wanajeshi wa rugalo mnatukomoa abilia, wengine tunaumwa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
kutokana na daraja linalo unganisha kawe na tank bovu kubomoka, wanajeshi wa rugalo ndo wanasimamia movement za watu na magari wakati wa kuvuka daraja. lakini umbali walio uweka ikishuka gari ili upande gari lingine ni mkubwa sana. mtu unashuka njia panda ya kawe unaenda kupanda tank bovu. halafu wanaamulisha utafikili sisi sote wajeda. kwani magari yasingekuwa yanafika darajani kabisa yaani ukishuka gari unapanda gari? mtu hadi upande gari ushalowa.haipendezi. ova
 
Alaaa! kumbe! Basi kesho tunabadili zoezi tutawatembeza kutoka Mikocheni hadi Tegeta tena huku mkiimba nyimbo za kikakamavu.
 
Kwani Tanganyika kuna Jeshi au wacheza karate, Wanajeshi wetu wavivu wa kila kitu. Wanachikijua wao ni kuonea raia
 
kutokana na daraja linalo unganisha kawe na tank bovu kubomoka, wanajeshi wa rugalo ndo wanasimamia movement za watu na magari wakati wa kuvuka daraja. lakini umbali walio uweka ikishuka gari ili upande gari lingine ni mkubwa sana. mtu unashuka njia panda ya kawe unaenda kupanda tank bovu. halafu wanaamulisha utafikili sisi sote wajeda. kwani magari yasingekuwa yanafika darajani kabisa yaani ukishuka gari unapanda gari? mtu hadi upande gari ushalowa.haipendezi. ova

Tumia reasoning mkuu, wajeda wako sahihi kabisa wameweka umbali unaotakikana kiusalama kwa vituo vya mabasi kushushia abiria toka katika daraja lililobomoka.
 
Ukitaka kuwajua kama machizi na vituko jifanye kugoma au hauwezi kutembea ndipo utakapo omba ni bora usombwe na maji ukafie mbele kuliko kukutana na wanajeshi vimbora wa serikali legelege ya ccm.
 
Tumia reasoning mkuu, wajeda wako sahihi kabisa wameweka umbali unaotakikana kiusalama kwa vituo vya mabasi kushushia abiria toka katika daraja lililobomoka.
Ni kqweli kabisa maana asibuhi leo kabla hawajafika kulikuwa na vurugu kweli kweli na dalada nyingi zilizkuwa zinakosakosa kuwagonga abiria na kukwaruzana zenyewe lilikuwa ni jambo la kawaida tu
 
Poleni sana. Kwa wale ambao sio wagonjwa kama wangepitia JKT iyo hali wangeiona ni ya kawaida.
 
Mkuu kwa kweli pale sasa hivi kuna ustaarabu. Daladala zimeelekezwa eneo la kugeukia (huku posta) na si palepale njia panda walipokuwa wanageuzia kiholela, halafu uzuri zaidi wanajeshi hawaruhusu hata bodaboda kupita darajani, bila hivyo aisee sijui hali ingekuwaje wangeaachia mambo holelaholela
 
Poleni sana. Kwa wale ambao sio wagonjwa kama wangepitia JKT iyo hali wangeiona ni ya kawaida.

Mkuu umbali wenyewe wa kutembea anaoulalamikia mleta thread ni kama hatua mia nne tu hivi toka kila upande wa daraja. Inastaajabisha!
 
Back
Top Bottom