wanaJF niliokutana nao.....wamenisababishia balaa

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,585
497
Mim na shemeji yeni tulienda mahala kupata dinner,wkt tunasubiri tuletewe chakula tukiwa tumekaa kwenye viti shemeji yenu akaniaga kuwa anakwenda kujisaidia,alipoondoka nikatoa laptop yangu nikaanza kusurf JF nikiwa nimesign in.

Meza yetu ilikua karibu na mlango wa kuingilia ktk hotel hiyo na mim nilikua nimeupa mgongo mlango huo,kwa maana hiyo mtu anayeingia aliweza kuona kilichopo ktk screen ya laptop yangu.Mwanzon nilikua naficha screen ili mtu sione ninachofanya ila baada ya kuingia JF na kuanza kusoma moja ya thread nilijisahau kabisa kuficha screen.

Haukupita muda nikashangaa wakaka watatu nisiowafahamu wakija mbele yangu wakiwa na mshawasha wa ajabu.Nikiwa bado najiuliza hawa ni wa kina nani mbona kama wananifahamu mmoja wao akasema"Cheusimangala habari yako mkuu".Nikatamani kubisha kuwa mm sio Cheusimangala maana huwa sipendi kabisa urain wajue kuwa Cheusimangala wa JF ndio mim kwani huko uraian wana image tofauti kabisa na hii ya cheusimangala.Nikiwa sijui niwajibu nin mwingine akasema"Yaani cheusie daah kweli hizi avatar zinatudanganya sana maana nilikua na picha nyingine kabisa juu yako tofauti na unavyoonekana."

Nikiwa bado nafikiria jinsi ya kukana kuwa mim sio cheusimangala mara nikamuona shemeji yenu anarudi kutoka maliwatoni alipokua huku akiwatizama vijana wale watatu kwa sura yenye kujiuliza ni wa kina nani.Alipofika karibu ikabidi niwaambie vijana wale" huyu ndiye shemeji yenu" nikitumai kwamba wataondoka na kuniachia nafasi ya kujua nitamweleza nini juu ya watu wale ambao hajawahi kuwaona.

Baada ya utambulisho ule mmoja akasema "ooh bwana shemeji nice to meet you" kisha akaendelea" yaani jamii forums ni pana sana unaweza kukutana na members wenzio katika mazingira usiyotegemea kabisa"
Kisha shemeji yenu kwa mshangao akaniuliza"ina maana mpenzi unaifahamu jamii forums?kabla sijamjibu akauliza swali jengine"wewe ni member au unapita kusoma soma tu kwa nje?Nikiwa na mim nashangaa kuwa kumbe na yeye anaijua jamii forums akaniuliza swali jengine"unatumia username gani huko jamii forums"swali hilo lilinizidishia hofu kwani katika vitu nilivyokua sitaki ajue ni kuwa mim ni cheusimangala wa jamii forums lakini nikiwa bado nafikiria haraka haraka nini cha kumdanganya nikasikia mmoja wa wakaka wale akikohoa kidogo huku wote watatu wakionekana kujisikia vibaya kutokana na shemeji yenu kuonekana kupaniki kwa kugundua kuwa naijua jamii forums akasema" cheusie acha sisi tukuage bana nice to see you".Roho yangu ilidunda sana baada ya yule kaka kuniita kwa jina la cheusimangala.

"Ina maana mpenzi wewe ndiye cheusie!...cheusimangala...!this can not be true!no no no"This is a night mmmm...."shemeji yenu hakumaliza alichotaka kusema kwani alidondoka chini na kupoteza fahamu huku michuzi iliyomwagika kutoka mikononi mwa muhudumu aliyekua karibu yake tayari kwa kutuwekea chakula mezani ikiwa imechafua shati lake zuri la blue alipendalo kuliko yote na bila kuchelewa niliwaona wale vijana watatu wakitoka mbio bila hata kutoa msaada kwa mwenzao Huku nikiwasikia wakiambiana"hii tukairushe wapi wakuu habari mchanganyiko au chit chat?"Nikiwa najiandaa kupiga yowe la kuomba msaada alarm yangu ikanishitua kutoka usingizini.

Unafikiri ni kwa nini ktk ile ndoto shemeji yenu alizimia baada ya kugundua kuwa mim mpenzi wake ndiye cheusimangala?Je mim ni mcharuko sana, hapa jf LOL ,au kwa vile ilionesha kuwa na yeye ni member mwenzetu je labda aliwahi kunitongoza pm nikamkubali kirahisi?
 
Cheusi huishi visa wallahi maana nilikuwa nafikiria huo msukosuko uliishaje uzuri ni ndoto...
 
sheeeeeeeenzi nimepoteza muda wangu woote huu kusoma hii SHIGONGO kumbe mwisho wa siku ni ndoto.

:focus: shemegy hawezi kukuacha inategemea labda ashawahi kukutongoza kupitia pm na ukalainika.

hivo kachanganyikiwa.
 
ah ah ah lol u made mai dei,nadhani amekuwa akisoma threads zako,na maybe aliwahi kukutongoza ukakubali as u said,au amekuwa akikerwa na huyo cheusi mangala,so kashangaa mtu anaemkera ndo mkewe mpz,nadhani nimejitahidi kujibu na kuchambua ndoto yako kama joseph(bible)au tukamuulize sheikh tafsiri ya ndoto hiyo? but uwazi na ukweli ni muhim,mm popote na yyte anaenifaham niite tu pearl walaaaaaaaaaaaaaaa sina tatizo kabisaaaaaaaaa
 
Ashukuriwe mungu ni ndoto maana.....!
Yote yanaomgeleka ishu itakuja km alisha kutongoza kwa pm na sijui mliishiaje,
Mbona inakuwa balaa,
Jaman tuwen makin hata ukimstukia mtu haya mambo ya kuvamiana na kuita id sio poa kbs,
Yani nimeijin hiyo picha na kupata kizunguzungu!
 
hahaha Cheusimangala, vituko vyako hivi hivi ndo vilivyomfanya shemeji kazimia kwenye ndoto. Hebu fikiria ikitokea live si ndo utamuua kabisa shemeji yetu? punguza vituko bana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom