WANAJESHI wameanza kufyatuka kupaza sauti kudai mabadiliko

Nadhani humjui Tumaini Makene, ni nani Chadema, kwa kukusaidia ni msemaji wa Chadema kachukuwa nafasi ya Regia Mtema (R.I.P) ndio maana nimejibu hivyo wewe bila kujua umerukia kumjibia.

Ondoa umbumbumbu wako hapa. Tangu lini marehemu Regia alikuwa msemaji wa Chadema? Kama kitu hukijui ni vizuri kuuliza kuliko kujifanya kujua kila kitu na kuishia kuongopea watu.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani humjui Tumaini Makene, ni nani Chadema, kwa kukusaidia ni msemaji wa Chadema kachukuwa nafasi ya Regia Mtema (R.I.P) ndio maana nimejibu hivyo wewe bila kujua umerukia kumjibia.
Nilianza kwa kujadili contents,nikaenda kuisoma linki,nikachanganya na zangu,sijaona pahala popote panapoonyesha huyo mwanajeshi ni chadema.Wewe umemjadili mleta hoja,umeona?Na sijarukia kumjibia na kiswahili chako kibovu kabisa.Nilikuuliza kama umeisoma link,halafu hilo gazeti si pro fisadi?Kichwa mbali na kufugia nyewe,kina kazi ya kufikiri,kitumie kwa ajili hiyo pia.Utilize your brain my friend.
 
Ni hatari sana kushabikia uasi wa wanajeshi kwa tamaa za kisiasa. Wanajeshi wakidai mabadiliko wanatumia risasi. Ni mtanzania gani anataka kuchochea wanajeshi watumie hivyo vyombo vya moto eti kutaka mabadiliko?

Wanajeshi hawana tamaa kama mbayuwayu wa chadema kila kukicha kupaza sauti na kuchonganisha watanzania eti wafanye vurugu ili slaa awe rais. Hizo ni kerere za chura kama mliyoambiwa jana. Vurugu zikitokea mkeo au mumeo anaweza kuwa wakwanza kufa. Tuliona kule rwanda na burundi na hatutakiii. Endeleeni kuchochea lakini tunajua mbinu zenu zoote zimekwama.

Acheni mawazo ya ki renamo na conservative union.
 
Nimeisoma maoni yao yalikuwa dhidi ya mafisadi wanataka wanyongwe sio kuwa wanadai mabadiliko.
Kama hayo sio mabadiliko kwani sasa mafisadi wananyongwa? Si umesikia Twiga wetu wamepandishwa ndege za waarabu adhabu iliyotolewa jamaa wamesimamishwa kazi. Jairo na Luhanjo wanakula kuku tu, EL wa RICHMOND anaitwa KASTAAFU - Hivi anakula pensheni za PM mstaafu? tunaomba tuulizie maana CCM bwana yote yanawezekana.

Mabadiliko hapo ni kwamba hao jamaa waliohusika kuwagawia waarabu twiga wetu walambwe risasi, na waliohusika na RICHMOND na DOWANS wapigwe risasi, MEREMETA, KAGODA, DEEPGREEN nk wote wapigwe risasi. Hayo ndio mabadiliko yanayodaiwa na askari wetu sasa. Nadhani nao wamechoka sasa na usanii wa magamba.
 
Chadema wamekuwa watu wa kurukia matukio na kuyatolea matamko sasa huyu msemaji wa Chadema amekuwa msemaji wa Wanajeshi, kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa Wanajeshi walichosema wanataka mabadiliko ya kiutawala Chadema wachukue nchi.

Uko nje ya mada.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ondoa umbumbumbu wako hapa. Tangu lini marehemu Regia alikuwa msemaji wa Chadema? Kama kitu hukijui ni vizuri kuuliza kuliko kujifanya kujua kila kitu na kuishia kuongopea watu.

Hivi wewe ni Chadema kweli au ni Chadema-Kata hujui kama marehemu Regia alikuwa ndio msemaji wa Chadema humu JF, Dr Slaa kamleta Tumaini Makene baada ya marehemu...unajifanya Chadema kumbe hujui lolote.
 
