WanaJF! Leo nimekutana na makundi kwa makundi la kabila la Maasai. Mwenye kujua,JUZA!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Katika hali ya kutokuwa ya kawaida! Tangu leo asubuhi kuna makundi makubwa ya kabila la Maasai na hususan vijana wa kiume ktk umri tofauti na wakiwa wengi sana kwani huku kwe2 Sakina wamepita kama m2 800 na wakati nikiwa tena kule barabara ya Arusha Dodoma nikakutana na raia tena kama 1000 na nikiwa tena huku Ngaramtoni nikakutana tena na kundi lenye m2 kama 800 ama na ushee! Nikakosa mwenyeji wa kunivumbua vema kwn kila mtu mwenye asili ile alikuwa katika pilika ya huku na huko! Na ktk msafa haya karibu wote na bendera zinazoashiria AMANI na ikiandika sehemu watokako. Na wakati nakutana na hawa wenyeji sikuwa hata na camera kwani ingependeza sana mngeona walivyojipamba na wakakubalika kweli kweli! Swali: Je? Ni nini kimewasibu sana hawa ndg ze2? Kama mwenye fununu a2juze humu jamvini. NAWASILISHA JF!!
 
hata mimi nimekutana nao maeneo ya St Costantine.....nimejilaumu sana kutokuwa na camera wakati huo....wamevaa kimila wamependeza sana na wengine wameweka taji la manyoya ya simba kichwani....sijui itakuwa ni nini
 
Kweli dada yangu??

Labda wanaenda kumpokea Rais wao akirudi toka Magogoni kuonana na ******!!
 
hata mimi nimekutana nao maeneo ya St Costantine.....nimejilaumu sana kutokuwa na camera wakati huo....wamevaa kimila wamependeza sana na wengine wameweka taji la manyoya ya simba kichwani....sijui itakuwa ni nini

Best! Wamependeza kiukweli na hata kwa uchunguzi wa kuibia maana Mi huwa nawahanya hawa ndg ingali si wakorofi,Nimewaona kuna wasichana wachache ktk kila kundi na hata wakinana mama wamebeba vibuyu na nimehisi walienda masafa halafu wakawa wanafuatwa na wakinamama kwa kuwawezesha kwa angalau maji kidogo ama chakula kile nzuri na maarufu waitacho LOSHOROO na hakika ile chakula ni nzuri sana kwn nimebahatikaga kunywa. Inapendeza sana! NA NAHISI NDIYO KABLA AMBALO BADO LINA MSIMAMO AFRICA. Wamependeza kiukweli!
 
hata mimi nimekutana nao maeneo ya St Costantine.....nimejilaumu sana kutokuwa na camera wakati huo....wamevaa kimila wamependeza sana na wengine wameweka taji la manyoya ya simba kichwani....sijui itakuwa ni nini

Kumbe na wewe mtoto mzuri unakaa A-Town? nitakuja huko soon
 
I whish ningewaona na mimi, ila tusuburi tu, lazima kuna mtu alikua na camera atatuletea picha.
 
wangepenza zaidi kma wangekuwa wanakusanyika kuikomboa nchi.
 
naskia wanaenda kwenye jando,sijaithibitisha lakini kwan hata mimi nimekutana nao maeneo ya ngara ya chini
 
Hata mimi nimekutana nao wakati natoka nyumbani kwangu. Ila nimesikia wana mpango wa kuanzisha chama chao cha kisiasa. Ngoja tusubiri tuone.
 
Hayo ni makundi ya vijana wakisindikizwa na wenzao wanaenda kufanyiwa tohara na kuwa morani ( wanaume ). Walikuwa watoto ( laiyon ) sasa wanakuwa wanaume! Huwa inafanyika kila baada ya miaka kama mitano hivi.
Nimekutana nao jioni hii, wameleta foleni kubwa sana mjini.
 
Hayo ni makundi ya vijana wakisindikizwa na wenzao wanaenda kufanyiwa tohara na kuwa morani ( wanaume ). Walikuwa watoto ( laiyon ) sasa wanakuwa wanaume! Huwa inafanyika kila baada ya miaka kama mitano hivi. Nimekutana nao jioni hii, wameleta foleni kubwa sana mjini.
lakini jando kuelekea mjini...?.....si huwa nasikia wanaenda maeneo ya poripori......au hii imekuwaje?...na wamama ndani...?
 
lakini jando kuelekea mjini...?.....si huwa nasikia wanaenda maeneo ya poripori......au hii imekuwaje?...na wamama ndani...?

Wametoka maeneo mbalimbali ya mkoa. Maeneo ya Ilboru, ngaramtoni, moshono, Kiding'a na mengineyo na wanaelekea duka bovu. Huko ndio wanakofanyiwa tohara. Wamama nadhani ni wasindikizaji kwaajili ya menu!
 
Nimewaona muda si mrefu, naka sakina karibu na dar express,vijana wanaenda jando.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom