Elections 2010 Wananchi igunga walalamikia rushwa ya pikipiki na baiskeli

Mchokonoaji

Member
Oct 1, 2009
26
1
:crying:Ikiwa ni mwitikio wa wito wa kukataa rushwa uliorushwa na Asasi ya Agenda Participation 2000 kwenye ITV, Channel 5 na East Africa Radio, Wananchi wengi wa jimbo la Igunga wamepiga simu na kutuma SMS kwa taasisi hiyo wakilalamika kuwa rushwa ya pikipiki inatolewa na TAKUKURU wamekaa kimya kama hawaioni!

Kinachosikitisha ni kuona ni wala na watoa rushwa fulani tu wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani!
 
TAKUKURU inafanya kazi kwa maslahi ya nani?, mimi naamini kwa dhati kabisa ROSTAM azizi hata akimtukana Rais hadharani hatakamatwa kwasababu anaijua siri kubwa iliyomwingiza JK madarakani ikiwamo dhambi ya mauti, ipo siku makubwa yatafumuliwa hapa na watu watauwawa kwa mawe.
 
Kama ilivyo ngumu kukamata sterling wa Kagoda ndivyo ilivyo ngumu pia kumkamata aliyetoa fedha za manunuzi ya pikipiki na baiskeli hizo huko Igunga!!! Ni mtu hatari huyo!!!
 
kazi kweli kweli, wenye nchi ndo sisi hapa! hapa imebaki moja, tupige kura harafu watu waibe tuanze kushugulikiana. Naona hakuna tena utaifa kuna ubaguzi, manyanyazo na kila aina ya uvunjwaji wa haki za binadamu.

watu wanatumia elimu duni ya wananchi kujinufaisha! tuna wazawa kibao, smart people they can run this country and become one of the leading country interms of everything lakini wakubwa zetu hawataki kutumia resources za watu kuendeleza nchi.
 
Wale alafu kura wasitoe....then its a win win situation for the people and a lose lose for mafisadi watoa rushwa!!!
 
sisiemu iliuzwa na kununuliwa na mtu mmoja anayeimiliki igunga na watu wake. mtamwambia nini kama hata uraia wake si halali lakini hawekewi pingamizi?

tuitoe sisiemu madarakani ndipo tutaweza kurudisha utawala mikononi mwa wananchi.
 
sisiemu iliuzwa na kununuliwa na mtu mmoja anayeimiliki igunga na watu wake. mtamwambia nini kama hata uraia wake si halali lakini hawekewi pingamizi?

tuitoe sisiemu madarakani ndipo tutaweza kurudisha utawala mikononi mwa wananchi.

Mkuu mwaka 2005, wakati RA alikuwa kati ya masterminds waliyomuingiza mbayuwayu Ikulu. Mbayuwayu huyu huyu ndiye aliye mteua Dr. Hosea. Na mtoa hongo na wizi wa kura plus uchafu woooote Igunga, Nzega, Bukene ni huyu huyu aliyehakikisha mbayuwayu ni raisi. Wale wazee waliokuja dar kumuona mabyuwayu waeleze shida zao, afadhali warudi Igunga kuanza kukusanya nguvu za uzalishaji mali maana hawatasikilizwa kamwe.

Cha msingi warudi huko na kuchagua watu makini toka vyama vingine tu.
 
Back
Top Bottom