Elections 2010 Wanajamii forum je mnafahamu kuwa rais bora atatoka ccm?

Mkatamiti

Member
Apr 21, 2010
11
0
KWA NINI WATANZANIA HAWAWEZI KUWAPA DOLA WAPINZANI!
  • Hadi sasa hawajafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya viongozi wao kuongoza dola, wamekurupuka na kuacha maswali mengi ikiwa kuwa na wagombea wenye dosari ambazo zinaepukika!
  • Ikulu sio mahala pa mchezo, utani wala pa kuhadaa Watanzania kwa kuuza sera zisizotekelezeka!
  • Halikadhalika wapinzani wameshindwa kujitandaza barabara nchi nzima tokea 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanza!
  • Lakini pia hawajaonyesha ukomavu wakuwa na mtandao wa umoja miongoni mwao dhidi ya CCM!
  • Uchu wa madaraka umezidi uwezo wao wa kudhibiti nchi jambo la hatari sana, hata kama baadhi ya taasisi za habari na wasomi zinajaribu kuwafagilia ili wakamate dola kwa njia za mkato!
  • CCM bado ni chama makini chenye mtandao wa uhakika unaofika vijijini japokuwa kinaendeshwa na binadamu ambao sio malaika!

Siku ya kwanza ya kampeni mwaka huu pale Agosti 21, 2010 dereva wa teksi niliokodi kuniwaisha Jangwani akasema CCM hawana haja ya kufanya kampeni ya kufa mtu kwa vile bado inaungwa mkono na kiasi kikubwa cha Watanzania nchini, tamko hilo alilitoa kutokana na kupata taabu sana kupenyapenya hadi tulipofika pale Jangwani, kwa vile maandamano ya Wana-CCM yaliotanda kila kona ya barabara zote zilizokuwa zinaelekea viwanja vya Jangwani ! Hata hivyo nilimueleza huu ni wakati wa mfumo wa vyama vingi vya siasa huwezi kujua Washindani wa CCM watakuja na mikakati gani! Lazima Wagombea wa CCM wafanye kampeni za kutosha ikiwa pamoja na kueleza kile walichoahidi katika Ilani yao ya 2005 kiasi gani wametekeleza na kile ambacho hakijatekelezwa ni kwa sababu gani na kwa nini Watanzania kwa Ilani mpya ya 2010 bado waendelee kuiamini na kuendelea kuipa hatamu za dola. Wakati Wapinzani wana kazi moja tu ni kubeza kila kitu kwa vile kufikiria wanaweza kuelezea jinsi watakavyo tekeleza sera zao itakuwa sawa na kuifagilia CCM. Hapa unaweza kusema ni sawasawa mwanafunzi wa Kidato cha kwanza kushindana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu mwenye uzoefu mkubwa tu kitaaluma.

Kwa hiyo sio ajabu mikakati ya wapinzani na wale wanaowaunga mkono silaha yao kubwa ni kukwepa kwa hali yeyote kusema ukweli kwa yale yote muhimu ya maana yaliyotekelezwa kwa umakini mkubwa na Serikali ya Awamu ya Nne kwa miaka 5 iliyopita katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Ushirikiano wa Kimataifa na kadhalika pamoja na kuenzi na kutunza tunu zetu kuu yaani amani , utulivu, usalama na mshikamano.

Wapinzani watakubaliana nami hali nchini ni shwari kabisa ukiacha zile sehemu za nchi hii ambako ama kuwepo na uchaguzi au usiwepo hulka za wananchi huko nikuwa na mtafaruku wa kiukoo na kuwa na tabia za kulipizana visasi, wakati mwingine kuwepo mfumo wa vyama vingi vya siasa sehemu hizo husika kumechochea hali kuwa mbaya zaidi kwa kukosekana uvumilivu ikilinganishwa na wakati wa mfumo wa siasa wa chama kimoja! (Suala hili la mapigano ya kiukoo liko nje ya mada ya makala hii)

Kukazia hapo hapo ukiachia tukio la kusikitisha lililotokea juzi kule Maswa alikouawa Mwana-CCM mmoja, hivi sasa wagombea Udiwani, Ubunge na Urais wanaendesha kampeni zao bila kizuizi mashariki hadi magharibi, Kaskazini hadi Kusini kutoka Mrima hadi Visiwani bila ya bughuza yeyote hata Mgombea mmoja amekuwa maarufu sana kuwa kila akiingia katika wilaya hudiriki kuomba kura binafsi ya Mkuu wa wilaya ofisini hali inayoleta burudani ya kutosha!

Uzoefu na kujiamini kwa CCM na Rais wa sasa aliye madarakani ndio kumeleta yote hayo, kuwapa marejeo kuwa Tanzania ndio kisiwa cha amani hapa Afrika Mashariki ni kwamba kuna nchi wanachama wenzetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivi karibuni walikuwa katika chaguzi na nyingine inajiandaa mwakani, huko kusema ukweli wana utamaduni wa kutovumiliana! Kuna mmojawapo wa wapinzani waliodai kufanya propaganda ya kusema uwongo dhidi ya hali halisi ya maafa yaliyotokea miaka ya karibuni katika nchi yake na matokeo yake ni kusekwa ndani mara moja na hivi sasa kesi inaendelea dhidi yake. Nchi nyingine wapinzani wenyewe baada kuona mambo magumu walijitoa kugombea nafasi zote kuanzia Udiwani, Ubunge na Urais. Aidha nchi ya tatu ambayo Watanzania walimwaga damu yao kuikomboa miaka ya mwisho ya 70 huko ukikarabia uchaguzi kunakuwa na sarakasi mgombea wa upinzani wa kutumainiwa akijaribu tu kumwaga sera , kesi ya uhaini inafunguliwa dhidi yake na hivyo kunyimwa fursa ya kushiriki harakati za uchaguzi inavyopaswa!

