WanaJF nisaidieni, naomba mnisaidie

Wazo zuri sana,tenaaa litakusaidia kuweza kuwasaidia wananchi wa kata yako kwa namna moja ama nyingine na piaaaaaaaa,....on the other side its a political uplift,....jiulize umewahi kusikia diwani anae vuma kwa kufanya jambo lolote?

Try this,am sure ukielezea hali kama hizi kwa waandishi wa habari utapata harambee ya kutosha tu

Speaker... nashukuru... i am also glad for stretching the idea ... yes inawezekana kabisa ukatengeneza a very irritating video documentary itakayo onyesha the actual situations on the ground...isifiche kitu wala kuchakachua.....onyesha tangu mwanafunzi anavyotoka nyumbani labda hata kifungua kinywa hapati...akitembea umbali wa kilometer mbili plus.....onyesha vyoo in bare outlook na jinsi madarasa, madawati na vitendea kazi kwa walimu yalivyo duni na finyu na uhalisia wote kwa ukweli na uwazi ...ducumentary itakuwa pread all over the country through popular media (lobby for kipindi maalum) pia ikawa distributed even to international media like Euro news..BBC na pia kuna documentary channels nyingi ..., hii itaweza kufanya pia serikali kushinikizwa na nchi wafadhili kukumbuka majukumu pia itashawishi na kufanya kuwepo na uwezekano wa ufadhili kutoka kwa good Samaritans if not donor governments, angel well wishers and other international stakeholders... documentary hii inaweza ika attract hata volunteer professionals both local and international like teachers (world youth organization can be one).... mimi ni Quantity Surveyor ninaweza ku prepare Bills of Quantities na emergency schedule/program of works ya maendeleo ya ujenzi na uboreshaji wa shule for free ... something like that
 
LAT, nashukuru sana. Nitakutumia projects ambazo zinahitajika ili utusaidie kwenye suala la BoQ.

Nitafurahi kutembelea kata au kijiji chako nikiwa na wanafunzi wawili waliofaulu vizuri waweze kuona kwamba Tanzania ni zaidi ya kata ya mabogini. Tafadhali nialike nitapanga kuja.
 
Kwakweli hali ni mbaya na sio sehemu moja.
Ubaya wa hawa watu wanakula halafu hatuoni wanachokifanya.
Mimi nafikiri ingekuwepo sheria itakayowataka wabunge wachangie asilimia fulani za mishahara yao ambayo itatumika moja kwa moja kwa maendeleo ya majimbo yao huku wakiendelea kusubiria hizo bajeti.
Kwa mfano kama mbunge anapoke 12m per month, akichangia let say 30%
30% ya 12m = 3.6m
kwa mwaka mzima 3.6m times 12= 43,200,000.
Kwa kata kama uliyoielezea hizo 43.2m zinataweza kusaidia kuongezea madarasa na huduma zingine.
Tukichukua hizo 43.2m tuzidishe kwa miaka yao mitano= 216m.
Kwahiyo fungu lao kutoka serikalini na percent watakazochangia zitasaidia sana kupiga hatua katika majimbo yao.

Kuna kitu kinaitwa mfuko wa jimbo. Tatizo lake kubwa ni matumizi hayaeleweki na Mbunge anautumia si kwa kungalia tatizo lililopo bali mtaji wa kisiasa. Fedha kidogo atakazozitoa zitaenda kule kwenye maslahi ya kisiasa zaidi.
 
LAT, nashukuru sana. Nitakutumia projects ambazo zinahitajika ili utusaidie kwenye suala la BoQ.

Nitafurahi kutembelea kata au kijiji chako nikiwa na wanafunzi wawili waliofaulu vizuri waweze kuona kwamba Tanzania ni zaidi ya kata ya mabogini. Tafadhali nialike nitapanga kuja.

thanks na karibu sana
 
Mh tunahitaji kwenda kijijini tulipotoka tukaangalie hali halisi maana huku town huenda hatujui ya kuhoko, Alberto umenifanya hivi vibia 2 ninavyokunywa nijifikirie mara mbili.