Last edited by a moderator:
Nilianza kwa kujadili contents,nikaenda kuisoma linki,nikachanganya na zangu,sijaona pahala popote panapoonyesha huyo mwanajeshi ni chadema.Wewe umemjadili mleta hoja,umeona?Na sijarukia kumjibia na kiswahili chako kibovu kabisa.Nilikuuliza kama umeisoma link,halafu hilo gazeti si pro fisadi?Kichwa mbali na kufugia nyewe,kina kazi ya kufikiri,kitumie kwa ajili hiyo pia.Utilize your brain my friend.

Mkuu kiswahili changu kibovu kabisa tajifunza wewe mwenye kiswahili kizuri haya maneno ni nini "kufugioa" "nyewe"
 
Hatari kweli kweli hii! Itabidi kuwa na siku za "mapumziko" kitaifa kwa ajili ya kuzika.

Now, more than 80% ya wanachama wa CCM (5,000,000?) ni mafisadi. Suppose, 30% tu ya hao 80% watatiwa hatiani na hizo adhabu kutekelezwa ndani ya wiki moja baada ya hukumu. Bwa ha ha ha ha ha!

Hii maana yake, ndani ya wiki moja tutapiga risasi na kuzika mafisadi 30% x 80% x 5,000,000 = 1,200,000. Nashauri wazikwe kwenye makaburi ya jumla au wachomwe moto watatumalizia tu ardhi na muda hawa.

Mkuu punguza hasira! Bwa ha ha ha ha. Makaburi ya jumla? Bwa ha ha ha! Bora wachomwe nasikia mtu mmoja majivu yake hayajai viberiti viwili kanafasi ka kuzika ka square mita moja tunaweka masifadi nyomi!
 
Mkuu kiswahili changu kibovu kabisa tajifunza wewe mwenye kiswahili kizuri haya maneno ni nini "kufugioa" "nyewe"
Hiyo ni typo, halafu sema "nitajifunza",baada ya hapo,uweke full stop,halafu ndo uendelee kusema "Wewe mwenyewe kiswahili...".Lafudhi yako sijui ya wapi?kihindi?

Huwa nilikuwa nikidhani ni just typos,lakini nimegunduwa kiswahili huwa kinakupa shida kukitype humu.

Kwamfano kama unazungumzia sentesi ya kukanusha ie "Hukufanya...",wewe huwa unasema "ukufanya..."

Ni mfano tu,hata mimi sijui kiswahili sana,lakini sina matatizo kama yako.

Hapo juu umesema "Wewe mwenyewe kiswahili kizuri",halafu more ramblings,mkuu humu tunajifunza pia,kubali kujifunza.Kama hujui kiswahili,kachukuwe kozi ama tembelea jukwaa la lugha.
 
Twiga wanauzwa na wanasafirishwa kwenda nje kama walivyo. Tena mchana kweupe. Madini ndio usiseme. Unategemea nini?
 
“Katiba ijayo iweke wazi, kuwa kiongozi anayepewa dhamana ya kuongoza jamii, ikiwa ni waziri kafanya ubadhirifu, napendekeza anyongwe ili iwe fundisho, akija mwingine ajue kuna kitanzi, kwa sisi wanajeshi, apigwe risasi.

“Tunasikia mambo ya Dowans na Richmond na tunachukia kusikia yanaendelea, halafu wahusika wanapewa nafasi ya kujitetea na wakifika mahakamani, wanapigwa faini,” alisema Nyansango ambaye ana elimu ya darasa la saba.

Nimeisoma maoni yao yalikuwa dhidi ya mafisadi wanataka wanyongwe sio kuwa wanadai mabadiliko.

Ndugu hapo kwenye bold, kwani mabadiliko kwako yana maana gani??
 
Chadema wamekuwa watu wa kurukia matukio na kuyatolea matamko sasa huyu msemaji wa Chadema amekuwa msemaji wa Wanajeshi, kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa Wanajeshi walichosema wanataka mabadiliko ya kiutawala Chadema wachukue nchi.
Mkuu, huwa unasoma habari hadi mwisho au unasoma katikati ya mistari? Dah!!!!
 
aaaah wajedaaaa.....kazeni uzi huo huo kama mnavyokaza buti......
 
Kujibizana na ritz ni kupoteza wakati unaopaswa kujadili hoja muhimu kama hii, wanajeshi wamenena mafisadi hawatakiwi kabisa, ni kunyongwa na kupigwa risasi hii ndo dawa yao
 
so Ritz unaogopa mafisadi wasinyongwe, hii inaonesha kabisa wewe na ccm wote mafisadi tuu
 
Back
Top Bottom