Wanajeshi watoa kipigo Dawasco

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
351
na Amana Nyembo



ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), jana walivamia ofisi za Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani (DAWASCO) zilizoko eneo la Ubungo Terminal jijini Dar es Salaam na kutoa kipigo kwa watumishi wa taasisi hiyo ya umma.
Tukio hilo lililosabisha kujeruhiwa kwa wafanyakazi wanne wa Dawasco lilitokea muda mfupi baada ya amri ya wanajeshi hao kutaka mabomba yao ya maji yaliyokatwa yakaunganishwe kukataliwa.

Dawasco ilichukua uamuzi wa kukata maji hayo juzi kama sehemu ya zoezi lake linaloendelea la kuwakatia maji wateja wake wote ambao hawalipii ankara zao. Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa JWTZ ni moja ya wadaiwa sugu wa Dawasco kwani inadaiwa kiasi cha sh milioni 276.

Vurugu hizo zilianza majira ya saa 4:00 asubuhi muda mfupi baada ya wanajeshi watano kufika katika ofisi hizo wakiwa katika gari lao aina ya Land Rover na wakawaamuru wafanyazi wa Dawasco kuondoka nao na kwenda kurejesha maji waliyowakatia juzi.

Akizungumza na Tanzania Daima jana alasiri, Meneja Uhusiano wa Dawasco, Badra Masoud alisema baada ya kuona jitihada hizo zikishindikana, wanajeshi hao waliwachukua kwa nguvu wafanyakazi watatu wa Dawasco katika gari lao na kuondoka nao hadi katika kambi ya Jeshi la Lugalo.

Walipofika Lugalo, wanajeshi hao walianza kuwapa adhabu za kuwaviringisha ardhini ‘drill’, na kuwarusha kichura kabla hawajawachukua tena na kuwarejesha katika ofisi zao za Ubungo majira ya saa 8:00 mchana.

Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wafanyakazi wa Dawasco, Samuel Massawe, ambaye alipata kipigo na kuumia sehemu za uso na mguu wa kulia, alisema kuwa wanajeshi hao walifika katika ofisi zao wakiwaamrisha wafanyakazi hao wawafungulie maji ambayo yalikatwa juzi.

Alisema kuwa, wanajeshi hao walisema wasipowafungulia maji watakwenda kufungua wenyewe katika mtambo wao mkubwa wa Ruvu Juu.

Massawe alisema kuwa baada ya wao kukataa agizo hilo, ndipo askari hao walipoanza kuchukua hatua za kuwapiga huku wakitumia virungu, hali iliyosababisha yeye na wafanyakazi wenzake watatu; Josephina Kombe, Malik Rajabu na Zuhura Salumu kujeruhiwa.

Alisema kuwa wakati wakijaribu kujinusuru kwa kupiga simu Makao Makuu ya Dawasco, wanajeshi hao waliwadhibiti na kuzichukua simu zao, kabla ya kuzirejesha muda mfupi baadaye.

Tukio hili lilisababisha maofisa wa Dawasco makao makuu kuwasili Ubungo majira hayo hayo ya saa 8:00 na muda mfupi baadaye wanajeshi hao wakiwa katika gari lao waliwasili tena hapo na wakaanza kuzozana na Ofisa Biashara wa Dawasco, Raymond Mndolwa.

Mzozo huo uliendelea kwa wanajeshi hao kumkamata Mndolwa na wakaanza kumvuta nje ya eneo kwa lengo la kuondoka naye, jitihada ambazo hata hivyo zilishindikana.

Baada ya kubaini kuwa tukio hili lilikuwa likirekodiwa na wanahabari, wanajeshi hao walimvamia mpiga picha wa gazeti la Mwananchi, Fidelis Felix na wakamnyang’anya kamera yake baada ya kupiga picha zilizokuwa zikionyesha jinsi Mndolwa alivyokuwa akizingirwa na askari hao na kumvuta atoke nje ya ofisi.

Muda wote wakati wa mzozo huo, Mndolwa alikuwa akiwalaumu wanajeshi hao kwa kujichukulia sheria mkononi na kuwaumiza wafanyakazi ambao kimsingi hawakuwa na makosa yoyote.

“Kama kuhusika na kukata maji ni mimi, na kama wanataka kumpiga mtu wanipige mimi na si nyinyi wafanyakazi na kama kila mtu akichukua sheria mkononi hii itakuwa nchi gani? Nimesikia wanataka kwenda kufungua mtambo wa Ruvu Juu,” alisema Mndolwa.