Hapa Tanzania kwa busara ya CCM na Rais Kikwete hakujatokea vituko vya aina hiyo japokuwa tokea filimbi ya utawala wa awamu ya nne kupulizwa mapema 2006 kuna vyombo vya habari na waandishi habari binafsi vilifunguliwa mbwa katika kuchapisha taarifa zenye kebehi, dhihaka na majungu tu ya kuudhi dhidi ya CCM na hasa kwa Ndugu JK kama Rais. ( Kuna makala moja ikaenda mbali na kumdhihaki Kamanda JK kuwa uwezo wake ni kuwa kongozi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya kutoa misaada -NGO na nyingine ya hivi karibuni inamwita Baba Krismasi! - Mungu awarehemu wazazi wa huyu mwandishi!) Imekuwa jambo la kawaida na labda ishazoeleka ukisoma majarida hayo lazima kuna kebehi au dharau dhidi ya Rais na Serikali yake kwa ujumla. Kati ya waandishi wa makala hizo anuwai namfahamu binafsi mmojawapo alishindwa kumaliza masomo yake ulaya kwa vile tu wazungu walimfanyia vitendo vya ubaguzi na kumdharau. Kwa sisi tuliokaa majuu ( Binafsi Urusi niliishi miaka 6 nikisoma masomo ya uzamili); kusema kweli kule ulaya kunyanyaswa ni jambo la kawaida ‘kutemwa mate ukipita na wengine walikuwa wanatuita ‘shetani’ au ‘nyani’ katika mabasi wanatunyanyapaa na kutuachia viti; kama majuzi tulivyosikia mshambuliaji nguli wa mchezo wa kandanda wa Kameruni na Inter Milan Samuel Eto’o akiwa uwanjani wapenzi wa Cagliari ya Italia kwa kumhofia walimwita nyani waziwazi, hakutetereka lakini aliweka umakini na kuwafunga Wataliana hao kama kazi! Lakini Mungu si Athumani, nauliza Mwandishi huyu hana hata chembe ya hisia ya makala zake za kumkashifu na kumkebehi Rais kama binadamu, anajisikiaje, je yeye angeliweza kuvumilia? Uzoefu wake wa kushindwa kumaliza masomo ulaya unadhihirisha huyu mwandishi kwa kweli ingelikuwa yeye anasakamwa kama anavyomfanyia Ndugu Rais haki ya Mungu angelijinyonga tu! Rais laiti angelitamka hivi vyombo na waandishi husika wachukuliwe hatua bila ya shaka wangefichwa mara moja, lakini hii sio hulka ya JK na nafahamu huviasa vyombo vya dola kwa kuwaambia..’ achaneni nao hao wamefilisika kisera na hatimaye Watanzania watawasikiliza na kuwafahamu wamesimamia upande gani na wataamua pumba zipi na mchele safi uko wapi..’!
Viko vikundi vichache hapa nchini kutokana na hamasa za kisiasa wanavuka mipaka lakini hao hawaungwi mkono na Watanzania walio wengi. Hata hivyo lazima nisema wazi kuna baadhi ya taasisi za mawasiliano na jamii zinaonyesha upendeleo wa wazi kwa wafuasi wa upinzani na kwamba fujo zikifanywa na CCM huwa nongwa! Baadhi ya taasisi hizo ni zile zilizojitokeza kudhihaki tamko safi la Vyombo vya Usalama nchini la kutahadharisha jamii kuwa Wanasiasa chonde chonde wasihubiri uchochezi ila wazingatie jukumu lao kufafanua sera zao na kuhakikisha wafuasi wao wa vyama vyao hawajiingizi katika kampeni za kashfa, matusi dhidi ya wapinzani wao. Asasi zile ziliponda tamko hilo kama kwamba vyama vya upinzani bila kuhubiri vitisho na uchochezi na kuua watu havitapigiwa kura, nasema asasi hizi zimefanya jambo la hatari na pia kama wasomi nahisi ni wanafiki na wala hawaitakii mema nchi yetu na uzalendo wao ni wa kutiliwa mashaka kabisa. Watanzania wapuuzeni na wakataeni wapenda ugomvi hao waliovalia majoho ya amani lakini ndani yake wameficha majambia!

Nafikiri watu wengi wanaendelea kupigwa na butwaa jinsi ya kiwango cha uvumilivu na subira ya Ndugu J K, nasema hiki ni kipaji maalum alichojaaliwa na Mola maana kama hatua za kiserikali zingechukuliwa Tanzania haingekuwa tofauti na nchi tatu nilizozitaja hapo awali ( sio Kenya) maana kule mtu ukijidai una akili sana tayari rungu la dola liko juu ya utosi wako.
Napenda kusisitiza kuwa katika wagombea wote wa kiti cha Urais nchini mwaka huu ni JK pekee tu aliye na uzoefu wa kutosha na kwamba hali hii inadhihirishwa na jinsi anavyotumia madaraka yake kwa busara, unyenyekevu na tahadhari kubwa. Madaraka ya dola akipewa mtu mwenye papara, asiye na uzoefu, mtu aisiyejali hisia za wenzake bali zake peke yake tutajikuta tunaumia Watanzania wote bila ya kujali unastahili au hapana. Na ndio maana hoja ya maandalizi ya muda mrefu kwa mgombea wa Urais ni lazima na wakati huo huo kuwepo mtandao wa kisiasa ulioenea nchini nzima na pia unaoaminika ili ufuatiliaji wa maamuzi ya Serikali yawe na ufanisi.

Tathmini zinaonyesha mgombea ambaye ameibuka kwa makeke mwaka huu hakuandaliwa kabisa kugombea nafasi hiyo ya juu na ndio maana ahadi zake ni maskhara matupu. Maana huyu kwa jinsi alivyo na ‘huruma’ sana kwa Watanzania kila kitu anataka kuwapa Watanzania bure chakula, nyumba, elimu na sio ajabu akasema kwa wale waseja akawapatia mke na mume bure, wahenga wanasema kua uone mambo! Hata hivyo tathmini zaidi zinaonyesha kuingia kwake katika kinyang’anyiro kunatokana na shinikizo kubwa kutoka nje ya chama husika ambapo ‘wafadhili hao’ walimuahidi kusafishwa kwa gharama yeyote dosari zozote alizonazo kwa lengo ya kuipeleka puta CCM na mgombea wake. Lengo kubwa la kundi linalompigia debe mgombea huyo ni kupunguza umaarufu wa JK na CCM na kwamba ifikapo 2015 waweze kuiangusha au kuunda hali ya kuwepo utawala legelege.
Watanzania ni watu makini hawatakuwa tayari kusokomezwa kooni Kiongozi ‘kibudu’ ki-maadili na laghai ambaye mfano wake sijapata kuuona!. Mfumo wa utoaji elimu na afya inayogharamiwa na Serikali kwa asilimia 100 uliachwa wakati Mwalimu Nyerere akiwa hai na alifahamu kwa nini hatua ya kubadili mfumo ilichukuliwa ( mchakato wa utoaji elimu bora na gharama zake ni mada ndefu sana makala hii sio lengo lake). Mgombea anayesema Serikali yake itatoa huduma bure ni sawa na mwanamume ambaye hamiliki hata baiskeli lakini ana mlaghai mwanamke anayemchumbia kuwa akimkubali atamnunulia ‘ndege’. Narudia Watanzania ni watu makini, nawasihi Watanzania watafakari kwa makini na wakubali kuwarudisha wapinzani darasani wakajifunze zaidi . Ni dhahiri kama wangetengeneza mtandao wa kisiasa unaoeleweka wangeweza kupata wagombea wazuri kwa majimbo yote 239 ya ubunge bara na visiwani na kuepuka hali ya sasa ya kuokoteza wagombea huko na huko na hasa wale wachache waliojiunga nao kwa chuki baada ya kushindwa kwenye mchakato wa kura za maoni wa CCM.
Aidha taasisi za mawasiliano na habari na Asasi za kiserikali –NGO’s zilizokuwa zinashabikia na kushinikiza kusambaratika kwa CCM japokuwa walikuwa hawawatendei haki Watanzania nawapa changamoto kwa kuona hali halisi ya sasa waanze kazi ya kuvipa ushauri nasaha vyama vya upinzani kuanzia sasa hadi 2015 viunde mtandao wa kisiasa utakaoenea nchi nzima bara na visiwani. Nazishauri taasisi na asasi hizi kuacha mara moja kampeni za kuifitinisha CCM wenyewe kwa wenyewe na kwa Watanzania, kwa vile kufanya hivyo hawawatendei haki Watanzania kwasababu silaha zinazopandwa za udini , ukabila hazitokomea kuiua CCM bali jamii yote ya Watanzania ! Swali hivi unavyotengeneza hii sumu kali dhidi ya jamii tukuweke fungu gani wewe ni mwanga au punguani au ni wakala uliotumwa kutoka nje?

Rai kwa upinzani kwa vile ni Watanzania wenzangu wasome alama za nyakati waanze mara moja baada ya uchaguzi huu mchakato wa kuunganisha nguvu jambo hili likitokea litawafanya Watanzania wawaamini kuwa ni watu makini na hivyo kuwafikiria katika azma yao ya kukamata dola siku za baadae. Fikiria hivi sasa hakuna chama cha upinzani kilichoweka wagombea katika majimbo yote 239 ya ubunge zaidi ya CCM ..huu ni upungufu mkubwa wengine wameweka 70 aliyejitahidi ameweka 90. Kama hivi ni vitambaa kwa ajili ya suti ya ‘serikali’ inabidi uamue kushona ama shati au kaptura maana hata suruali haitoshi na tena itakuwa inabana sana ! Kuendesha dola hutakiwi kufanya majaribio , Watanzania wanathamini usingizi wao ( ukiachia vijambazi vinavyootea otea siku moja moja!) wanathamini kushiriki katika shughuli zao za kijamii bila bughuza hawawezi kuiweka rehani tunu yetu ya amani na utulivu kukidhi uchu wa watu wachache wanaotaka kutwaa madaraka kwa gharama yeyote.

Ni dhahiri nafasi ya Urais ni nyeti kwa vile ndiye anayeidhibiti na wakati huo huo ni msimamizi mkuu wa rasilimali zote za nchi hivyo basi akikabidhiwa dhamana hii mtu mwenye nusu mtandao wa kisiasa nusu ya pili itabidi atumie mitulinga tu na pia hata ugawanyaji wa rasilimali utakuwa wa kidikteta bila ya shaka! Wananchi watakapo jaribu kuhoji na kukosoa hali halisi bila ya shaka yeyote watakabiliana na vitisho ikiwa pamoja na kuswekwa ndani bila hatiya na hatimaye wananchi wataanza kuikimbia Tanzania hii hii!
Unaweza kufanya majaribio katika mambo kama ya kuendesha vilabu vya usiku vya michezo ya kamari na disko lakini sio mamlaka ya kuendesha nchi itakuwa kama tumeamua kuchakachua maisha yetu!

Mtandao wa kisiasa ikiwemo kuwa na madiwani na wabunge wa kutosha ndio unaomwezesha Rais kuweza kugawa rasimali za nchi inavyopaswa kwa vile ndio wafuatiliaji; kuwapa uongozi wa dola kikundi cha kisiasa chenye sera za ulaghai na ushahidi uliowazi wa kulinda na kujali maslahi binafsi hata kwa kile kidogo walichofanikiwa ni kucheza kamari na kama hujui mbinu zake za kucheza utaliwa bila ya kufahamu!
Hivi sasa kimfumo CCM ndio yenye uongozi ulio karibu na wananchi popote pale nchini iwe mijini na vijijini huu ni mtaji tosha ! . Mtaji turufu kwa CCM ni uwekezaji uliofanyika 2005 kwa kumteua Ndugu JK kuwa mgombea wake na mwaka huu 2010 CCM inavuna ushindi kwa uwekezaji mzuri waliokwisha ufanya mwaka 2005!
Utendaji kazi na uthubutu wake Ndugu Rais unanikumbusha kiongozi wa China mwana mageuzi Deng Xiaoping pale 1979 alipoanzisha mageuzi ya modeninaizesheni ya uchumi ambayo mwaka jana 2009 waliadhimisha miaka 30 kwa mbwembwe kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana! Mwaka 1979 Deng alipotembelea Marekani, Komredi Fidel Castro wa Cuba alimkebehi sana Deng kwa kumuita kuwa ni kiongozi mwenye akili iliyofubaa! Ningependa kumuuliza leo Mzee Castro kama alikuwa sahihi kwani matokeo ya kazi safi ambayo msingi wake uliwekwa na Deng imedhirika. Ukweli ni kwamba sasa China limegeuka taifa mshindani na sio mshiriki kiuchumi duniani kote bidhaa na huduma zake zinakubalika dunia kote!

