wanaJF nimedanganywa au ndio mapenzi na nishaurini basi

Mfalme Daud

Senior Member
Feb 3, 2012
166
109
Asalaaam aleykum ndugu zangu, ninalo zito moyoni mwangu. Nilikuwa na mpenzi wangu tumefahamiana zaidi ya mwaka sasa. Mwezi wa tisa mwaka jana nikiwa field mikoa tofauti nilimwomba aje ili angalau tupunguziane zile hamu. N.B Toka nimefahamiana naye nilikuwa sijawawahi ''kula vyombo'' na kumbuka kuwa tunasoma chuo kimoja. Alikuja nilikaa naye wiki moja kama kawaida nikawa najisevia wakati mwingine ''pekupeku''. Siku ya mwisho nilijisevia akadai nimemgawia katumbo. Nilifurahi sana kwani ni furaha ilioje kuitwa baba. WanaJF, nikawa naendeshwa kweli hapa chuoni na huyu "wife'' mara akawa anahitaji ukwaju na vitu vingine vichachu nikawa nampa kila anachohiji nikijua ana ''kiumbe'' changu na ni my wife to be. Haaa!! miezi ilivyozidi kusonga, dalili za tumbo angalau kuongezeka sikuziona. Akanitaka nianze kuishi naye, misikuwa tayari kwa muda huo si mnajua Koziweki zinabana? Tulipanga kuanza maisha Mwaka Kesho baada ya kugraduate. MWISHONI AKANAMBIA ALIKUWA ANANIDANGANYA, WALA HANA MIMBA YANGU. WANa JF nilijisikia hoooooooovyo na nikamwona hana thamani tena kwangu. Naomba ushauri anaendelea kunifatafata na kujitangaza kwa washkaji kuwa mi wake. Mpaka sasa sitaki ata kumwona kwa alichonifanyia. Mchango wako ni wa maana sana kwangu pliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiz
 
WANa JF nilijisikia hoooooooovyo na nikamwona hana thamani tena kwangu. Naomba ushauri anaendelea kunifatafata na kujitangaza kwa washkaji kuwa mi wake. Mpaka sasa sitaki ata kumwona kwa alichonifanyia. Mchango wako ni wa maana sana kwangu pliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiz
Sasa ushauri gani tena na wewe umeisha muona hana thamani :biggrin:
 
We umeshasema unamwona hovyo na hutaki kumwona. . endelea kukaa nae mbali. Anayodai huko mtaani wala yasikusumbue, we mwache abwabwaje tu atakaeondoka na aibu ni yeye wala sio wewe.
 
mwanaume akishamega utamuona tu...kipi alichofanya ambacho hakisameheki?
 
asalaaam aleykum ndugu zangu, ninalo zito moyoni mwangu. Nilikuwa na mpenzi wangu tumefahamiana zaidi ya mwaka sasa. Mwezi wa tisa mwaka jana nikiwa field mikoa tofauti nilimwomba aje ili angalau tupunguziane zile hamu. N.b toka nimefahamiana naye nilikuwa sijawawahi ''kula vyombo'' na kumbuka kuwa tunasoma chuo kimoja. Alikuja nilikaa naye wiki moja kama kawaida nikawa najisevia wakati mwingine ''pekupeku''. Siku ya mwisho nilijisevia akadai nimemgawia katumbo. Nilifurahi sana kwani ni furaha ilioje kuitwa baba. Wanajf, nikawa naendeshwa kweli hapa chuoni na huyu "wife'' mara akawa anahitaji ukwaju na vitu vingine vichachu nikawa nampa kila anachohiji nikijua ana ''kiumbe'' changu na ni my wife to be. Haaa!! Miezi ilivyozidi kusonga, dalili za tumbo angalau kuongezeka sikuziona. Akanitaka nianze kuishi naye, misikuwa tayari kwa muda huo si mnajua koziweki zinabana? Tulipanga kuanza maisha mwaka kesho baada ya kugraduate. Mwishoni akanambia alikuwa ananidanganya, wala hana mimba yangu. Wana jf nilijisikia hoooooooovyo na nikamwona hana thamani tena kwangu. Naomba ushauri anaendelea kunifatafata na kujitangaza kwa washkaji kuwa mi wake. Mpaka sasa sitaki ata kumwona kwa alichonifanyia. Mchango wako ni wa maana sana kwangu pliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiz

kama huyo ambae ajagraduate alikuona ovyo ma graduate humu si watakuita *****
anyway tuyaache hayo...nimesikitka kushangilia kuitwa baba boko haramu...ni wachache wanaofurahia mimab kabla ya ndoa lakini nikajiuliza tenaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

ulichomoa kukaa nae sababu ya coursework ukweli halisi naujua nisifike huko....5000 aitoshi hata kidogo..kwako binafsi..sasa hili liwe fundisho kwa wana boko haramu wooote wa jf ..mkitegemea mimba za dizaini hii mtafanywa ma ndondocha..samahani kumshukuru huyo binti kwa kukuheshimu kuna dada chuoni aliweka nguo akawa amezibana huko mbele kila mweziz nakwambia siku ya siku jamaa akaambiwa imetoka chooni ndani ya wiki akarudi shule kama kawa weeeeeeeee temamate chini
 
Jitahidi umpe cha ukweli mzidi kupendana, au umpende zaidi maana naona wewe mapenzi yako ni mtoto na si vingine.
 
if you love her, msamehe kwa sababu alikuwa anapima upendo wako kwake na kujitangaza kwa washkaji inaonekana anakukubali. Ila mchunguze sana na umpe maonyo ya kutosha sometimes mzingue mpaka ajione hafai then akivumilia basi atakuwa anafaa. Ni hayo tu ma brada coz unaweza kumwacha huyo ukajapata goma la ajabu zaidi.
 
Huyo aliichomoa iyo mimba!
Ndo tabia ya mabinti wa vyuoni.
Ukikaa vibaya akiwa kabeba ujauzito ambao wewe mwanafunzi mwenzake ndio baba. Anachoropoa.
 
Back
Top Bottom