Katika hali inayoonyesha kana kwamba kauli hiyo haikuwafurahisha wanajeshi hao, walimtaka Mndolwa atoke nje ya ofisi wakazungumze naye, hoja ambayo aliikataa.

Hatua hiyo ilisababisha mmoja wa wanajeshi hao kuwaamuru wenzake wamtoe nje kwa nguvu hali iliyosababisha kuanza kuvutana kabla ya hatua hiyo kugonga mwamba.

Kuona hivyo, Mndolwa aliamua kwenda kupanda gari ili aondoke eneo hilo juhudi ambazo hata hivyo zilikwama baada ya wanajeshi hao kukimbilia getini kulifunga wakimzuia kutoka.

Hatua hiyo ya wanajeshi iliyodumu kwa zaidi ya nusu saa ilisababisha watu washindwe kutoka au kuingia katika ofisi hizo kwa muda wote huo, kabla wanajeshi hao hawajaamua kuondoka.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Badra alisema tayari walikuwa wameshafungua faili la malalamiko polisi na kupewa hati ya watuhumiwa hao kukamatwa ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa.

Hata hivyo, katika hatua nyingine, Jeshi la Ulinzi jana lilitoa taarifa likilalamikia uamuzi huo wa Dawasco kulikatia maji jeshi na kutangaza taarifa hizo kupitia katika vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, jeshi hilo linasema kiasi cha fedha kinachotolewa na serikali kwa ajili ya gharama za maji ni kidogo na kwamba bili zinazotolewa na Dawasco si sahihi na zinapaswa kuhakikiwa.
Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/23/habari1.php
 
wazee habari zenu.Nimesoma hii post ya wanajeshi imenisikitisha sana.sijui watu mnaichukuliaje lakini hii kitu inaonyesha jinsi gani Serikali zetu zinavyoendeshwa kienyeji na kihuni.Tunashangilia misaada ya mamilioni ya fedha za kama ndio yatatutoa kwenye matatizo lakini mimi naona tunachoitaji ni msaada wa kupambana na uprimitive na kuomba mungu atuondoe kwenye hivi vichwa vya uwendawazimu.Ahsanteni sana
 
Hawa wanajeshi ni watovu wa nidhamu sana. Mara nyingi wanawapiga raia pasipo sababu. Sasa kama hawataki kulipia maji wanataka DAWASCO wakale wapi? Na shirika litajiendeshaje?
 
Hawataki kulipa...wanataka kuwa kama tanga cement na Tanesco?
Au wanataka na shirika la maji lifikie hatu kama ya Tanesco?

Huu ndio mwanzo wa kuua mashirika kwa ajiri ya kutolipa.
Madeni...sasa wao ni nani wasikatiwe maji kama hawalipi?
Harafu kuna wanajeshi wanafikiri kuwa mwanajeshi ni kutumia nguvu bila akiri..,sijui hawa walitumwa nao hawana akili...kuwa usipo kuwa na hera hata soda dukani uhudumiwi.
 
This could only happen where disciplined forces have no discipline at all. What a shame? Soldiers should never take the law into their own hands. It is called mutiny when they do that.

Mutiny need not start with soldiers taking over the State House. It starts with men and women in uniform generally taking the law into their own hands. The TPDF is doing just that.

Serikali angalieni: msipoziba ufa mtajajenga ukuta.
 
Ndugu wana JF

Pongezi sana kwa kazi mliyoifanya na mnayoendelea kuifanya mimi nilikuwa naisikia JF lakini mara nyingi nilikuwa sijaifuatilia sana kujua yanayojiri. Baada ya kusikia misukosuko iliyotokea na baada ya kusoma habari kupitia KLH news na kugundua kwamba imerudi hewani nimeamua kujisajiri ili nami niwe mwanachama na kuweza kuungana na wenzagu wanaoitakia mema nchi yetu nzuri ya Tanzania.

a) Pongezi za pekee kwa waanzilishi wa JF pamoja na Mwanakijiji na wengine kazi mnayofanya ni kubwa na inataka moyo sana. Kwa ilo ni naomba mpokee pongezi zangu.

b) Sasa tufanye kazi kwa bidii tufanyeni utafiti wa kina na tuwafikie hata wale watu wasio na uwezo wa kupata habari tuweze kuwafahamisha ni jinsi gani maisha yao yanadumazwa na mafisadi wasio na huruma hata kidogo.


c) Kama kuna michango inahitajika kuweza kuimarisha JF mimi niko tayari kuhamasisha na pia niko tayari kuchangia kwa hali na mali. Hivyo mwanakijiji na wengine iwapo kuna msaada utakaotakiwa tuwasiliane kwenye "PM".

d) Ikiwezekana tuwe na watu wa kutuletea habari toka pande zote za nchi. Wale ambao wana moyo wa kujitolea na ambao wanaweza kuwa wanakusanya matukio mbalimbali ambayo mara nyingi huwa hayawafikii watanzania walio wengi.

e) Tuna safari ndefu sana ya kuutokomeza UFISADI Tanzania. Sasa inabidi tuangalie nini mustakabali wa JF miaka 3, 5, 10, 15 ijayo mbele. Iwepo mikakati mizuri na ya hali ya juu katika kuhakisha kwamba JF unakuwa ni mtandao imara unaoweza kuwaunganisha wale wote wanaoitakia mema nchi yetu ya Tanzania.

f) Ebu jiulize wamarekani na hao wazungu toka nchi za dunia ya kwanza waliopo sasa kama si kuteseka kwa mababu zao unadhani wangekuwa wanafaidi...msingi mzuri kwao ulijengwa miaka 50, 100, 200 iliyopita na sisi sasa. Sasa Watanzania wenzagu tuamke na kuhamasishana ili wajukuu zetu na vitukuu waweze kuiona Tanzania nzuri. Hawa walioko madarakani sasa hawawezi kutufikisha popote...

Jamani wote tuamke sauti zisikike na tuijenge Tanzania kuanzia leo na si kesho...

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki JF
Mungu wajaze nguvu waanzilishi na wanachama wote wa JF ili waweze kufichua maovu....[/SIZE
]
 

Serikali angalieni: msipoziba ufa mtajajenga ukuta.


Kwa JW ukuta uko hoi, na nyufa zake ni kubwa na labda ukarabati wake ni gharama hivyo inabidi labda uangushwe ili ujengwe upya.

JW wamekuwa wababe na wakorofi hata katika mambo ya kijamii, kama ile issue ya kufungwa (kwenye mpira) kule morogoro.

Serikali (waajiri) wao inawafumbia macho na sioni kama wanachukua hatua za haraka za kukabiliana na vitendo vyao vya kihuni wanavyovifanya.

Wamepiga raia ovyo na wameharibu mali za raia kule mbeya, morogoro, kunduchi.
Wamewapiga madereva wa madaladala na sasa wameingia dawasco-ofisini.

Nafikiri tutakuja kuona watu wakishushwa kwenye magari yao pale mitaa ya lugalo na kupewa kichapo kwa sababu wamewanyima lifti.
 
Nafikiri tutakuja kuona watu wakishushwa kwenye magari yao pale mitaa ya lugalo na kupewa kichapo kwa sababu wamewanyima lifti.

Mkuu,
Hii ishatokea sana tu.
Kwa sisi wengine ambao tumekulia mitaa ya Tangibovu tunajua sana kadhia za namna hii, kuna makonda kibao sana wamepigwa kutokana na kuwakatalia jamaa kujazana katika dala dala moja kwa mpigo.
Ila kila lenye mwanzo lina mwisho, kuna siku raia watachoka na manyanyaso haya watadai haki yao bila kujali magwanda!
Sijui nini hatima yake, ila lisemwalo lipo!
 
Si vizuri mwanajeshi ndani ya uniform kukaa barabarani anaomba lifti. Kwanza anakwenda wapi? Kama ametumwa kikazi apelekwe na gari la Jeshi. Kama anakwenda kwa shughuli binafsi basi atoe uniform na kuvaa mavazi binafsi huko huko kambini ndipo atoke barabarani aombe lifti.

Nguo za kivita zitumike kwa heshima inayotakiwa. Askari wachukuliwe na magari yao asubuhi na warudishwe nyumbani jioni. Wasijitafutie usafiri wenyewe, na huku wana uniform zao.

Wanajeshi wanatakiwa kulinda usalama wa raia. Watatekelezaje hilo kama wanawapiga raia? Ikifika mahali raia tukachoka kupigwa tukaamua kupambana nao itakuwaje?

Askari waliojichukulia sheria mkononi na kuwapiga na kuwafunga wafanyakazi wa DAWASCO ni waasi. They should be court martialled.
 
Back
Top Bottom