Wapinzani wa CCM na hasa baadhi ya wasomi wanalaumu kuachwa utekelezaji wa siasa ya ujamaa na kujitegemea wengine wanasema kilichoachwa ni kugawana umasikini na ujamaa uko palepale na kwamba mfumo wa sasa ni mbinu ya kukuza uchumi tu! Labda niseme kuwa kuna tofauti kubwa yetu sisi na China na ni kutokana na ukubwa wake ikiwa na mtaji wa watu zaidi ya bilioni 1.3 na uwezo ilionao wa maendeleo ya sayansi na teknolojia katika viwanda vya kisasa vya uzalishaji na ili kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi, Chama cha Kikoministi chini ya Deng kiliamua kwa makusudi kabisa katika sekta maalum zilizoteuliwa kuruhusu wajasiriamali kufanya vitu vyao hali iliyopelekea hata Waingereza walipoikabidhi Hongkong 1997 ikaweza kutambuliwa na kuachwa iendelee na mfumo wake wa kiuchumi wa soko huria (kwa miaka 50) kwa vile vi-hongkong vidogo vidogo vingi vilishaanzishwa sehemu maalum mbali mbali nchini China. Aidha wawekezaji binafsi kutoka nje wamewekeza katika maeneo maalum ya kiuchumi yalioanzishwa kuanzia mwaka 1979 nakupata mafanikio makubwa!. Nasi kwa vigezo vyetu kwa uongozi unaoona mbali wa JK muda sio mrefu tutafikia lengo la kuwa nchi yenye uchumi wa kati kama isemavyo ilani ya uchaguzi 2010 na Dira ya Maendeleo ya 2025!

Wasomi wetu wasiwe wanafiki kama wale Maprofesa Wa-kitanzania niliokutana nao Gaberone Botswana Oktoba mwaka 1998 katika sehemu moja ya burudani ambako nilipelekwa na mwenyeji wangu; pale nikaona ni mwage sera za ‘bongo’ wale jamaa walikuwa wanafanya kazi zenye hadhi kule Botswana wengine walikuwa wakuu wa taasisi na wengine wahadhiri waandamizi katika Chuo Kikuu cha Botswana! Nikawaambia kwa bashasha kuwa mafanikio yao yanatokana na msingi mzuri uliowekwa na Mwalimu Nyerere! Pema hapo walinirukia jamaa wakasema mafanikio yao hayatokani na Mwalimu Nyerere ni kwamba ni jitihada zao binafsi na wakanipa onyo kali kuwa kama nimechoka pale kustarehe niondoke! Nikaufyata kumbuka 1998 hayati Mwalimu alikuwa amebakisha kama mwaka mmoja afariki dunia! Miaka 11 baadae hawa jamaa nasema baadhi yao lakini wanatumia haiba ya msimamo wa kisiasa wa Hayati Mwalimu kwa malengo yao ya kisiasa. Mathalani mmoja wa Profesa maarufu nchini wakati akiwa mshauri wa kiongozi maarufu wa chama cha upinzani mwaka 1995 alimshauri Mwenyekiti wake aende nchi za nje kuongeza kiwango cha elimu yake kwa vile alikuwa na stashahada ya kawaida tu ya Ualimu! Yule Mwenyekiti akawa mbogo kwa vile alifahamu wasomi wanataka kumuengua madarakani kiulaini, hata hivyo cha kusikitisha mtafaruku huo uliendelea ambapo ulikitafuna chama husika hadi kikapoteza umaarufu wake! Cha kustaajabisha mwaka huu wa 2010 Profesa huyo huyo ana taarifa kuwa mgombea mwenza wa Urais wa chama anachokipigia debe mwaka huu amehitimu elimu ya msingi maana hata stashahada hana lakini amekuwa kimyaa! Msomi wa aina hii ana lengo gani kwa Taifa letu kwa vile ana hulka ya kusema uwongo kwa jambo lolote asilolipenda au kuliafiki!
Labda kwa muhtasari naweza kusema kuwa JK bado anakubalika sana na Watanzania ushuhuda ni maelfu yao walivyojitokeza kila alipopiga kampeni zake za nguvu katika mikoa yote 26 ya sasa Tanzania.(Mikoa mipya inaanza Julai, 2011).

Tukiacha ushabiki wa kisiasa vipimo vyote vinaonyesha bado CCM ndio yenye mtandao wa uhakika ambao unamhakikishia mwananchi wa kawaida kuihoji serikali katika ngazi zote kuanzia vijiji, vitongoji, kata, wilaya , mkoa na serikali kuu. Chini ya Amiri Jeshi Mkuu Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ambaye hana papara, msikivu, mvumilivu na anayeshaurika mfumo huu wa uendeshaji lazima uenziwe na udumishwe kwa kura yako wewe Mtanzania makini ambapo zaidi ya kupata fursa za kuendesha maisha yako pia kwako tunu za amani, usalama, utulivu na mshikamano zitalindwa! . Tujikumbushe Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere amewahi kusema katika uhai wake bila kumeza mate kuwa kwa mazingira ya Tanzania na naamini hadi leo ni sahihi kuwa: ‘ Rais bora nchini Tanzania atatoka CCM’! Kwa hiyo halikadhalika Wabunge na Madiwani bora pia watatoka CCM. Nasisitiza chagua maendeleo, amani, utulivu, usalama na mshikamano chagua CCM!
Mungu Ibariki Tanzania ,
Mungu Ibariki Afrika!
Mwandishi wa makala hii anapatikana kupitia barua pepe: mkatamiti@yahoo.com
 
hivi naomba nikuulize ar u out of ur mind?do u have any stress maybe,or any mental problem?
 
Hata hii ikiwa ni kweli, Dr Slaa katokea ccm kuingia chadema.
Kwa hiyo utabiri wako bado unatimia mwaka huu kwa kumchagua Dr Slaa (PhD) kuwa raisi wa tano wa JMT.
 
Mkatamiti
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
  • email.png
    Send Email
user-online.png
Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateWed Apr 2010Posts3Thanks0Thanked 2 Times in 1 Pos
 
Mimi bila kupitia thread ndefu kama shuka!! nakuuliza wewe mwandishi uliambiwa Jf nichama pinzani?copy and post hutumii akili maana ukikaa ukakatulia huwezi ukaandika vitu vyenye hombwe.
 
du mwandishi una weledi mkubwa ni kweli jf ni chama cha siasa ukimpinga slaa rais wao ujue utatukanwa na kukashifiwa
 
KWA NINI WATANZANIA HAWAWEZI KUWAPA DOLA WAPINZANI!
  • Hadi sasa hawajafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya viongozi wao kuongoza dola, wamekurupuka na kuacha maswali mengi ikiwa kuwa na wagombea wenye dosari ambazo zinaepukika!
  • Ikulu sio mahala pa mchezo, utani wala pa kuhadaa Watanzania kwa kuuza sera zisizotekelezeka!
  • Halikadhalika wapinzani wameshindwa kujitandaza barabara nchi nzima tokea 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanza!
  • Lakini pia hawajaonyesha ukomavu wakuwa na mtandao wa umoja miongoni mwao dhidi ya CCM!
  • Uchu wa madaraka umezidi uwezo wao wa kudhibiti nchi jambo la hatari sana, hata kama baadhi ya taasisi za habari na wasomi zinajaribu kuwafagilia ili wakamate dola kwa njia za mkato!
  • CCM bado ni chama makini chenye mtandao wa uhakika unaofika vijijini japokuwa kinaendeshwa na binadamu ambao sio malaika!
Siku ya kwanza ya kampeni mwaka huu pale Agosti 21, 2010 dereva wa teksi niliokodi kuniwaisha Jangwani akasema CCM hawana haja ya kufanya kampeni ya kufa mtu kwa vile bado inaungwa mkono na kiasi kikubwa cha Watanzania nchini, tamko hilo alilitoa kutokana na kupata taabu sana kupenyapenya hadi tulipofika pale Jangwani, kwa vile maandamano ya Wana-CCM yaliotanda kila kona ya barabara zote zilizokuwa zinaelekea viwanja vya Jangwani ! Hata hivyo nilimueleza huu ni wakati wa mfumo wa vyama vingi vya siasa huwezi kujua Washindani wa CCM watakuja na mikakati gani! Lazima Wagombea wa CCM wafanye kampeni za kutosha ikiwa pamoja na kueleza kile walichoahidi katika Ilani yao ya 2005 kiasi gani wametekeleza na kile ambacho hakijatekelezwa ni kwa sababu gani na kwa nini Watanzania kwa Ilani mpya ya 2010 bado waendelee kuiamini na kuendelea kuipa hatamu za dola. Wakati Wapinzani wana kazi moja tu ni kubeza kila kitu kwa vile kufikiria wanaweza kuelezea jinsi watakavyo tekeleza sera zao itakuwa sawa na kuifagilia CCM. Hapa unaweza kusema ni sawasawa mwanafunzi wa Kidato cha kwanza kushindana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu mwenye uzoefu mkubwa tu kitaaluma.

Kwa hiyo sio ajabu mikakati ya wapinzani na wale wanaowaunga mkono silaha yao kubwa ni kukwepa kwa hali yeyote kusema ukweli kwa yale yote muhimu ya maana yaliyotekelezwa kwa umakini mkubwa na Serikali ya Awamu ya Nne kwa miaka 5 iliyopita katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, Ushirikiano wa Kimataifa na kadhalika pamoja na kuenzi na kutunza tunu zetu kuu yaani amani , utulivu, usalama na mshikamano.

Wapinzani watakubaliana nami hali nchini ni shwari kabisa ukiacha zile sehemu za nchi hii ambako ama kuwepo na uchaguzi au usiwepo hulka za wananchi huko nikuwa na mtafaruku wa kiukoo na kuwa na tabia za kulipizana visasi, wakati mwingine kuwepo mfumo wa vyama vingi vya siasa sehemu hizo husika kumechochea hali kuwa mbaya zaidi kwa kukosekana uvumilivu ikilinganishwa na wakati wa mfumo wa siasa wa chama kimoja! (Suala hili la mapigano ya kiukoo liko nje ya mada ya makala hii)

Kukazia hapo hapo ukiachia tukio la kusikitisha lililotokea juzi kule Maswa alikouawa Mwana-CCM mmoja, hivi sasa wagombea Udiwani, Ubunge na Urais wanaendesha kampeni zao bila kizuizi mashariki hadi magharibi, Kaskazini hadi Kusini kutoka Mrima hadi Visiwani bila ya bughuza yeyote hata Mgombea mmoja amekuwa maarufu sana kuwa kila akiingia katika wilaya hudiriki kuomba kura binafsi ya Mkuu wa wilaya ofisini hali inayoleta burudani ya kutosha!

Uzoefu na kujiamini kwa CCM na Rais wa sasa aliye madarakani ndio kumeleta yote hayo, kuwapa marejeo kuwa Tanzania ndio kisiwa cha amani hapa Afrika Mashariki ni kwamba kuna nchi wanachama wenzetu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivi karibuni walikuwa katika chaguzi na nyingine inajiandaa mwakani, huko kusema ukweli wana utamaduni wa kutovumiliana! Kuna mmojawapo wa wapinzani waliodai kufanya propaganda ya kusema uwongo dhidi ya hali halisi ya maafa yaliyotokea miaka ya karibuni katika nchi yake na matokeo yake ni kusekwa ndani mara moja na hivi sasa kesi inaendelea dhidi yake. Nchi nyingine wapinzani wenyewe baada kuona mambo magumu walijitoa kugombea nafasi zote kuanzia Udiwani, Ubunge na Urais. Aidha nchi ya tatu ambayo Watanzania walimwaga damu yao kuikomboa miaka ya mwisho ya 70 huko ukikarabia uchaguzi kunakuwa na sarakasi mgombea wa upinzani wa kutumainiwa akijaribu tu kumwaga sera , kesi ya uhaini inafunguliwa dhidi yake na hivyo kunyimwa fursa ya kushiriki harakati za uchaguzi inavyopaswa!