Mkuu, kama hujafanya hivyo jitahidi ufanye ziara.
Hali ni mbaya kila eneo la huduma za jamii. Ukianzia na hizi shule zilizoanzishwa fasta (za kata) pamoja na vituo vya afya yaani ni disaster!! Yaani ni majengo tuu..huduma ni sawa na hakuna
 
issue hapa ni kubadilika kwa mitazamo yetu kuhusu uzalendo wetu kwa taifa hili. kila mtu anapiga kelele nyingi kama ni mzalendo wa kweli lakini ukitazama zaidi yupo kimaslahi binafsi zaidi na si kwa taifa hili na jamii masikini inayomzunguka. kwahiyo ndugu alberto resource ya hayo uliyoyataja hapo yapo within your society, start from the scratch kaa na jamii yako waface wadau mbalimbali kama wakugurenzi na kadhalika. naamini utatatua matatizo ya jamii yako unayoitumikia na mwisho utakuwa kama mfalme kwao. la msingi kwako unatakiwa uwe committed kweli kwa ajili ya watu wako maana vikwazo vingi vitakuwepo hata kwa wale ambao unategemea wangekuwa msaada kwako. taifa hili linahitaji sisi vijana tuanzishe vita vya kubadili mindset zetu na kuondoa hali hii ya ubinafsi ambayo tumemezwa nayo maana maendeleo ya kweli yatapatikana tu pale taifa hili litakapokuwa ni la thamani na bora zaidi kuliko mtu mmoja kwa nafasi yake elimu yake au uwezo wake na ndipo kila mmoja atatoa jasho lake kwa ajili ya taifa hili ambalo kwalo tumebarikia nalo.
 
Ulipo ndio pa kuanzia sasa utajua mahitaji yao hasa ni nini,anza na priority kufuatilia,hakikisha bajeti ya halmashauri inafanya kazi kwa 100%,ili ufanikiwe ni lazima ufunge mshipi kiunoni msuli usije anguka,maana najua utakayokumbana nayo.Mabadiliko ya fikra kwa wapiga kura wako ni muhimu sana na ulisisitize hasa kwa nguvu zako zote watakuelewa tu,hii ni kwa faida yao,kuonysha dira ni muhimu sana.Serikali ya CCM imefanya vioja sana usishangae kwako ni afadhali kwingine ni balaa tupu utafikiri serikali haipo na kila wakiamka kidumu cha map......... huku wanakufa,hakuna hospitali,hakuna shule na kadhalika,tunachotakiwa kuhakisha watanzania wote wajitambue walikotoka na wanakokwenda.Tutafika tu.
 
Swala ni priority zetu ktk resource allocation ziko wrong.
Nahisi anachotaka kusema Alberto ni kwamba; tujiulize: hivi kweli kipa umbele chetu ni kuwa na wabunge karibia 350 ktk nchi hii iliyojaa umaskini kama alivyouelezea Alberto kwa kutumia mfano wa kata yake?
Kwa kuwepo na wabunge wote hawa na wanaotugharimu resources nyingi kiasi hiki; je hawa wananchi (na sisi wote) tunapata faida gani?
Je si ingekuwa ni tija kwa nchi na wanannchi wake iwapo hili bunge lisingekuwepo ktk muundo huu wa sasa, na badala yake tukawa na wabunge wachache, (labdammoja au wawili kwa kila mkoa) specifically kwa ajili ya kujadili na kupitisha miswaada na sheria tu.

Kwa kufanya hivi mikopo, fedha ya jimbo na marupurupu na mishahara minono wanayolipwa hawa wabunge kwa kwenda kuimba taarabu (hasa wabunge wa ccm) itakuwa released kwenda kule walipo wancnchi, ie kwenye kata na vitongoji mbalimbali tanzania kote.

Kwa hiyo Alberto nachoweza kukushauri, ni kuwapa wananchi unaowawakilisha (kama ambavyo umeanza kufanya) ktk kata yako elimu ya uraia na haki zao, ili waelewe kwamba viongozi wote wanatakiwa wawatumikie wananchi, ili ifikapo 2015, iwe rahisi kuwapeni ridhaa ya kuongoza na hence an opportunity for your party to make huge changes in the lives of Tanzaniana. How??

Kwa kubadilisha katiba iwe wananchi oriented!!
Hakuna haja ya kuwa na wabunge karibu mia nne ambao hawasaidii ku add value ktk maisha ya Mtanzania.
Watu wanaojua hali ya maisha ya kila siku ya mtanzania ni viongozi wa serikali za mitaa na hapa ndipo panahitaji viongozi makini na wenye committment.
 
