Wanamuziki wa Tanzania wanajulikana kama Wakenya?

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,783
Happy new year

Sio mpenzi wa miziki ya kizazi kipya, ila katika pitapita yangu kwenye utube nikakutana na miziki ya kizazi kipya na nikawa nasoma comment

wanamuziki wengi wa Tanzania wanajulikana huko nje kama ni wakenya.

nani ana host kenyans.org ???

Je hawa wanamuziki wa Tanzania wanajua hilo? mameneja wao na maproducer wanajua hilo??

Ukiangalia kwa mfano kwenye link hiyo hapo chini inaonyesha kuna mtu anabisha kabisa kuwa huyu si Mtanzania kwani watanzania hawaongei kiswahili kizuri kama Mombasa! hawa wote wanamuziki wa kitanzania wanajulikana kama wakenya, au wasomali!

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=GSHPoZaW0VA&feature=related[/ame]

http://www.youtube.com/user/KenyaMedia

Kenya wanachukua kila kitu kizuri cha watanzania na wanavitangaza kama vyao!

kumweka mtanzania anaimba at the same time ukaweka link kuwa huyo ni Mkenya, is wrong!

Kuna mtu anaweza kulisemea hili? I may be wrong but I sense danger
 
they are opportunistic fellas!!
labda wanajua kwa kuwa sie ni wastaarabu hatuna mikikimikiki ndo mana watufanyia haya ila siku zaja maana their market has been lost nasi ndo twaja juu zaidi yao
still after 15 years tz will be better than kenya
 
heeeeee walibia weee eti mlima k'njaro wao!!! hata wabongo fleva nao wao???? kazi kweli kweli!!!
 
tatizo lingine kubwa ni kwa watanzania kutojitambua ndo maana hawa jirani zetu wanatumia udhaifu huo. Halafu na mabalozi wetu nje hawafanyi kazi ipasavyo.
 
Tunawapiga bao hao wakenya ndo maana sasa wanatapatapa na kuiba ujuzi wetu
 
wanamuziki wetu inabidi waamke na kuweka masharti ili wawe kwenye website zao. tatizo wanamuziki wetu hali zao tunazijua, kuna uwezekano mameneja wao wanajua na wanawazunguka!
 
Kama kawaida wa kenya tena? walianza na Mlima kilimanjaro, Tanzanite (madini), na sasa sanaa (muziki) aagh!

Jamaa wanaona uwizi ni deal sic!
 
Mbona hilo niliwahi kuliongelea siku nyingi sana hapa baada ya kuona wimbo huu:

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=Xt9uGRwF1VM[/ame]

Sikumbuki nilijibiwaje lakini niliamini kuwa huo ulikuwa upotoshaji; na kwa bahati mbaya sana zipo nyimbo nyingi sana za kibongo zina lebo hiyo ya Kenyans.org
 
Hii website ya kenyans.org inaonyesha kazi za vijana wote wa East africa,kama ambavyo TV au website za kibongo zinavyoweza kuwaonyesha vijana wa kenya au Uganda lakini si dhani kama kuna mahali wanawatambulisha vijana wetu km ni wakenya.
 
Nimefurahi kuona hili jibu kwani nilikua nimeanza kujiuliza maswali kadhaa.

Hamtashangaa kujua kwamba mimi ni mkenya na niko Kenya.

Sikujua kwamba hii forum sana ni ya wa Tanzania lakini sidhani mtanifukuza.

Ha ha ha ati tuliwaibia mlima kilimanjaro, aje?

Madini, hiyo inawezekana kwani yalikua yakipitishwa mpakani hadi Kenya

hata hivi sasa nafikiri bado jambo hili la endelea.
 
Nimefurahi kuona hili jibu kwani nilikua nimeanza kujiuliza maswali kadhaa.

Hamtashangaa kujua kwamba mimi ni mkenya na niko Kenya.

Sikujua kwamba hii forum sana ni ya wa Tanzania lakini sidhani mta ni
fukuza.

Ha ha ha ati tuliwaibia mlima kilimanjaro, aje?

Madini, hiyo inawezekana kwani yalikua yakipitishwa mpakani hadi Kenya

hata hivi sasa nafikiri bado jambo hili la endelea
.
Sasa kwanini mnakuwa na tabia za wizi? Halafu mnataka EAC, lengo lenu ni kuendelea kuziibia nchi nyingine kirahisi kwa mwamvuli wa hiyo jumuiya sio?
 
Hii website ya kenyans.org inaonyesha kazi za vijana wote wa East africa,kama ambavyo TV au website za kibongo zinavyoweza kuwaonyesha vijana wa kenya au Uganda lakini si dhani kama kuna mahali wanawatambulisha vijana wetu km ni wakenya.

Asante kwa jibu zuri sana, je hawa wanamuziki wa Tanzania wanajua hilo?
 
mimi nadhani wabongo tuna tabia ya uoga, au niseme paranoia. hivi ni wapi waliposema marlaw ni mwanamuziki kutoka kenya?

ina maana ukienda eastafricantube.co ukakuta nyimbo za burundi au rwanda, basi automatically watanzania tumeiba wasanii wa nchi hizo mbili - kwa mfano.

isitoshe hapo wa kulalamikiwa ni youtube ambao wana-host hizo video, in a way hata wewe ukiwa na website unaweza ku-link directly - zipo you tube za kumwaga.

nadhani wakati mwingine wajumbe tunakosa uelewa wa mambo, tuwe wadadisi na kutafuta majibu kabla ku-rush kubandika post. we're exposing ourselves. yapo mambo yanayofanywa na wakenya ambayo hayakubaliki, but this one sioni issue hapa.
 
Nimefurahia jibu lako. Tunatakiwa kuwa makini sana kwa kuacha au kujizuia kulalamika na kulaumu watu kabla ya kufanya uchambuzi na ufuatiliaji wa kina.

Mwezi Novemba nilikuwa Nairobi, kumbi nilizotembelea zinapiga bongo flava kuzidi aina nyingine zote za muziki. Pia niliambiwa kuwa hata sinema za Bongo zina wapenzi wengi kiasi kwamba zinashindana na zile za Nigeria. Kwa hiyo tuwe waangalifu kwani tunatakiwa kurekebisha makosa ya huko nyuma (mfano suala la mlima K'njaro) na wakati huo kutoleta mizozo inayoweza kutupotezea fursa ambazo kwa kweli zinatujia kwa kasi kubwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom