Wananchi Geita: Mkuu wa Wilaya anavuta Millioni 42 kwa Mwezi toka Kampuni ya Madini GGM

natamani kuitukana serikali ya kikwete pamoja na mkuu mwenyewe, ila naogopa kupigwa ban, japo ndiyo nimemaanisha hivyo
 
Wananchi ambao ni wakazi wa Wilaya ya Geita Wamelalamika juu ya matendo mabaya wanayotendewa na walinzi wa kampuni ya GEITA GOLD MINE [GGM] ya kuwaumisha mbwa wananchi wanaokwenda kuokota mabaki ya mawe ya mchanga wa dhahabu unaotupwa baada ya uchambuzi wa kuchotwa kwa dhahabu.

Kingine kinachoendeshwa na walinzi hao ni kuwavua nguo wanaume wanaokamatwa na kuwashikisha nyeti zao kama polisi wanavyowafunga watuhumiwa mashati ili kuweka ulinzi haswa wanapokuwa hawana pingu.Kwa kiswahili cha kisasa ni mtungo [kuunganisha] lakini kupitia kila moja kushika nyeti ya mmoja uku mwingine naye akimshika mwingine na kutengeneza mstari.

Kingine kibaya cha matendo hayo ni kuwabaka wakina dada wanaokamatwa kwenye maeneo hayo.Kwa Matendo hayo ambayo yamesemwa na wananchi hao huku wakionyesha vidonda vya kuumwa na mbwa [taarifa ya habari ITV].Walipofikisha taarifa juu ya matendo hayo ya KINYAMA yanayofanywa na Walinzi hao wa GGM,Viongozi wa Serikali walipofikishia malalamiko hayo hakuna chochote walichopata kama msaada kwa matendo hayo ya kinyama.

Wananchi walifanya uchunguzi kujua mbona malalamiko yao juu ya matendo ya kampuni hiyo ya GEITA GOLD MINE [GGM] hayana majibu kuna ni?Utafiti [Uchunguzi] wakagundua kuwepo taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita ambae ndiye msimamizi na mwakilishi wa Rais wa jamhuri ya Muungano kwa Wananchi wa Geita anachukua Fedha kutoka kampuni hiyo kiasi cha shilingi Millioni 42 kwa Mwezi.

Hakika kwa wanaojua watwambie madai ya wananchi hao ambao kwa waliongalia taarifa ya habari ni kweli baadhi ya watu wanamakovu ya vidondo baadhi vikiwa bado vibichi.

Mtujuze wale wanaojua habari zaa Mgodi wa Geita [GGM] na Mahusiano yake na Mkuu wa Wilaya huyo.

Niliiona hii jana kwenye taarifa yao ya habari(ITV) saa 2 usiku.

Kuna mzee mmoja alieleza mbele ya halaiki kuwa (nanukuu), .." Ninao ushahidi kuwa Mkuu wa Wilaya (Geita) analipwa na mgodi (GGM) kiasi cha Tshs 42m @mwezi na ushahidi ninao!" mwisho wa kunukuu.

HAPA HOJA NI KWANINI HUYU DC ALIPWE NA GGM? AU ZINAPITIA TU KWAKE NA KWENDA KWA WAKUU WAKE? TAKUKURU KAZI KWENU!
 
Poleni sana lakini siwashawishi kusogelea eneo la mgodi, ni hatari sana

Tumia akili yako japo kidogo, sio kila siku unafikiri kwa kunatumia ile kitu alotwambia masaburi.

Kati ya mgodi na wananchi, nani kamsogelea mwenzake? huo mgodi si umewakuta hao wananchi hapo??

Hizi akili za kushikiwa ni hatari sana.
 
natamani kuitukana serikali ya kikwete pamoja na mkuu mwenyewe, ila naogopa kupigwa ban, japo ndiyo nimemaanisha hivyo

Unaweza kumaliza hasira zako nje ya keyboard kwa maslahi ya uwepo wako ndani ya forum hii.
 
Hapo ndio utajuwa dini ya haki ni ipi.

Huu ni wizi ambayo ni tabia ya ma CCM haswa kwenye mali za umma na dhuluma haina dini ni tabia tu tujikite kwenye mada tuache upuuzi wa kututoa kwenye mada.
 
Polen sana wanageita na watarime. Siku zao zinahesabika katika hizo nafasi....... Ee mola walikukosea nini waja wako mpaka wanakuwa wahanga ndani ya ardhi yao? Hivi shelutete na henjewele ni watanzania wenzetu kweli? Time will tell.
 
Halafu mjinga mmoja kutoka ccm anadai eti wanarudisha imani kwa wananchi,Nape ungekuwa mstaarabu ungefunga bakuli lako ni imani ipi mnayowarudishia wanyonge hawa?au kupigwa na kudharirishwa ni kurudisha imani?ungesema hivi tungekuelew,CCM INARUDISHA IMANI KWA MAFISADI WASIWE NA WASI WASI BADO TUKO PAMOJA,serikali lege lege inawaogopa wezi na kuwapigia magoti,HIVI HII SERIKALI TUMEKODISHA AU NI YA KWETU?
 