Nimekupa thanks kwa kutoa habari ya uhalisia, inawezekana ktk baadhi ya mambo ukafanikisha mwenye kwa ushirikiano na wananchi wa eneo hilo, kuhusu vyoo wananchi & wanafunzi wanaweza shirikiana na kutatua hilo.
 
Utafiti wako ni wa muhimu sana kwa kutumia vigezo vya utafiti huu ,unaweza ukatumia majibu haya kuwahamasisha wananchi wa kata yako na wilaya yako hata taifa kiujumla kuyafahamu haya yote unaweza kutengeneza vipeperushi au ubao ukaitisha ukawa unaitisha mkutano wa wazi nakuwaeleza matokeo ya utafiti wako huo na kuwauliza kama uliyoyaona nao wameyaona hivyo wakisema ndio basi waulize mufanyeje kwa pamoja ili kutatua matatizo hayo halafu mtengeneze mikakati namna ambavyo mutaweza kufuatilia kwa pamoja
 
Yaani ninakusoma nakuku-feel sana hata machozi yananidondoka..
sio siri inauma sana, ninavyofikiria mazingira ya hao watoto ni kama wametelekezwa tu.
Ninaona shauku walio nayo, na sio siri natamani sana ningekupa support kama ningekuwa karibu nawe.
LAT, nakushukuru sana sana. Nafarijika mno ninapoona kwamba wapo watu ambao wako tayari kusaidia maendeleo ya nchi yetu.

Tuliobahatika kupata elimu tuna moral obligation ya kusaidia regardless ya itikadi.

Naamini kama wanaJF tukiamua kuchangia maendeleo hata kwa kujitolea muda wetu italeta mabadiliko.

Nimeandaa utaratibu wa 'jumamosi ya diwani' kwa wanafunzi wa darasa la saba na form four. Lengo ni kuzungumza nao as a brother and friend. Make them believe kwamba inawezekana regardless ya mazingira magumu. I did it kwenye mazingira kama yao.

Nakuhakikishia the impact is massive. Watoto wa shule ya msingi are my friends and you should see their faces when promising me to perform. I abruptly step in a school during break time and all will come running showing me their books.

I wish some JF members could make these trips. Nchi yetu ina umasikini wa fikra lakini tunaweza kujikwamua kwa kufanya mambo madogo ambayo hayahitaji fedha wala uwezo mkubwa!
 
yes this is good idea
Speaker... nashukuru... i am also glad for stretching the idea ... yes inawezekana kabisa ukatengeneza a very irritating video documentary itakayo onyesha the actual situations on the ground...isifiche kitu wala kuchakachua.....onyesha tangu mwanafunzi anavyotoka nyumbani labda hata kifungua kinywa hapati...akitembea umbali wa kilometer mbili plus.....onyesha vyoo in bare outlook na jinsi madarasa, madawati na vitendea kazi kwa walimu yalivyo duni na finyu na uhalisia wote kwa ukweli na uwazi ...ducumentary itakuwa pread all over the country through popular media (lobby for kipindi maalum) pia ikawa distributed even to international media like Euro news..BBC na pia kuna documentary channels nyingi ..., hii itaweza kufanya pia serikali kushinikizwa na nchi wafadhili kukumbuka majukumu pia itashawishi na kufanya kuwepo na uwezekano wa ufadhili kutoka kwa good Samaritans if not donor governments, angel well wishers and other international stakeholders... documentary hii inaweza ika attract hata volunteer professionals both local and international like teachers (world youth organization can be one).... mimi ni Quantity Surveyor ninaweza ku prepare Bills of Quantities na emergency schedule/program of works ya maendeleo ya ujenzi na uboreshaji wa shule for free ... something like that
 
Mallaba, you have already supported the cause. Am sure with time we will get there. This country needs us. The children need us. When we are old and done they will hold our hands and help us. We will look back and be proud of what we have achieved as a country. It is why we must start achieving it now. Anytime after it will be late.
 
Bwana Alberto. Kwanza nikupe hongera kwa kuleta hii mada hapa ambapo watanzania wenzako wanaona ni jinsi gani uongozi unaweza kuwa mzigo. Pili, nikupe hongera ya kuchagua kuleta mabadiliko kwenye jamii yako, badala ya kwenda pale kisutu na kula buku kumi kumi za kupigia watu mihuri. For that i salute you my brother, your the hero for those kids and many of us.

