Wanajamii msaada wa haya mapaka!

G M S

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
502
53
Wanajf naomba msaada nifanye nini na hawa paka wa jirani ana paka zaid ya mmoja na usiku wanapanda batini na kuleta usumbufu hivi nifanye nini kuwadhibiti hawa paka batini kwangu?
 
Hivi si ulishaleta thread kama hii juzu juzi au?
 
Hivi si ulishaleta thread kama hii juzu juzi au?

ni kweli naomba unisaidie uliiona wapi ndugu kwasab niliiweka kwenye jukwaa la technologia na baada ya hapo sikuiona tena thred hii!
 
ni kweli naomba unisaidie uliiona wapi ndugu kwasab niliiweka kwenye jukwaa la technologia na baada ya hapo sikuiona tena thred hii!

Sikukumbuki ni jukwaa gani lakini ulipata majibu kidogo. wengine wakasema ueke sumu batini hao paka wafe....wengine waksema uwazoee tu usiwafikirie kabisa usiku
 
Kwani batini kwako wanafanya nini? Na unajuaje ni paka? Na unajuaje ni wa jirani yako? Na wanakaa muda gani? Unasikia wakifanya nini?
 
weka sumu kaka..kama mtu anafuga madudu yake na anashindwa kuyacontrol,just kill them
 
wengine ni paka watu,
hakuna namna ya kufa kwa sumu,
wataondoka kwa maombi tu.
 
Kwani batini kwako wanafanya nini? Na unajuaje ni paka? Na unajuaje ni wa jirani yako? Na wanakaa muda gani? Unasikia wakifanya nini?

khs wanapotokea am sure ni hapa kwa jiran labda kama wmamewaarika na wengine! Na mara zote huwa wanafanya njia ya kupita na wanapotembea huwa na kishindo kiasi kwamba wanaporuka sehemu moja had nyingine ni usumbufu mkubwa na kama inavyofahamika usiku ni muda kupata utulivu ila hapa nyumban ni kinyume labda nijaribu swala la sumu kwenye nyama af niweke batini!
 
Kama una amini katika Jina la YESU KRISTO kemea kwa jina la YESU KRISTO, weka damu ya YESU kwenye bati kwa imani ....kama ni ya kishirikina hayatakaa kamwe.....kama sio wewe mwambie tu BWANA YESU nahitaji kulala usingizi maana ni haki yangu itokayo kwako mwenyewe....naomba hawa paka wasikanyage tena katika paa langu...basi yeye anajua namna ya kuyaondoa...omba kwa imani pata wako usingizi wala hutawasikia tena.....kumbuka kuwa toka mwanzo tumepewa amri ya kuwatawala hawa wanyama....kama una imani wewe fanya hivyo na hao mapaka unaowaona hutawaona tena juu ya bati lako........kila la heri

mix with yours
 
Back
Top Bottom