Guys, this is too much to me ... nina dini yangu inanitaka kusamehe, lakini natamani kuiasi..
 
Naamini ipo siku watu watachoka kuona unyama huu, hata kwambia m2 cha kufanya bali nafsi yako itakwambia la kufanya. Utasikia la m2 yoyote bali la moyo wako. Iyo siku inakaribia mana saiz kila m2 anaongelea shida na manyanyaso anayopata utadhan hakuna serikali ya kutatua kero hizo
 
yanayosemwa kwenye hii thread mengine yana ukweli na mengine ni uongo. Mimi nakaaa Geita na nafanya kazi mgodi wa Geita lakini sijaajiriwa na GGM ( hapa kuna makampuni mengi). Madai ya wananchi kuwa wananyanyaswa na walinzi wa mgodi yawezekana ni kweli. Madai kuwa kuna wakimbizi wa wanaolala kwenye tents ni kweli na mimi linaniuma sana upumbavu huu. Madai kwamba wananchi wnaokota uchafu wa dhahabu mgodini na kwamba wanazuiwa ni kweli. Madai kuwa mkuu wa wilaya anapewa Mil 42 kila mwezi cna ushahidi lakini sina shaka ni uongo.
Udongo unaotupwa na mgodi kama uchafu imekuwa ni dili kwa baadhi ya wanchi hapa mjini. Mimi nakuwepo kwenye mikutano ya wakuu wa idara na imekuwa mtihani mkubwa kukabiliana na jambo hili. Swali kwa wanaofikiri jambo hili ni rahisi kama wanavojadili hapa utawezaje kuhakikisha usalama wa mgodi ukiwaruhusu watu kuingia mgodini kuokota mawe? Hii ni dhahabu watu wanatafuta ukiwaruhusu kuingia tu watu watavamia kwa fujo na itakuwa hatari hata kwa maisha yao (kumbuka watu wanavokufa kwenye machimbo ya madini yasiyodhibitiwa).
Kitu kingine kwenye jambo hili ni kuwa wezi wametumia hiyo nafasi kupenyeza hata kuiba mchanga wa dhahabu pale yalipohifadhiwa. Hawa wezi wanafadhiliwa na wafanyabiashara wa dhahabu wa hapa mjini kufanya kazi hiyo. Ukweli ni kuwa ukiruhusu watu kuingia mgodini kuchukuwa mchanga uliotupwa hautakuwa tena mgodi wenye mpangilio na uendeshaji ila vurugu.

Upande mwingine serikali ya CCM ndio ya kulaumiwa kwa kiasi kikubwa kwa dhuluma walizotendewa wananchi ambao wanalala kwenye tents kama wakimbizi kwa kweli wanatisha. Nitawawekea picha zao hizo tents make nilizipiga wiki moja iliyopita. Kwa ufupi ni kuwa kampuni iliyokuwa mmiliki wakati wananchi wanaondolewa kipindi hicho ASHANTI GOLDFIELDS ya Ghana ilitoa pesa ya kutosha kulipa wanchi kipindi hicho lakini wananchi hawa walidhulumiwa na viongozi wa serikali kipindi hicho wakiwepo mkuu wa wilaya kipindi hicho, mkurugenzi na viongozi wengine. Kwa ufupi fedha zilitolewa za kutosha lakini wajanja wakala. Tatizo la pili ni sheria yenyewe ya fidia ambayo inalipa mali iliyopo juu ya ardhi na si thamani halisi ya mali ya madini kwa mwananchi.

Kuhusu huduma za jamii kama maji serikali inabeba lawama kubwa manake muda mrefu GGM wakijua kabisa ubadhirifu ulioko wilayani walitaka kuendesha mradi wa kuleta maji Geita lakini walaji wakagoma wakitaka wapewe mradi wale na GGM wakagomea pesa zao manake hawakuwa tayari kufanya mradi chini ya kiwango.

Sisemi kuwa GGM ni malaika hawakosei lakini lawama kubwa zinaenda kwa viongozi wa serikali ambao hawatumii ipasavo fursa zinazotolewa na GGM. Mimi kwenye kampuni yangu kati ya makampuni 30 yaliyoko hapa tunailipa halmashauri ya Geita shilingi milioni mia moja kila mwezi hizi fedha wanazipeleka wapi? Makampuni yote yanawalipa shilingi ngapi? wanazipeleka wapi? WANAKULA.

Wakati mwingine watu tumelaumu pasipo kujua lakini ukweli ni kuwa wenye matatizo ni CC. Hata kumwachia mzungu achukue dhahabu zote bila sisi kuchukua sehemu ya dhahabu hiyo au pesa zake zikafanya kazi kwetu huwezi kuwalaumu wazungu. Ni ujinga wetu na hasa serikali ya wezi ya CCM.
 
Baada ya malalamiko ya mbunge wa Geita, kumbukumbu yangu imerudi hapa. Enzi ambazo mwananchi wa nchi hii alinyanyaswa na wageni wakati viongozi tuliodhani wana akili timamu kutuongoza wakiwepo.
 
Na hao wananchi wanafata nini eneo la mgodi? Na wanajua fika kuwa huko kuna walinzi na hawaruhusiwi kusogea?

Wananchi wameona ni heri waambulie makinikia ya dhahabu... Maana mgodi haujawasaidia ktk kuondokana na umasikini...
 
Wananchi ambao ni wakazi wa Wilaya ya Geita Wamelalamika juu ya matendo mabaya wanayotendewa na walinzi wa kampuni ya GEITA GOLD MINE [GGM] ya kuwaumisha mbwa wananchi wanaokwenda kuokota mabaki ya mawe ya mchanga wa dhahabu unaotupwa baada ya uchambuzi wa kuchotwa kwa dhahabu.

Kingine kinachoendeshwa na walinzi hao ni kuwavua nguo wanaume wanaokamatwa na kuwashikisha nyeti zao kama polisi wanavyowafunga watuhumiwa mashati ili kuweka ulinzi haswa wanapokuwa hawana pingu.Kwa kiswahili cha kisasa ni mtungo [kuunganisha] lakini kupitia kila moja kushika nyeti ya mmoja uku mwingine naye akimshika mwingine na kutengeneza mstari.

Kingine kibaya cha matendo hayo ni kuwabaka wakina dada wanaokamatwa kwenye maeneo hayo.Kwa Matendo hayo ambayo yamesemwa na wananchi hao huku wakionyesha vidonda vya kuumwa na mbwa [taarifa ya habari ITV].Walipofikisha taarifa juu ya matendo hayo ya KINYAMA yanayofanywa na Walinzi hao wa GGM,Viongozi wa Serikali walipofikishia malalamiko hayo hakuna chochote walichopata kama msaada kwa matendo hayo ya kinyama.

Wananchi walifanya uchunguzi kujua mbona malalamiko yao juu ya matendo ya kampuni hiyo ya GEITA GOLD MINE [GGM] hayana majibu kuna ni?Utafiti [Uchunguzi] wakagundua kuwepo taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita ambae ndiye msimamizi na mwakilishi wa Rais wa jamhuri ya Muungano kwa Wananchi wa Geita anachukua Fedha kutoka kampuni hiyo kiasi cha shilingi Millioni 42 kwa Mwezi.

Hakika kwa wanaojua watwambie madai ya wananchi hao ambao kwa waliongalia taarifa ya habari ni kweli baadhi ya watu wanamakovu ya vidondo baadhi vikiwa bado vibichi.

Mtujuze wale wanaojua habari zaa Mgodi wa Geita [GGM] na Mahusiano yake na Mkuu wa Wilaya huyo.
Sioni jipya katika hili.Ni jana tu nilikuwa naangalia documentary fulani inayoihusha Barick Gold katika kuwapa mrungura viongozi mbalimbali wa Domican Republic, ili pollution wanayofanya katika rivers za nchi hiyo zisiwe exposed na zisiwe questioned.
Nimeyashuhudia haya hata kwenye viwanda vya nguo kule Bangladesh na Indonesia to mention just a few places.Makampuni haya yote without exception yanawa-bribe viongozi, ili their evils,hasa pollution zisiwe exposed.

Frankly hakuna asiyejua kwamba mambo haya yapo.Kosa la mamlaka husika ni kuto-monitor viongozi wa chama na serikali katika maeneo yenye migodi ili kuhakisha kwamba hawajihusishi na ufedhuli huu, at the expense of the health of our people.

Hii inanikumbusha pollution za water sources kule North Mara,sijui ile scandal iliishia wapi.
 
Mamtu nayo hovyo sasa simwende na mawe na silaha za jadi, kingine nawashauri wajipake mafuta ya simba dume, yaani mbwa hasogei
 
dini ya haki ni ipi ? hebu tujuze! Labda kama haina fisadi hata mmoja nasi tuifuate!
Uislamu. Nenda zanzibar ukaone jinsi watu walivyistaarabika hata ukidondosha simu utatafutw urudishiwe au itatangazwa redioni. Hii yote ni kwa sababu ya kumwogopa allah. Mikristo dhambi kwao ni kama kawa. Angalia akina mzee wa upako na wengineo wanavyowatapeli waumini wao. Halafu pombe kwenu ni kama juice.
 
Anachofanya Mkuu wa wilaya chini ya utawala wa jpm ni cha kawaida sana. Sidhani kama mamlaka take ya uteuzi itachukua hatua.
 
Back
Top Bottom