Hapa Tanzania kwa busara ya CCM na Rais Kikwete hakujatokea vituko vya aina hiyo japokuwa tokea filimbi ya utawala wa awamu ya nne kupulizwa mapema 2006 kuna vyombo vya habari na waandishi habari binafsi vilifunguliwa mbwa katika kuchapisha taarifa zenye kebehi, dhihaka na majungu tu ya kuudhi dhidi ya CCM na hasa kwa Ndugu JK kama Rais. ( Kuna makala moja ikaenda mbali na kumdhihaki Kamanda JK kuwa uwezo wake ni kuwa kongozi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya kutoa misaada -NGO na nyingine ya hivi karibuni inamwita Baba Krismasi! - Mungu awarehemu wazazi wa huyu mwandishi!) Imekuwa jambo la kawaida na labda ishazoeleka ukisoma majarida hayo lazima kuna kebehi au dharau dhidi ya Rais na Serikali yake kwa ujumla. Kati ya waandishi wa makala hizo anuwai namfahamu binafsi mmojawapo alishindwa kumaliza masomo yake ulaya kwa vile tu wazungu walimfanyia vitendo vya ubaguzi na kumdharau. Kwa sisi tuliokaa majuu ( Binafsi Urusi niliishi miaka 6 nikisoma masomo ya uzamili); kusema kweli kule ulaya kunyanyaswa ni jambo la kawaida ‘kutemwa mate ukipita na wengine walikuwa wanatuita ‘shetani' au ‘nyani' katika mabasi wanatunyanyapaa na kutuachia viti; kama majuzi tulivyosikia mshambuliaji nguli wa mchezo wa kandanda wa Kameruni na Inter Milan Samuel Eto'o akiwa uwanjani wapenzi wa Cagliari ya Italia kwa kumhofia walimwita nyani waziwazi, hakutetereka lakini aliweka umakini na kuwafunga Wataliana hao kama kazi! Lakini Mungu si Athumani, nauliza Mwandishi huyu hana hata chembe ya hisia ya makala zake za kumkashifu na kumkebehi Rais kama binadamu, anajisikiaje, je yeye angeliweza kuvumilia? Uzoefu wake wa kushindwa kumaliza masomo ulaya unadhihirisha huyu mwandishi kwa kweli ingelikuwa yeye anasakamwa kama anavyomfanyia Ndugu Rais haki ya Mungu angelijinyonga tu! Rais laiti angelitamka hivi vyombo na waandishi husika wachukuliwe hatua bila ya shaka wangefichwa mara moja, lakini hii sio hulka ya JK na nafahamu huviasa vyombo vya dola kwa kuwaambia..' achaneni nao hao wamefilisika kisera na hatimaye Watanzania watawasikiliza na kuwafahamu wamesimamia upande gani na wataamua pumba zipi na mchele safi uko wapi..'!
Viko vikundi vichache hapa nchini kutokana na hamasa za kisiasa wanavuka mipaka lakini hao hawaungwi mkono na Watanzania walio wengi. Hata hivyo lazima nisema wazi kuna baadhi ya taasisi za mawasiliano na jamii zinaonyesha upendeleo wa wazi kwa wafuasi wa upinzani na kwamba fujo zikifanywa na CCM huwa nongwa! Baadhi ya taasisi hizo ni zile zilizojitokeza kudhihaki tamko safi la Vyombo vya Usalama nchini la kutahadharisha jamii kuwa Wanasiasa chonde chonde wasihubiri uchochezi ila wazingatie jukumu lao kufafanua sera zao na kuhakikisha wafuasi wao wa vyama vyao hawajiingizi katika kampeni za kashfa, matusi dhidi ya wapinzani wao. Asasi zile ziliponda tamko hilo kama kwamba vyama vya upinzani bila kuhubiri vitisho na uchochezi na kuua watu havitapigiwa kura, nasema asasi hizi zimefanya jambo la hatari na pia kama wasomi nahisi ni wanafiki na wala hawaitakii mema nchi yetu na uzalendo wao ni wa kutiliwa mashaka kabisa. Watanzania wapuuzeni na wakataeni wapenda ugomvi hao waliovalia majoho ya amani lakini ndani yake wameficha majambia!

Nafikiri watu wengi wanaendelea kupigwa na butwaa jinsi ya kiwango cha uvumilivu na subira ya Ndugu J K, nasema hiki ni kipaji maalum alichojaaliwa na Mola maana kama hatua za kiserikali zingechukuliwa Tanzania haingekuwa tofauti na nchi tatu nilizozitaja hapo awali ( sio Kenya) maana kule mtu ukijidai una akili sana tayari rungu la dola liko juu ya utosi wako.
Napenda kusisitiza kuwa katika wagombea wote wa kiti cha Urais nchini mwaka huu ni JK pekee tu aliye na uzoefu wa kutosha na kwamba hali hii inadhihirishwa na jinsi anavyotumia madaraka yake kwa busara, unyenyekevu na tahadhari kubwa. Madaraka ya dola akipewa mtu mwenye papara, asiye na uzoefu, mtu aisiyejali hisia za wenzake bali zake peke yake tutajikuta tunaumia Watanzania wote bila ya kujali unastahili au hapana. Na ndio maana hoja ya maandalizi ya muda mrefu kwa mgombea wa Urais ni lazima na wakati huo huo kuwepo mtandao wa kisiasa ulioenea nchini nzima na pia unaoaminika ili ufuatiliaji wa maamuzi ya Serikali yawe na ufanisi.

