Wananchi kujali zaidi halaiki kuliko kumsikiliza rais ni utovu wa nidhamu?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,681
1,109
Sherehe za maazimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu J K Nyerere na mapokezi ya uzimaji mwenge ni matukio makubwa yaliyojiri mwishoni mwa wiki hii mkoani Shinyanga kwenye manispaa ya Shinyanga mjini.Maazimisho haya yalipambwa na halaiki ya watoto wadogo ambao walipata mafundisho ya kutosha kiasi cha kuweza kukonga nyoyo za wakazi wa manispaa hii na viunga vyake.

Nikiwa mmoja wa mashuhuda waliohudhuria sherehe hizi nilitafakari mengi ambayo mwalimu Nyerere aliyowatendea Watanzania katika kipindi cha uongozi wake akiwa madarakani.Nilitafakari tulikotoka,tulipo na tuendako ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili ya jamii hususani kati awamu hii ya nne.

Mmomonyoko huu wa maadili ninao uzungumzia ni mmomonoyko wa maadili ya viongozi wa umma katika kusimamia rasilimali za nchi yetu.Nilifananisha awamu zote baada ya mwalimu na awamu ya mwalimu,niligundua kuna hitaji spirit ya kweli katika kuutokomeza mfumo mbovu wa uongozi unao sababisha mmonyoko wa maadili wa viongozi wa umma.

Watanzania wamekosa uzalendo ,wanacho jali ni mkate wao wa siku.Wananchi wamekosa mvuto kwa viongozi wao hususani wa serikali kiasi cha kuwa na mvuto na matukio ambayo yanatumika kama burudani na kuifanya sehemu ya kupotezea muda.

Tukio la jana ambalo limenigusa kiasi cha kupelekea kuandika uzi huu ni ile ari ya wananchi kupungua kutokana na viongozi wao kutokuwa karibu nao na kuwakumbuka kipindi cha kampeni za uchaguzi tu.Kupungua kwa ari hiyo ndiko kulikopelekea umati uliofurika uwanjani hapo kuondoka ghafla mara baada ya halaiki ya watoto wetu kumaliza onyesho lao kabla hata ya hotuba ya rais, kiongozi wao waliye mchagua kwakura nyingi.

Niltafakari mengi na kujiuliza kama kweli kiongozi wao mpendwa waliye mchagua kwa kura nyingi ni kitu gani hasa kilichowakumba ghafla na kutotaka kumsikiliza ilihali alikuja na maneno ya kuwaeleza Watanzania.SI mila na desturi zetu Watanzania kuwakimbia wageni wetu wanapokuja kututembelea.Kitendo cha wananchi wengi kumkimbia mgeni wao wa kitaifa ambaye walimchagua na kumkubali kuwa kiongozi wao kinaashiria wnanchi kutokuwa na imani na viongozi wao.

Sherehe kama hizi enzi za mwalimu watu walizi sherehekea kwa bashasha na hamasa kubwa na kila mwananchi alikuwa na shauku ya kutaka kujua mwalimu leo ataongea nini.Wengine walitaka tu hata kumuona na kumpa mkono ilikuwa ni faraja kwao.Lakini siku ya kumkumbuka mwalimu viongozi wetu wana kimbiwa tena mbele ya mama wetu wa taifa mama Maria Nyerere.

Ni muda muafaka kwa viongozi tuliowapa dhamana kujiangalia na kubadilika tabia,wananchi wamechoshwa na madudu yenu kiasi mmeamua kujikita zaidi katika mambo yenu binafsi na kuacha kuitumia fursa mliyopewa na wananchi katika kudumisha na kuboresha ustawi wa maisha ya kila Mtanzania.Tukio la jana liwe fundisho kwa viongozi wengine ambao ndiyo wanao muangusha rais wetu.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.
 
Wanaakili wanajua kwenye hotuba hakuna jipya! Halaiki inafurahisha na kuburudisha wakimaliza watu wanachapa malapa, hivyohivyo kwenye kampeni wakishamaliza kina Joti na Mpoki wanaondoka isipokuwa wale walioletwa na malori toka mbali!
 
kipindi cha nyerere watu walikuwa mazuzu. na ilikuwa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti.
 
