Elections 2010 Wanakijiji watakapotoa somo kwa "wamjini".. get ur suit ready and champaigne!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Najua watu wengine wanapata presha kweli maana kwanza matokeo yanaonekana hayaji kwa haraka sana na pili matokeo yanaonekana kuwa karibu sana. Jamani kuna vituo zaidi ya 50,000!! Hii ina maana we have a long way to go. Lakini kuna mambo ambayo napenda kuwaangaliza maana wengine wameshaanza kupata presha hasa wa "mgombea wetu".

a. Tatizo kubwa limekuwa kwenye kupiga kura za wabunge na madiwani kuliko za Rais.
b. Turn out ni kubwa kuliko watu walivyotarajia, msichanganyikiwe na kura zinaonesha idadi ndogo ya watu kwenye kituo kimoja, kuna vituo vingi ambavyo watu wamejitokeza mapema sana na kupiga kura hivyo wengine mlipoamka mtakuta watu hawatokei tena.. kumbuka kila kituo hakikuzidi watu 500. Hadi hivi sasa nimeonoa kuwa turn out iko a little over 60 percent na tukijua zaidi matokeo ya mikoani nadhani turn out inaweza kuwa juu zaidi ya hapo.
c. TAtizo kubwa hadi hivi sasa halijawa kwa wapiga kura, wapiga kura wamefanya beyond superb, tatizo ni vyombo husika hususan NEC wamejiabisha - I will leave that kwa siku nyingine.
d. Take a break, nenda kapige soga do something to enjoy the day bcuz this is history happening b4 ur eyes
e. Baadaye kidogo tutarusha matangazo ya ITV kupitia Bongoradio.com kwa hiyo tune kwenye Bongo radio kupata live update kwa wale walio mbali na nyumbani au mbali na luninga..

Otherwise, kama hujanunua champagne bado basi wewe ni miongoni mwa "wenye imani haba".
 
Mwaka huu uchaguzi huu utakuwa somo kubwa sana Kwa Watanzania viongozi ambao walifikiri Watanzania ni wa kuwabeza. Walishindwa wakoloni itakuwa hawa majambazi bandia wachache kwenye Chama Cha Majambazi?
 
mkubwa mwanakijiji, mbona habari zisizo rasmi toka Musoma mjini zinasema turn-out ilikuwa chini ya 50%? je kuna ukweli wowote ktk hili?
 
Mzee Mwenzangu,

Nina uhakika kabisa kuna wabunge wengi watapozeza majimbo yao..hasa wa CCM...

Jk atashinda ila kwa margin ya less than 30%..so far ka 'inzi' kutoka Nyamagana kameeeleza kuwa Lau ameanza kuwaomba 'wakuu wa kazi' wamsaidie ila ana khali mbaya sana..

Mambo magumu ila watu watulie kwa sasa ila watu watashangazwa sana na matokeo ya ubunge..
 
God is on our side! Jamani vijijini naona so far wamejitahidi ukizingatia intimidation na mambo mengine. It has been a good run!
 
Asante mkuu lakini naona huku naamini zaidi kuliko kwenye hivi vyombo vya habari sijui tatizo ni nini? Hebu endeleeni kutupa Data.
 
We mwenye imani haba hatalini utaendelea kusema JK atashinda wakati wa ukombozi ni sasa tuendelee kuomba Mola wetu atujalie na afya Njema kwa Dr wetu wa Ukweli awe Ikulu. Amen
 
MATOKEO YA KITUO CHANGU CHA UCHAGUZI

KURA ZA URAIS:

CHADEMA: 108+128+119+85+94 = 534
CCM: 88+70+58+80+77 = 373

KURA ZA UBUNGE:

CHADEMA: 135+134+126+99+111 = 605
CCM: 58+58+45+63+51 = 275

KURA ZA UDIWANI:

CHADEMA: 109+108+115+86+88 = 506
CCM: 80+70+54+71+68 = 343

*KITUO CHA SINZA A (NICE) OFISI YA KITONGOJI
 
Back
Top Bottom