Tathmini zinaonyesha mgombea ambaye ameibuka kwa makeke mwaka huu hakuandaliwa kabisa kugombea nafasi hiyo ya juu na ndio maana ahadi zake ni maskhara matupu. Maana huyu kwa jinsi alivyo na ‘huruma' sana kwa Watanzania kila kitu anataka kuwapa Watanzania bure chakula, nyumba, elimu na sio ajabu akasema kwa wale waseja akawapatia mke na mume bure, wahenga wanasema kua uone mambo! Hata hivyo tathmini zaidi zinaonyesha kuingia kwake katika kinyang'anyiro kunatokana na shinikizo kubwa kutoka nje ya chama husika ambapo ‘wafadhili hao' walimuahidi kusafishwa kwa gharama yeyote dosari zozote alizonazo kwa lengo ya kuipeleka puta CCM na mgombea wake. Lengo kubwa la kundi linalompigia debe mgombea huyo ni kupunguza umaarufu wa JK na CCM na kwamba ifikapo 2015 waweze kuiangusha au kuunda hali ya kuwepo utawala legelege.
Watanzania ni watu makini hawatakuwa tayari kusokomezwa kooni Kiongozi ‘kibudu' ki-maadili na laghai ambaye mfano wake sijapata kuuona!. Mfumo wa utoaji elimu na afya inayogharamiwa na Serikali kwa asilimia 100 uliachwa wakati Mwalimu Nyerere akiwa hai na alifahamu kwa nini hatua ya kubadili mfumo ilichukuliwa ( mchakato wa utoaji elimu bora na gharama zake ni mada ndefu sana makala hii sio lengo lake). Mgombea anayesema Serikali yake itatoa huduma bure ni sawa na mwanamume ambaye hamiliki hata baiskeli lakini ana mlaghai mwanamke anayemchumbia kuwa akimkubali atamnunulia ‘ndege'. Narudia Watanzania ni watu makini, nawasihi Watanzania watafakari kwa makini na wakubali kuwarudisha wapinzani darasani wakajifunze zaidi . Ni dhahiri kama wangetengeneza mtandao wa kisiasa unaoeleweka wangeweza kupata wagombea wazuri kwa majimbo yote 239 ya ubunge bara na visiwani na kuepuka hali ya sasa ya kuokoteza wagombea huko na huko na hasa wale wachache waliojiunga nao kwa chuki baada ya kushindwa kwenye mchakato wa kura za maoni wa CCM.
Aidha taasisi za mawasiliano na habari na Asasi za kiserikali –NGO's zilizokuwa zinashabikia na kushinikiza kusambaratika kwa CCM japokuwa walikuwa hawawatendei haki Watanzania nawapa changamoto kwa kuona hali halisi ya sasa waanze kazi ya kuvipa ushauri nasaha vyama vya upinzani kuanzia sasa hadi 2015 viunde mtandao wa kisiasa utakaoenea nchi nzima bara na visiwani. Nazishauri taasisi na asasi hizi kuacha mara moja kampeni za kuifitinisha CCM wenyewe kwa wenyewe na kwa Watanzania, kwa vile kufanya hivyo hawawatendei haki Watanzania kwasababu silaha zinazopandwa za udini , ukabila hazitokomea kuiua CCM bali jamii yote ya Watanzania ! Swali hivi unavyotengeneza hii sumu kali dhidi ya jamii tukuweke fungu gani wewe ni mwanga au punguani au ni wakala uliotumwa kutoka nje?

Rai kwa upinzani kwa vile ni Watanzania wenzangu wasome alama za nyakati waanze mara moja baada ya uchaguzi huu mchakato wa kuunganisha nguvu jambo hili likitokea litawafanya Watanzania wawaamini kuwa ni watu makini na hivyo kuwafikiria katika azma yao ya kukamata dola siku za baadae. Fikiria hivi sasa hakuna chama cha upinzani kilichoweka wagombea katika majimbo yote 239 ya ubunge zaidi ya CCM ..huu ni upungufu mkubwa wengine wameweka 70 aliyejitahidi ameweka 90. Kama hivi ni vitambaa kwa ajili ya suti ya ‘serikali' inabidi uamue kushona ama shati au kaptura maana hata suruali haitoshi na tena itakuwa inabana sana ! Kuendesha dola hutakiwi kufanya majaribio , Watanzania wanathamini usingizi wao ( ukiachia vijambazi vinavyootea otea siku moja moja!) wanathamini kushiriki katika shughuli zao za kijamii bila bughuza hawawezi kuiweka rehani tunu yetu ya amani na utulivu kukidhi uchu wa watu wachache wanaotaka kutwaa madaraka kwa gharama yeyote.

Ni dhahiri nafasi ya Urais ni nyeti kwa vile ndiye anayeidhibiti na wakati huo huo ni msimamizi mkuu wa rasilimali zote za nchi hivyo basi akikabidhiwa dhamana hii mtu mwenye nusu mtandao wa kisiasa nusu ya pili itabidi atumie mitulinga tu na pia hata ugawanyaji wa rasilimali utakuwa wa kidikteta bila ya shaka! Wananchi watakapo jaribu kuhoji na kukosoa hali halisi bila ya shaka yeyote watakabiliana na vitisho ikiwa pamoja na kuswekwa ndani bila hatiya na hatimaye wananchi wataanza kuikimbia Tanzania hii hii!
Unaweza kufanya majaribio katika mambo kama ya kuendesha vilabu vya usiku vya michezo ya kamari na disko lakini sio mamlaka ya kuendesha nchi itakuwa kama tumeamua kuchakachua maisha yetu!

Mtandao wa kisiasa ikiwemo kuwa na madiwani na wabunge wa kutosha ndio unaomwezesha Rais kuweza kugawa rasimali za nchi inavyopaswa kwa vile ndio wafuatiliaji; kuwapa uongozi wa dola kikundi cha kisiasa chenye sera za ulaghai na ushahidi uliowazi wa kulinda na kujali maslahi binafsi hata kwa kile kidogo walichofanikiwa ni kucheza kamari na kama hujui mbinu zake za kucheza utaliwa bila ya kufahamu!
Hivi sasa kimfumo CCM ndio yenye uongozi ulio karibu na wananchi popote pale nchini iwe mijini na vijijini huu ni mtaji tosha ! . Mtaji turufu kwa CCM ni uwekezaji uliofanyika 2005 kwa kumteua Ndugu JK kuwa mgombea wake na mwaka huu 2010 CCM inavuna ushindi kwa uwekezaji mzuri waliokwisha ufanya mwaka 2005!
Utendaji kazi na uthubutu wake Ndugu Rais unanikumbusha kiongozi wa China mwana mageuzi Deng Xiaoping pale 1979 alipoanzisha mageuzi ya modeninaizesheni ya uchumi ambayo mwaka jana 2009 waliadhimisha miaka 30 kwa mbwembwe kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana! Mwaka 1979 Deng alipotembelea Marekani, Komredi Fidel Castro wa Cuba alimkebehi sana Deng kwa kumuita kuwa ni kiongozi mwenye akili iliyofubaa! Ningependa kumuuliza leo Mzee Castro kama alikuwa sahihi kwani matokeo ya kazi safi ambayo msingi wake uliwekwa na Deng imedhirika. Ukweli ni kwamba sasa China limegeuka taifa mshindani na sio mshiriki kiuchumi duniani kote bidhaa na huduma zake zinakubalika dunia kote!

Wapinzani wa CCM na hasa baadhi ya wasomi wanalaumu kuachwa utekelezaji wa siasa ya ujamaa na kujitegemea wengine wanasema kilichoachwa ni kugawana umasikini na ujamaa uko palepale na kwamba mfumo wa sasa ni mbinu ya kukuza uchumi tu! Labda niseme kuwa kuna tofauti kubwa yetu sisi na China na ni kutokana na ukubwa wake ikiwa na mtaji wa watu zaidi ya bilioni 1.3 na uwezo ilionao wa maendeleo ya sayansi na teknolojia katika viwanda vya kisasa vya uzalishaji na ili kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi, Chama cha Kikoministi chini ya Deng kiliamua kwa makusudi kabisa katika sekta maalum zilizoteuliwa kuruhusu wajasiriamali kufanya vitu vyao hali iliyopelekea hata Waingereza walipoikabidhi Hongkong 1997 ikaweza kutambuliwa na kuachwa iendelee na mfumo wake wa kiuchumi wa soko huria (kwa miaka 50) kwa vile vi-hongkong vidogo vidogo vingi vilishaanzishwa sehemu maalum mbali mbali nchini China. Aidha wawekezaji binafsi kutoka nje wamewekeza katika maeneo maalum ya kiuchumi yalioanzishwa kuanzia mwaka 1979 nakupata mafanikio makubwa!. Nasi kwa vigezo vyetu kwa uongozi unaoona mbali wa JK muda sio mrefu tutafikia lengo la kuwa nchi yenye uchumi wa kati kama isemavyo ilani ya uchaguzi 2010 na Dira ya Maendeleo ya 2025!

Wasomi wetu wasiwe wanafiki kama wale Maprofesa Wa-kitanzania niliokutana nao Gaberone Botswana Oktoba mwaka 1998 katika sehemu moja ya burudani ambako nilipelekwa na mwenyeji wangu; pale nikaona ni mwage sera za ‘bongo' wale jamaa walikuwa wanafanya kazi zenye hadhi kule Botswana wengine walikuwa wakuu wa taasisi na wengine wahadhiri waandamizi katika Chuo Kikuu cha Botswana! Nikawaambia kwa bashasha kuwa mafanikio yao yanatokana na msingi mzuri uliowekwa na Mwalimu Nyerere! Pema hapo walinirukia jamaa wakasema mafanikio yao hayatokani na Mwalimu Nyerere ni kwamba ni jitihada zao binafsi na wakanipa onyo kali kuwa kama nimechoka pale kustarehe niondoke! Nikaufyata kumbuka 1998 hayati Mwalimu alikuwa amebakisha kama mwaka mmoja afariki dunia! Miaka 11 baadae hawa jamaa nasema baadhi yao lakini wanatumia haiba ya msimamo wa kisiasa wa Hayati Mwalimu kwa malengo yao ya kisiasa. Mathalani mmoja wa Profesa maarufu nchini wakati akiwa mshauri wa kiongozi maarufu wa chama cha upinzani mwaka 1995 alimshauri Mwenyekiti wake aende nchi za nje kuongeza kiwango cha elimu yake kwa vile alikuwa na stashahada ya kawaida tu ya Ualimu! Yule Mwenyekiti akawa mbogo kwa vile alifahamu wasomi wanataka kumuengua madarakani kiulaini, hata hivyo cha kusikitisha mtafaruku huo uliendelea ambapo ulikitafuna chama husika hadi kikapoteza umaarufu wake! Cha kustaajabisha mwaka huu wa 2010 Profesa huyo huyo ana taarifa kuwa mgombea mwenza wa Urais wa chama anachokipigia debe mwaka huu amehitimu elimu ya msingi maana hata stashahada hana lakini amekuwa kimyaa! Msomi wa aina hii ana lengo gani kwa Taifa letu kwa vile ana hulka ya kusema uwongo kwa jambo lolote asilolipenda au kuliafiki!
Labda kwa muhtasari naweza kusema kuwa JK bado anakubalika sana na Watanzania ushuhuda ni maelfu yao walivyojitokeza kila alipopiga kampeni zake za nguvu katika mikoa yote 26 ya sasa Tanzania.(Mikoa mipya inaanza Julai, 2011).

Tukiacha ushabiki wa kisiasa vipimo vyote vinaonyesha bado CCM ndio yenye mtandao wa uhakika ambao unamhakikishia mwananchi wa kawaida kuihoji serikali katika ngazi zote kuanzia vijiji, vitongoji, kata, wilaya , mkoa na serikali kuu. Chini ya Amiri Jeshi Mkuu Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ambaye hana papara, msikivu, mvumilivu na anayeshaurika mfumo huu wa uendeshaji lazima uenziwe na udumishwe kwa kura yako wewe Mtanzania makini ambapo zaidi ya kupata fursa za kuendesha maisha yako pia kwako tunu za amani, usalama, utulivu na mshikamano zitalindwa! . Tujikumbushe Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere amewahi kusema katika uhai wake bila kumeza mate kuwa kwa mazingira ya Tanzania na naamini hadi leo ni sahihi kuwa: ' Rais bora nchini Tanzania atatoka CCM'! Kwa hiyo halikadhalika Wabunge na Madiwani bora pia watatoka CCM. Nasisitiza chagua maendeleo, amani, utulivu, usalama na mshikamano chagua CCM!
Mungu Ibariki Tanzania ,
Mungu Ibariki Afrika!
Mwandishi wa makala hii anapatikana kupitia barua pepe: mkatamiti@yahoo.com

Thesis ya great thinker haiwezi kuwa ndefu namna hii! Nimetupilia mbali thread yako, sina muda wa kuchambua mchele kwenye lundo pumba almost 98%!
 
talumba mkiwa;
"du mwandishi una weledi mkubwa ni kweli jf ni chama cha siasa ukimpinga slaa rais wao ujue utatukanwa na kukashifiwa"

Ni kweli ila Break Jumapili mabox ya kura yataongea. Kauli nyingi na majigambo tumeyasikia, sasa imebaki zamu yetu kuongea kwenye vile vyumba vya siri tukitumia haki zetu.

Ewe Mola usitupoke uhai kwa siku hizi ili tuwaone wale watakaolia na kusaga meno. Amin!
 
Back
Top Bottom