Unadhani hawajui Kwamba Raisi kila wakati anawambia uongo kwa nini wapoteze muda ebo
 
Sammosses
''umati uliofurika uwanjani hapo kuondoka ghafla mara baada ya halaiki ya watoto wetu kumaliza onyesho lao kabla hata ya hotuba ya rais, kiongozi wao waliye mchagua kwakura nyingi.''

Ni dalili tosha M4C imewawezesha wananchi kifikra na kujitambua kuwa wamechoshwa na ahadi tele zisizotekelezwa huku viongozi wa CCM wakiendelea kunawiri, lakini viongozi hao hao wa CCM wanadai nchi yetu ni masikini na hawana jawabu kwa nini nchi ni masikini.
 
hotuba za kuandikiwa huwa hazina mvuto. watu wanajua hukuna jipya.mtu kam nyerere hotuba alikuwa aandikiwi. ndo maana watu walikuwa wanapenda kumsikiliza kwa sababu hauchoki kumsikiliza
 
kipindi cha nyerere watu walikuwa mazuzu. na ilikuwa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti.

Hotuba za Mwalimu zilikuwa na mashiko na zilikuwa na lengo la kumkomboa mnyonge,pia Mwalimu alitembea ndani ya maneno yake na hakuwa Fisadi
 
Sherehe za maazimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu J K Nyerere na mapokezi ya uzimaji mwenge ni matukio makubwa yaliyojiri mwishoni mwa wiki hii mkoani Shinyanga kwenye manispaa ya Shinyanga mjini.Maazimisho haya yalipambwa na halaiki ya watoto wadogo ambao walipata mafundisho ya kutosha kiasi cha kuweza kukonga nyoyo za wakazi wa manispaa hii na viunga vyake.

Nikiwa mmoja wa mashuhuda waliohudhuria sherehe hizi nilitafakari mengi ambayo mwalimu Nyerere aliyowatendea Watanzania katika kipindi cha uongozi wake akiwa madarakani.Nilitafakari tulikotoka,tulipo na tuendako ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili ya jamii hususani kati awamu hii ya nne.

Mmomonyoko huu wa maadili ninao uzungumzia ni mmomonoyko wa maadili ya viongozi wa umma katika kusimamia rasilimali za nchi yetu.Nilifananisha awamu zote baada ya mwalimu na awamu ya mwalimu,niligundua kuna hitaji spirit ya kweli katika kuutokomeza mfumo mbovu wa uongozi unao sababisha mmonyoko wa maadili wa viongozi wa umma.

Watanzania wamekosa uzalendo ,wanacho jali ni mkate wao wa siku.Wananchi wamekosa mvuto kwa viongozi wao hususani wa serikali kiasi cha kuwa na mvuto na matukio ambayo yanatumika kama burudani na kuifanya sehemu ya kupotezea muda.

Tukio la jana ambalo limenigusa kiasi cha kupelekea kuandika uzi huu ni ile ari ya wananchi kupungua kutokana na viongozi wao kutokuwa karibu nao na kuwakumbuka kipindi cha kampeni za uchaguzi tu.Kupungua kwa ari hiyo ndiko kulikopelekea umati uliofurika uwanjani hapo kuondoka ghafla mara baada ya halaiki ya watoto wetu kumaliza onyesho lao kabla hata ya hotuba ya rais, kiongozi wao waliye mchagua kwakura nyingi.

Niltafakari mengi na kujiuliza kama kweli kiongozi wao mpendwa waliye mchagua kwa kura nyingi ni kitu gani hasa kilichowakumba ghafla na kutotaka kumsikiliza ilihali alikuja na maneno ya kuwaeleza Watanzania.SI mila na desturi zetu Watanzania kuwakimbia wageni wetu wanapokuja kututembelea.Kitendo cha wananchi wengi kumkimbia mgeni wao wa kitaifa ambaye walimchagua na kumkubali kuwa kiongozi wao kinaashiria wnanchi kutokuwa na imani na viongozi wao.

Sherehe kama hizi enzi za mwalimu watu walizi sherehekea kwa bashasha na hamasa kubwa na kila mwananchi alikuwa na shauku ya kutaka kujua mwalimu leo ataongea nini.Wengine walitaka tu hata kumuona na kumpa mkono ilikuwa ni faraja kwao.Lakini siku ya kumkumbuka mwalimu viongozi wetu wana kimbiwa tena mbele ya mama wetu wa taifa mama Maria Nyerere.

Ni muda muafaka kwa viongozi tuliowapa dhamana kujiangalia na kubadilika tabia,wananchi wamechoshwa na madudu yenu kiasi mmeamua kujikita zaidi katika mambo yenu binafsi na kuacha kuitumia fursa mliyopewa na wananchi katika kudumisha na kuboresha ustawi wa maisha ya kila Mtanzania.Tukio la jana liwe fundisho kwa viongozi wengine ambao ndiyo wanao muangusha rais wetu.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

hiyo ni shida kubwa kwa CCM.Kikwete alikwenda mbeya na ze original komedi, wakaperfom walipomaliza watu nao wakaondoka.Baadaye ikabidi Ze komedi wawekwe mwishoni watu wakawa wakichelewa na kujifanyi akazi zao karibu na maeneo ze akina masanja wakipanda jukwaani watu wanaambina tena na kuja kwa wingi kisha kuondoka.
 
Kwa hali kama hii tunategemea nini?Miaka iliyobaki kumaliza muda wake miaka miwili lakini ni miwili iliyojaa taabu na mateso.Mbaya zaidi hata wale walioaminika kama Pro. Muhongo anaye ana pigwa vita vya chini kwa chini.Laiti ningekuwa mimi rais hata kama sijui kusoma lakini kutazama picha najua,basi ningefanya maamuzi magumu sana bila kutaka ushauri popote maana kila napoomba ushauri kwa wana matandao wenzangu wana niingiza mkenge.
 
Unaweza kututhibitishia pasipo na shaka kwamba alichaguliwa kwa kura nyingi?Hayo ni matokeo yakuchakachua na pia Wananchi wa Shinyanga wana hasira yakudhulumiwa haki yao pale Hayati Shelembi ambae ndie alikuwa kipenzi na chaguo la Wanashinyanga kwa uwazi,ubabe na kwanguvu kubwa matokeo yake yakachakachuliwa afu leo wakamsikilize mtu aliyewafanyia mabaya yote hayo huo siutakuwa ni uwendawazimu.
 
Pamoja na kuchakachuliwa kwa matokea ya ubunge na mheshimiwa mmoja kujitangaza kuwa yeye ni mto Manonga anayepita mbele yake lazima aende na maji,lakini haitoshi kuwafanya wananchi wamkimbie rais wao ambaye aliaminika kama chagua la Mungu kwa viongozi wa dini kumnadi.Mi nafikiri kuna zaidi hayo ya kuchakachua,ndio maana lengo langu hasa ni kutaka kujua kunani ikiwa rais kaheshimiwa wakaamua kumkimbia lakini Pinda yeye alizomewa!
 
Kuliko Waatnzania kumkimbia rais wao ni bora watoe kauli ya umoja wao kuwa hawamtaki,hawana imani naye,analea mafisadi na kujifanya kuichukia rushwa wkati rushwa na ufisadi vyote vinapikika chungu moja.Huwezi kusema samaki mimi siipendi lakini wkati huu una kula ugali kwa mchuzi wa samaki,huo utakuwa ni unafiki
 
Watasikiliza nini toka kwake,wanajua hana jipya

Huwezi amini alizungumzia rushwa yaani inatia kichefuchefu ndio maana wenye akili timamu baada ya kuburudisha akili wanaondoka.Ushauri wa bure wawe wanaalika viongozi wa upinzani, hao ndio wananchi wanawataka.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom