WanaJFwawili wajadili Majukwaa Hatari hapaJF

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
WanaJF wawili,Kabakabana naTHK DJAYZZ wakutana nakuzungumzia majukwaa ya JF.Mazungumzo yao yalienda hivi:
Kabakabana:Jukwaa la siasa naliogopa sana.
THK: Kisa? Hupendi siasa?
Kabakabana:Si kwamba sipendi siasa ila wee acha tu.THK,una habari kwamba Jukwaa la Siasa lina mods wengi kuliko majukwaa mengine?
THK: Kwani hapo tatizo ni nini?
Kabakabana:Yaani kujazana mods wengi hapo wewe huoni tatizo? Kwanza: Ni rahisi mtu kushushiwa ban kwenye jukwaa hili. Yaani ukikosea kuweka 'k' kwenye jina la rais halafu ukaandika kiwete, umekwisha! Unakamatwa juu kwa juu.
THK:Wacha wee!
Kabakabana:Unafikiri? Halafu majina ya hao mods yamebeba hisia za ukali
THK:Ehe! Kama vile?
Kabakabana:paw, si unajua kiganja cha mguu wa simba kilivyo hatari? Ndo jina la mod rafiki yangu.Mwingine ni Silencer, yaani mnyamazishaji. Halafu kuna Fang yaani meno ya nyoka mwenye sumu. Kisha kuna Painkiller, yaani mwondoa maumivu utakayopata ukishushiwa ban. Halafu usimsahau RR, Russian Roulette.unawekewa mtutu wa bastola kichwani!
 
Dah hii nimeipenda sana aisee Ngoja nikawaite wahusika waje waisome faster
 
Mbona mmesahau moderator aitwae X-.PASTER. Huyu mod namkubali sana kwa maamuzi yake yenye busara na hekima.
 
Mbona mmesahau moderator aitwae X-.PASTER. Huyu mod namkubali sana kwa maamuzi yake yenye busara na hekima.
Yaelekea Kabakabana aliyakumbuka majina yenye maana katika hisia zake. Kwa ajili hii akalisahau jina la X-PASTER.
 
Back
Top Bottom