Kwa wana JF please quit blame everyone on this and let us all assist our friend Alberto.

Mbili, mimi ni pro aide. Means I hate aide, i strong believe misaada ndio imeifikisha Tanzania hapa ilipo. I strong support budget balance and proper allocation of scarce resources. Baada ya kusema hayo naamini ni government obligation kujenga shule, vituo vya afya na kutoa huduma nyingine za kijamii.

Swala la kupunguza uwiano kati ya mwalimu na mwanafunzi nadhani lazima liwe long term plan. Kwanza ni lazima uweke mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha kiasi fulani kidogo cha wanafunzi wanaomaliza hapo wanapata moyo wa kurudi na kujitolea kufundisha katika community yenu. Hilo utalifanya kwa kuinspire hao watoto kwamba japo kuwa umesoma lakini umeamua kurudi nyumbani na kusaidia community hivyo unatoa wito kwa wengine kufanya jambo kama lako. Believe me some will join the suit.

Lazima ukae chini na walimu mjadili swala zima la wananchi kuchanga 9000 ni ngumu sana, hivyo either kutengenezwe payment plan ambapo wazazi watachangia kwa portion. Au wale ambao hawana kabisa pesa lazima utafutwe mchakato wa wao kuchangia either chakula au nguvu zao. Lakini lazima iwekwe principle ambayo itazuia mtu kuchangia nguvu au chakula kila siku. Inaweza kuwa in lifetime una chance tatu tuu za kuchangia nguvu au chakula. That will limit slucks.

Hospital/ zahanati inataka wauguzi, madaktari na wafanyakazi. Hapa ni lazima serikali kuu ingilie kati. Nadhani unaweza kuwasiliana na wabunge wengine uka lobby kupata government support kwenye hili. Vile vile budget inapopatikana hakikisha unazuia mianya yote ya utumiaji wa fedha kiolela.

Mwisho, lazima mtengeneze mchakato ambao utaongeza pato la mtu kwa mwaka. Labda kwa kuongeza uzalishaji wa mazoa kwa kila familia au kwa kushawishi kila familia kutafuta shughuli mbadala ya kufanya pindi msimu wa kilimo unapo kwisha. Hili litaongeza kipato cha familia.

Kuhusu ujenzi wa vyoo zaidi, tafadhali kaa chini na wazazi wa watoto na walimu. Jadilini gharama za ujenzi wa vyoo, kisha lazima mkubaliane kwamba wazazi lazima washiriki katika ujenzi. Lazima wajitolee either nguvu au fedha kidogo. Nafahamu pesa itapatikana kidogo, itakayo kuwa imepungua mimi nakuhaidi nitafanya fundraising na campaign ili kusecure fund. Lakini lazima wazazi wachangie sababu hili ni lao.

Afya bora ni wajibu wa kila mwananchi. Serikali haiwezi kuwaambia watu wafanyeje kuwa na afya bora. Ni wajibu wa viongozi wa chini kuelimisha watu wao kuhusu afya bora. wewe kama kiongozi, wasiliana na ofisi ya bwana afya kuona kama itakupa muwakilishi atakae kuja kuelimisha. Zipo documentary ambazo zinaonyesha umuhimu wa afya, tafuta hizi documentary na jitahidi zionyeshwe mashuleni.

Education scholarship Fund kwa exceptional students ni lazima. Na hii mifuko ambao unaweza kuuanzisha na wazamini wakajitokeza. condition sio tuu mtoto awe na akili na ni lazima akubali kurudi kijiji kila mwisho wa semester na kuja kuwa tutor na sio mwalimu kwa wale wadogo alio waacha.

Jenga community ambayo iko responsible kwa maendeleo yao, na sio serikali iwaambie wafanyeje. Bali serikali ishirikiane nao kujenga.....

Goodluck my friend, this is a long journey to success but those few who walk along the path will get to promise land.
 
WanaJF,

Nawaombeni kama watu wenye uwezo wa kufikiri mnisaidie kufikiri. Tafadhalini sana nawaomba mnisaidie katika hili. I believe this is a noble task.

Mimi ni kiongozi wa wanachi. Ni Diwani. Kata ya Mabogini kwa tiketi ya Chadema. Ni wakili wa kujitegemea. Wengi wanaamini ni kijana kutokana na kuzaliwa wakati vyeti vya kuzaliwa vinatolewa!

