaya aliyelia mbele ya viakao vya majambazi wenziwe. Au nenda kamjulie hali majeruhi Bendera maana hali yake ni mbaya........
 
Poor woman! Tanzania bila Kikwete haiwezekani? What a joke and an insult to Tanzanians.
 
Back
Top Bottom