Wanajeshi kortini kwa ufisadi wa mabilioni

Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
624
Sikuamini macho yangu, huyu mukulu wa mradi wa yale Matrekta ya Suma JKT pakle Mwenge maarufu kama "Kilimo Kwanza" nimeshuhudia leo akishuka kwenye gari ya Takukuru akiwa anafikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka pamoja na wenzake. Kulikoni? Ni Mjeshi huyu.

Mara ya mwisho tulikaa nae kwenye ndege kwenye viti vya jirani na tukazungumza mengi, alikuwa ana hulka ya kilokole na mwenye kujawa na busara akichukizwa na uovu, sasa sijui imekuwaje tena.

Anyway tuiachie Mahakama.
Gazeti la Mwananchi ukurasa wa tatu linaripoti wanatuhumiwa wako sita, nao ni Lt Col Ayoub Emu Mwakang'ata (CEO SUMA/JKT), Lt Col Mkochi Chacha Kisongo, Lt Col Paul Andrew Mayavi, Major Peter Mabula Lushika, Sajenti John Andrew Laizer na Major Yohana Leonard Nyuchi. Gazeti hilo limebandika picha zao front page wakienda mahakamani.
UPDATES:
Maofisa sita wa Jeshi nchini na wanajeshi ambao ni Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma-JKT), wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kula njama na matumizi mabaya ya ofisi na kuhamisha Sh. bilioni 3.8 kutoka kwenye akaunti ya Kampuni ya Tanzania Korea Patnership (Takopa), kwenda akaunti ya Suma-JKT.

Washtakiwa hao, Kanali Ayoub Mwakang'ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo, Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Sajini John Laizer, Meja Yohana Nyuchi na Luteni Kanali Felix Samillan, watumishi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana.

Upande wa mashtaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Donasian Kessy, akisaidiana na Ben Linkolin.

Kessy alidai katika shtaka la kwanza Machi 5, mwaka 2009 kwenye ukumbi wa mikutano wa Suma JKT jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa kukusudia walitumia madaraka vibaya kuipa zabuni Kampuni ya Takopa ya kununua magari na vyuma chakavu bila kibali cha bodi ya kampuni hiyo.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Machi 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wakiwa wajumbe wa bodi hiyo, walitumia madaraka vibaya kwa kununua magari na vyuma chakavu bila kutii Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 58 (3).

Kesi alidai kuwa katika shtaka la tatu, Machi 16, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa wa pili Kichogo na wa saba Samillan , walihamisha Sh. 2,744,432,545 kupitia hundi namba 000010 kutoka akaunti 011103031753 ya Takopa kwenda akaunti namba 01110307094 ya Suma-JKT, zilizopo Benki ya NBC kinyume cha Kifungu cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 156 ya mwaka 2001.

Aliendelea kudai kuwa katika shtaka la nne, Aprili 3, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Kichogo na Samillan, walihamisha Sh. 489,677,878.30 kupitia hundi namba 000011 kutoka akaunti namba 011103031763 ya Takopa kwenda akaunti namba 011103017094 ya Suma-JKT zilizopo benki ya NBC kinyume na Kifungu cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 156 ya mwaka 2001.

Mwendesha Mashtaka huyo, alidai shtaka la tano, Aprili 4, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Kichogo na Samillan, walihamisha Sh. 269,519,093.60 kupitia hundi namba 000012 kutoka akaunti namba 011103031753 ya TAKOPA kwenda akaunti namba 011103017094 ya Suma-JKT zilizopo NBC kinyume cha Kifungu cha Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 156 ya mwaka 2001.

Katika shtaka la sita, Mei 4, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Kichogo na Samillan, walihamisha Sh. 350,000,000 kupitia hundi namba 000015 kutoka akaunti namba 011103031753 ya Takopa kwenda akaunti namba 011103017094 ya Suma-JKT zilizopo benki ya NBC kinyume cha Kifungu cha 156 Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001.

Alidai katika shtaka la saba, kati ya Machi na Mei, mwaka 2009 jijini Dar es Salaam washtakiwa , walikuwa njama ya kuhamisha Sh. 3,853,629,416.90 kutoka akaunti namba 011103017094 ya Takopa iliyopo NBC kinyume cha Kifungu Cha 156 Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001.

Washtakiwa hao walikana mashtaka yao kwa nyakati tofauti.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana dhidi ya washtakiwa na upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hakimu Katemana aliwataka washtakiwa kujidhamini kwa hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. milioni 25, kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani hiyo ya fedha kila mmoja.

Aidha, washtakiwa walitimiza masharti hayo na wako nje kwa dhamana hadi Agosti mosi, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.

Mapema saa 3:23 asubuhi washtakiwa hao walifikishwa katika viunga vya Mahakama hiyo, wakiwa kwenye magari mawili tofauti, T 529 ASM na DFP 8763 za rangi nyeupe aina ya Toyota Land- Cruiser.


CHANZO: NIPASHE
 
Yale matrekta uchina ni dola 2000 na kama wangeagiza mengi wangeweza uziwa moja kwa dola 1500 mpaka 1200.wamepiga pesa ndefu.
 
Mkuu mbona huyo Mukulu cha mtoto. Huu "mradi" unaoitwa Kilimo Kwanza huko tuendako utavunja rekodi kwa ufisadi kuliko mradi mwingine wowote uliowahi kuwepo nchi hii; yetu macho Mungu atuache hai muda si mrefu litabumburuka - EPA, Meremeta, Richmond, IPTL yote hii itakuwa vidagaa.

Magamba wanataka kuutumia kama "lango" la kutokea kupitia wakulima masikini lakini soon utabadilika kaburi lao.
 
Na Tshs 305 billions zipo Swiss za vigogo 6.... hii nchi tamu kweli....na hakuna anayekamatwa wala kuulizwa....!!

Mkuu mbona huyo Mukulu cha mtoto. Huu "mradi" unaoitwa Kilimo Kwanza huko tuendako utavunja rekodi kwa ufisadi kuliko mradi mwingine wowote uliowahi kuwepo nchi hii; yetu macho Mungu atuache hai muda si mrefu litabumburuka - EPA, Meremeta, Richmond, IPTL yote hii itakuwa vidagaa.

Magamba wanataka kuutumia kama "lango" la kutokea kupitia wakulima masikini lakini soon utabadilika kaburi lao.
 
nimesikia leo asubuhi kwenye taarifa ya habari E.A radio kuwa ameficha hela south africa
 
Sikuamini macho yangu, huyu mukulu wa mradi wa yale Matrekta ya Suma JKT pakle Mwenge maarufu kama "Kilimo Kwanza" nimeshuhudia leo akishuka kwenye gari ya Takukuru akiwa anafikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka pamoja na wenzake. Kulikoni? Ni Mjeshi huyu. Mara ya mwisho tulikaa nae kwenye ndege kwenye viti vya jirani na tukazungumza mengi, alikuwa ana hulka ya kilokole na mwenye kujawa na busara akichukizwa na uovu, sasa sijui imekuwaje tena. Any way tuiachie Mahakama.
Mkuu tuwekee majina yake yote na cheo chake tafadhali
 
Mambo ya Kikwete hayo, wamuone anacheka-cheka tu, yule ni komando wa ukweli.
 
Sina hakika na cheo chake kama ni kanali au nani but his name is Samilani..muumini wa muda mrefu kwa mama St Marys
 
umenikumbusha zile trilion 3 za mnadhimu kule kwa madiba - kweli Tz imenyonywa imebakia mifupa , jeshi nalo linapiga business, kila mtu anaiba kwa pale alipo as long as kuna loophole
 
Back
Top Bottom