Nawaomba mnisaidie kufikiri kuhusu haya yafuatayo;

1. Kata yangu ina shule 2 za sekondari za kata. Matokeo ya kidato cha nne mwaka huu Div Zero ni 70 kwa 76 shule zote mbili.

2. Kuna shule ya primary, Fredrik Sumaye ina watoto wa darasa la 1 na la 2 zaidi ya 100 lakini ina jengo la darasa moja. Leo hii!

3. Shule zote za primary kwenye kata yangu hazina vyoo vya uhakika. Vimejaa. Walimu na wanafunzi wanatumia vyoo kwa pamoja. Shule ina wanafunzi 500 ina matundu sita ya choo.

4. Kata yenye wananchi zaidi ya elfu kumi na tano haina ward ya kujifungulia kina mama. Dispensary moja ina chumba kina 'ward' haina sink la kunawa mikono, choo ni cha nje cha kuchuchumaa. Kipo zaidi ya hatua ishirini!

5. Zimetengwa mil 60 kujenga kituo cha afya. Kwa mfano tuseme sawa zinatosha kujenga jengo la OPD, wodi za watoto, kina mama na wanaume je watakaolazwa wakizidiwa usiku inakuwaje? Kuna vituo vya afya kibao havijalaza mgonjwa kwa zaidi ya mwezi! Ila serikali inataka kila kata iwe na kituo cha afya.

6. Serikali za vijiji haziitishi mikutano mikuu ya vijiji. Wananchi hawajui chochote kuhusu mapato na matumizi! Sheria inasema mkutano mkuu wa kijiji angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu.

7. Upungufu wa walimu. Shule ina walimu 9 wa primary. Wanafunzi wako kati ya 450 na 700. Tatizo ni shule zote.

8. Kila mtoto anatakiwa kuchangia sh 9500 kwa ajili ya mlinzi, uji/ugali maharage mchana na mpishi. Wazazi wanaomba wapewe muda mpaka tarehe 15 kupata hiyo hela! Hawana.

9. Asilimia 90 ya wananchi wa kata yangu ni wakulima. Mvua ndio hizo. Kama hakuna mvua then hakuna kilimo. Wanakuwa kina nani?

10. Maji ya kunywa ni shida. Kuna visima vichache ila wamekatiwa umeme. Hawana uwezo wa kulipa bill.

11. Kuna dispensary (yenye wodi isiyo na sink na choo ndani) bila choo cha nje as first phase. Second phase ndio ujenzi wa choo unaoendelea. Choo ni cha kuvuta so wanahitaji pump ya maji na tenki! Havipo kwenye bajeti. Kwa kuanzia wabebe maji na ndoo. Lakini pia, wamekatiwa umeme toka oktoba wanadaiwa laki 120. Hapo hawakuwa na pump ya maji.

Na mengine mengi, mengi tu.

Mimi binafsi inaniuma sana. Hiyo ndio hali ya huko walipo wananchi ambao hii ni nchi yao. Mbunge leo anachukua mkopo wa milioni 90.

Nisaidieni kufikiri. Mfikirieni mwananchi wa Mabogini kama kielelezo cha wananchi katika kata na mitaa yetu. Mfikirie mtanzania masikini. Mfikirie anayepanga. Mfikirie Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa. Mfikirie Waziri, mfikirie Raisi.

Fikiria siasa za nchi hii. Fikiria viongozi na wasomi wa nchi hii. Nisaidieni kufikiri.

Nimeona ni bora niombe msaada wenu kufikiri. Najiuliza, kama Diwani niko sehemu sahihi na elimu yangu? Je walioniambia 'Albert kagombee ubunge una maslahi' au 'Albert bungeni utatuletea maendeleo kwetu' walikuwa sahihi? Ni wangapi wametelekeza kata na vijiji vyao kwa ajili ya maslahi na kuamini kwamba ndio njia ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia Bunge?

Kwa hali hii tutafika? Nini tufanye wanaJF, wasomi, viongozi, wanaharakati nk!

