Wanajeshi kortini kwa ufisadi wa mabilioni

Dah! huyu Lt Col Paul Andrew Mayavi nilisoma nae Tabora Sekondari pamoja na akina Makongoro Nyerere miaka ile ya sabini. Mayavi alikuwa Chief Hog. Mara ya mwisho nilikutana naye miaka 30 iliyopita akiwa Luteni wa JKT. Chief Mayavi alikuwa mtu mwungwana na mwadilifu kweli kweli, kama tuhuma hizi ni za kweli basi nadhani system imembadilisha; sitegemi mtu yule afanye madudu kutokana na jinsi alivyokuwa na maadili ya hali ya juu sana.
 
Maofisa sita wa Jeshi nchini na wanajeshi ambao ni Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma-JKT), wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kula njama na matumizi mabaya ya ofisi na kuhamisha Sh. bilioni 3.8 kutoka kwenye akaunti ya Kampuni ya Tanzania Korea Patnership (Takopa), kwenda akaunti ya Suma-JKT.

Washtakiwa hao, Kanali Ayoub Mwakang'ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo, Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Sajini John Laizer, Meja Yohana Nyuchi na Luteni Kanali Felix Samillan, watumishi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana.

Upande wa mashtaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Donasian Kessy, akisaidiana na Ben Linkolin.

Kessy alidai katika shtaka la kwanza Machi 5, mwaka 2009 kwenye ukumbi wa mikutano wa Suma JKT jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa kukusudia walitumia madaraka vibaya kuipa zabuni Kampuni ya Takopa ya kununua magari na vyuma chakavu bila kibali cha bodi ya kampuni hiyo.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Machi 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wakiwa wajumbe wa bodi hiyo, walitumia madaraka vibaya kwa kununua magari na vyuma chakavu bila kutii Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 58 (3).

Kesi alidai kuwa katika shtaka la tatu, Machi 16, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa wa pili Kichogo na wa saba Samillan , walihamisha Sh. 2,744,432,545 kupitia hundi namba 000010 kutoka akaunti 011103031753 ya Takopa kwenda akaunti namba 01110307094 ya Suma-JKT, zilizopo Benki ya NBC kinyume cha Kifungu cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 156 ya mwaka 2001.

Aliendelea kudai kuwa katika shtaka la nne, Aprili 3, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Kichogo na Samillan, walihamisha Sh. 489,677,878.30 kupitia hundi namba 000011 kutoka akaunti namba 011103031763 ya Takopa kwenda akaunti namba 011103017094 ya Suma-JKT zilizopo benki ya NBC kinyume na Kifungu cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 156 ya mwaka 2001.

Mwendesha Mashtaka huyo, alidai shtaka la tano, Aprili 4, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Kichogo na Samillan, walihamisha Sh. 269,519,093.60 kupitia hundi namba 000012 kutoka akaunti namba 011103031753 ya TAKOPA kwenda akaunti namba 011103017094 ya Suma-JKT zilizopo NBC kinyume cha Kifungu cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 156 ya mwaka 2001.

Katika shtaka la sita, Mei 4, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Kichogo na Samillan, walihamisha Sh. 350,000,000 kupitia hundi namba 000015 kutoka akaunti namba 011103031753 ya Takopa kwenda akaunti namba 011103017094 ya Suma-JKT zilizopo benki ya NBC kinyume cha Kifungu cha 156 Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001.

Alidai katika shtaka la saba, kati ya Machi na Mei, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam washtakiwa , walikuwa njama ya kuhamisha Sh. 3,853,629,416.90 kutoka akaunti namba 011103017094 ya Takopa iliyopo NBC kinyume cha Kifungu Cha 156 Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001.

Washtakiwa hao walikana mashtaka yao kwa nyakati tofauti.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana dhidi ya washtakiwa na upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hakimu Katemana aliwataka washtakiwa kujidhamini kwa hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. milioni 25, kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani hiyo ya fedha kila mmoja.

Aidha, washtakiwa walitimiza masharti hayo na wako nje kwa dhamana hadi Agosti mosi, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.

Mapema saa 3:23 asubuhi washtakiwa hao walifikishwa katika viunga vya Mahakama hiyo, wakiwa kwenye magari mawili tofauti, T 529 ASM na DFP 8763 za rangi nyeupe aina ya Toyota Land- Cruiser.


CHANZO: NIPASHE
 
Maana yake hata watu wakipelekwa JKT hakuwafanyi kuwa wazalendo. Uzalendo ni utashi wa mtu binafsi.
 
Kama junior officer anahomola mabilioni je hao mabosi wao wamehomola trilioni ngapi. 2015 zote zitarudi kwa wananchi hizo.
 
huyu jamaa ni jirani yangu kimara,ndo watu wa kwanza kujenga ghorofa kimara,yeye na mkewe anatambela HUNDAI Brand new.anainekana ana mali nyingi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom