Wanajeshi kadhaa wa JWTZ kikosi cha mizingo wanaoishi katika mji wa Monduli wamewatesa vijana wawili waliowatuhumu kwa kuwaibia vifaa vya elektroniki. Mateso hayo ya kipigo kwa siku mbili mfululizo yamepelekea kijana mmoja kati ya walioteswa kwa kupigwa mbele ya maafisa wa jeshi la polisi na UWT kupoteza maisha. Ndugu wa kijana aliyeuwawa wamekataa kuuchukua mwili hospitalini kwa ajili ya maziko hadi uchunguzi unaoridhisha utakapofanyika na wauaji kufikishwa mahakamani. Inasemekana kuwa askari hao wa JWTZ walitoa taarifa ya kuibiwa mali zao kituo cha polisi Monduli. Baada ya kuona polisi hawachukui hatua kwa haraka kama walivyotarajia ndipo walipoamua kujichukulia sheria mkononi.
Hii ndiyo nchi ya amani na utulivu.
Hii ndiyo nchi ya amani na utulivu.