Sio lazima upost fikra zako hasa zikiwa za matusi au kejeli. Wafikirie walio kwenye kata yako. Jifikirie mwenyewe!

matatizo ni mengi sana kwenye eneo lako mkuu, lakini ni challenge ya kawaida naomba nikushauri

1. Angalia mapato halisi yanayowezeka kupatikana eneo hilo (ambayo mnaweza kutoza kodi ndogo) mfano...mimi ni mwenyekiti wa mtaa tunatoza kodi kwa wanaofetua matofali na wabeba mchanga katika eneo letu tunapata income nzuri kwa aijili ya maendeleo yetu

2. Pili angalia matumizi ya eneo lenu kijiji kwa kijiji unaweza kupata sehemu ndogo mkijadiliana vema na viongozi wenzako

3. Angalia funds zinazopelekwa kutoka serikali kuu hapo wilaya na mgao wake (mkuregenzi atakusaidia). kuna remmitance kutoka serikali kuu za afya, ujenzi (barabara), elimu, etc..check zinatumika na kufika katika eneo lako..wakuregenzi wanakula sana hizo ...

4. Angalia taasisi NGO zilizo katika eneo lako kama wanaweza kutengeneza umoja wao na kuwaeleza priorit ya eneo lako...zungumza noa unaweza kupata misaada kama ya vitabu, ujenzi nk.

5. Angalia nguvu kazi za wananchi..haiwezekani ukashindwa kuwaambia watu wako wasichimbe choo cha shule..vijana wengi hawana kazi unaweza kuwapa pesa wakafanya kazi hiyo kwa bei poa (achana na quatation za ma-engineer hawa ni mafisadi). source..kutoka 1-4 above.

6. Acha kulalamika na kujipendekeza kwa watoto wa shule ili upate sympathy na cheap politics, leta impact ya maana waache watoto wasome usionyesha kuwa kuna tatizo utakuwa baba mpuuzi..
 
umeshakula pilau na Tambwe Hiza ..sasa ni ushuzi tuu
 
Albeto,

pole sana ndugu yangu lakini pia welcome home!
Nikuulize tu kama unaweza kuwa karibu sana na Dr. Slaa kwa kuwa alifanya makubwa kule Karatu na hali ilikuwa kama unavyoieleza. Kwa kuwa yeye ni Katibu wako mkuu nadhani pia atakuwa na muda mwingi wa kukushauri na kukuelekeza nini kifanyike.

Bajeti ya halmashauri baba, pesa zipo tatizo ni zimeelekezwa kwenye vipaumbele gani
 
matatizo ni mengi sana kwenye eneo lako mkuu, lakini ni challenge ya kawaida naomba nikushauri

1. Angalia mapato halisi yanayowezeka kupatikana eneo hilo (ambayo mnaweza kutoza kodi ndogo) mfano...mimi ni mwenyekiti wa mtaa tunatoza kodi kwa wanaofetua matofali na wabeba mchanga katika eneo letu tunapata income nzuri kwa aijili ya maendeleo yetu

2. Pili angalia matumizi ya eneo lenu kijiji kwa kijiji unaweza kupata sehemu ndogo mkijadiliana vema na viongozi wenzako

3. Angalia funds zinazopelekwa kutoka serikali kuu hapo wilaya na mgao wake (mkuregenzi atakusaidia). kuna remmitance kutoka serikali kuu za afya, ujenzi (barabara), elimu, etc..check zinatumika na kufika katika eneo lako..wakuregenzi wanakula sana hizo ...

4. Angalia taasisi NGO zilizo katika eneo lako kama wanaweza kutengeneza umoja wao na kuwaeleza priorit ya eneo lako...zungumza noa unaweza kupata misaada kama ya vitabu, ujenzi nk.

5. Angalia nguvu kazi za wananchi..haiwezekani ukashindwa kuwaambia watu wako wasichimbe choo cha shule..vijana wengi hawana kazi unaweza kuwapa pesa wakafanya kazi hiyo kwa bei poa (achana na quatation za ma-engineer hawa ni mafisadi). source..kutoka 1-4 above.

6. Acha kulalamika na kujipendekeza kwa watoto wa shule ili upate sympathy na cheap politics, leta impact ya maana waache watoto wasome usionyesha kuwa kuna tatizo utakuwa baba mpuuzi..

Wewe jamaa nakutamani nikupe knuckles za pua!! Nakwambia utatafuta pa kukimbilia kipenga kikilia.
 
unaweza anzisha mfuko na fungua account chini ya jina la kata yako "Mabogini" halafu weka hiyo account namba humu ndani tutaona jinsi ya kukusaidia hata $ 10 tutakusaidia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom