sexologist
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 2,283
- 976
Wakuu,
Nimefatilia kwa ukaribu mijadala na maoni ya wadau mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uteuzi wa wabunge wapya watatu akiwemo prof. Muhongo. Ambapo wengi wameshauri apewe wizara ya nishati na madini kutokana na utaalamu wake ktk madini kwenye masuala ya geology.
Mtazamo wangu, profesa muhongo kama tunamfikiria awe waziri wa nishati kutokana na weledi wake kiutaalam ktk sekta hyo si sahihi hata kidogo. Tukumbuke kuwa matatizo ya nchi yetu mengi hayapo kwenye ukosefu wa utaalamu, bali ni upungufu au kutokutekelezwa kwa sera husika. Hvyo ni sera ndizo zinatuletea matatizo yote haya, ikiwemo umaskini wetu. Kwa maneno mengine mtaalamu wa madini anatakiwa kuajiriwa kwenye sekta ya madini direct kama ni ukurugenzi au utendaji wa kawaida ili alete tija stahili.. Uwaziri anahitajika mtu mwenye uwezo wa kutekeleza au kutengeneza sera [as long as ni mbunge] kwa CV niliyoiona ya Muhongo nadhani anastahili ukatibu mkuu. Pia wadau tumekuwa tukiongozwa na prof. Mwakyusa, prof. Msolwa, na wengine wengi ktk wizara husika za taaluma zao lakini bdo hakukuwa na tija. Ni kwa sababu nilizozitaja.
Naomba kuwasilisha.