Wanajeshi Arusha wafanya ukatili wa kutisha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Baadhi ya wanajeshi kutoka kikosi cha TMA Monduli wanaolinda chanzo cha maji katika kijiji cha Olgilai Arumeru wamemtesa kwa kipigo msichana Neema Alfred baada ya kuwakatalia tendo la ndoa walilohitaji baada ya msichana hiyo kupita eneo hilo wakati akitoka kuokota kuni.

1481358810009.jpg
 
Baadhi ya wanajeshi kutoka kikosi cha TMA Monduli wanaolinda chanzo cha maji katika kijiji cha Olgilai Arumeru wamwmtesa kwa kipigo msichàna Neema Alfred baada ya kuwakatalia tendo la ndoa walilohitaji ,baada ya msichana hiyo kupita eneo hilo Wakati akitoka kuokota kuni
.....5W+1H, JITAHIDI KUIKAMILISHA HABARI YAKO..
 
Kwa watu tuliowahi kuishi karibu na kambi za jeshi, hayo mambo yanatokea mara nyingi sana. Kuna mzee mmoja alishawahi kupigwa na wanajeshi mpaka akavunjwa mbavu kisa ng'ombe wake walikatiza eneo la jeshi. Kambi siitaji.
 
Nilivyoona "ukatili wa kutisha" nikajiandaa kuona watu wamechinjwa na kukatwakatwa viungo kumbe kapigwa arghhhhhh
 
Kama hilo tukio ni la kweli,wananchi wajaribu kufikiria nini kingetokea hao wanajeshi wangekua kwenye nafasi zote za polisi,na polisi wangekua kwenye nafasi za wanajeshi,hakika naamini kua polisi wangependwa na kunenewa mazuri wakati wanajeshi wangenenewa mabaya.Pole wewe dada kama kweli umefanyiwa hivyo.Tambua kua hao ni walinzi wa wananchi na unakatwa kodi ili wale vizuri na kupata mishahara inayoridhisha.
 
Aseme tu ukweli alikopigwa mwanajeshi akupige utoke hivi mbona kama kapigwa na khanga?kule mikanda yenye vyuma nilitalajia kuona matundu na nyama zikiwa nje,leteni ya misingi tujadili
 
Wanajeshi wetu wawe na nidhamu.
Bakiza akiba ya maneno hii habari haijajitosheleza
Inatia shaka askari wampige mdada? Ngumu
Kama kweli walimpiga anza kuwaza yafuatayo
1. Alijibu nyodo baada ya kupita njia au sehemu asiyoruhusiwa kupita kwa wakati huo
2. Yaweza kua alipita na mtu wake na wakajibu nyodo kwa askari ndo wakapewa adabu kidogo.
3. Kadundwa na mtu wake ambae ni askari

Kwa kawaida askari akiwa zaidi ya mmoja ni ngumu kumshambulia raia hasa mwanamke bora angekua mwanaume, sheria za kijeshi ziko complicated sana askari hawezi kumshambulia raia bila sababu maana kufanya hivyo ni kujitia risk kwenye kazi yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom